Rwanda inatuwashia double indicator & full Light, CCM ondokeni hatuwataki

Rwanda inatuwashia double indicator & full Light, CCM ondokeni hatuwataki

Nikuonyeshe kitu kama hicho ili iweje ? Sijui unaelewa kinachozungumzwa ? Cjui unaelewa tunapotoka na tulipo na tunapokwenda ? Ikiwa Rasi anakwenda kufungua daraja ya RoadCross huoni kama kuna tatizo hapo ,Ikiwa Raisi ananyamaza katika issue kubwakubwa ambazo alitakiwa azifuatilie ,azijue azitolee maelezo kwa anaowaongoza ,ila Ugonjwa umetolewa maelezo ,tunachokiona sasa ni kukashifiwa kwake ndicho mnachovuna miccm. Yaani hamjui wananchi wanahitaji kuenziwa na kuwazungumzia na kuwaonyesha maendeleo yaliopo ,hakuna kitu mnaweza kusifu kuwa kimemsaidia mwananchi ,Raisi anaenda kufungua barabara jambo lililokuwa lifanywe na Mkuu wa mkoa tu au meya ,yaani hata zile kazi za mtembea na mikasi sasa anazifanya Raisi.

HIyo Beach ilitakiwa itoe hela kama mbuga za wanyama zinavyotoa ,tatizo kuwa beach na mbuga na milima madini ya thamani ,hakumsaidii mwananchi kupata hata panadoli ya bure ,hela inakwenda wapi ? Mwananchi wa kawaida asie na kipato cha uhakika ilitakiwa apate huduma za mwanawe pale shule ,leo anachangishwa na serikali ya miccm ,haina hata aibu ,haya zimewatoka ,masikini anauza maandazi na mihogo ya kukaanga angalau apate hela ya kumnunulia uniform mwanawe ,serikali inaona masikini huyo anafaidi ,inatafuta njia za kumkamua ,mwananchi huyo atoe mchango kujenga maabara,atoe mchango kujenga kituo cha polisi ,atoe mchango kujenga choo cha shule,atoe mchango huu na ule ,kuibeba serikali au sio ,wewe jiulize mapato yote yatokanayo na kodi yanaenda wapi ,hela ya utalii inaenda wapi ,unajua kulala hoteli ya ngorongoro inatakiwa ulipe dola ngapi ? Faida inaenda wapi hata umuonyeshe mwananchi ?

Hela yote inapelekwa hazina au sio ,huko wajanja wachache wanatafuta njia za kuichota,nchi haina maendeleo ya uhakika ni kubahatisha tu !
 
Kigali sio Rwanda.Jiji la kigali linakula sehemu kubwa mno ya bajeti ya Serikali kuliko miji mingine ya Rwanda.Miji mingine iko hoi.Kila siku serikali inaongelea kupaka poda na hina jiji la kigali. Masterplan za miji mingine ya Rwanda ziko wapi?
Kigali inajifanya ndio Rwanda Washamba wengi hasa kutoka Tanzania wakitembelea Kigali wakirudi Utasikia Rwanda kuzuri hivi ajabu Tanzania bure kabisa! Niwaulize swali Kigali ndio Rwanda? Unaijua miji mingine ilivyo hovyo Rwanda?

Nakubaliana na wewe hata Kampala serikali ya Uganda imewekeza sana lakini miji kama Masaka hovyoooooo!
 
Mleta mada inaonesha huna ufaham na kinachoendelea nchini. Kupitia gazeti la mwananchi palioneshwa satelite city project ambayo itaafanywa na NHC Arusha.Bado kuna project kubwa inayotazamiwa kufanywa Tanga. Rwanda imeji centrolise pale kigali tofauli na Tz issue ziko extended. Hongera kwa kujua vya wenzako bila kujua vyakwako.

Hiyo ni miradi ya kifisadi wala sina hamu kuifahamu kwa kina ,ni mikakati ya kulifilisi Taifa . NHC unalijua hili au basi unaingia kwenye maji usiyoyajua kina chake ?
 
Anatuletea habari za kufikirika mwaka 2014!

Jivunie ulichonacho sasa hivi, usijivunie ndoto za mwenzako.

Amma kweli kuna misukule si mchezo.

