Hili ni swala la kisheria na mambo yakuombeana mungu hayana nafasi sana hapa. Kila mtu ahukumiwe kwa kosa alilofanya na kwasheria zilizopo. Kwakua mahakama ndio chombo cha kutafsiri na ksuimamia sheria, na kwakua mahakama nma hakimu Lyamuya na Jaji Mihayo wote waliamini hawa watu walitenda vitendo hivi viovu dhidi ya watoto wetu, binti zetu, waaalimu na madaktari wa kesho basi lazima waendelee kuwajibika
Ni vigumu kuamini watu hawa baba na watoto wamefanya hili jambo kwa pamoja, ila kwakua nalo ni vigumu kuamini mtu mzima kubaka na kulawiti katoto ka miaka mitatu, na kwakua hii imekua ikitikea, basi binafsi nakila sababu katika ugumu huo huo kuamini mahakama imesimama ktk ukeli.
Jiweke ktk nafasi ya mzazi ambae mwanae alifanyiwa hivyo na utajua ungekua na nafasi kuinfluence hukumu hii ungefanyaje .
Yetu macho
Tuache hayo, leo ni leo, rufaa yake inaanza kusikilizwa, nataka maoni, je tumuombee ashinde rufaa yake ajiunge nasi uraiani au ashindwe aendelee kuozea jera?!, ni vyema basi tuwe na sababu.
hata sisi ni wazazi na tuna uchungu sana tatizo hatujui ukweli umesiamamia wapi ???
Babu Seya na watoto wake Watatoka.
FirstLady
kama mahakama ndicho chombo tunachokiamini kusimamia haki na tafsiri ya sheria, ni nani basi mwingine unataka aje atueleze ukweli. Je si vielelezo na ushahidi ulitolewa wakati wa kesi. Ni kweli kwamba unataka tuambia wanakuburudisha kwa music kiasi kwamba hata wakiwalawiti wanao unawaonea huruma?
Tuziamini mahakama zetu maana wao ndio tumewapa dhamana ya kusimamia sheria. Binafsi sitegemei kuona lolote geni kutoka kwa Jaji Natalia Kimaro wala Massati kwenyr hili maana najua watasimamia misingi tya sheria na sheria ni ile ile ilotumika na wenzao kuwafikisha hapo walipo.
Hivi hawa watu hawawezi kunyonga? Mahakama hii hiawezi kuwaongezea adhabu? au maana ya rufani ni kupunguza adhabu ya awali?
Naomba msaada kisheria
Hivi hata kama mnapenda ngono kiasi gani, baba anaweza kufanya hivyo mbele ya watoto kweli?, na kama kweli kafanya hivyo iweje wananchi watake kuandamana kwa ajili yake? kwani ni wangapi wamefungwa kwa ajili hii na wananchi wako kimya?
hapa ni lazima kuna kitu, na mkitaka kupata ukweli fuatilia magazeti ya leo jioni (kwa wale walioko Dar) yatauzwa sana kwa ajili yake, hapo hampati jibu kweli?
kama ZOMBE alitoka hawa nao watoke.
MIAFRIKA NDIO TULIVYO
Sio suala la kujuta, kwa wanaofuatilia rufaa yao, ukweli uko wazi,