Hizi ndo akili zetu...sijui umetumia kigezo gani kusema Putin anatumia akili ya zamani sana,in short tutapiga kelele humu ila hatutajua chanzo chake hasa hadi wamefika/amefikia hapo......We are African lets solve our problem 1st before looking outside our boundary ambayo hata tungeachiwa changamoto zao hata robo tu tutakesha miaka mia mbili hatumalizi hata robo ya tatizo.
Kama una akili kuliko huyo Putin tusaidie kuondoa matatizo ya kiuchumi hapa Tanzania au jambo kubwa kuliko hilo dogo la huko Russia la msongamano wa magari Dar-Es-Salaam.
Hebu tulia ujadili hoja iliyoko mbele yetu, siyo kukurupuka na ku-question akili zangu. Kama unataka nitatua matatizo ya Dar es Salaama, niko tayari kufanya hivyo iwapo utanipa madaraka hayo. Siwezi kutatua matatizo ya Dar wakati umewapa madaraka watu wasiokuwa na akili.
Kama wewe unadhani kuwa tendo la Putin ni sawa basi tuambia uhalali wake ni nini. Huwezi kuchukua jeshi lako na kuliingiza nchi ya jirani yako wakati hamjagombana. Matatizo ya Ukraine yalikuwa yao ya ndani, yeye kuingilia ni kosa ambalo litakuwa ni hasara kwa urusi. Kuvamia nchi ya jirani kwa sababu tu rafiki yake kaondolewa madarakani na wabunge wa nchi hiyo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo ni kusa sana. Ni akili ya kizamani kudhani kuwa Ukraine bado ni sehemu ya USSR wakati ni wao Russia wakiongozwa na Yelstin ndio waliovunja muungano ule na kuacha kila nchi ijiendeshe yenyewe.
Amejenga mazinigira ambayo nchi nyingine zote zilizokuwa sehemu ya USSR kuanza kujijenga kijeshi kwa kuogopa kuvamiwa na urusi; waliwahi kuivamia Georgia, na sasa wamefanya hivyo kwa Ukraine kwa hiyo nchi nyingine zilizobaki zinajua kuwa wana bully jiranni yao. Kumbuka kuwa Ukraine ndiyo iliyokuwa na silaha nyingi sana za Nyuklia kuliko republic nyinginje yoyote huko USSR, wakaombwa sana waziharibu na hapo mwaka 1994 wakawekeana mkataba wa kuziharibu mradi tu usalama wao usitishiwe na urusi. Kwa vile Putin amekiuka mkataba huo, basi Ukraine inaweza kuanza tena kujilimbikiza silaha hzio, jambo ambalo linakuwa ni hatari siyo tu kwa usalama wa dunia bali kwa Urusi pia.
Nchi nyingi zilizokuwa za USSR na zile za Warsaw pact zinaanza kuhamia NATO haraka haraka kwa sababu ya matendo ya Putin; hilo halitakuwa jambo zuri kwa Urusi.
Kichuguu nmegundua kuwa kwa akili zako unadhan Putin alilala na kuamka akaamua tu apeleke majeshi UKRANE,na unadhan wabunge wa bunge la URUSI walikunywa mvinyo wakalewa kabla ya kumpa ruhusa putin ya kupeleka jeshi Ukrane..
KIUFUPI HAUJUI KINACHOENDELEA NA MVIVU WA KUJIFUNZA,HVO NA KUSHAURI KWA KULINDA HESHIMA YAKO TU KAA KIMYA..
Na hii ni neema kwa nchi zinazoendelea...sasa tutapumua... na tutafanya mambo yetu kwa nafasi.
Wote manotetea kitendo cha Putin mbona hamkumtetea Amin alipoingiza majeshi yake pale Kagera tena sehemu ndogo tu akiwa anatafauta mpaka aliouita wa asili, yaani mto? Kuna wahaya pande mbili za mpaka lakini tulitetea sana eneo letu tena kwa nguvu zote hadi uchumi wetu ukaharibia. Kitendo cha Putin ni uvamizi na uchokozi usiokuwa na maana; acheni ushabiki mwingine usiokuwa na mantiki. Mkishbikia kitendo cha taifa moja kuvamia taifa jingine kwa mapenzi ya kiongozi wake basi msishangae siku Tanzania nayo ikivamiwa na taifa moja kubwa sana. Kuna mataifa mengi yenye nguvu yanayoweza kuivamia Tanzania.
Watu mnashindwa kuelewa kwa nini marekani inapotaka kuivamia nchi yoyote hujenga sana ile coalition kupitia umoja wa mataifa na kujenga kesi yao kuwa kweli ni lazima uvamizi ufanyike. Hata kama tunaona kuwa uvamizi huo ni halali, at least huwa umeshapitia ngazi zote za kisheria katika UN: Putin kakurupuka.
Katika watu ambao si wapendi ni dizain yako.....Kuna aina ya watu humu duniani asipolisikia/kuona jambo yeye kwa masikio/macho yake anahalalisha kuwa jambo linalozungumziwa halipo au halijatokea.
MAWAZO UJENZI sijasikia kuwa hawa watu wameongea chochote coz sipo na media 24hrs ila aliyesema sio mpuuzi na walichoongea haviwezi kuwa wazi sana na mara nyingi habari ambazo huwa zinatolewa kwa wananchi ni zile zisizo kuwa na athari but am sure 85% ya mazungumzo ya aina hiyo huwa zinafichwa.
"The process that put Aksyonov(newly elected crimenian PM by Crimean Parliament) in power violated
the Ukrainian constitution, since Kiev is supposed to appoint the regional prime minister. But
then again, so did the process through which Oleksandr Turchynov(newly elected - by the Ukranian
Parliament- PM) became acting president of Ukraine, because, as Daisy Sindelar, a senior
correspondent for Radio Free Europe/Radio Liberty, has pointed out, former President Viktor
Yanukovych's ouster did not follow constitutional protocol. One can argue that the cases are
somewhat equivalent: In both, parliamentary majorities supported a new leader."
Mkuu Kichuguu, hakuna aliye madarakani kihalali hapo. Wote wana uhuru wa kuomba msaada wa kijeshi!
jana kwenye UN security council,Russia walionyesha barua iliyoandikwa na rais victor kabla hajapinduliwa iliyokua ikiomba msaada wa kijeshi toka russia.OK,
Sasa Urusi inaingiaje kwenye mgogoro wa Ukraine mpaka kupeleka jeshi huko; hawajasema waliombwa na upande wowote wa mgogoro bali wamesema wanakwenda kulinda warusi wenzao. Huo ni mgogoro wa ndani ya Ukraine kuna sheria na taratibu zao zinahusu kutatua migogoro yao ya ndani. Hiyo quote yako ni single sided, kwani inasahau kuwa bunge la Ukraine lina mamlaka ya kumwondoa rais madarakani. Katiba za nchi nyingi ikiwamo hata ya Tanzania inatoa mamlaka kwa Bunge kumwondoa rais madarakani. Mgogoro wa Ukraine ulikuwa Kiev, na ndipo Bunge lilipomwondoa rais madarakani kihalali kabisa, Urusi ikatengeza mgororo mwingine huko Crimea kwa sababu zao binafsi. Tataizo kubwa ni kuwa hakupewa muda wa kujitetea lakini katiba hiyo pia inaruhusu bunge kuchukua hatua za dharura katika hali ya hatari. Yule alitolea kwa vile nchi ilishakuwa katika mgogor wa muda mrefu na watu wengi kuwa wampoteza maisha. Puti angeingia pale kama Big Brother kusaidia kumaliza mgogor angefanya vizuri lakini yeye anakwenda pale akiwa upande mmoja wa mgogor tena kwa kutumia mabavu, hiyo ni kutumia akili za ki-USSR ambazo ni za kizamani sana zilizowahi kutumika Czechslovakia na Afghanstan zamani sana.
OK,