Ruzuku kwa mwezi: CCM milioni 800/-, Chadema 200/-, CUF 117/-

Nadhani inatakiwa iwe ugomvi kwa wananchi wote wa tanzania. Kwa nini serikali itoe hela kugharimia vyama vya siasa ambavyo ni vyama vya hiari. Je watu ambao hawana vyama serikali inawatreat vipi. Watanzania tupo millioni 43 wanachama wa vyama vya siasa hawazidi millioni kumi hii ina maana kuwa kuna karibia watu 33 milioni ambao hawapati hiyo advantage ya kuchangiwa na serikali kila mwezi kwenye mambo ya siasa.

Wanasheria tusaidieni katika hili naona kama sheria inaruhusu ruzuku ni ya kibaguzi sana.

Yani mkuu....embu chukua tano. Nadhani wati kibao wame-miss hii point yako. Inabidi ufungue thread specieal ya ku-address hii kitu. Yani katika kodi ya Mtanzania...Billion moja inaenda kwenye vyama vya siasi kwa mwezi?????
huu ni utani. Kujenga hospitali moja ni kiasi gani wakuu?
kusomesha madkatari pale muhimbili ni kiasi gani?
hii billion moja kwa mwezi ingewawezesha walimu wangapi tanzania?
alafu leo mnaambiwa ni nchi maskini mnaitikia kama makondoo....
AM TIRED OF THIS BULL***
Lazima tuamke...
Uwe CHADEMA, CCM, CUF, nk....sema no to RUZUKU!!
 
Gazeti la Nipashe la leo linatujulisha ya kuwa Msajili wa vyama vya siasa Bw. John tendwa ametangaza ruzuku kwa vyama vya siasa na mgawanyiko wake ni kama ifuatavyo...................................

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi..................

Chadema.......................Tshs 200 Million kwa mwezi........................

Cuf...................................Tshs 110 kwa mwezi..................

Jamani hizi pesa sasa zisiwe chanzo cha mifarakano ya ubinafsi na ufujaji wa mali ya umma......................

Niwajuavyo CHADEMA hapo mgawo tayari umeisha pangwa, Slaa Tshs 50m, Mbowe Tshs 50m, Lissu Tshs 30m , Zitto Tshs 20m , na zinazobakia ndizo za kuendesha chama. Kweli tutafika namna hii ??????
 
Tz = Tanganyika + Zanzibar. Hivi CDM ina Wabunge wangapi Zbar? au ni chama cha Wadanganyika tu? Kweli Tz hakuna chama cha upinzani.

Tukumbushane ni chama kipi kina wabunge Tanganyika?
 
Niwajuavyo CHADEMA hapo mgawo tayari umeisha pangwa, Slaa Tshs 50m, Mbowe Tshs 50m, Lissu Tshs 30m , Zitto Tshs 20m , na zinazobakia ndizo za kuendesha chama. Kweli tutafika namna hii ??????

EL,RA & Co. wana ngapi kwenye hizo 800..?
 
Wadau hapa JF,

habari zenu na poleni kwa shughuli za kulijenga taifa letu. Ndugu wana JF kama mjuavyo hivi karibuni mjadala wa suala la ruzuku kwa vyama vya siasa limepamba moto,hasa vya upinzani,hususani CHADEMA, kuna tuhuma zinazotengenezwa na wapinzani wa vyama husika kujaribu kuaminisha umma kuwa matumizi ya ruzuku itolewayo na serikali kwa vyama sio mazuri,na baadhi ya viongozi kutuhumiwa kujikopesha fedha hizo badala ya kujenga chama.

Nimeona nianze na chama tawala, ccm,na nikipata majibu stahiki nitaendelea na chama kingine. Maswali yangu ni kama ifuatavyo: je CCM wanapata Ruzuku kiasi gani toka serikalini kila mwezi? Je matumizi ya fedha hizo ni yapi?

Je nani anakagua mahesabu ya Ruzuku ya chama hicho? Je ndani ya CCM kuna mfumo wa kukopeshana? Kama tunavyosikia kwenye vyama vingine? Karibuni wadau,unaweka kutuwekea hata document,ambazo zitatufanya wadau tuelewe kwa mapana zaidi.

Nawasilisha.
 
Subiri sasa hivi uzi huu utafutwa?

"Wakati ni swali gumu sana na linaitaji majibu magumu"
 
Hao Magamba hata uwanyonge hawawezi wakatoa hesabu zao hapa ya ruzuku. we waulize vitegauchumi vyote walivyopora baada ya kuanzishwa vyama vingi zinafanya nn. maana hawa wana Viwanja na majengo makubwa kila wilaya na kila mkoa. Muje hapa Ritz na timu yako mkisaidiwa data na Mwigulu maake anazijua zote hizo Mali ingawa alishindwa kuzitumia kukijenga kiuchumi na kubaki kuwa omba omba kwa matajiri na wafanya biashara wakubwa wakwepa kodi humu nchini.
 
Subiri sasa hivi uzi huu utafutwa?

"Wakati ni swali gumu sana na linaitaji majibu magumu"
mkuu,hakuna haja ya kuufuta huu uzi,na ningewaomba mods wasiuondoe huu uzi mpaka tupate majawabu,maana hela zinazotumika ni za walipakodi wa nchi hii. Uwazi na ukweli.
 
Hata Tendwa kwa nafasi yake atagwaya kuhoji matumizi ya ruzuku ndani ya CCM. Lakini kwa uhakika usio na shaka, mojawapo ya matumizi ya hovyo ni kuwalipa vibaraka wake kudhoofisha upinzani. Aibu kubwa sana!!
 
ccm wanapata TZS 1.4 BILION PER MONTH.mbali na mapato ya mikataba ya majengo ya kupangisha kama ccm DAR,ARUSHA,MWANZA na viwanja vikubwa kama Kirumba,arusha,tabora,mbeya na ofsi za kulaza magari kila kona ya dsm.Lakini kwenye uchaguzi wa ndani wa mwaka 2012 walichangisha watumishi kwa nguvu kwenye Halmashauri, WAKURUGENZI WALILAZIMISHWA KUTOA ZAIDI YA 200,000, WAKUU WA IDARA ZAIDI YA 100,000 NA WATUMISHI WENGINE KIASI CHOCHOTE.MIMI NI MWATHIRIKA WA MICHANGO HIYO.CCM KAMA INASHINDWA KUSIMAMIA MALI ZAKE JE ZA SERIKALI ITAWEZAJE?, KUMBUKENI MASHIRIKA KAMA SUKITA WALIUA WENYEWE CCM KWA UFISADI HIVYO CCM NA UFISADI NI SAWA MGONJWA NA UJI
 
Swali gumu sana hilo kwa hawa akina Ritz,Bethlem,zeMarcopolo na wengineo!

Hata Nape hili swali haliwezi!!Lkn topic ingekuwa CHADEMA watolee ufafanuzi kwa nn walimruhusu Dr Slaa achukue shiling 10,000 kumlipa yaya hapo wangekuja sasa hivi kuomba maelezo!

(Sijakosea TARAKIMU nimeandika kwa uhakiki;AKICHUKUA Dr Slaa ELFU 10 KUMLIPA YAYA AKINA Ritz1 WANGESHINDA HAPA KUOMBA MWONGOZO;LKN HAMNA HATA MMOJA ATUAMBIE WHY CCM IWE MASKINI HADI WANALAZIMISHA MICHANGO KWA WATUMISHI WA SERIKALI ILI HALI KWA MWAKA CHAMA HIKI KINACHOTA SI CHINI YA BILLION 17 KAMA RUZUKU UKIACHILIA MBALI VITEGA UCHUMI VYAO LUKUKI)!
 
ccm wanapata TZS 1.4 BILION PER MONTH.mbali na mapato ya mikataba ya majengo ya kupangisha kama ccm DAR,ARUSHA,MWANZA na viwanja vikubwa kama Kirumba,arusha,tabora,mbeya na ofsi za kulaza magari kila kona ya dsm.Lakini kwenye uchaguzi wa ndani wa mwaka 2012 walichangisha watumishi kwa nguvu kwenye Halmashauri, WAKURUGENZI WALILAZIMISHWA KUTOA ZAIDI YA 200,000, WAKUU WA IDARA ZAIDI YA 100,000 NA WATUMISHI WENGINE KIASI CHOCHOTE.MIMI NI MWATHIRIKA WA MICHANGO HIYO.CCM KAMA INASHINDWA KUSIMAMIA MALI ZAKE JE ZA SERIKALI ITAWEZAJE?, KUMBUKENI MASHIRIKA KAMA SUKITA WALIUA WENYEWE CCM KWA UFISADI HIVYO CCM NA UFISADI NI SAWA MGONJWA NA UJI
mkuu mliandikiwa barua? Au ilikuwaje? Mpaka mkalazimishwa?
 
duu,mkuu ina maana watumishi wao hulipwa nin? Na je wao hawakopeshani???

kati ya watumishi wa nchi wanalipwa ovyo ni wa ccm,ndiyo maana makatibu wa ccm wilaya na mikoa ununuliwa na wagombea wakati wa uchaguzi wa wabunge na wa ndani. Ndio wakati watumishi wa ccm kununua viwanja na kujenga nyumba baada ya hapo ni njaa tu nafuu hata watumishi wa serikali.watumishi wa ccm ni sawa na askari wa kampuni binfsi za ulinzi.
 
mkuu mliandikiwa barua? Au ilikuwaje? Mpaka mkalazimishwa?
ujui kuwa Wakurugenzi ukaribishwa kwenye vikao vya Kamati za siasa za Wilaya za CCM?.Je wakimwambia kuwa tunataka kitu fulani kifanyike inakuwaje?.Hasa kwa wakurugenzi wepesi wanaburuzwa kwenye kikao kama hicho. Pia jiulize kwa nini CAG-Werema anahudhuria vikao vyote vya ccm ngazi ya Taifa?
 
ina maana CAG anahudhuria kama nani? Mjumbe au mualikwa? Na kama mualikwa je anaweza alikwa na vyama vingine vya siasa?
 
kaka hizi na zingine ni siri za nchi. cha msingi uwe mvumilivu wakati chama kinaendelea na mchakato wa kukutafutia maisha bora wewe, familia yako na taifa kwa ujumla.

Maisha bora ni pamoja na hii gesi ya Mtwara -- ifikapo june 2014 tutakuwa tumekata mzizi wa fitna kati ya serikali ya chama cha mapinduzi na wananchi wake kuhusu tatizo sugu la umeme pia tutawauzia na majirani zetu

Kuweni waangalifu na viongozi wanaopandikiza chuki - mtwara oyeeee!!!!!! gesi oyeeeee!!!!!

asanteni kwa kunisikiliza -- kidumu chama cha mapinduzi!!!!!!
 
Back
Top Bottom