Rushwa inavyotawala uandikishaji watoto Darasa la Kwanza. Case study ya Olympio na Diamond Primary Schools

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,524
2,000
Kweli ‘mujini’ mipango, salamu kwenu ndio kitu cha bure. Karibuni kwenye mada.

Shule tajwa ni kati ya shule bora na kongwe mjini Dar es Salaam ambazo zipo chini ya serikali na zikiendesha masomo kwa lugha ya Kingereza, zimekuwa kimbilio la wanyonge kulingana na Ada zake kuwa nafuu sana kulinganisha na ubora wa elimu itolewayo pale, pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi hivyo basi pongezi nyingi sana kwa hili.

Kwa kuzingatia sifa hizo basi nikawiwa kusomesha mtoto wangu katika shule moja kati ya hizo, hivyo nikaanza mapema kabisa kukusanya taarifa na kufuatilia kwa ukaribu kujua ratiba yao, vigezo na masharti ili kuweza kusajiliwa pale.

Nikafika shuleni na kuelekezwa kuwa zoezi litafanyika mapema mwezi Novemba hivyo niandae tu viambatanisho, ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa mtoto, paspoti picha na cheti cha kuhitimu elimu ya awali.

Nilitimiza yote hayo na muda ulipowadia nilifika pale shule kuchukua fomu kwa ajili ya usaili (ni kulipia 10,000/-), kisha ikapangwa siku ambayo watoto wote walioomba walipaswa kufanya usaili (mtihani) ili kuchujwa kwa uwezo wao na ikafanyika hivyo.

Baada ya takribani wiki moja majina ya waliofanikiwa kupata nafasi (waliofaulu usaili) yakabandikwa, hapo ndipo vilio vilitamalaki mioyoni mwa wanyonge wazalendo.

Sehemu kubwa ya wazazi niliokutana nao siku ile majina yao hayaonekani, huenda ni kweli watoto wetu wetu ni vilaza kwa uwezo mdogo ila hasha mwanangu si mmoja wao.

Ndipo katika stori za hapa na pale miongoni mwetu kukatokea wenyeji na wajuvi waliotutonya siri ya ushindi, kwamba mjini mipango.

Kwamba mkono mtupu haulambwi, yale majina pale unakuta zaidi ya 80% ni geresha tu, ambayo ‘yatauzwa’ kwa watoto wa wajanja na vibosile kwa bei ya Tzs 300,000/- (Laki Tatu).

Mbinu wanayotumia ili kubadili majina ni kusingizia kuwa waliopata nafasi zile wameshindwa kulipa ada, (kumbuka ada ya darasa la kwanza pale inatakiwa kulipwa kwa mkupuo, Laki Tatu ya mwaka mzima) hivyo nafasi imetolewa kwa mtoto mwingine.

Na huu ni utaratibu wao miaka na miaka hivyo umezoeleka kwa wenyeji, mmoja akatuhakikishia hilo kuwa ‘andaa Laki Sita hapa mtoto wako aandikishwe’ sharp (kwa maana ya Ada na Hongo). Hasira zilinipanda kwa uzalendo nilionao ila sikuwa na namna nimeamua kutumia jukwaa hili kufikisha kilio cha wengi.

Siko pekee yangu, laki 3 naweza kuipata ila kwangu uzalendo mbele. Kwa pamoja tupaze sauti kukemea rushwa na urasimu wa namna hii.

Nchi yetu sote hii, elimu bora ni haki ya kila raia mwenye kuihitaji. Karibuni kwa ushuhuda na ushauri kwa mamlaka husika zifanye uchunguzi na kuchukua hatua kali.

Nawasilisha.
 

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,524
2,000
Mbona shule zipo nyingi tu nzuri siyo lazima umpekeke huko. Wanangu wamesoma Mlimani primary wako vzr tu.
Nimezingatia makazi yangu mkuu, target zangu zimevurugwa kwa maana sikupanga kupeleka ‘shule yoyote’ tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom