Ni kwenye rufaa tu!Yule aliyeanzisha kesi au yule aliyeshtakiwa NDIYO TU WANAOTAKIWA KISHERIA WAENDELEE NAYO KWENYE HATUA YA RUFAA!Kwa mfano waliomshtaki LEMA wangeshindwa kesi Mama BATILDA asingeweza KUKATA RUFAA hata kama angependa kufanya hivyo maana HAYUMO KWENYE ORODHA YA WASHTAKI na yy aliitwa kama SHAHIDI TU!
Jaji Rwakabalila aliyemvua LEMA ubunge aliongelea chochote kwenye kipengele"cha haki ya mtu asiyegombea ubunge kushtaki kulalamikia uchaguzi ili hali yeye HAKUWA MGOMBEA?Wakili wa LEMA aliweka pingamizi kuomba mahakama iifute kesi kwani Mama Batilda mwenyewe HAJALALAMIKA KAMA ALITUKANWA?Zilionyeshwa hata DVD zozote za LEMA akitukana?
Tuache mahakama ya rufaa iamue lkn mm tayari NIMENUSA KITU!
Kuna kitu ambacho nimekuwa najiuliza kwa muda sasa. Hivi mtu anayekuwa amekashfiwa si ndiye anayekasirika na anayetakiwa kufungua lalamiko? Sasa iweje mtu mwingine achukue umamuzi wa kufungua mashtaka na hata aliyekashfiwa asifike mahakamani kutoa ushahidi?
Maana hata mwanao akikashfiwa huwezi sema unakwenda fungua mashtaka? Labda kama amepigwa na kuumizwa na kukawa na ushahidi wa daktari.
Ndiyo maana hili la Lema lilinishinda kabisa kuelewa. Ama kwa hakika Mh. Tundu Lisu Taifa linamhitaji sana, tena tunahitaji wawepo wengi zaidi.
Kuna jambo pia hunishangaza sheria ya uchaguzi haiweki wazi kuwa Vyama vya siasa vinatakiwa vipate kibali kwa Polisi ili kufanya maandamano, lakini sheria nyingine inayokinzana nayo inawapa Polisi ruhusa ya kutoa au kutotoa kibali cha maandamano. Ama kwa hakika tabia zetu zinajionyesha wazi hata kwenye sheria za nchi.