Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Hoja ya msingi sana hii.
Mrunya amesha staff NCAA. Huyu jamaa ni kiazi kwa kwenda mbele. Vipi amefanikiwa ubunge wa EA ? Nilisikia anagombea.Asilimia kubwa hawana utashi wala maarifa ya kuongoza watu. Ila ndo hivyo tena...siasa na mifumo inawabeba na kuwapendelea
Tatizo lenu ni kutumia hili neno UBUNGE wakati nchi za wenzenu hutumia neno "Representative", kitu ambacho hata Zanzibar wamekifanya.
Nani alikuambia kwamba uwakilishi ni ajira? Kama ni ajira ni taasisi gani imemuajiri? Ingekuwa hivyo basi uwakilishi wowote ukiwamo uwakilishi wa kijiji au hata udiwani basi ungekuwa ni ajira.
Kuna sheria ya ajira. Sasa wawakilishi wanakuwa coverede vipi na hii. Muda wa kazi unajulikana ni masaa mangapi kwa wiki. Je, muwakilishi muda wake kwa wiki ni kiasi gani kwa kulingana na ajira?
Sheria ya ajira inaweka likizo siku 28 kama sikosei. Je huyo mwakilishi {mbunge} likizo yake ni muda gani kama ulishawahi kusikia mbunge ameenda likizo?
Hivyo, huyo dada yuko sahihi kabisa. Kama nitahitajika kufafanua zaidi basi nasubiri michango yenu.
Oh kumbe ubunge sio ajira! Ni nini basi mbona umepaacha wazi? Mama lishe ambaye anafanya kazi zaidi mara utakavyo ya isemavyo hiyo sheria yako ya ajira, hana ajira....au kwa vile hana likizo ya siku 28! Tafsiri yako ya ajira ni so narrow kama ndio hivi. Basi the unemployed ni wengi kuliko data zitolewazo!
Kabla ya kuuliza maswali zaidi jibu swali langu kwamba iwapo unadhani ubunge ni ajira basi ni taasisi gani imemuajiri?
Kabla ya kuuliza maswali zaidi jibu swali langu kwamba iwapo unadhani ubunge ni ajira basi ni taasisi gani imemuajiri?
Leo wakati anachangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira Mbunge wa Viti maalumu Mtoto wa kike wa
Mzee Kawawa alianza kuchangia kwa kudeclare interest kwamba yeye bado ni mfanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii ambao hakuutaja jina na kwa sasa tokea ameteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu (ccm) yupo kwenye likizo ndefu ya bila malipo.
kwa uelewa wangu mimi Serikali ilitoa waraka wa kuwataka watumishi wote wa umma ikiwemo watumishi wa mifuko ya hifadhi ya jamii watakaogombea ubunge na majina yao yakishapitishwa na NEC anatakiwa astaafu utumishi wa umma.
Inakuaje huyu mheshimiwa binti wa mzee kawawa bado ni muajiriwa wa mfuko huo aliodeclare interest na kwamba eti yupo likizo bila malipo.
Mi nadhani kwa uelewa wangu si sahihi anapaswa kwa maelekezo ya serikali alitakiwa awe amestaafu na sio kuwa likizo bila malipo au labda yeye ni wa viti maalumu au anaupendeleo maalumu kwa kuwa binti wa Mzee kawawa?
Naomba kujuzwa zaidi kuhusiana na hili suala labda uelewa wangu sio sahihi
Kwa Tanzania mbunge/ubunge ni AJIRA ndiyo maana wanalipwa MISHAHARA, PENSHENI baada ya kumaliza kipindi chao cha miaka mitano.
Taasisi iliyowaajiri ni OFISI YA BUNGE, Jana tumesambaziwa waraka unaonesha mishahara ya WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE japo ya WABUNGE ILIFICHWA.
Kama Ubunge usingekuwa kazi ya ajira basi ofisi ya bunge isingehangaika kuwalipa mishahara na kiinua mgongo
Mh D. Kamala alikua mbunge wa Nkenge baada ya kushindwa ubunge alirudi kwenye ajira yake ya mwanzo. mwininge ni Dk Sengongo Mvungi mwaka 2005 aligombea Uraisi kupitia NCCR baada ya uchaguzi akarudi kwenye ajira yake ya mwanzo. Wapo wengi wenye kesi kama hizo siyo huyo tu.
Oh kumbe ubunge sio ajira! Ni nini basi mbona umepaacha wazi? Mama lishe ambaye anafanya kazi zaidi mara utakavyo ya isemavyo hiyo sheria yako ya ajira, hana ajira....au kwa vile hana likizo ya siku 28! Tafsiri yako ya ajira ni so narrow kama ndio hivi. Basi the unemployed ni wengi kuliko data zitolewazo!