Rusumo Falls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rusumo Falls

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Mar 18, 2011.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  As Kidatu and Mtera dams falls short of water, why not try this source? Nimepita hapa majuzi nikastaajabu mwenyewe, nimechukua hii video ili niwashirikishe watanganyika wenzangu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Thanks! My question however is that why do we have ONLY to depend on water falls for umeme? Are there no other alternative as songas? What about umeme wa jua? Nuclear? etc. Sikuzote tutaendelea kulalama tu mvua hakuna kwahiyo kutakuwa na mgao, mgao, mgao ....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Good thing with this source is that it never get dry!
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  lakini kipo mpakani, hivyo kuhatarisha usalama wa nchi
   
 5. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nadhani biggest challenge watanzania na waafrika tuliyonayo ni inadequate or rather lack of imagination/innovation and long term planning.

  Unajua hayo maporomoko ya Rusumo kwa watu ambao tungekuwa na vision yangeweza kussuply umeme Kagera/Kigoma/Shinyanga etc..na mwingine tukauza Rwanda na Burundi. Alternatively tungetafuta strategic investor both Rwanda and Tanzania tukapata umeme. Sasa hebu jiulize mwananchi wa Ngara asubiri umeme wa Kidatu! Wapi na wapi? I am really sick with my country. Hatuna vision kabisa. Viongozi are thinking of next election and how to steal from their people. Tungekuwa na mipango endelevu vizazi vijavyo vingeifanya Tanzania kuwa Geneva. Yet they can only do so, kama tumewawekea misingi. And we cannot move foward bila kuwa na vyanzo vya umeme vya uhakika. Hata muuza ice cream anahitaji umeme wa uhakika!

  Sasa imagine miaka hamsini baada ya uhuru, Raisi wetu bado anakwenda Marekani (kwa kutumia kodi zetu) kuomba vyandarua vya kujikinga na Malaria! And you say we are serious na maendeleo?

  Bwana utuhurumie *3
   
 6. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,128
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  yapo wap nikamshauri zitto na nssf waende huko wakaanzishe cha kwao na kutuachia mgodi wetu wa kiwira
   
 7. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  halafu decision makers watapataje rushwa ya capacity charge?
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yapo mpakani kabisa mwa Rwanda na Tanganyika katika mkoa wa Kagera njia ya Benako (Ngara)
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huu mradi uliwahi kuwa katika mipango ya kuendeleza umeme katika kile kilichoitwa Kagera Basin Development Authority; miaka ya 1980 kuelekea 1990, mipango hiyo iliingiliwa na siasa za matumizi ya maji ya Mto Nile hivyo kukosa ufadhili kisha baadae vita ya Burundi na Rwanda miaka ya Mwanzoni mwa 1990.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu si vibaya kuhusu other alternative sources, lakini kwanza we rather exhaust zile zote zilizopo na the cheapest ones,na umeme wa maji ni rahisi zaidi, kama una vyanzo vya kutosha why not use them all.

  Halafu unakuta sources kama hizi za water falls zimetapakaa in zones zote za nchi.
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Hapo ni kwenye border ya Tanzania na Rwanda. Good news!!! Huo ni mpango tosha wa kuondokana na umeme wa mgao, maana tutakuwa na umeme wa kutosha na majirani zetu.

  Unajua nchi jirani ni za East African Community, so we can share this source!!!!!!!!!!
   
 12. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  ile falls ingewasaidia wakazi wa Rusumo,benaco,k9,kabanga na Rulenge.sema ccm wanaifanyia siasa.ngara giza tupu.
   
 13. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umeme wa kutumia maji ndo umeme wa gharama nafuu zaidi kuliko umeme wa aina zote. Ukishindwa kujenga na kusimamia umeme wa kutumia nguvu ya maji basi ujue hakuna aina ya umeme unayoiweza.

  Katika kuzalisha umeme kuna vitu muhimu wiwili. (i) Majenereta yanayozalisha umeme (ii) Mashine zinazoyazungusha hayo majenereta ili yazlishe umeme.

  Katika mfumo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji, mashine za kuyazungusha majenereta ili yatoe umeme zinaitwa "water turbines". Hizi water turbines huendeshwa na msukumo wa maji yanashuka kutokea kwenye maporomoko. kuendesha water turbine huhitaji kufanya chochote mbali na kujenga mfumo wa kuyazuia maji na kuyafanya yaende kwa nguvu zaidi. Hili hufanyika kwa kujenga Mabwawa (Dams). Kwa hiyo gharama ya mfumo wa umeme wa maji iko kwenye ununuzi wa majereta na ujenzi wa dams na water turbines. Hivi vitu vikishawekwa gharama ya kuviendesha ni ndogo mno! Kwa hiyo pamoja na kuwa gharama za kuanzia ni kubwa (sababu ya ujenzi wa ma-Dams) katika kipindi cha muda mrefu umeme huu ni gharama nafuu sana.

  Kwenye umeme wa makaa ya mawe, unahitaji "steam turbines" ambazo zinaendeshwa na moto wa makaa ya mawe. Hivyo inabidi uwe na mgodi wa makaa ya mawe, uyachimbe halafu uyachome yatoe moto unaochemsha maji na kutoa mvuke. Mvuke huo utumike kuendesha "steam turbines" zinazoendesha majenereta yanayozaa umeme. Gharama hapa ipo kwenye kuchimba mkaa wa mawe, kujenga matanuru ya kuuchomea mkaa huo, kujenga turbines na kununua majenereta. Ili upate umeme kila siku itabidi uchome tani kadhaa za makaa ya mawe hivyo gharama ya uendeshaji ni kubwa. Unahitaji kuhudumia matanuru ya kuchoma makaa vile vile kuhudumia genereta za kuzalisha umeme.

