Ruge Mutahaba: Mr II aniombe msamaha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ruge Mutahaba: Mr II aniombe msamaha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tumsifu Samwel, Mar 12, 2010.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (T.H.T) Bw. Ruge Mutahaba amemtaka Mkurugenzi wa Deiwaka Production Bw. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu amwombe msamaha dhidi ya tuhuma zilizotolewa juu yake kuhusiana na kampeni ya Malaria No More.  Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana Mikocheni jijini Dar,Ruge Mutahaba amesema kuwa amempa Mr II masaa 72 ili aweze kumuomba msamaha/radhi dhidi ya shutuma ambazo amezisambaza dhidi yake kuhusiana na sakata hilo la Malaria No More  "Kiukweli nimeamua kuwaita waandishi wa habari ili niweke sawa haya mambo, mimi nilipewa tenda na kampuni ya Roundtrip kusimamia upande wa wasanii, jukwaa pamoja na`kusimamia mambo mengine hilo ndiyo lilikuwa jukumu langu mimi kama mimi,haya mambo mengine yanazungumzwa juu yangu sijui yanatoka wapi,hivyo namuomba Mr II aniombe radhi/msamaha kwa vyombo vile vile vya habari alivyovitumia kunidhalilisha mimi na kunivunjia uaminifu kwa jamii ninayoiongoza"alisema Ruge Mutahaba.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Hivi ni vibweka sasa!
  Mr II alisema anakwenda mahakamani huko America na akiomba msamaha ataonekana hakuwa na uhakika na alichodai.
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  CarthbertL, PJ, chanzo halisi nini hapa? Blind kabisa!
   
 4. F

  FM JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  zinduka
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,182
  Trophy Points: 280
  Ruge, utapeli ni jadi yako.
  Wewe uaminifu ni adui yake.
  Hivi wale watoto wa t. H. T wananufaika vipi na sanaa wanayoifanya?
  Wale waruka sarakasi umewakatia bima kweli au ndio bora punda afe mzigo ufike?
  Ruge ulichokifanya unakijua, na ukome kuwafanya watanzania kuwa ni mazuzu wasio na akili.
  Kwa muda mrefu tumekusoma na sasa tunakujua na kukuelewa ndani nje ndani.
   
 6. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Huu utamaduni wa kukimbilia media bado haujafanikiwa katika kutatua migogoro katika jamii, manake huwa mnaanzia katika media halafu mnaelekea mahakamani na kuishia katika visasi. Ruge mtafute Sugu mkae chini kama washkaji na kumaliza tofauti zenu mambo ya media waachieni wazee na wanasiasa.

  Manake kwa umri wenu mtakuja kununuliana bastola mpasuane vichwa.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  well said Mkuu............ushauri mzuri sana huu...........sina hakika na understanding kuhusu hii issue na wahusika wenyewe........if you know what I mean..........
   
 8. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sasa huyu ndugu yetu anataka aombwe msamaha kwa lipi haswa?
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Hebu tupeni mwanga jamani.............nini kimetokea.???
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Tulishajadili sana hii mada hapa JF, lakini kwa kuanzia mnaweza kutembelea kuanzia katika thread hii, ili kusoma kisa kizima cha Mr II na Ruge Mutahaba.

  Lakini pia habari hiyo imeendelezwa na Tanzania daima katika makala hii.
   
 11. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wa mjini wala hawakushangaa kwa maana ndo zake, anasubiri wenzie wapike ye anakuja kupakua tu. kaka noma!
   
Loading...