MSAADA: Jinsi ya kumpeleka mwanangu Shule ya Msingi Olympio 2024

Gentleman 446

Senior Member
Mar 26, 2021
112
399
Ndugu zako naombeni muongozo kidogo, kuna shule nimeifuatilia nimeambiwa ni shule ya serikali ila ni ya kulipia na ada zake ni nafuu, nikafikiria mwakani nimpeleke mwanangu hapo ajiunge na wenzake ili aipate hiyo elimu.

Sasa katika kuuliza baadhi ya watu hawanipi majibu ya kueleweka mara wengine wanakwambia ili mtoto ajiunge lazima upenyeze rupia (hongo), kuna mwingine anasema unaweza toa chochote na bado mtoto wasimpe nafasi.

Ndugu zangu mnaohusiana na hiyo shule nisaidieni direction nzuri, najua kuna watu wana watoto wao wanasoma huko na wengine ni watumishi.

Tupeni A, B, C, D mapema, si mnajua mwaka umeisha huu.
 
Ile shule siyo ya WALALA HOI Nakuhakikishia kwa kauli hii UMEKOSA NAFASI TAYALI tafta shule nyingine.
 
Namba za dereva wa bus la root ya Kinondoni..0674 92.. ( **)

Vijana wangu wawili wanasomea Olympio.

Nimefuta namba nimeogopa usije ukapigwa huko ukaanza kuleta lawama kwangu..

Dereva ungemuomba namba za mwalimu halafu huyo mwalimu angekusaidia kupata nafasi but ungetakiwa kutoa hela kwanza na kutoa hela kwanza sio guarantee kwamba utapata nafasi ( unless otherwise ) uwe na connection.

Kama UNAISHI mbali na upanga .mpeleke shule ya kata tu au kama upo karibu na Chamazi mpeleke Chamazi Islamic ada yao sh laki Sita kwa mwaka
 
Hiyo chamazi islamic wana sekondari,ada pia ikoje
 
Olympio au diamond bila Rushwa kupata nafasi ni ishu embu jaribu muhimbili,United Nations,Bunge,Upanga,Maktaba na zenyewe ni nzuri
 
Back
Top Bottom