Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Panga la mabadiliko katika Majimbo ya Uchaguzi, linaweza kuyakumba Majimbo ya Uchaguzi nchini yapatayo 264 endapo Mapendekezo yanayotolewa na wadau, yatakubaliwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
Kulingana na taarifa zilizoandikwa na Jamhuri, kuna Mapendekezo kuwa, Majimbo ya Uchaguzi yaendane na Halmashauri zilizopo Tanzania Bara ambazo ni 186 (plus 16 wa kuteuliwa). Vilevile, nafasi ya viti maalum inapendekezwa kuwa asilimia 35% ambazo zitakuwa sawa na Viti 69. Hivyo, Bunge litakuwa na Wabunge 271 badala ya 393 na hivyo tofauti kuwa 122.
Mishahara, posho, marupurupu na kiiinua mgongo cha Wabunge hao 122, kwa kipindi cha miaka mitano, ni sawa na Tsh. bilioni 122.