Rufaa Igunga: Kafumu atofautiana na CCM

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Wakati aliyekuwa mbunge wa Igunga Bw Dalaly Peter Kafumu amesema hatakata rufaa kupinga hukumu iliyotengua "ushindi" wake wa ubunge, chama chake kupitia kwa Mwigulu Nchemba kimesema kitakata rufaa hiyo. Mwigulu amesema hivyo kwenye mikutano ya chama hicho inayoendelea jimboni Igunga wakati Kafumu ametoa tamko hilo alipohojiwa na Star Tv.

Source: Star Tv Habari.

My take: Mambo si shwari ndani ya ccm maana tangu Mwigulu aanze mikutano yake Igunga, Kafumu hajawahi kuonekana.
 
Chama kilimwacha solemba mpaka akashindwa sasa hv ndo wanajidai kukata rufaa.Akina magufuli hawakweta kumtetea,anaona aachane na siasa uchwara za magamba
 
Chama kilimwacha solemba mpaka akashindwa sasa hv ndo wanajidai kukata rufaa.Akina magufuli hawakweta kumtetea,anaona aachane na siasa uchwara za magamba

na kama walimtosa katika kesi, hawaoni wanakumbuka shuka kumekucha?
 
Hata mimi ningekuwa Dr.Kafumu ningekataa. Kwanini CCM hawakumlazimisha Mh.Magufuli afike mahakamani wakati alipohitajika? Pia walimuharibia sana kwa kugawa mahindi ya njaa, kuwatishia wananchi kwa bastola, kuwababmbikizia wananchi kuchoma kibanda cha kuku na karatasi kusalimika, kuahidi uongo daraja la Mbutu, kuwachukulia makada wake zao nk. Hata mimi nisingependa uchonganishi kama huu utokee tena. Nampongeza sana Dr. Kafumu.
 
Mhusika mkuu Kafumu ameridhika na hukumu. CCM inata rufaa kama nani? Wanatapatapa waache waendelee kujimaliza hata kabla ya kipenga cha 2015.
 
Walishachemka. Kafumu anakwepa aibu ya pili, CCM wanataka kumtumia kama human shield ya aibu waliyoipata kwa ulaghai wao.
 
Hata mimi ningekuwa Dr.Kafumu ningekataa. Kwanini CCM hawakumlazimisha Mh.Magufuli afike mahakamani wakati alipohitajika? Pia walimuharibia sana kwa kugawa mahindi ya njaa, kuwatishia wananchi kwa bastola, kuwababmbikizia wananchi kuchoma kibanda cha kuku na karatasi kusalimika, kuahidi uongo daraja la Mbutu, kuwachukulia makada wake zao nk. Hata mimi nisingependa uchonganishi kama huu utokee tena. Nampongeza sana Dr. Kafumu.

mkuu, pointi hii ya kugawa mahindi ndio anayotamba yano mwigulu nchemba kulalamikia cdm eti hawana utu sababu watu wenye njaa wamesaidiwa, wao wametumia msaada huo kupokonya mtu ubunge. anatamba majukwaa ya Igunga now akihubiri kuwa chadema hawana utu kwa kutaka watu wafe na njaa
 
Mhusika mkuu Kafumu ameridhika na hukumu. CCM inata rufaa kama nani? Wanatapatapa waache waendelee kujimaliza hata kabla ya kipenga cha 2015.

nadhani wanafanya delaying tactic ukizingatia kuwa huenda sumbawanga uchaguzi ukafanyika soon, wasijikute wamepoteza majimbo mawili kwa mpigo bora wadondoshe moja baada ya jingine kwa kujipa muda
 
mkuu, pointi hii ya kugawa mahindi ndio anayotamba yano mwigulu nchemba kulalamikia cdm eti hawana utu sababu watu wenye njaa wamesaidiwa, wao wametumia msaada huo kupokonya mtu ubunge. anatamba majukwaa ya Igunga now akihubiri kuwa chadema hawana utu kwa kutaka watu wafe na njaa

mahakama pia ni ya chadema? maana ndiyo iliyotoa maamuzi. jamani tuwaelimishe ndugu zetu wasirubuniwe ili kazi ya ukombozi iwe rahisi. wasiwasi wangu ni kwamba baadhi ya watz hasa wa vijijini kwa uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo huwa wanaamini upuuzi huo.
 
Inawezekana huyu msomi aliteleza kama mwanadamu tu, kisha akajiingiza mkenge kwenye siasa.

Lakini kama msomi na binadam huenda sasa ametambua kosa lake na kujifunza.

So asihangaike na hao wahuni kama akina Nape na Mwigulu. Asimamie ukweli na pia aikubali dhamiri yake kisha akae pembeni. Of coz ajiuguze kisha akipona aende kwenye fani yake ya madini na miamba.
 
Unlike those certain grabbers; life is always full of enjoyment and oportunities to all.
But for some creatures of doubtful origin whose breed so populate CCM.....life is an utter miserable and should be kept as such.

I will like if they (CCM as an institution) appeals. They have everything to loose there.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom