Rwanda: Kagame ayafungia maelfu ya makanisa ya Kiinjili

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Serikali ya Rwanda imechukua hatua ya kufunga maelfu ya makanisa ya kiinjili nchini humo, kufuatia ongezeko lake la kasi ambalo limeibua wasiwasi miongoni mwa mamlaka za serikali.

Mamlaka zimeyakosoa makanisa hayo kwa kuyataja kuwa yamepoteza mwelekeo wake wa msingi, yakidaiwa kugeuka kuwa “mapango ya wezi” badala ya kutoa huduma za kiroho na kijamii zinazotarajiwa kwa waumini na jamii kwa ujumla.

1766391663538.png

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amekuwa mstari wa mbele katika kuyakosoa makanisa ya kiinjili yanayoibuka kwa wingi katika nchi hiyo iliyopo ukanda wa Maziwa Makuu. Hatua hiyo ya serikali inakuja wakati kukiwa na malalamiko kuhusu utaratibu wa uendeshaji na malengo ya baadhi ya taasisi hizo za kidini.

Licha ya uamuzi huo, sensa ya Rwanda ya mwaka 2024 inaonesha kuwa idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo ni Wakristo. Hali hii imesababisha changamoto kwa waumini wengi, wanaoelezwa kulazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama zaidi ili kutafuta maeneo mbadala ya kufanyia ibada.

Uamuzi wa kufunga makanisa hayo unaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali kuimarisha udhibiti na usimamizi wa karibu. Baadhi ya makanisa yanadaiwa kukiuka Sheria ya mwaka 2018, inayotaka kila taasisi ya kidini kuwasilisha mipango ya utekelezaji ya kila mwaka, ikieleza kwa kina jinsi shughuli zake zinavyoendana na maadili ya kitaifa.

View attachment 3518973

Duh mambo ya upako wa bwana yashakuwa magumu.
 
yuko sawa kabisa, kisheria hata hapa tanzagiza ilikuwepo kwa maana tumerithi hizo sheria ktk kwa Christians, ni kwamba ili Kanisa lisajiliwe ni lazima likidhi vigezo kimojawapo na cha kwanza kabisa mchungaji ni lazima awe amesomea theolojia, i.e awe na degree ya theology, mengineyo kama idadi ya waumini pia inahusika, lkn huwezi kuja tu ulikotoka na kufungua kanisa ni sawa na hospitali au famasi huwezi kwa hali ya kawaida kufungua hospitali kama wewe siyo daktari.

sasa matokeo ya kutokufwata hiyo misingi tunayaona hapa kwetu kanisa linafunguliwa na serikali kawe kwa malengo maalumu ya kisiasa kudhoofisha Christianity, hata shehe anaweza kufungua kanisa tanzagiza na akapata usajili ...
 
Serikali ya Rwanda imechukua hatua ya kufunga maelfu ya makanisa ya kiinjili nchini humo, kufuatia ongezeko lake la kasi ambalo limeibua wasiwasi miongoni mwa mamlaka za serikali.

Mamlaka zimeyakosoa makanisa hayo kwa kuyataja kuwa yamepoteza mwelekeo wake wa msingi, yakidaiwa kugeuka kuwa “mapango ya wezi” badala ya kutoa huduma za kiroho na kijamii zinazotarajiwa kwa waumini na jamii kwa ujumla.

View attachment 3518973

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amekuwa mstari wa mbele katika kuyakosoa makanisa ya kiinjili yanayoibuka kwa wingi katika nchi hiyo iliyopo ukanda wa Maziwa Makuu. Hatua hiyo ya serikali inakuja wakati kukiwa na malalamiko kuhusu utaratibu wa uendeshaji na malengo ya baadhi ya taasisi hizo za kidini.

Licha ya uamuzi huo, sensa ya Rwanda ya mwaka 2024 inaonesha kuwa idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo ni Wakristo. Hali hii imesababisha changamoto kwa waumini wengi, wanaoelezwa kulazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama zaidi ili kutafuta maeneo mbadala ya kufanyia ibada.

Uamuzi wa kufunga makanisa hayo unaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali kuimarisha udhibiti na usimamizi wa karibu. Baadhi ya makanisa yanadaiwa kukiuka Sheria ya mwaka 2018, inayotaka kila taasisi ya kidini kuwasilisha mipango ya utekelezaji ya kila mwaka, ikieleza kwa kina jinsi shughuli zake zinavyoendana na maadili ya kitaifa.

Naomba na hili tanzania lifike maana yapo mengi mno
 
Kibongo Bongo, kanisa likionekana linakemea maovu ya serikali ndio inafungiwa, ila ukisifia maovu mnapewa sapoti mana mnakuwa mmebeba idadi kuwa ya wajinga kama ilivyo kwa mwamposa.
 
Rwanda imefunga zaidi ya Makanisa 10,000 ya Kiinjilisti kwa kushindwa kufuata Sheria ya mwaka 2018 iliyoundwa kudhibiti maeneo ya ibada.

Rwanda ilianzisha Sheria mpya kuhusu afya, usalama, na ufichuzi wa kifedha na inawataka Wahubiri wote kuwa na mafunzo ya Kitheolojia.

Rais Paul Kagame amekuwa akikosoa Makanisa ya Kiinjilisti ambayo yamechipuka katika nchi hiyo ndogo katika eneo la Maziwa Makuu barani Afrika.

Idadi kubwa ya Wanyarwanda ni Wakristo, kulingana na sensa ya 2024.

Sheria ya 2018, inayataka Makanisa kuwasilisha mipango ya utekelezaji ya kila mwaka inayoeleza jinsi yanavyopatana na Maadili ya kitaifa.

Michango yote lazima ipitishwe kupitia akaunti zilizosajiliwa.

#KitengeUpdates
 
Attachments

  • FB_IMG_1766396744706.jpg
    FB_IMG_1766396744706.jpg
    151.8 KB · Views: 10
Rwanda itapiga sana hatua katika haya maamuzi

Hizi dini kuna muda huwa zinafanya watu wawe kama misukule, makanisa yanayotakiwa kubaki ni Roma, Luthera, Sabato na Moravian, hayo mengine ya kina kiboko ya wachawi na keki za upako ni vurugu mechi miradi ya familia, yamewaruga watu wengi kisaikolojia
 
Paul kagame ni Mkatoliki (Mkristo).
Sasa ndiyo sijajua udini unaingiaje hapo.
Mleta mada anazingua sana.
Kama Kagame ni mkatoliki (mkristo) na ukristo ndiyo dini iweje awe mdini kwa kufungua makanisha ya kiinjili ambayo nayo ni ya kikristo?

Katoliki &makanisa ya kiinjili = makanisa ya kikristo.
Kagame (mkristo) 🤔🤔🤔.
 
Yupo sahihi
Serikali ya Rwanda imechukua hatua ya kufunga maelfu ya makanisa ya kiinjili nchini humo, kufuatia ongezeko lake la kasi ambalo limeibua wasiwasi miongoni mwa mamlaka za serikali.

Mamlaka zimeyakosoa makanisa hayo kwa kuyataja kuwa yamepoteza mwelekeo wake wa msingi, yakidaiwa kugeuka kuwa “mapango ya wezi” badala ya kutoa huduma za kiroho na kijamii zinazotarajiwa kwa waumini na jamii kwa ujumla.

View attachment 3518973

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amekuwa mstari wa mbele katika kuyakosoa makanisa ya kiinjili yanayoibuka kwa wingi katika nchi hiyo iliyopo ukanda wa Maziwa Makuu. Hatua hiyo ya serikali inakuja wakati kukiwa na malalamiko kuhusu utaratibu wa uendeshaji na malengo ya baadhi ya taasisi hizo za kidini.

Licha ya uamuzi huo, sensa ya Rwanda ya mwaka 2024 inaonesha kuwa idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo ni Wakristo. Hali hii imesababisha changamoto kwa waumini wengi, wanaoelezwa kulazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama zaidi ili kutafuta maeneo mbadala ya kufanyia ibada.

Uamuzi wa kufunga makanisa hayo unaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali kuimarisha udhibiti na usimamizi wa karibu. Baadhi ya makanisa yanadaiwa kukiuka Sheria ya mwaka 2018, inayotaka kila taasisi ya kidini kuwasilisha mipango ya utekelezaji ya kila mwaka, ikieleza kwa kina jinsi shughuli zake zinavyoendana na maadili ya kitaifa.

Rwanda itapiga sana hatua katika haya maamuzi

Hizi dini kuna muda huwa zinafanya watu wawe kama misukule, makanisa yanayotakiwa kubaki ni Roma, Luthera, Sabato na Moravian, hayo mengine ya kina kiboko ya wachawi na keki za upako yamewaruga watu wengi kisaikolojia
maoni ya kijuha juu ya ukristo, ukristo haujengwi na madhehebu hayo ya kale, Mungu alishayaacha yajiendee kwa taratibu zao za kujiundia. Umewahi kusikia babeli mkuu mama wa makahaba? Elewa mwenendo na muelekeo wa ukristo duniani na changamoto uliopitia
 
Rwanda itapiga sana hatua katika haya maamuzi

Hizi dini kuna muda huwa zinafanya watu wawe kama misukule, makanisa yanayotakiwa kubaki ni Roma, Luthera, Sabato na Moravian, hayo mengine ya kina kiboko ya wachawi na keki za upako yamewaruga watu wengi kisaikolojia
Hakika mkuu Naunga mkono hoja.
 
hata miskiti hataki ijengwe sana
Hana shida na misikiti kwa kuwa ipo michache ya kuhudumia watu wengi.
Ka nchi kaliko lingana na mkoa mmoja wa tanzania kana makanisa zaidi ya 6000 ni aibu!!!
Kenya nao wamesha anza, Ruto anataka wafanya miujiza waende huko mahospitali wakaponyeshe wagonjwa na sio kutapeli wakenya
 
Back
Top Bottom