Rushwa inavyotawala uandikishaji watoto Darasa la Kwanza. Case study ya Olympio na Diamond Primary Schools

Ingewekwa sheria kali kwamba watoto wa viongozi wa umma lazima wasome shule sa serikali na kutibiwa hospitali za umma. Yaani marufuku nzito kusomesha mtoto shule binafsi.

Hapo huduma za elimu na afya zingeboreshwa tu.
 
Kuna mtu namfahamu mtoto wake kapata nafasi hapo olympius mwaka huu bila kutoa chochote, we mwanao itakua alichemka interview. Ila jamaa kaambiwa japo mwanae kafaulu na kupata nafasi akishindwa kulipa ada kwa pamoja hiyo nafasi atapewa mtu mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa mfano wa mtoto mmoja tu uliyesikia kapata bila kutoa chochote haibatilishi hoja hii, sio wote wanaotoa ila ni kwa kiasi kikubwa.... hata ukiongea vema na huyo mzazi kuhusu hili nina uhakika amewahi kulisikia.

Rushwa ni kila mahali kila wakati kama ilivyokuwa ‘Mungu ni mwema’.... mfano kidogo niliwahi kupata fursa kuandikisha SENSA mwaka 2012 bila kutoa kitu wala kushikwa mkono ila kila niliyekutana naye kwenye semina aliuza ‘nimeletwa na Nani’.
 
Nilienda pia Oysterbay nikaambiwa nimechelewa usaili umepita, ila yule ‘mama’ akanipa tumaini kuwa ingekuwa mtoto amefanya ‘intavyuu’ pale angejua cha kufanya.
Hua wanafanya siku moja shule zote za serikali za English medium

MTC | 101|
 
Sasa huku Dar kuna mibus kama walivyosena wadau ya watu binafsi sasa watoto jamani wanajazana, wana banana wanapakatana khaaaaa aaaaa.
Mtu anakaa mbezi lakini mtoto anampelekea Diamond.
Mtoto anaamka saa 10 alfajr hata utoto wake haufaidi.
Ni vyema watoto wa some shule za karibu kuliko hizo shule mnazotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sure mkuu huduma zao sio poa hasa usafiri ni mateso kwa wanetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona shule zipo nyingi tu nzuri siyo lazima umpekeke huko. Wanangu wamesoma Mlimani primary wako vzr tu.
Mlimani wameanza mtaala wa kufundisha kwa kiingreza?
Last time walikuwa wanasema wataanza kichina na kiingereza.
BTW, Shule nzuri sana isipokuwa walikuwa wanazingua kukomaa na mtaala wa kiswahili.
 
Majungu haya kama kweli nenda TAKUKURU upate msaada

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hakuna kificho, ni kweli hizo shule bila rushwa labda uwe mtoto wa kigogo lakini sio Kigogo2014.
Hiyo rushwa hakuna namna ndio njia ya kuwapunguza waombaji.
Watu wanao omba ni wengi sana zaidi ya mara 10 ya idadi inayotakiwa na wanaofaulu usahili wengi kupita kiasi, sasa wafanyeje?

Wapange majina kwa herufi kisha ikifika idadi wapige mstari? Inabidi tu watu watoe pesa ya ziada ili mwenye kisu kikali ale nyama.
Kwa mzazi anae jali kuhusu huduma za mtoto wake hizo shule hazifai kwakweli sema uwezo wa kusomeasha private unakuwa haupo.
Watoto wengi sana huku huduma muhimu za chakula, maji, usafiri na idadi sahihi ya wanafunzi wanao takiwa kuhudumiwa na mwalimu ni duni.

Angalia wengine wanavyo teseka kwenye Mwendokasi au daladala za kawaida kisa wakasome English Medium ya bei rahisi. Hawa baadhi yaoi wakiwa wakubwa wakipata nafasi ofisi za umma wanataka wanainchi wenzao nao wateseke kupata huduma flani wakija ofisini kwake.
 
Sasa huku Dar kuna mibus kama walivyosena wadau ya watu binafsi sasa watoto jamani wanajazana, wana banana wanapakatana khaaaaa aaaaa.
Mtu anakaa mbezi lakini mtoto anampelekea Diamond.
Mtoto anaamka saa 10 alfajr hata utoto wake haufaidi.
Ni vyema watoto wa some shule za karibu kuliko hizo shule mnazotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wanabanana hasa na hili joto sana na homa ya ini ilivyoshamiri. Mimi nilishapanda gari usiku na mtoto anatoka shule mida ya saa moja anakaa Mbezi makabe anasoma diamond.
 
Wanafundisha kiswahili Ila watoto wanatoka na uelewa mpana sana, confidence na nidhamu. Kichina wanafundisha pia kama somo tu.
Nilisikia kuanzia Grade 1 wa mwaka 2017 wataanza kutumia mtaala wa kiingereza na kichina kama somo la ziada tu, what went wrong?
 
Shule zetu hizi ‘elimu bure’ ni majanga tupu, zipo shule kadhaa japo chache za serikali za kulipia (English Medium) na zinafanya vizuri sana.... mzazi haoni shida kulipia kwa maana ada ni nafuu ukilinganisha na shule binafsi za hadhi hiyo.

Sijui serikali yetu imekwama wapi kuongeza hizi shule, zimekuwa kimbilio na zinadahiri watoto wengi mno kwa mwaka.... unakuta darasa moja wanafunzi 400+.

Pia kuna Oysterbay japo haichukui idadi kubwa kama hizo mbili tajwa, na kwa mikoani zipo katika baadhi ya miji.... ni wito kwa serikali kuliona hili kwa kuwa limeonesha matokeo chanya.

Mkuu samahani Arusha ni zipi za mfumo wa English ?
 
Mimi siyo profesa na wala sifanyi kazi udsm. Vigezo ni mtoto atoke maeneo ya ubungo, makongo,changanyikeni na kimara lkn siyo atoke gongolamboto au Chanika aje asome mlimani huyo hapati nafasi.
Siku hizi kama unatoka Kimara ukipata basi una bahati.Kama unatoka Makongo ukipata una bahati.Wanachukua watu wa jirani sana na mwisho ni wanafunzi 45 tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom