'Ruksa' kwa watumishi wa umma kushiriki siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Ruksa' kwa watumishi wa umma kushiriki siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Jul 21, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kati ya maswali na masuala ambayo watumishi wengi wa umma wamekuwa wakijiuliza ama kuyatakakari baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ni haki, wajibu na mipaka yao katika kujihusisha na siasa zikiwemo za vyama.

  Aidha majibu mepesi ya maswali hayo yamekuwa ni hisia finyu kuwa watumishi wote wa umma hawapaswi kujihusisha na vyama vya siasa. Ama kwa kwa upande mwingine yamekuwepo pia mawazo potofu kwamba watumishi wa umma wanapaswa kujihusisha na chama kinachotawala pekee na hawapaswi kabisa kujihusisha na vyama vya upinzani. Aidha wapo watumishi wa umma ambao wamekuwa wakitoa maneno ama kufanya vitendo ambavyo hawaruhusiwi kufanya katika ushiriki wao katika siasa.

  Kabla ya chaguzi ndogo za Busanda na Biharamulo niliandika mfululizo wa makala nne kuchambua suala hili mintaarafu Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi kwa kurejea pia sheria na kanuni zinazohusika. Nawaletea makala hizi hapa, kama sehemu ya kuendeleza mjadala kuhusu suala husika.

  Katika mfululizo huu, sijachambua hatua ambazo mtumishi wa umma anayetaka kugombea uongozi wa kisiasa anapaswa kuzifuata, sijachambua masuala mahususi kuhusu Ubunge wa Afrika Mashariki na sijazungumzia mambo ambayo si ruhusa kwa watumishi wa umma kuyafanya kuhusiana na ushiriki wao kwenye siasa. Uchambuzi wa masuala hayo na mengine utafuata katika hatua ya baadaye. Nawatakia mjadala mwema

  JJ


   
 2. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ‘Ruksa’ kwa watumishi wa umma kushiriki siasa-1


  Na John Mnyika

  Kati ya maswali na masuala ambayo watumishi wengi wa umma wamekuwa wakijiuliza ama kuyatakakari baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ni haki, wajibu na mipaka yao katika kujihusisha na siasa zikiwemo za vyama. Aidha majibu mepesi ya maswali hayo yamekuwa ni hisia finyu kuwa watumishi wote wa umma hawapaswi kujihusisha na vyama vya siasa. Ama kwa kwa upande mwingine yamekuwepo pia mawazo potofu kwamba watumishi wa umma wanapaswa kujihusisha na chama kinachotawala pekee na hawapaswi kabisa kujihusisha na vyama vya upinzani. Makala hii itachambua suala hili mintaarafu Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi kwa kurejea pia sheria na kanuni zinazohusika.

  Utumishi wa umma katika nchi yetu unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake. Kwa madhumuni ya makala hii Neno Mtumishi wa Umma lina maana kama iliyoanishwa katika Kanuni za kudumu za utumishi kifungu Na. A.1(66) ambacho kinatafsiri mtumishi wa umma kama mtu yoyote anayeshikilia ofisi ya umma ambayo imepewa mamlaka ama inatekeleza wajibu wenye asili ya umma, iwe chini ya utawala wa moja kwa moja wa Rais au la. Na inajumuisha maofisa walio chini ya Serikali za Mitaa ama Mashirika ya umma; lakini haijumuishi wanaoshikilia nafasi hizo kwa sehemu ya muda wa ziada(Part Time basis).

  Kwa mantiki hiyo, tafsiri hii inafanya wafanyakazi wote wa serikali na taasisi zake kuwa ni watumishi wa umma. Hii inajumuisha Rais, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri na Mashirika ya umma, watendaji wa kata nk. Orodha hii inahusisha pia waajiriwa wa kawaida wa serikali mathalani walimu wa shule za umma, watumishi wa sekta ya afya wa serikali, maofisa wote waajiriwa wa halmashauri/serikali za mitaa nk. Watumishi wa umma ni pamoja pia watumishi wa mihimili mingine ya serikali kama mahakama kwa maana ya majaji na mahakimu na Bunge kwa maana ya wabunge na watumishi wa bunge. Watumishi wa umma ni pamoja na wafanyakazi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo askari wa majeshi mbalimbali. Ukiitafakari orodha hii ndefu utaona kwamba jambo hili linahusu watu wengi; hivyo suala la ushiriki wao katika siasa katika mfumo wa vyama vingi linapaswa kutafakariwa na kujadiliwa na umma.

  Uzoefu katika nchi mbalimbali duniani unaonyesha kuwa ziko njia mbalimbali za watumishi wa umma kuweza kujihusisha na vyama vya siasa. Njia iliyozoeleka zaidi ni ile ya kushiriki katika kupiga kura ama kuweza kushiriki katika kupigiwa kura kwa maana ya kugombea. Kushiriki katika kupiga kura kunaweza kuwa ni katika kupiga kura za kuchagua viongozi wa umma wa kiserikali ama kupiga kura katika kuchagua viongozi wa ndani ya chama. Kwa upande wa kugombea nayo inaweza ikawa katika chaguzi za kiserikali ama kugombea katika nafasi za uongozi za ndani ya chama cha siasa. Katika hali hiyo, njia nyingine ya watumishi wa umma kujihusisha na vyama vya siasa ni kwa kuwa wanachama wa vyama hivyo. Aidha katika nchi ambazo demokrasia imeendelea, ushiriki wa watumishi wa umma katika vyama vya siasa na siasa kwa ujumla unahusisha ushiriki wao katika kupiga kura kuhusu masuala mbalimbali(issue voting) mathalani kura za maoni(referendum). Pia, watumishi wa umma wanaweza kujihusisha kwa kutoa maoni na mitazamo yao kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na yanayohusu vyama vya siasa kwa kutumia njia mbalimbali.

  Kuanzia mwaka 1965 hadi 1992 Tanzania ilipokuwa na mfumo wa siasa wa chama kimoja kundi lote hili la watumishi wa serikali na vyombo vyake siyo tu waliruhusiwa bali ilionekana ni wajibu wao kushiriki katika mambo ya kisiasa. Shughuli nyingi za kiserikali na za kisiasa zilikwenda kwa pamoja na palikuwepo na maingiliano makubwa kati ya sehemu hizi mbili katika shughuli zote za kiutendaji, kiuongozi na kiitikadi.

  Na kwa kweli suala hili lilianza mara baada ya uhuru kabla hata ya nchi kutangaza kuingia katika mfumo wa chama kimoja. Mathalani, baada ya Maasi ya Jeshi ya mwaka 1964 uamuzi wa Rais wa Kwanza Hayati Mwalimu Nyerere wa kulisuka upya jeshi ambalo lilirithiwa toka kwa mkoloni, kuunda jeshi la wananchi wa Tanzania ulihusisha fungamano la kipekee baina ya Jeshi na Chama tawala. Wakati ule, sehemu kubwa ya wanajeshi ilichaguliwa kutoka vijana wa chama TANU. Hodhi hii iliendelezwa zaidi chini ya mfumo wa chama kushika hatamu ambao ulioweka mahusiano ya karibu baina ya chama kinachotawala na serikali ikiwemo vyombo vyake vya dola. Ni fungamano hili kati ya watumishi wa umma wa kada zote, na chama ndio uliofanya chama kinachotawala kuwa chama dola; suala lenye athari mpaka hivi sasa hususani katika nyakati za uchaguzi.

  Mapendekezo ya Tume ya Nyalali ya mwaka 1991 na marekebisho ya Katiba ya mwaka 1992 kuingia katika mfumo wa vyama vingi na marekebisho ya sheria yaliyofuata yameweza kupunguza kwa kiasi hali hiyo. Lakini bado fungamano kati ya chama tawala na serikali ikiwemo vyombo vya dola linahitaji kujadiliwa ili mabadiliko ya kweli yaweze kufanyika. Mabadiliko hayo ya kikatiba, kisheria na kimitazamo yatawezesha kuwa na tunu za kitaifa, misingi kamili ya haki za raia, mifumo ya uwajibakaji wa viongozi na uwanja sawa wa kisiasa. Mabadiliko hayo yatawezesha pia kujenga taasisi za kitaifa, uongozi bora na dira ya pamoja yenye kuunganisha nguvu za umma katika kupambana na ufisadi, kutetea rasilimali na kusimamia fikra mbadala zenye kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote. Taifa wananchi wanaweza kuneemeka na uwezo ambao wamejaliwa wao na nchi kwa ujumla.

  Wakati tunapoanza kutafakari namna ambayo watumishi wa umma wanavyoweza kujihusisha na vyama vya siasa kwa sasa na kuwa wakala wa mabadiliko wanayotaka kuyaona, ni muhimu kama taifa tukakumbuka ushiriki wao katika wakati uliopita na taathira yake katika demokrasia katika wakati huu. Hii itawezesha kuchukua maamuzi thabiti ya kuweka mwelekeo mwafaka wenye kujenga katika mafanikio ya zamani na wakati huo huo kutibu majeraha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yaliyotokana na hodhi ya chama kimoja ambayo sasa taifa linadhamiria kuondokana nao.
   
 3. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  “Ruksa” kwa watumishi wa umma kushiriki siasa-2


  Na John Mnyika

  Katika makala iliyopita tulijibu swali nani ni ‘mtumishi wa umma’, tukadokeza uzoefu kutoka mataifa mbalimbali kuhusu namna ambavyo watumishi wa umma wanaweza kushiriki katika siasa. Kadhalika, makala iligusia ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa kuanzia mwaka 1965 mpaka 1992 wakati huo nchi ikiwa katika mfumo wa siasa wa chama kimoja. Katika makala hii tutaangalia ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa katika kipindi cha awali cha mfumo wa vyama vingi kuanzia mwaka 1992 mpaka mwaka 2000.

  Ni muhimu kusisitiza kuwa wakati tunatafakari namna ambayo watumishi wa umma wanavyoweza kujihusisha na vyama vya siasa kwa sasa na kuwa wakala wa mabadiliko wanayotaka kuyaona, ni muhimu kama taifa tukakumbuka ushiriki wao katika wakati uliopita na taathira yake katika demokrasia katika wakati huu. Hii itawezesha kuchukua maamuzi thabiti ya kuweka mwelekeo mwafaka wenye kujenga katika mafanikio ya zamani na wakati huo huo kutibu majeraha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yaliyotokana na hodhi ya chama kimoja ambao sasa taifa linadhamiria kuondokana nao.

  Kufuatia mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika Julai, 1992 na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa kurejea Tanzania, Serikali ilitoa maelekezo ya jinsi watumishi wa umma watavyoshiriki katika mambo ya Siasa kupitia waraka wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa mwaka 1992. Waraka huu uliotolewa wakati wa Urais wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, maarufu kama “Ruksa”. Na wa kweli waraka huo ulitoa ruksa pana ya ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa ukilinganisha na waraka uliofuatia ambao tutaurejea katika makala inayofuata.

  Utaratibu uliotolewa na waraka huo uliwagawa watumishi wa umma katika makundi mawili na kuweka masharti ya namna watavyoshiriki katika siasa. Watumishi wa kundi “A” walijumuisha Watumishi wa ngazi za juu wa Serikalini, Serikali za Mitaa na Katika Mashirika ya Umma wanaoshughulikia uandaaji na usimamizi wa sera. Hawa walikuwa ni watumishi waandamizi kwenye madaraka kuanzia ngazi za mkurugenzi na kuendelea juu, Meneja Msaidizi na kuendelea juu na ngazi ya Mkurugenzi Mtendaji. Watumishi wa Kundi “B” walijumuisha watumishi wa ngazi za chini na kati ambao hawahusiki na maandalizi ya sera mbalimbali.

  Chini ya waraka Na. 1 wa mwaka 1992 watumishi katika kundi “A” na “B” walipewa masharti kuhusu mambo wanayoruhusiwa kufanya na wasiyoruhusiwa kufanya kuhusu ushiriki wao katika siasa ikiwemo za vyama.

  Waraka huu uliotoa mwanya wa watumishi wa umma kushiriki katika siasa hususani kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na pia chaguzi za Serikali za Mitaa zilizofanyika katika ngazi za Mitaa, Vitongoji na Vijiji mwaka 1994 na 1999.

  “Ruksa” iliyotolewa na waraka huo iliotoa uhuru wa watumishi wa umma kushiriki katika masuala ya siasa na kwa kiasi kikubwa watumishi wengi wa umma wakati huo walijitokeza kuunga mkono vyama vya siasa; hususani vya upinzani. Harakati hizo za watumishi wa umma kushiriki siasa wakati huo pamoja ni moja ya sababu zilizochangia upinzani kupata viti vingi bungeni katika uchaguzi wa mwaka 1995 ukilinganisha na chaguzi zote zilizofuata.

  Hata hivyo, baada ya chaguzi hizo serikali ilionyesha dhahiri kutoridhishwa na hali hiyo na kueleza kwamba ‘ruksa’ hiyo ya watumishi wa umma kushiriki kwenye siasa ‘imeathiri maadili ya msingi ya utendaji kazi serikalini na vyombo vyake”.

  Ilipofika mwanzoni mwa mwaka 2000, wakati taifa likiwa linajiandaa na uchaguzi mkuu wa pili chini ya mfumo wa vyama vingi serikali ya wakati huo chini ya Urais wa Benjamin Mkapa ilieleza kutoridhishwa na kiwango cha ‘ruksa’ ambayo watumishi wa umma wamepewa kushiriki katika siasa.

  Serikali ikaeleza kwamba uhuru ambao watumishi wa umma wapewa kushiriki kwenye siasa unafanya baadhi yao kutotekeleza kwa dhati sera za chama tawala. Kadhalika serikali ikalalamika kwamba wapo watumishi wa umma wanaoikashifu serikali kufuatana na msimamo wa kisiasa. Pia yalikuwepo malalamiko ya pande zote kuhusu athari za kujihusisha na masuala ya siasa mahali pa kazi na wakati wa saa za kazi. Baadhi ya watumishi wa umma pia walilalamikiwa kwa kutoa huduma za kiutumishi kwa upendeleo unaotokana na msimamo wa kisiasa. Kwa upande mwingine, waliokuwepo pia watumishi wa serikali kuu waliojitokeza kugombea nafasi za uongozi/siasa katika serikali za mitaa jambo ambalo lilikwenda kinyume na dhana ya utenganishaji wa madaraka kati ya watungaji wa sera ambao ni viongozi wenye mwelekeo wa kisiasa na wale watekelezaji wa sera ambao kwa kawaida wanatakiwa kuwa watendaji.

  Aidha palikuwepo na utata kuhusu mgawanyo wa watumishi katika makundi “A” na “B” kutokana na vigezo kutokuwa wazi na kutoeleweka vizuri hivyo wakati mwingine ulizua mkanganyiko juu ya mtumishi yupi yupo katika kundi lipi.

  Kwa kiasi kikubwa baadhi ya kasoro zilichangiwa na ombwe na udhaifu iliokuwepo kwenye waraka wenyewe. Kwa mfano mbali na makundi ambayo nimeyadokeza hapo juu kuna makundi ya watumishi wa umma ambao hawakuorodheshwa kabisa katika waraka lakini kwa mujibu wa katiba wametajwa. Hawa ni watumishi ambao katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza wazi kwamba hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa. Hawa ni watumishi wa umma ambao ruksa yao pekee ya kushiriki kwenye vyama vya siasa ni ya kupiga kura. Ni kundi la watumishi wa umma ambao hawaruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote zingine za kisiasa isipokuwa kupiga kura tu. Ibara ya 147(3) na (4) ya Katiba imewataja Askari wa Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Polisi na Magereza. Pia Ibara ya 113A imewakataza majaji na mahakimu wa ngazi zote. Kadhalika Ibara 74(14) na (15) imewazuia wajumbe na watumishi wa Tume ya Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi.

  Kasoro nyingine ya waraka huo ilikuwa ni kutoyaraja makundi mengine ambayo pamoja ni kuwa hayajakatazwa na katiba kushiriki kwenye shughuli za kawaida za kisiasa lakini kwa mujibu wa kazi zao wanapaswa kushiriki kwa kupiga kura tu. Mathalani, watumishi wa idara ya usalama wa taifa, taasisi ya kuzuia rushwa(wakati huo), msajili wa vyama vya siasa, watumishi wa ofisi ya bunge na mawakili wa serikali.

  Kutokana na hali hiyo, ilipofika Mwezi Juni mwaka 2000 serikali ilitangaza kufuta waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa Mwaka 1992 na kutoa waraka mwingine kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao tutaufanyia mapitio kuanzia makala inayofuata. Sababu kuu iliyopelekea serikali kufikia maamuzi hayo ni kile kilichoelezwa kuwa ni ‘vitendo vya watumishi wa umma vinavyokiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kisingizio cha uhuru uliotolewa wa kushiriki katika mambo ya siasa’.

  Hata hivyo kwa watetezi wa demokrasia na maendeleo waraka huo wa mwaka 1992 ulionekana kuwa na udhaifu wa msingi wa kimaudhui na kimaadili. Waraka huo haukuweza kuviruka viunzi vya kikatiba na kisheria ambavyo vilikuwepo ambavyo vimeendeleza fungamano kati watumishi wa umma, chama kinachotawala na serikali ikiwemo vyombo vya dola na hivyo kuathiri ushindani wa kisiasa. Ikumbukwe kwamba mapendekezo ya Tume ya Nyalali ya mwaka 1991 na marekebisho ya Katiba ya mwaka 1992 kuingia katika mfumo wa vyama vingi na marekebisho ya sheria yaliyofuata yameweza kupunguza kwa kiasi hali hiyo.

  Lakini bado fungamano kati ya chama tawala na serikali ikiwemo vyombo vya dola linahitaji kuendelea kujadiliwa ili mabadiliko ya kweli yaweze kufanyika. Mabadiliko hayo ya kikatiba, kisheria na kimitazamo yatawezesha kuwa na tunu za kitaifa, misingi kamili ya haki za raia, mifumo ya uwajibakaji wa viongozi na uwanja sawa wa kisiasa. Mabadiliko hayo yatawezesha pia kujenga taasisi za kitaifa, uongozi bora na dira ya pamoja yenye kuunganisha nguvu za umma katika kupambana na ufisadi, kutetea rasilimali na kusimamia fikra mbadala zenye kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote. Taifa wananchi wanaweza kuneemeka na uwezo ambao wamejaliwa wao na nchi kwa ujumla. Sehemu ya wananchi hao ambao ushiriki wao kwenye siasa unapaswa kuwa wa maana na wenye manufaa ni watumishi wa umma.
   
 4. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  “Ruksa” kwa watumishi wa umma kushiriki siasa-3

  Na John Mnyika


  Makala zilizotangulia zimedokeza wakina nani ni watumishi wa umma na ushiriki wao katika siasa katika vipindi vilivyotangulia; wakati wa mfumo wa chama kimoja 1965 mpaka 1992 na kipindi cha awali cha mfumo wa vyama vingi 1992 mpaka 2000. Makala hii inalenga kuanza kufanya mapitio ya kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanzia mwaka 2000 na tunapoelekea katika chaguzi za mwaka 2009 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Ikumbukwe kuwa utumishi wa umma katika nchi yetu unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake. Kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kinampa mamlaka Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi kutoa waraka kuhusu taratibu mbalimbali za utumishi wa umma.

  Chini ya Mamlaka hayo, Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo akiwa Martem Y.C. Lumbanga tarehe 26 Juni, 2000 alitoa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma na. 1 wa mwaka 2000 wenye kumb. Na. SHC/C.180/2/113. Waraka huu ulihusu maadili ya Watumishi wa Umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Waraka huo ulianza kutumika kuanzia Julai 2000 na ulifuta waraka wa mwaka 1992.

  Katika waraka huo serikali imeamua kwamba hakutakuwa na makundi mawili ya watumishi kama ilivyokuwa hapo awali, bali watumishi wote wa umma sasa watatawaliwa na masharti yanayofanana. Katika waraka huo serikali pia imeamua kuanisha utaratibu utakaozingatiwa na watumishi wa umma watakaoamua kugombea ubunge kupitia viti maalumu, pamoja na wale walioteuliwa na Rais kwa mujibu wa katiba kuwa wabunge.

  Pia mnamo tarehe 22 Aprili mwaka 2002 Mkuu wa Utumishi alitoa Rekebisho Na. 1 lenye kumb. Na. SHC/C.180/2/152 kwa lengo la kuboresha baadhi ya masharti yaliyotolewa na waraka wa mwaka 2000. Marekebisho hayo yalihusu wagombea udiwani, wagombea ubunge wa viti maalum, ubunge wa kuteuliwa na Rais katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wagombea Ubunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Hizi ni nyaraka ambazo si za siri za serikali, ni nyaraka za wazi anazopaswa kupatiwa kila mtumishi wa umma mara anapoajiriwa. Hata hivyo, watumishi wengi wa umma, hawafahamu kuhusu nyaraka hizi na hivyo kuwafanya kutotambua haki, wajibu na mipaka waliyonayo kuhusu ushiriki wao katika siasa ikiwemo za vyama.

  Katika mazingira hayo ndipo zipozushwa hisia finyu kuwa watumishi wa umma hawaruhusiwi kushiriki kwenye siasa ama mawazo potofu kwamba watumishi wa umma wanajibika kushiriki kwenye siasa kupitia chama kinachotawala pekee. Hii ni changamoto kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, kuweza kutumia njia zote kuhakikisha waraka huu unafahamika kwa watumishi wa umma na wadau wengine wa siasa wakiwemo wananchi.

  Kila mtumishi wa umma ni muhimu akahakikisha anafahamu waraka huu ambao madhumuni yake ni kuweka utaratibu ambao pamoja na masharti yake, unazingatia umuhimu wa kuendelea kuwa watumishi wa umma nafasi ya kutumia haki ya kikatiba ya kushiriki kwenye siasa. Kwa mtizamo wa serikali, waraka huo unalenga pia kuweka mipaka ili kuepuka madhara yanayoweza kuathiri utendaji wa shughuli za umma.

  Kabla ya kufanya mapitio kuhusu yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kufanywa na watumishi wa umma katika ushiriki kwenye siasa ni vyema tukapitia kwanza misingi ya utumishi wa umma kwa kadiri ya katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali. Hii ni misingi ambayo mataifa mbalimbali wanaitumia katika kuongoza maadili ya watumishi wa umma.

  Ikumbukwe kwamba watumishi wa umma ni waajiriwa wote kamili wa serikali na taasisi zake. Hii inajumuisha Rais, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri na Mashirika ya umma, watendaji wa kata nk. Orodha hii inahusisha pia waajiriwa wa kawaida wa serikali mathalani walimu wa shule za umma, watumishi wa sekta ya afya wa serikali, maofisa wote waajiriwa wa halmashauri/serikali za mitaa nk. Watumishi wa umma ni pamoja pia watumishi wa mihimili mingine ya serikali kama mahakama kwa maana ya majaji na mahakimu na Bunge kwa maana ya wabunge na watumishi wa bunge. Watumishi wa umma ni pamoja na wafanyakazi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo askari wa majeshi mbalimbali.

  Hawa wote wanapaswa kutekeleza wajibu wao kama watumishi wa umma bila kufanya upendeleo wala ubaguzi wa chama chochote cha siasa. Wanapaswa kuwa na utii kwa serikali ya chama kinachotawala kwa kutekeleza kwa dhati na kwa ufanisi sera za serikali. Wanapaswa kutoshiriki katika mambo ya siasa yanayozuia utendaji mzuri katika vyombo vya umma(hii haimaanishi kwamba hawaruhusiwi kujiunga na vyama au kushiriki kwenye siasa). Maadili yanawahitaji kutoa huduma kwa misingi ya haki na kufanya kazi kwa hekima na uadilifu. Pia wanawajibika kutunza siri za serikali, serikali za mitaa na taasisi za mashirika ya umma. Na kwa ujumla wanapaswa kuheshimu maadili ya taaluma. Maadili hayo yamefafanuliwa vizuri katika kijitabu cha Maadili ya Utendaji katika utumishi wa umma, Tanzania kilichotolewa na Idara Kuu ya Utumishi Serikalini, mwaka 1998.

  Tunaweza kufanya tathmini na kujaza kurasa nyingi za mifano ya ambavyo maadili hayo yamekuwa yakikiukwa na watumishi wa umma wa ngazi mbalimbali kuanzia ya juu kabisa katika taifa mpaka ngazi ya chini. Kuanzia mwaka 2000 waraka huo ulipotolewa taifa limeshuhudia baadhi ya watumishi wa umma wakishiriki katika kufanya ubaguzi na upendeleo wa chama cha siasa, hususani kinachotawala. Imekuwa ni kawaida kusikia wananchi wakiambiwa na watumishi wa umma kwamba mkichagua upinzani mtanyimwa maendeleo ama watumishi wa umma wakilazimishwa kuunga mkono chama kinachotawala kwa vitisho vya kuondolewa katika utumishi wa umma. Aidha ziara za kiserikali za watumishi wa umma zimekuwa zikiingiza masuala ya kisiasa yenye kubagua na kubomoa vyama vingine. Ukiukwaji huu wa maadili umekuwa ukifumbiwa macho na Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi.

  Aidha suala la utii na kutekeleza sera za chama kinachotawala limezua mzozo baina ya serikali kuu na serikali za mitaa katika maeneo ambayo vyama vinavoongoza ni tofauti. Mathalani, wakati CCM ni chama tawala katika serikali kuu; katika halmashauri ya Karatu, CHADEMA ni chama kiongozi. Sasa kwa kuwa CCM ni chama cha upinzani katika halmashauri hiyo, watumishi wa umma katika halmashauri wanapaswa kuwa na utii kwa serikali ya chama kinachotawala kwa kutekeleza kwa dhati na kwa ufanisi sera za serikali hiyo ya CHADEMA. Hii ni katika masuala ambayo yako chini ya utekelezaji wa halmashauri chini ya mfumo wa mgawanyo wa madaraka baina ya serikali kuu na serikali za mitaa. Watumishi hao watafuata maelekezo ya serikali kuu katika masuala yanayosimamia kiutekelezaji na serikali kuu pekee.

  Pamoja na kuwa maadili yanawahitaji watumishi wa umma kutoa huduma kwa misingi ya haki na kufanya kazi kwa hekima na uadilifu katika kipindi hiki umeshuhudiwa ufisadi mkubwa na/ama matumizi mabaya ya madaraka kuanzia uongozi wa juu kabisa wa taifa mpaka ngazi za chini za utumishi wa umma. Badala ya kuwa na utamaduni wa uwajibikaji pamekuwa na mazoea ya ufisadi kwa kisingizio cha ‘kila mbuzi kula kwa kadiri ya urefu wa kamba yake’. Wakati katika kada za juu za utumishi wa umma, hali hii ikichangiwa na ubinafsi katika kada za chini hali hii imechagiwa na mishahara/maslahi duni ya watumishi wa umma. Asili ya yote haya ikiwa ni mmomonyoko wa maadili kwa ujumla wake katika taifa. Mambo haya yanataathira kubwa katika ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa na hivyo kuzalisha mfumo mpya wa ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa wa ‘nipe nikupe’ au ‘ambao ni hatari kwa mwelekeo wa taifa.

  Katika mazingira haya ya uozo wa kimaadili ndipo walipozuka baadhi ya watumishi wa umma wenye uzalendo ambao wameamua ‘kukiuka’ maadili ya kutunza ‘siri’ za serikali na kuanza kuvujisha nyaraka za kiserikali za ‘kifisadi’. Ni wazi, hakuna maadili ya utumishi wa umma yanayomtaka mtumishi wa umma kutunza siri ya serikali hata kama ikiwa ni siri ya wizi; kwani ni kosa la jinai kuficha wizi. Suala hili limezua zogo hivi karibuni bungeni mlengwa mkuu wa kuonyooshewa vidole akiwa ni Mbunge wa Karatu, Dr Wilbroad Slaa kutokana na kuwa mstari wa mbele kuzitumia nyaraka kama hizo katika mapambano ya kupinga ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa. Ni vyema watanzania wakakumbuka kuwa ni ushiriki wa namna hiyo wa watumishi wa umma wazalendo ndio uliowezesha Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini kuibua kashfa ya Buzwagi, na baadaye ikafuatiwa na Dr Slaa kusoma Orodha ya Mafisadi pale Mwembe Yanga Septemba 15 mwaka 2007. Matukio yaliyofuata baada ya hapo yakiwemo ya kuzomewa kwa watumishi wengine wa umma waliokuwa wakizunguka mikoani kukanusha tuhuma hizo za ufisadi kwa kizingizio cha kutetea uzuri wa bajeti ndio yaliyosukuma kuundwa kwa Kamati ya Bomani kuhusu Madini, Kamati Teule ya Bunge Kuhusu Richmond, Kamati Kazi(Task Force) kuhusu fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje(EPA). Kutokana na hayo taifa limeshuhudia baadhi ya watumishi wa umma wakijiuzulu, na wengine wakipelekwa mahakamani. Hata hivyo, iliweke wazi kwamba safari bado ni ndefu hivyo ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa ni jambo linalohitaji mjadala endelevu. Hivyo katika makala ijayo tutafanya mapitio ya mambo ambayo yanaruhusiwa kufanywa kwa uwazi kabisa na watumishi wa umma wanaopenda kushiriki kwenye siasa.
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  “Ruksa” kwa watumishi wa umma kushiriki siasa-4

  Na John Mnyika


  Makala zilizotangulia zimedokeza wakina nani ni watumishi wa umma na ushiriki wao katika siasa katika vipindi vilivyotangulia; wakati wa mfumo wa chama kimoja 1965 mpaka 1992 na kipindi cha awali cha mfumo wa vyama vingi 1992 mpaka 2000. Pia nilianza kufanya mapitio ya kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanzia mwaka 2000 na tunapoelekea katika chaguzi za mwaka 2009 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Katika makala hii tutafanya mapitio ya mambo ambayo watumishi wa umma wanaruhusiwa kuyafanya kama sehemu ya ushiriki wao katika siasa. Makala ijayo tutafanya mapitio ya mambo yasiyoruhusiwa kufanywa na watumishi wa umma katika ushiriki wao kwenye siasa.

  Kwa ujumla washiriki wa umma wanaruhusiwa kushiriki katika siasa. Ikumbukwe kuwa utumishi wa umma katika nchi yetu unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake. Kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kinampa mamlaka Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi kutoa waraka kuhusu taratibu mbalimbali za utumishi wa umma.

  Chini ya Mamlaka hayo, Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo akiwa Martem Y.C. Lumbanga tarehe 26 Juni, 2000 alitoa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma na. 1 wa mwaka 2000 wenye kumb. Na. SHC/C.180/2/113. Waraka huu ulihusu maadili ya Watumishi wa Umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Waraka huo ulianza kutumika kuanzia Julai Mosi, mwaka 2000.Waraka huo umetoa ruhusa kwa watumishi umma kushiriki katika mambo ya siasa na umeelekeza wazi kwamba wanaweza kushiriki katika shughuli ambazo tutazipitia katika makala hii.

  Mtumishi wa umma anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa anachokipenda isipokuwa watumishi wachache ambao wametajwa kwenye waraka huo. Tafsiri ya waraka huo ni kwamba wafanyakazi mbalimbali wa serikali na taasisi zake wanaweza kujiunga na vyama vya siasa mathalani Rais, Mawaziri, wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri na Mashirika ya umma, watendaji wa kata nk. Orodha hii inahusisha pia waajiriwa wa kawaida wa serikali mathalani walimu wa shule za umma, watumishi wa sekta ya afya wa serikali, maofisa wote waajiriwa wa halmashauri/serikali za mitaa nk. Kumekuwa na baadhi ya watumishi waandamizi wa serikali wanawakataza watumishi wa kawaida mathalani walimu kujiunga na vyama vya siasa wanavyovipenda; ni vyema ikaeleweka kwamba vitendo hivyo ni vya uvunjaji wa haki za kikatiba, kisheria na kitaratibu hivyo watumishi hao wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwa vyombo na wadau wanaohusika kwa ajili ya hatua kuweza kuchukuliwa.

  Watumishi pekee wa umma wasioruhusiwa kushiriki katika mambo ya siasa ni wale walio katika makundi ya utumishi maalum.

  Hawa ni watumishi ambao katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza wazi kwamba hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa. Ni kundi la watumishi wa umma ambao hawaruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote zingine za kisiasa isipokuwa kupiga kura tu. Ibara ya 147(3) na (4) ya Katiba imewataja Askari wa Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Polisi na Magereza. Pia Ibara ya 113A imewakataza majaji na mahakimu wa ngazi zote. Kadhalika Ibara 74(14) na (15) imewazuia wajumbe na watumishi wa Tume ya Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi.

  Pia waraka huo na. 1 wa mwaka 2000 umeyataja makundi mengine ambayo pamoja ni kuwa hayajakatazwa na katiba kushiriki kwenye shughuli za kawaida za kisiasa ikiwemo kujiunga na vyama vya siasa. Mathalani, watumishi wa idara ya usalama wa taifa, taasisi ya kuzuia rushwa(sasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-TAKUKURU), watumishi wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, watumishi wa ofisi ya bunge na mawakili wa serikali. Hata hivyo, nao wanaweza kushiriki kwenye siasa kwa kupiga kura. Hivyo, kwa ujumla, raia wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliofikia umri wa kupiga kura wanaruhusa ya kushiriki kwenye siasa ikiwemo watumishi wote wa umma kwa kupiga kura.

  Haki na wajibu huu wa watumishi wa kupiga kura unazaa ruhusa ya watumishi wa umma kuhudhuria mikutano halali ya kisiasa nje ya saa za kazi kama msikilizaji. Inafahamika kwamba wapo watumishi wa umma ambao huwatishia watumishi wao wa kawaida wasihudhurie mikutano ya kisiasa hata baada ya kazi. Utata wa ziada unaibuka hapa ni kuhusu watumishi wa umma ambo kwa asili ya kazi yao hawaruhusiwi ‘kujihusisha na shughuli za kisiasa isipokuwa kupiga kura’. Swali la kujiuliza: Je, zuio hili linahusu vile vile kuwazuia kushiriki mikutano ya hadhara ya vyama wakati wa kampeni na wakati wa kawaida kwa ajili ya kusikiliza sera ama ilani za vyama na viongozi ama wagombea? Kwa tafsiri ya kawaida; jibu ni ndio. Kama hivyo ndivyo, sasa kundi hili ina maana limepewa haki ya kupiga kura lakini halina haki ya kusikiliza ili kuweza kufanya maamuzi sahihi ya nani mtumishi husika wa umma ampigie kura? Hivyo, ni vyema waraka husika ukafanyiwa marekebisho katika eneo hili ili kuondoa utata wa tafsiri. Katiba, Sheria na Taratibu zinapaswa tu kuwakataza watumishi hawa maalumu wa umma kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa, na si kuwakataza hata kuhudhuria mikutano halali ya kisiasa.

  Pia, waraka huo umeelekeza kwamba watumishi wa umma wanapaswa kuhudhuria mikutano ya kisiasa kama wasikilizaji tu. Huku ni kuminya uhuru wa kikatiba wa kutoa maoni na wa kuzungumza. Haiwezekani ukawa na raia ambaye amepewa haki ya kujiunga na chama cha siasa lakini hana haki ya kuzungumza katika mikutano, tafsiri yake ni kwamba hana hata haki ya kuzungumza katika vikao vya wanachama. Lakini tumeona wakati wote watumishi wa umma, ikiwemo waandamizi wa serikali wakivunja kipengele hiki kwa kuzungumza katika mikitano ya kisiasa; ya ndani na hata ya hadhara. Hivyo, kifungu hiki nacho kinapaswa kufanyiwa marekebisho kwa kuwa hakitekelezwi wala hakitekelezeki.
  Waraka Na. 1 wa Mkuu wa Utumishi wa Umma pia umeruhusu mtumishi wa umma kutoa michango yake binafsi kwa ajili ya chama chake akiwa nje ya mahali pa kazi na nje ya saa za kazi. Haki hii inamaanisha kwamba mtumishi wa umma anaweza kutumiza wajibu wa kuchangia chama chake kwa maana ya kulipa kiingilio na ada ya uanachama. Hii inamaanisha pia kwamba watumishi wa serikali wa uhuru wa kuchangia rasilimali zao kwa ajili ya kufanikisha harakati za kisiasa, hii ni pamona na kuwa na ruhusa ya kuchangia wagombea katika kampeni za uchaguzi. Hata hivyo, ruhusu hii nayo ina utata wa kitafsiri kwa kuwa hakuna mali kumefafanuliwa maana ya neno ‘michango’. Kwa tafsiri ya juu juu na kwa kuzingatia mipaka ilidokezwa hapo juu ya kumtaka mtumishi husika kuwa msikilizaji pekee; tafsiri ya michango inayokusudiwa hapa inaweza kuonekana kuwa ni michango ya fedha na mali.

  Hata hivyo, ieleweke kwamba katika medani ya siasa, uzoefu wa kimataifa unaonyesha kwamba katika michakato ya kidemokrasia michango ni zaidi ya fedha na mali. Rasilimali kwa sasa zinatafsiriwa kwa upana wake kujumuisha nguvu kazi ikiwemo vipaji, utaalamu na hata mawazo. Kwa maneno mengine, michango ambayo mtumishi wa umma anaweza kutoa kwa chama chake inaweza pia kuhusisha kuchangia mawazo, kutumia muda wake, vipaji vyake na utaalamu wake. Jambo hili ni muhimu sana likatafakariwa kwa umakini wake kwa kuwa kati ya changamoto zinazokabili ujenzi wa oganizesheni ya vyama vya siasa hususani vya upinzani ni upungufu wa rasilimali watu ya kutosha yenye utaalamu mbalimbali. Kitendo cha kuwazuia watumishi wa umma, ambao kwa kiasi kikubwa wanahusisha kada ya wasomi hususani katika maeneo ya vijijini kunaacha vyama vya siasa kuungwa mkono na umma wa wananchi wa kawaida bila mchango wa kutosha wa kada hii muhimu kwa mwelekeo wa taifa.

  Katika muktadha huo, kama sehemu ya ushiriki wao katika siasa watumishi wa umma wanapaswa wakiwa nje ya maeneo ya kazi na nje ya saa za kazi kuchangia katika mwelekeo wa vyama vya siasa. Mathalani, mwalimu anaweza kabisa kuchangia mwelekeo wa kisera wa chama cha siasa kuhusu masuala ya elimu na haki za walimu. Kadhalika mtumishi wa sekta ya afya anaweza kufanya hivyo hivyo kwenye eneo lake la uzoefu. Maofisa Kilimo ama Madini nao wanaweza kutoa mchango mkubwa kutokana na utaalamu wao. Kwa ujumla kama ambavyo watumishi wa umma wanapaswa kusaidia watumishi wengine wa kiserikali wakiwa kazini ndivyo ambavyo wanapaswa kusaidia kimawazo na kirasilimali viongozi wa vyama vyao vya siasa. Yapo mambo ambayo kutokana na tofauti za kiitikadi na kisera, mtumishi wa umma anaweza akayependekeza lakini yasiweze kutekelezwa na chama kilichoko madarakani. Masuala kama hayo anaweza kuyatoa katika chama chake chenye mwelekeo anaoubaliana nayo na pindi yakiweza kutekelezwa matokeo yake yanaweza kuleta tija kwa taifa kwa ujumla. Hizi ndizo siasa ambazo zinafanywa na nchi ambazo zina demokrasia ya vyama vingi kwa muda mrefu zinazotambua kwamba siasa sio uadui bali ni mfumo wa uwagawanyaji rasilimali unaopaswa kuongozwa kwa ushindani wa hoja mbadala.


  Pamoja na kutumia fursa zilizomo kwenye waraka Na. 1 wa Mkuu wa Utumishi wa Umma kama nilivyozidokeza na haja ya kufanya marekebisho katika waraka huo ili kutoa tafsiri zinazoeleweka ni muhimu pia kuendeleza harakati za kufanya mabadiliko ya kweli katika sekta ya utumishi wa umma. Harakati hizi zinapaswa kuendeshwa na vyama vya wafanyakazi hususani wa sekta ya umma. Mabadiliko hayo ya kikatiba, kisheria na kimitazamo yatawezesha kuwa na tunu za kitaifa, misingi kamili ya haki za raia, mifumo ya uwajibakaji wa viongozi na uwanja sawa wa kisiasa. Mabadiliko hayo yatawezesha pia kujenga taasisi za kitaifa, uongozi bora na dira ya pamoja yenye kuunganisha nguvu za umma katika kupambana na ufisadi, kutetea rasilimali na kusimamia fikra mbadala zenye kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote. Taifa wananchi wanaweza kuneemeka na uwezo ambao wamejaliwa wao na nchi kwa ujumla. Watumishi wa umma wanapopigania ongezeko la mishahara na uboreshwaji wa maslahi waelewe kwamba uongozi wa kisiasa umeshikilia hatma yao. Hivyo, ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa ni suala lenye maslahi kwao binafsi na kwa taifa kwa ujumla. Watumishi wa umma Tanzania wakumbuke wosia wa Hayati Kwame Nkurumah ya kwamba ‘utafuteni ufalme wa siasa’ na yote mtaongezewa.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Good kijana.
  lakini kama ungeweka hii kitu kwenye magazeti pia, jambo hili lingekuwa jema sana badala ya kuishia JF pekee.
  WAtu bwana wanatishwa na hawajui haki zao.
  Very constructive
  kijana keep up
   
 7. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  well mh, hili suala lina onekana ni compelecated, limekua na mabadiliko mengi hila inaonekana mengi tena yanahitajika. kwa jinsi nilivyoisoma na kuzi elewa atricle zako inaonekana tatizo sio watumishi wa Umma tu kujiunga na vyama bali secta zingine za Umma inabidi ziundiwe mbinu mpya za kuongozwa independent of the ruling party just for the sake of impartiality. kwa sababu inaonekana itakua vigumu kwa baadhi ya sehemu muhimu za jamii kuendeshwa na serikali its all part of vyama vingi na capitalism ila serikali iwe kama financial supporter to.

  kitu kingine viti vya sehemu zote za utumishi wa umma especially where wajumbe wana husika inabidi vigombewe vinginevyo uonevu utatokea lakini mtu anaechaguliwa na watu na haki na nafasi yake mpaka uchaguzi mwingine.

  sehemu za law na ulinzi hawa watu ndio wawe wa kwanza kuwachiwa uhuru na vyama huko ndio visiwev na influence yeyote na viongozi wa kundi A hao ndio wasiruhusuiwe kabisa publicly nor privately to discuss party politics.
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha mada kinapotosha.

  Mnyika, tujifunze kuandika ukweli.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Fafanua tafadhali
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,310
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hongera mnyika mimi nakukubali sana...najua wewe ulishinda ubunge pale ubungo....
   
 11. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #11
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kutokana na yaliyojiri katika sakata la Baregu, nimeona ni vyema nikavuta kumbukumbu za mjadala huu na maandiko ambayo niliwahi kuyaandika siku za nyuma kuhusu suala hili.

  Mosi, kuna watu wametaka kujua maudhui ya waraka wa watumishi wa umma. Makala zangu hapo juu zimeeleza na kunukuu vifungu vya waraka husika. Kwa bahati mbaya wakati huo sikuandika makala mbili za kumalizia mjadala huu: marekebisho yaliyoongezea suala la Afrika Mashariki na makatazo yaliyopo na taratibu zinazohusika. Pia, kwa matukio yaliyojitokeza baadaye napaswa pia kuandika makala ya saba- kuhusu marekebisho yaliyofanywa na Luhanjo ya kuingiza suala la serikali za mitaa.

  Pili; naomba mnaojadili mtenganisha kati ya nafasi za ajira za kiutendaji kwenye vyama vya siasa na nafasi za uwakilishi za kisiasa ili tusiiingie kwenye mtego ambao Hawa Ghasia amejiingiza kuhusu Baregu. Ikumbukwe kwamba Baregu hajawahi kuwa mtendaji wa CHADEMA, amekuwa kwenye chombo cha uwakilishi tu. Kwa maoni yangu, nikiwa nimepitia waraka huo mara nyingi toka mwaka 2005 nilipoingia rasmi kwenye siasa waraka husika haujakiukwa. Nitaelezea nikipata wasaa.


  Naomba kwenye mjadala tujadili kwa kina yafuatayo:

  1. Je, ni kweli waraka huu unakataza watumishi wote wa umma kuwa wajumbe kwenye vyombo vya kimaamuzi vya vyama vya siasa? Kama ni kweli inakataza, kwa kuwa sasa Waziri Ghasia ameanza kutangaza kuwa wataondoa watumishi wote(kwamba sio suala la kulenga Baregu pekee) naomba tutengeneze hapa watumishi wote wa umma walioko kwenye vyombo vya vyama; iwe ni mkutano mkuu, baraza/halmashauri kuu, kamati kuu, kamati za siasa nk na iwe ni kwa ngazi zote kuanzia taifa, mkoa, wilaya, jimbo, kata na hata matawi. Na iwe ni watumishi wa umma wote, kuanzia Rais wa nchi mpaka walimu walioajiriwa na halmashauri.

  Mimi kwa kuanzia nawaweka wafuatao kwenye orodha:
  i. Rais Jakaya Kikwete- Mwenyekiti wa CCM Taifa
  ii. Waziri Mkuu Pinda-Mjumbe wa Kamati Kuu CCM
  iii. Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu, Kamati Kuu na wale ambao ni Makatibu wa NEC ya CCM ambao wao ukiukwaji wao wa waraka ni mkubwa zaidi kwa kuwa ni watendaji kabisa katika sekretariati ya CCM
  iv. Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya ambao ni wajumbe kwa kulazimishwa na Katiba ya CCM wa Kamati za Siasa
  V. Tafadhali Endeleza Orodha ukitaja majina ya watu, nafasi zao katika utumishi wa umma na vyeo vyao katika chama.

  2. Kama waraka unakataza kama anavyodai Waziri, je sheria mama Katiba ya nchi inasemaje? Je, na sheria nyingine zinasemaje? Kama waraka umekiuka katiba na sheria je; ni waraka halali? Kwa nini usifutwe?

  3. Ni mapendekezo gani tunatoa katika kuboresha utumishi wa umma kwenye siasa?

  Ps: Nawaombeni suala hili tulijadili kwa kina sana, linaweza kutizamwa kwamba ni la Baregu lakini ukweli ni kuwa linahusu mwelekeo wa taifa na linaathari kubwa sana kwa haki za kidemokrasia za raia za kushiriki kwenye siasa lakini pia linahusu uhai wa vyama vya siasa hususani vya upinzani.

  Timing ya maamuzi haya tunapoelekea uchaguzi mkuu inalenga kujenga hofu wa watumishi wengi wa umma juniors ambao wengine wameshaanza kuwaza kugombea uongozi wa kisiasa na wengine wamewaza kuunga mkono vyama kwa namna mbalimbali katika uchaguzi.

  It's a blessing in disguise kwamba Waziri Ghasia ameanzisha hii ghasia! Tujadili

  JJ
   
 12. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #12
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Katika kujadili ushiriki wa watumishi wa umma kwenye siasa ni muhimu tukatofautisha ngazi/aina mbalimbali za ushiriki:

  1. Kuna kushiriki kwa kutoa maoni ya kisiasa nje au ndani ya vikao vya vyama vya siasa
  2. Kuna kushiriki kwa kuwa mwanachama
  3. Kuna kuwa mjumbe wa vikao vya chama ikiwemo vyombo vya maamuzi vya kuchaguliwa- mathalani Kamati Kuu(hapa ndipo Baregu anaangukia)
  4. Kuna kushika nafasi za uongozi za kisiasa(Mathalani Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na ni mtumishi wa nchi kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu)
  5. Kuna kushika nafasi za kiutendaji katika chama(Mathalani Membe ni mtumishi wa Umma kwa nafasi yake ya Waziri wa Mambo ya Nje na Pia ni Katibu wa NEC ya CCM wa Mambo ya Nje kwa hiyo ni mjumbe wa Sekretariati ya CCM ambayo ni chombo cha kiutendaji)
  6. Kuna kugombea nafasi za uongozi wa kiserikali kupitia chama cha siasa(hapa mtumishi wa umma anatakiwa kuchukua likizo wakati wa kugombea na akishinda anatakiwa kuchagua kati ya kuchukua likizo ya muda mrefu ama kujiuzulu- hii ni kwa nafasi za kuajiriwa kama Ubunge nk kuepusha kuwa na ajira mbili. Lakini haihusishi nafasi za kiserikali ambazo si za kuajiriwa kama Udiwani. Hivyo technically, diwani anaweza kuwa mtumishi wa umma wakati huo huo akiwa diwani ilimradi asiwe mtumishi wa halmashauri ambayo yeye ni diwani ili kuepusha conflict of interest. Nina mfano wa Diwani Mbeya ambaye anaendelea na utumishi wake wa umma kama kawaida pamoja na kuwa wakati huo huo ni diwani wa CCM)
  7. Kuchangia chama cha siasa kwa hali na mali

  Kwa hiyo ukiangalia kwa kina ngazi/aina hizi za ushiriki, ngazi ambayo Baregu ameshiriki haikiuki sheria. Kwa sababu, kama waraka unaruhusu watumishi wa umma kuwa wanachama wa vyama vya siasa, na unawahuruhusu kuhudhuria vikao nje ya saa za kazi ama wakati wa likizo. Sasa ni vipi mtu akatazwe kuwa mjumbe wa vikao husika kama ilivyokuwa kwa Baregu ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya chama?


  JJ
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  JJ,

  Ili twende pamoja, naomba utoe ufafanuzi ili mimi labda na wanajamvi wenzangu tuelewe tunajadili. Mtumishi wa umma nini hasa?
   
 14. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #14
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Dark City

  Sehemu hii katika makala yangu ya kwanza inajibu swali ulilouliza kuhusu utumishi wa umma ni nini na mtumishi wa umma ni nani? Kwa case ya Baregu, UDSM ni taasisi ya umma ndio maana Waziri Hawa Ghasia(Menejimenti ya Utumishi wa Umma) ametoa tamko kuhusu suala lake.

  JJ
   
 15. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Angekuwa mjengoni kama alishinda,wacha propaganda!
   
 16. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ninachojua mtumishi wa umma kwa lugha kiingereza ni public service servants ambao ni permanent and pensionable. Kwa upande wa Wizara ni Katibu Mkuu hadi mhudumu wa ofisi. Upande wa serikali za mitaa ni Mkurugenzi hadi mhudumu. Hawa wote ni watumishi wa umma ambao wanaongozwa na standing orders as well as staff regulations. Hata upande wa Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, Magereza ni hivyo hivyo. Hao wote ni watumishi wa umma.

  Kuna upande wa wanasiasa. Kuanzia Rais, Spika, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wabunge, Madiwani, Wakuu wa Mikoa Wakuu wa Wilaya. Hawa ni viongozi wa kisiasa. Masharti yao ya ajira ni tofauti.

  Lakini uzoefu wa nchi hii unaonyesha inapokuja kwenye maslahi utaona wanasiasa nao wanajitambulisha kama watumishi wa umma. Mfano mzuri ni kwenye uuzwaji wa nyumba serikali. Technically waliostahili walikuwa ni wa kundi hilo la juu. Lakini inasemekana Mawaziri walikataa kuupitisha huo uamuzi kwa sababu na wao hawakuwa wanufaika.Basi lugha ikapambwa pambwa na Magufuli ambaye aliweza kumshawishi Mkapa nao wakauziwa. Lakini tuseme iliyo ya haki hawa wanasiasa hawakustahili hata kidogo.

  Suala la Baregu wala halina utata. Alichoeleza Waziri Ghasia ni sahihi kabisa. Lakini naye Baregu analia nini sasa? Mbona ana fora nyingi tu za kuwafikia watu. Hata pale Chuoni ni lazima afundishe si wanaweza kumualika na bado akapata fursa ya kuwaelimisha hao wanaotaka kumsikiliza?
   
 17. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #17
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Marigwe

  Unataka uniambia Sheria na Kanuni nilizozitaja hapo juu hazihusu Mawaziri nk? Mwendelezo wa hoja yako ni kwamba hata Sheria ya maadili ya viongozi wa umma nayo haiwahusu?

  Tunaomba nukuu ya vifungu husika ambavyo vinawandoa mawaziri, wakuu wa mikoa nk kwenye orodha ya watumishi wa umma.

  Kuhusu la nyumba ya serikali, naomba nilisilitolee maoni kwa kuwa ni mjadala tofauti kidogo

  JJ
   
 18. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Kushinda ni swala jingine na kuwa mjengoni ni jingine.
   
 19. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mie nilifikiri kuwa watumishi wa umma washaruhusiwa kushiriki siasa
  Hata hivyo excellent contents!
   
 20. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Tatizo ni kwamba wanasiasa wengi hawajui kiswahili. Kiingereza pia hawajui. Nashangaa wanaandika miswada kwa kizungu, bungeni wanaongea kiswanglish na wanashindwa kutafsiri vitu vya kimsingi kabisa.

  Sasa unapomkataza mtumishi wa umma asijihusishe na siasa ni kwa sababu ya ufinyu wako wa kufikiri kwa kina na wivu wa kijinga. Kwani kupiga kura sio siasa? Ni sayansi gani hiyo? Katiba ya nchi inasema mtu anayo haki kupiga na au kupigiwa kura. Hiyo haimaanishi mtu yuko free kufanya siasa?

  Inapofikia challange kwamba utapata washindani wanaokuzidi nguvu, unatumia nafasi uliyo nayo ya kuandika na kupayuka kuwazuia watu wasipigiwe ila wapige kura. Hapo sio kukinzana na Katiba yenye sheria mama?

  Leka
   
Loading...