  Kwenye umeme wa mafuta unahitaji kuwa na vitu viwili. Engine kubwa ya kuendesha majenerata. Engine hizi huhitaji kula mafuta au gesi ili kuzungusha genereta. Kwa hiyo kila siku ili upate umeme unahitaji kuchoma maelfu kadhaa ya lita za mafuta au cubic mita za gasi. Unahitaji kuhudumia Engine na kuhudumia genereta vile vile ambazo zote ni gharama kubwa.

  Umeme wa kutumia nyuklia hapa siuzungumzii kabisa kwani mbali ya kuwa uko mbali nasi, si upendi vile vile. Angalia yanayoendelea Japan utajua kuwa hii kitu haifai kabisa. Uwezo wa binadamu wa kudhibiti nyuklia bado ni mdogo hivyo hatari zake ni kubwa mno pamoja na teknolojia inayotumika kuwa ni ya wenye uwezo tu.

  Njia zingine kama Bahari (mawimbi), Upepo, jua, volkano (geothermal - Oldoinyo lengai inaingia hapa), n.k. bado uwezo wake wa kuzalisha umeme wa kiwango cha juu na wa uhakika ni mdogo. Hazitumiki sana duniani.

  Kwa hiyo, njia rahisi kabisa ya kuzalisha umeme ni maji. Katika njia zote hizo kuu unahitaji vitu viwili muhimu, jenerata na kitu cha kuizungusaha jenereta. Katika kuendesha miradi ya aina zote unahitaji kuhudumia vitu viwili jenereta na kitu cha kuizungusha jenereta. Sasa kwenye maji, kitu cha kuizungusha genereta ni maji yanayotembea. Huyanunui wala kuyagharimia, naam utalazimika kutunza bwawa hata hivyo. Kwenye makaa unalazimika kuchimba makaa au kuyanunua kama huna na kuyachoma, ikiwa ni pamoja na kuhudumia jenereta yenyewe. Kwenye mfumo wa mafuta na gesi unahitaji kuhudumia injini na jenereta na kununua mafuta na gesi.

  Ndo maana nchi nyingine zote zinaingia kwenye vyanzo vingine baada ya kumaliza potential zote zilizoko kwenye vyanzo vya maji! Marekani wana mbwawa zaidi ya 8,000. Nchi nyingi za Ulaya zina maelfu ya Mabwawa. Tanzania tuna Mtera, Kidata, Kihansi, Hale, Pangani, Nyumba ya Mungu tu; yaani mabwawa 6 tu. Kwa hiyo ni lazima tupate matatizo. Tukikimbilia kwenye vyanzo vingine umeme utakuwa wa gharama mno na watanzania hawatamudu. Hiyo ndo hali halisi.
   
 14. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kule Ifakara kuna kijiji kinaitwa Mbingu (njiani kuelekea Mahenge). Pale kuna masista wa kikatoliki wamenunua mtambo mdogo tu na kuuweka kwenye "viporomoko vya maji" na wanapata umeme wa kutosha hospitali, nyumba ya malezi, conference centre, sekondari, nyumba za majirani na sasa wametandaza nguzo kuelekea kitongoji cha Londo (kuna stesheni ya TAZARA). Huu umeme ni wa uhakika 24hrs, 240V sawa na wa Tanesco. Tatizo mafundi wa Tanesco wakiitwa kurekebisha mtambo ule wanaiba spea hadi imelazimu atafutwe injinia toka Ubelgiji. Miradi kama hii ingesaidia sana nchi hii. Mtumeni January huko akajionee mwenyewe.
   
 15. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Safi sana kiongozi umeitumia elimu yako vema kabisa kutuelewesha katika lugha rahisi na inayoeleweka.
   
 16. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umeme wa makaa ya mawe unalaumiwa sana kwa uchafuzi wa mazingira. Nyuklia ni hatari ikiwa ajali itatokea. Umeme wa mafuta nao huchafua mazingira kwa moshi mwingi wa mafuta kama ilivyo kwa makaa ya mawe. Gasi haichafui sana mazingira. Maji? Ni chanzo safi kabisa na ni sustainable kwani maji yatakuwepo for ever ikiwa hali ya mazingira haitabadirika.
   
 17. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nuclear Tanzania?????....... (who will takecare of the nuclear plant.CCM government or Tanesco..haha ) kwa uzembe,lack of seriousness na longolongo za Serikali na watendaji wake i dont suggest kabisa the use of Nuclear power maana tutatukua tunatengeneza bomu la kutulipua kutakufa nchi nzima na na watakao okoka watambiwa ni mapenzi ya Mungu...lol.......Transformer tu zimewashinda ku-manage kila siku zinalipuka iwe Nuclear Tanesco wataweza?...u must b kidding..
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hayo maporomoko ni hatari, walishajaribu wakashindwa.
   
 19. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani sometimes jaribuni kua serious basi hivi hapo pana hatari gani?...Niagara falls ni moja ya maporoko makubwa na strong duniani bt yanatumika kuzalisha umeme Canada...Rusumo falls na Niagara falls yapi ni strong?...and i believe hata Rifiji falls ni stronger than haya ya Rusumo....hapa suala ni watawala wapo kibiashara zaidi..Dowans,iptl,richmod et al....
   
 20. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hebu fafanua ni kwa vipi usalama wa nchi utakuwa hatarini maana sioni hatari yoyote mimi.
   
Loading...