Nilicho nacho kipi ,UFISADI ? au MAFISADI ? Tz haijawahi kukumbwa na vita ndani ya nchi vya kuwawa kwa maelfu ,kilichotokea Rwanda kinajulikana ,leo hii katika muda mfupi sana wamefanikiwa kuona wanakokwenda na matarajio ,Hapa Tz ni kiza huko tuendako matumaini yanakatishwa kila siku skendo jipya,wala hulijui mwisho wake,linafifia kiajabu ajabu ,walewale wanaotuhumiwa na kuondolewa wadhifa ndio wale wale wanaobandikwa vyeo na wengine kuthubutu hata kugombea Uraisi ,sijui wanataka kuja kulipiza kisasi ?(SMS)
 
Kigali sio Rwanda.Jiji la kigali linakula sehemu kubwa mno ya bajeti ya Serikali kuliko miji mingine ya Rwanda.Miji mingine iko hoi.Kila siku serikali inaongelea kupaka poda na hina jiji la kigali. Masterplan za miji mingine ya Rwanda ziko wapi?
Kigali inajifanya ndio Rwanda Washamba wengi hasa kutoka Tanzania wakitembelea Kigali wakirudi Utasikia Rwanda kuzuri hivi ajabu Tanzania bure kabisa! Niwaulize swali Kigali ndio Rwanda? Unaijua miji mingine ilivyo hovyo Rwanda?

Kigali ni wapi? haya Tanzania mji upi wa kujivunia? Maana hilo jiji la Dar ndio linaloongoza kwa kulipuka chemba za maji taka, au ndio maisha bora hayo kuonyesha kwamba watanzania wanashiba?
 
ahsante Mkuu kwa kumjuza huyo Mburula. Watu kama hawajatembea wanasumbua kweli
 
Kigali ni wapi? haya Tanzania mji upi wa kujivunia? Maana hilo jiji la Dar ndio linaloongoza kwa kulipuka chemba za maji taka, au ndio maisha bora hayo kuonyesha kwamba watanzania wanashiba?

mkuu, nadhani uliangalia kombe la dunia. Hata Rio de Janeiro huko Brazil pamoja na maendeleo waliyopiga vitu kama hivyo havikosekani. Wewe upo sehemu gani hapa Tanzania na umefanikiwa kutembelea miji mingapi japo kwenye nchi za Africa?
 
Nilicho nacho kipi ,UFISADI ? au MAFISADI ? Tz haijawahi kukumbwa na vita ndani ya nchi vya kuwawa kwa maelfu ,kilichotokea Rwanda kinajulikana ,leo hii katika muda mfupi sana wamefanikiwa kuona wanakokwenda na matarajio ,Hapa Tz ni kiza huko tuendako matumaini yanakatishwa kila siku skendo jipya,wala hulijui mwisho wake,linafifia kiajabu ajabu ,walewale wanaotuhumiwa na kuondolewa wadhifa ndio wale wale wanaobandikwa vyeo na wengine kuthubutu hata kugombea Uraisi ,sijui wanataka kuja kulipiza kisasi ?(SMS)

Rais wako Kagame ambaye anaua watu kila kukicha ataondoka lini madarakani? Nadhani ulipaswa kumshauri kwanza yeye badala ya kuilaumu ccm. Kumbuka ccm haijiweki madarakani bali inachaguliwa kihalali na wananchi
 
Hiyo ni miradi ya kifisadi wala sina hamu kuifahamu kwa kina ,ni mikakati ya kulifilisi Taifa . NHC unalijua hili au basi unaingia kwenye maji usiyoyajua kina chake ?

ndugu yangu, ona ulivyo mweupe hata kwenye shirika la NHC. Sijui kuna kitu unakifahamu hapa Tanzania? Nadhani uwezo wako ni wa kupika majungu tu na kujipendekeza kwa wanya Rwanda
 
Anatuletea habari za kufikirika mwaka 2014!

Jivunie ulichonacho sasa hivi, usijivunie ndoto za mwenzako.

Amma kweli kuna misukule si mchezo.
Tujivunie umaskini kama huu? Kweli???? We ndiye msukule namba moja
untitled+of+tz.jpg

Copy-2-of-Mr.-Simango-holding-baobab-shell-600x402.jpg
 
Ulibahatika kuona the new dar es salaam vision ya kigamboni???
 
Nakubaliana na wewe hata Kampala serikali ya Uganda imewekeza sana lakini miji kama Masaka hovyoooooo!

!... Mbona Tanzania Dar Hapatamaniki Na Hakuna Hata Mji Ulio Mzuri? Achana Na Kigali Wewe, Lile Jiji Litakuwa Dubai Ya Afrika
 
Hata nyinyi mmeshaanza,ila umesahau mlianza lini ,mikakati isiyotekelezeka ,na tumeshayasikia mengi sana ya kutoka kwenye vinywa vyenu vinavyonuka maneno ya ulaghai. Miccm na CCM yao ni jumba ya maneno ,nimeangalia hiyo Kigamboni ila haifikii hata siku moja MasterPlan ya Kigali ,ile masterplan ukiiangalia tu basi unatulia na kuona matumaini.

Tz tulitakiwa iwe tushavuka huko ,nchi zinaendesha uchumi kwa kutegemea Zoo ,hapa tuna mbuga lukuki kinachofanywa ni kuzitekeza kwa kuuza mazao yake na kuwaiwa wanyama ,eti na sisi tuna Kigamboni !

Kuna united African university. .. . Which was part of it na inafanya kazi now first enrollment
 
Hivi viongozi hawa wa kiCCM wanajua wanachokifanya au ni wao na kukumbatia ufisadi na kuikausha nchi kwa kujazana ikulu wakijaza matumbo yao ,hebu angalia hawa waKigali na matumaini yao ambayo utayapenda na kuwaonea wivu pengine ikazidi kukufanya uichukie miccm na ccm yao. Miccm ni kujisifu tu tuna mbuga,tuna bahari,tuna maziwa,tuna gesi ,tuna mafuta kama haitoshi tuna Uranium ,yule waziri aliesema Uranium itakuwa tayari 2011 yupo wapi leo tunaelekea 2015 ,Warwanda hao wanaitangazia dunia kule wanakoelekea, Miccm mnatuchelewesha ,ondokeni tushawachoka.

Rwanda kaiba rasilimali za kongo, Rwanda kaua wapinzani wake kwa risasi. Unashauri na Tanzania yafanyike hayo?
 
Last edited by a moderator:
.... Siku Zote Huwa Nasema, Kagame Ni Rais Mchapakazi, Siyo Kama Wa Kwetu, Anaumwa Kichwa Tu Huyooo Marekani
 
... Tanzania Ni Shyamba La Bibi, Watu Wanachuma Hela Tu
 
Nioneshe kitu kama hii Rwanda:

Hii ni neema ya mungu,, Ni wapi hapo tumetumia akili zetu,, hiyo ni fukwe ambayo tumepewa na mungu Sasa sijui unataka kusema nini!!!
Ujue dada toka tumepata uhuru, maendeleo yetu hayalingani na muda ambao CCM imekaa madarakani,,, toka 1961 bado tunajenga barabara, shule, maabara, nk... Yaani namaanisha toka 1961 mpaka leo bado miundombinu mibovu,elimu duni, huduma za afya shida,,,
kimsingi hata barabara zinazojengwa ni 10yrs life span,,,, tunapolalamika nikwamba tunauchungu na wachache wanaoitafuna hii nchi kwa manufaa yao na familia zao...
dada umeshawahi kupita kwenye hizi barabara zinazojengwa na wachina ukajionea Mwenyewe maisha ya hizi barabara???
 
Rais wako Kagame ambaye anaua watu kila kukicha ataondoka lini madarakani? Nadhani ulipaswa kumshauri kwanza yeye badala ya kuilaumu ccm. Kumbuka ccm haijiweki madarakani bali inachaguliwa kihalali na wananchi
Ni bora uuliwe kuliko kuteswa Serikali yako ya ccm na miccm inawatesa WaTanzania ,huduma za maji umeme kwa Tz nzima ni 0% ,hivi ni mji gani hapa Tz una taa za barabani zinazowaka usiku ? WALLAHI unapoingia kwa ndege jijini Dar usiku utafikiri unatua kwenye kambi ya kijeshi ,mji ni kiza tu zaidi ya taa za magari ,eti ndio kituo kikuu na mji mkubwa wenye kila kitu, mi ukiniita Mnyaruanda nafarijika sana kuliko kuniita kibaka.

CCM inachaguliwa na wananchi ni kweli wale mapolisi waliokimbia na masanduku ya kura Pemba ilikuwaje ? Matokeoa ya kura za siri BMK kucheleweshwa kwa masiku inakuwaje hapo ,watu wakizungumza bora mnyamaze kwani hamuwezi kabisa kuitetea CCM na serikali yake ,itakuwa kama mnamtetea mwizi aliyehukumiwa kunyongwa. eti inachaguliwa kihalali na wananchi safari hii itachaguliwa kiusingizi !
 
sioni sababu ya kutoa povu jingi unless unaishobokea rwanda ovyo. hiyo ni plan tu. dar ipo plan ya kigamboni na isitoshe tuna miji mingi kuliko rwanda na sio kwamba miji haina masterplan
 
Back
Top Bottom