Ruzuku kwa mwezi: CCM milioni 800/-, Chadema 200/-, CUF 117/-

1:Kugharimia shughuli zote za green guard!
2: Kugharimia taratibu zote za utengenezaji wa video feki na ung'oaji watu kucha na meno.
3:
4:
 
wewe weka data ulizopata kutoka kwenye hayo matawi.
na sisi tutaweka matumizi katika kila mkutano mmoja wa m4c na kila kiongozi anapokea kiasi gani charuzuku kwa kila mkutano.
tutatoa matumizi mlio yafanya igunga na baadhi ya chaguzi ndogo za madiwani pamoja na mabilioni yalioharibika karatu.
 
tunaomba chanzo cha mapato ya chadema.

zile billion 50 kcb bank tawi la mwanza zilizo kimbiwa na mwenyewe zilikuwa za nani?

bado tupo macho mtawapata wale ambao ni wavivu kufikiri.
 
Unlike other parties, CCM ina ofisi kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kila kijiji. Ofisi zote hizi zina makatibu wa chama na wa jumuiya. Shughuli za ofisi hizi zinaendeshwa na ruzuku pamoja na michango ya wanachama.

Pesa za viwanja vya mpira, pesa za maegesho ya magari kwenye ofisi za ccm nani anakula nani?
 
Hahahahahaaaa!!
Budget ya CCM ni kubwa kuliko budget ya nchi. Lakini wanachofanya ni kuua tembo wetu tu.

Mkuu usitegemee jibu kwa hao onyenye hapo juu.
Ni shida na njaa tu zinawasumbua hao

1.Mbona pamoja na milioni 800 hizo za Ccm lakini bado makatibu wa CCM bado wanapita kuombaomba dizeli ya magari kwa wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara huku wilayani, yaani diseli iliyotolewa kwa ajili ya kusafirisha dawa za wagonjwa vijijini na kuhudumia miradi ya vijijini leo makatibu wa CCM wanadokoa tena kwa shinikizo na vitisho vingi,
Hii je ni sawa,??????

2. kwani milioni hizo 800 za ruzuku haziji huku vijijini kwa makatibu waccm wilaya????.
3. Naomba maccm mnijibu hii fedha take maendeleo kuporwa na makatibu wenu siyo wizi jamani???????
4.je haya ni maagizo kutoka makao makuu ya chama????
5.je mbona Chadema hawapiti kuombaomba hiyo Dizeli?????
6.Je nini kimejifichakatika hili,?????? matumizi haya ni sahihi?????! na katika bajeti za wakuu wa idara kuna kifungu cha mafuta ya vyama vyamavya siasa????,
 
Pesa za viwanja vya mpira, pesa za maegesho ya magari kwenye ofisi za ccm nani anakula nani?
Sio kila tawi lina kiwanja au maegesho.
Kwenye viwanja na vitega uchumi hutumia vitega uchumi hivyo kwa shughuli za chama kadri mahitaji yalivyo.
 
Tofauti na tunavyoona hali ya mambo ndani ya CHADEMA ambacho kipo busy na shughuli za kisiasa nchini kwa kutumia vijipesa kidogo vya ruzuku na michango ya wananchi; chama cha mapinduzi chenye matrioni ya ruzuku kila mwaka hakijulikani kinazitumiaje hizo fedha.

Wadadisi wa mambo wanahoji, kama CHADEMA pamoja na uchanga wake, na karuzuku kadogo inakopata inaweza kufanya mambo mengi na makubwa kiasi hiki yanayoashiria ushiriki wa kweli katika shughuli za siasa, CCM yenye matrioni ya fedha si ilipaswa kufanya zaidi ya hapo?

CCM inatumia ofisi zilizojengwa na watanzania wote nchi nzima, hakilipi kodi ya pango la ofisi; CCM inakusanywa hela kutoka kwenye miradi iliyochangiwa na watanzania wote wakati wa chama kimoja: kama vile viwanja vya mipira, majengo ya kukodisha, pamoja na viwanda, na hivi sasa inajineemesha kutokana na kipato kitokanacho na miradi hiyo.

Kwa haraka haraka kama ukifanya tathimini ya kile ambacho CCM inauwezo wa kukusanya kwa mwaka na matumizi yake, matrioni ya fedha yanabaki mfukoni. Lakini chama hiki hakijishughulishi na jambo lolote linalohusu affairs za watu.

Hakijishughulishi kwenda kusikiliza kero za wananchi na kutoa maelezo juu ya masuala ambayo kiliahidi kutekeleza mwaka 2010 na hakikutekeleza. Hakijishughulishi na ukusanyaji wa maoni ya katiba (taarifa za ndani zinaonyesha kwamba kuna kikosi kazi kinatengeneza hayo maoni, badala ya kuyakusanywa kwa wananchi kama inavyofanya CHADEMA), na zaidi ya yote, chama hiki hakionyeshi kuguswa na matatizo yanayowakabili wananchi hata japo kwa kujaribu kuwa nao na kushirikiana nao kuyatatua.

Mimi najiuliza hapa, hizi ruzuku kubwa ambayo chama hiki kinaipata, inatumika wapi, na inatumikaje? Na pesa zile zinazokusanywa kwenye miradi mbalimbali ambayo ilijengwa na watanzania wote inatumika wapi?

Tunataka majibu yanayojitosheleza siyo longolongo. Kuna taarifa za ndani zinazoonyesha kwamba ruzuku ya chama chenu inawaneemesha baadhi ya vigogo ndani ya chama. Kama mtaleta hadidhi za sungura na paka mimi nitamwaga mboga hapa. Tayari nina data za matawi yenu ambayo yameripoti kutokupata hela yoyote kutoka makao makuu huku kila tawi likipangiwa kiasi cha fedha cha kuchangia makao makuu. Mtueleze ni kwanini huko makao makuu kunahitaji kuongezewa hela tu ilihali hakuna cha maana kinachoendelea katika harakati za kisiasa?

cc. HAMY-D, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Ritz, ZeMarcopolo, babayako utaifakwanza, FaizaFoxy, etc.
hayo mengi na makubwa ni yapi???????
 
Last edited by a moderator:
Unlike other parties, CCM ina ofisi kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kila kijiji. Ofisi zote hizi zina makatibu wa chama na wa jumuiya. Shughuli za ofisi hizi zinaendeshwa na ruzuku pamoja na michango ya wanachama.

Mwongo mkubwa wewe. Nina ndugu zangu kadhaa ambao ni viongozi wa ccm, wanalalamika hawapewi mgao wowote ndo maana wanawakamua wafanyabiashara.
 
Zinatumika kuhakikisha CCM inabaki kuwa namba wani.

Hivi chadema ina wabunge wangapi vile?
 
Vyama vya siasa ni wanyonyaji tu,karibia bilioni moja zinachezewa na vyama vya siasa wakati watoto wetu wanakaa chini mashuleni#au siasa ni ajira#wagonjwa wanalala chini mahospitali,alafu wanasimama majukwaani kuleta Chuki na Uhasama,sioni mrejesho chanya wa siasa kwa wananchi
#Ex Tanzania Simper aliquid novi#
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom