Rusumo Falls

Thanks! My question however is that why do we have ONLY to depend on water falls for umeme? Are there no other alternative as songas? What about umeme wa jua? Neuclear? etc. Sikuzote tutaendelea kulalama tu mvua hakuna kwahiyo kutakuwa na mgao, mgao, mgao ....

Yametushinda mabomu ya Gomz, tutaweza kudhibiti miale ya atomic? Maji ya Rusumo hayakauki na ni chanzo 'cheap' kwa kuzalisha umeme.
 
Yametushinda mabomu ya Gomz, tutaweza kudhibiti miale ya atomic? Maji ya Rusumo hayakauki na ni chanzo 'cheap' kwa kuzalisha umeme.

Nimesoma hoja zote za wachangiaji. The ideas are excellent. Hoja yangu kubwa ni kwamba suala la umeme ni la ki-mkakati zaidi. Na hii ni pamoja na matatizo mengi tuliyo nayo hapa nchini. Viongozi wetu ni porojo tuuuu; hakuna mwenye uthubutu wa kuweka mkakati na kuusimamia.

Nakubali kuwa vyanzo vyote vya umeme wa maji vilivyotajwa vingetumiwa tungekuwa na unafuu mkubwa. Hata hivyo naamini hiyo ingekuwa kwa muda tu. Ni kama miaka 15 hivi, kwa umeme tuliokuwa nao tulikuwa na ndoto ya kuziuzia umeme karibu nchi zote tunazopakana nazo. Leo maendeleo ya viwanda yamefanya tuwe na upungufu mkubwa sana pamoja na kwamba tumekuwa na nyongeza ya umeme utokanao na kuzalishwa kwa gesi ya Songas. Hivi ni nani ajuaye kitakachotukia miaka mingine 20 hivi?
Ahadi za JK mwaka jana zilijaa pipi na biskuti, sikusikia hoja za kimkakati zinazosema hiki kitafanyika katika kipindi cha miaka 3, 5 na 10 ijayo. Waziri mhusika (wa umeme) aliporudishwa kwenye wizara yake akatoa ahadi ya peremende. Akasema, Mgao sasa basi bila hata kutuambia kwa mkakati gani. Kilichotokea wiki moja baadaye kila moja wetu anakijua.

Serikali makini lazima ionyeshe mkakati bila kujali itakuwepo madarakani kwa muda gani. Obama leo anaendeleza mambo yaliyoanzisha na mtangulizi wake kwa sababu yalianzishwa kwa maslahi ya Taifa la Marekani na si kwa chama. Tunachokiona leo hapa nchini ni kwamba kiongozi anatetea maslahi ya chama chake kuwa madarakani na hivyo maslahi ya taifa yanawekwa nje.

Hivi ni nini kinaifanya serikali yetu isitaifishe mitambo ya Dowans? Ikiwa tulinunua lile dege bovu la rais kwa gharama ya watanzania kula nyasi (ambazo tunazila sasa, ni nini kinazuia leo sisi kununua majenereta kama hayo kama mpango wa muda mfupi wakati tukishughulikia vyanzo vingine?

Nasema: Viongozi wetu, kwa makusudi kabisa na kwa maslahi wanayoyajua wao, wamekuwa wavivu wa kufikiri
 
Mkuu mimi nadhani biggest challenge watanzania na waafrika tuliyonayo ni inadequate or rather lack of imagination/innovation and long term planning.

Wahandisi wote wamelala. Wahandisi ndio mstari wa mbele kwenye uvumbuzi mara inapotokea shida.

Unajua hayo maporomoko ya Rusumo kwa watu ambao tungekuwa na vision yangeweza kussuply umeme Kagera/Kigoma/Shinyanga etc..na mwingine tukauza Rwanda na Burundi. Alternatively tungetafuta strategic investor both Rwanda and Tanzania tukapata umeme. Sasa hebu jiulize mwananchi wa Ngara asubiri umeme wa Kidatu! Wapi na wapi? I am really sick with my country. Hatuna vision kabisa. Viongozi are thinking of next election and how to steal from their people. Tungekuwa na mipango endelevu vizazi vijavyo vingeifanya Tanzania kuwa Geneva. Yet they can only do so, kama tumewawekea misingi. And we cannot move foward bila kuwa na vyanzo vya umeme vya uhakika. Hata muuza ice cream anahitaji umeme wa uhakika!

Tujaribu kuendesha nchi bila ya vyama vya kisiasa.......Tutapata maendeleo makubwa sana

Sasa imagine miaka hamsini baada ya uhuru, Raisi wetu bado anakwenda Marekani (kwa kutumia kodi zetu) kuomba vyandarua vya kujikinga na Malaria! And you say we are serious na maendeleo?

Bwana utuhurumie *3

Tuige wachina wanavyofanya...........kiongozi wa serikali akituhumiwa rushwa hukumu yake ni KITANZINI. NA iwe Hivyo ili kila mtu aweke maslahi ya Taifa mbele na kuondokana na UMIMI unaotafuna maendeleo, rasilimali na mali asilia ya Tanzania.
TUBADILISHE MFUMO WA UONGOZI WA NCHI KWA KIPINDI KINGINE CHA MPITO (MIAKA 50) KWA MANUFAA YA WAJUKUU WETU.

EEH BWANA UTUREHEMU
 
Kikwete acharuka, amtaka Ngeleja awe makini
RAIS Jakaya Kikwete amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa makini na utatuzi wa suala hilo ili kuiepusha nchi kuingia katika kashfa kama iliyosababishwa na Mkataba wa Richmond. Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameagiza kuwekwa pembeni kwa ushabiki wa kisiasa katika utekelezaji wa miradi ya uzalishaji umeme ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha zaidi ya megawati 1,130 za umeme ifikapo mwaka 2013.
Rais Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na maofisa wa Idara na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini katika ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa wizara hiyo jana. "Katika suala hili la uzalishaji wa umeme wa dharura, naomba tujifunze kutokana na historia. Nakumbuka suala la Richmond lilitokana na suala kama hili la uzalishaji wa umeme wa dharura. "Nililisema hili pale katika kikao cha Baraza la Mawaziri, shughuli hizi zote za uzalishaji wa umeme wa dharura zianzie na kuishia palepale Tanesco. Bodi ya Tanesco isimamie mchakato mzima bila kuingiliwa na wizara, naomba tusirudi tena kule," alisema Rais Kikwete.
Kabla, Waziri Ngeleja alisema Wizara yake inachukua mikakati mbalimbali ya muda mrefu, muda wa kati na mikakati ya dharura katika kukabiliana na matatizo ya umeme nchini. Kuhusu mikakati ya dharura inayochukuliwa sasa ni kuagizwa kwa majenereta ya kufua umeme yanayotumia mafuta mazito yenye uwezo wa kuzalisha megawati 260 ambapo jana ilikuwa mwisho wa kupokea nyaraka za zabuni kwa ajili ya uagizwaji wake. "Mheshimiwa Rais, ni imani yetu kwamba katika wiki ya pili au ya tatu ya Mwezi Aprili, mwaka huu, majenereta haya yatakuwa yamewasili na lengo letu ni kuona kuwa umeme unaanza kuzalishwa ifikapo mwezi wa saba," alisema Ngeleja.
Waziri alisema pamoja na mpango huo wa dharura ni matumaini ya Wizara hiyo kuona kuwa kunakuwa na uzalishaji wa megawati 1,130 za umeme zitakazoingizwa kwenye gridi ya taifa ifikapo mwaka 2013 kutokana na kukamilika na kuanza kazi kwa miradi mbalimbali ya uzalishaji wa umeme. Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ule wa Kiwira (Mbeya) utakaozalisha megawati 200, Mnazi Bay (Mtwara) megawati 300, Kinyerezi (Dar es Salaam) utakaozalisha megawati 240 na Mwanza megawati 60.
Waziri Ngeleja alitaja mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika miradi ya umeme inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) yenye miradi 41 sasa, miradi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), miradi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na miradi ya uzalishaji umeme kupitia majenereta na mitambo inayosimamiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco). Akizungumzia miradi hiyo, Rais Kikwete alisema itaweza kukamilika kama ilivyopangwa kama watendaji ndani ya wizara hiyo watapeleka nguvu na fikra zao katika utekelezaji wa miradi na si maneno yasiyokuwa na nia ya dhati na ya kisiasa.
"Lengo langu ni kuona tunaondokana kabisa na umeme wa maji.Tukiweza kupata umeme wa Mtwara na Kiwira tu utaweza kabisa kutufanya tuachane na umeme wa Mtera na Kidatu. Umeme wa maji uwe umeme wa ziada na si tegemeo kama ilivyo sasa. "Mradi wa Kiwira haukuweza kukamilika kutokana na siasa kuingia ndani yake, lakini sasa mradi umerejeshwa serikalini na kuna hatua zinaendelea kuchukuliwa ili mradi uanze uzalishaji upya, hili likitekelezwa tutakuwa mbali," alisema.
Rais pia alieleza kuridhishwa kwa kiwango kikubwa na mikakati inayochukuliwa na Taneso chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi William Mhando na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) chini ya Mkurugenzi Mkuu, Haruna Masebu katika kuongeza miradi ya uzalishaji wa umeme na usambazaji. Alisema ili kufikia lengo la Wizara ya Nishati na Madini la kuona umeme unawafikia asilimia 30 ya Watanzania nchi nzima kutoka asilimia 14 za sasa ifikapo mwaka 2015, jitihada za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa na vyombo husika hasa REA, Ewura na Tanesco ili kuhakikisha miradi yote iliyoainishwa inatekelezwa.
Kampuni ya Richmond ilipewa zabuni na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ili kuzalisha umeme wa dharura baada ya nchi kukumbwa na nakisi kubwa ya umeme mwaka 2006 kutokana na kukauka kwa maji katika Bwawa la Mtera, kazi ambayo kampuni hiyo ilishindwa kuifanya. Hatua hiyo ilisababisha Bunge kuunda Kamati Teule ili kuchunguza mazingira ya mkataba huo baina ya serikali na Richmond chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, iliyobaini kuwa kampuni hiyo ilikuwa hewa na haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kama ilivyodai kwa serikali.
Kutokana na kitendo hicho Kamati hiyo ilipendekeza kujiuzulu kwa viongozi wa serikali waliohusika na mkataba huo wa Richmond kwa kuiingiza nchi katika hasara, hatua iliyomfanya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, kujiuzulu Februari 2008 na kumlazimisha Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri.
 
MY TAKE:
1. Mkakati uliopo ni wa kuweka mbali ushabiki wa kisiasa ili zizalishwe megawati 1130 kufikia 2013. Kwa maana nyingine, hata kama watachakachua tenda na mafisadi wao tuwaachie tu ili umeme uwepo na CCM waonyeshe kama mafanikio wakati wa kampeni 2015.
2. Mikakati mbalimbali ya muda mrefu, muda wa kati na mkakati wa dharura: Mkazo wa maelezo uko kwenye muda wa dharura wa kuzalisha Mw1130 kabla ya 2013.
3. Kuondokana na umeme wa Maji kwa kupata umeme kutoka Mtwara na Kiwira: Kinachozungumzwa ni siasa za wawekezaji katika miradi hiyo miwili. Mnaowaza maji ya Rusumo meipata hiyo? I just hope NSSF watapata hiyo tenda ya Kiwira japo sina hakika serikali (CCM) kama haina mkono huko kwa ajili ya kampeni za 2015. Maana mambo yote yanaelekea kulenga uchaguzi tu.
4. Umeme kuwafikia asilimia 30 ya Watanzania nchi nzima kutoka asilimia 14 za sasa ifikapo mwaka 2015: Hili ndilo lengo la wizara. Hawajasema kama ni la muda mrefu, kati au dharura. Swali langu ni lini tutawafikia 100% ya watanzania. Miaka 50 kutoka uhuru tunazungumzia asilimia 14 hadi 30? Ni muujiza gani utafanyika kuipandisha 14% kwa asilimia 114 ili tufikie asilimia 30. Je, ni meremeta nyingine? Kwa lengo hilo ni kufikia 2015?
5. Serikali haijatuambia mkakati wa muda mrefu ni upi?: (Samahani - Naomba niote) -Wanataka kuua mitambo ya Kidatu na Mtera kwa kutuletea Dowans nyingine. Nimelazimika kuota hivyo kwa vile nimekosa imani na serikali yangu kiasi kwamba kila kinachofanyika nadhani nahujumiwa.
 
Yale maporomoko ya rusumo ndo mto kagera hivyo kama ujuavyo kilichokuwa kinaleta pingamizi ilikuwa ni mikataba ya kimataifa juu ya matumizi ya maji ya Nile!Hivyo siyokwamba serikali hailitambui la hasha!Bali ni juu yamikataba ya kimataifa juu ya matumizi ya maji ya nile rever
 
Kujua ya umeme wa Kiwira na Mchuchuma waliouzungumzia JK na Ngeleja jana kama inawezekana ifikapo 2013 soma thread nyingine iliyorejeshwa leo baada ya kuwaposted na Mwanakijiji mara ya kwanza 25th June 2007 yenye title: Re: KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...
 
Wakuu nijuavyo mimi mpango wa kuzalisha umeme kutokana na hayo maporomoko ya Rusumo bado hupo. Mimi mwenyewe mwaka juzi nilishiriki kufanyie eneo hilo "socio-economic impact accessment study." Tatizo lililopo huu ni mradi wa nchi tatu; Burundi, Rwanda na Tanzania chini ya KBO, na kama sehemu ya mradi huo kunahitajika kujengwa bwawa ambalo litameza ardhi kubwa ya Rwanda; kwakuwa Rwanda ina eneo dogo jambo hilo halikubaliki. Katika kulipatia ufumbuzi tatazo hilo inapendekezwa kutengenezwa bwawa ndogo la kuzalisha 60mw tu, ambapo kila nchi itapata 20mw.
 
Wakuu nijuavyo mimi mpango wa kuzalisha umeme kutokana na hayo maporomoko ya Rusumo bado hupo. Mimi mwenyewe mwaka juzi nilishiriki kufanyie eneo hilo "socio-economic impact accessment study." Tatizo lililopo huu ni mradi wa nchi tatu; Burundi, Rwanda na Tanzania chini ya KBO, na kama sehemu ya mradi huo kunahitajika kujengwa bwawa ambalo litameza ardhi kubwa ya Rwanda; kwakuwa Rwanda ina eneo dogo jambo hilo halikubaliki. Katika kulipatia ufumbuzi tatazo hilo inapendekezwa kutengenezwa bwawa ndogo la kuzalisha 60mw tu, ambapo kila nchi itapata 20mw.

Huo mpango utatekelezwa lini? Watanzania tunasifika kwa mipango lukuki with little % kuitekeleza. Tutakuwa watu wa kupanga hadi lini?
 
Nuclear Tanzania?????....... (who will takecare of the nuclear plant.CCM government or Tanesco..haha ) kwa uzembe,lack of seriousness na longolongo za Serikali na watendaji wake i dont suggest kabisa the use of Nuclear power maana tutatukua tunatengeneza bomu la kutulipua kutakufa nchi nzima na na watakao okoka watambiwa ni mapenzi ya Mungu...lol.......Transformer tu zimewashinda ku-manage kila siku zinalipuka iwe Nuclear Tanesco wataweza?...u must b kidding..
Aisee hata mimi nakuunga mkono. Kuwa na umeme wa Nuclear hapa Bongo chini ya CCM ni kujitamkia hukumu ya kifo cha Taifa zima kwa nukta moja tu maana vibaka hawana dhamana. Wanaweza kuchomoa kifaa kimoja tu tukalipukiwa na kuwa mwisho wetu. Kama ni nyuklia labda tusubiri utawala mwingine na si huu wa wezi na vibaka. Hakika taifa linapita katika kipindi kigumu kabisa chini ya hawa walevi CCM. Anyway hakuna refu lisilo na ncha ingawa yaelekea ilikuwa rahisi kuuondoa ukoloni wa mwingereza kuliko huu wa vibaka CCM maana sasa wameamua kujitengenezea hata Katiba ya kuwalinda ili watawale milele.
 
Back
Top Bottom