Rwanda kuanza kutumia sindano badala ya vidonge vya kufubaza makali ya VVU

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,095
2,000
Tiba ya sindano badala ya vidonge vya kila siku kwa wagonjwa wa ukimwi nchini Rwanda yameshika kasi na sasa iko katika awamu ya mwisho

Tiba ya sindano badala ya vidonge vya kila siku kwa wagonjwa wa ukimwi nchini Rwanda yameshika kasi na sasa iko katika awamu ya mwisho.

Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza kwamba mnamo miaka michache ijayo, wagonjwa wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi hawatalazimika tena kutumia dawa za kila siku ikiwa sindano ambayo imekuwa ikifanyiwa majaribio itafanikiwa.

Rwanda ni mojawapo ya nchi zinazohusika na mpango wa jaribio la dawa ya sindano ya virusi vya ukimwi ambayo inachukuliwa kuwa njia bora zaidi ya matibabu.

Afisa mkuu wa mamlaka ya afya nchini Rwanda, daktari Sabin Nsanzimana, ametangaza kwamba majaribio ya matumizi ya sindano badala ya vidonge vya kila siku kwa wagonjwa wa ukimwi yameshika kasi na sasa yako katika awamu ya mwisho.

"Ni mwaka mmoja sasa tukiwa tunafanya haya majaribio ya kutumia sindano ambayo itakuwa ni moja kwa wiki 8 badala ya mgonjwa kumeza kidonge kimoja kila siku. Kuna dawa aina mbili zilizochanganywa kwenye sindano.''

Dkt Sabin Nsanzimana ameongeza kusema kwamba majaribio ya njia ya matumizi ya sindano ndiyo ya kisasa kabisa katika utoaji wa matibabu ya kupambana siyo tu dhidi ya ukimwi bali pia maradhi ya kudumu.

Hii ni habari iliyopokelewa vyema na baadhi ya wanaoishi na virusi vya HIV nchini Rwanda ambao hutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi.

2af1b117c262181770fbce3bd9d55154-1

Uchunguzi wa damu ni muhimu ili kubaini kama una virusi vya HIV
Mwanamke huyu ambaye hakutaka jina lake kutangazwa anasema alijua kwamba aliambukizwa ukimwi mwaka 2012 na kuanza kutumia dawa:

''Habari ya majaribio ya sindano nimeipokea vizuri kabisa kwa sababu natumia kidonge kimoja kila usiku. Kuna hatari hata ya kusahau kutumia kidonge kwa wakati mwafaka. Sindano ya kila miezi miwili ni afadhali kinachobaki tu najiuliza ni lini sindano hizo zitaanza kutufikia''

Wizara ya afya ya Rwanda inasema kwamba majaribio yamefika katika awamu ya nne ya utafiti ambayo ndio ya mwisho kabla ya dawa kusambazwa sokoni na kwamba hatua hiyo inaweza kuchukua muda usio chini ya mwaka mmoja kwanzia sasa.

Ripoti ya utafiti wa hivi karibuni kuhusu maambukizi ya ukimwi nchini Rwanda imebainisha kwamba ni 3% tu ya wananchi walioambukizwa virusi vya HIV.

Pia ripoti hiyo ilisema kuwa wanaotumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi ni asilimia 94.

Chanzo: BBC Swahili
 

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,909
2,000
Kama ndo hivi hata Mimi nitaenda kupima sasa

Maana siwezi kwenda kupima niambiwe ninao kisha nianze kubugia midawa kila siku hiyo kazi siiwezi aisee.
 

IJIGHA NDIO HOME

JF-Expert Member
Jul 13, 2019
641
1,000
inamaana kwa mwaka unachomwa karibu mara tano mwili huohuo sasa piga Esabu miaka ishirini utakua mtu ww
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom