Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Wakuu,
Naomba kuwasilisha kero inayowakabili wananchi wanaotumia usafiri wa daladala kutoka Mbezi kupitia Goba - Kawe na zile zinazoelekea Makumbusho.
Nyakati za asubuhi, kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa daladala. Magari yaliyopo kwenye ruti hii yanaonekana kuzidiwa uwezo, kiasi kwamba abiria hutumia muda mrefu vituoni wakisubiri usafiri. Daladala nyingi zinapita zikiwa zimejaa, na hali hii husababisha watu kuchelewa kufika kazini au kwenye shughuli nyingine za uzalishaji.
Katika jitihada za kusaidia kupunguza msongamano huu wa abiria, zipo daladala kutoka ruti tofauti ambazo hujitokeza kusaidia asubuhi kwenye maeneo haya. Hii hufanyika kwa nia njema ya kusaidia wananchi wapate usafiri wa haraka bila kuathiri daladala zilizo kwenye ruti husika – kwa sababu abiria ni wengi kila kituo.
Hata hivyo, kumekuwa na changamoto nyingine ambapo askari wa usalama barabarani (Traffic) wanaonekana kuzizuia daladala hizo za mikoa mingine kwa kuzikamata na kutoza faini. Hii huathiri jitihada za kusaidia abiria, wakiwemo wanafunzi ambao wakati mwingine hutumia zaidi ya masaa mawili wakisubiri usafiri.
Rai yangu kwa Jeshi la Polisi – Kitengo cha Usalama Barabarani (Traffic), tafadhali kaeni mkao wa kusaidia badala ya kuziba njia. Naomba mzingatie kuwa nyakati za asubuhi ni muhimu sana kwa wananchi kuwahi shughuli za kujenga taifa, na kwa wanafunzi kuwahi shule. Badala ya kuzuia msaada huu wa muda, tafadhali tafuteni njia bora ya kuratibu ili kuweka mfumo rasmi utakaoleta unafuu kwa wananchi bila kuathiri utaratibu wa usafirishaji.
Sambamba na hilo natoa rai kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kufanya tathmini ya kina ya hali ya usafiri hasa nyakati za asubuhi kwenye maeneo haya yenye msongamano mkubwa wa abiria asubuhi. LATRA inaweza kuruhusu magari ya ruti nyingine kusaidia katika muda husika kwa utaratibu maalum wa muda. Hii itasaidia kupunguza adha kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa huduma ya usafiri wa umma.
Ahsanteni kwa kuzingatia.