Rubani auchapa usingizi ndani ya ndege

Eidj5

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
504
419
Kwa ufupi,

Ndege hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 305 ikisafiri kutoka mji mkuu wa Pakistan, Islamabad kuelekea London, Uingereza.

Rubani auchapa usingizi ndani ya ndege, azua tafrani
Islamabad, Pakistan. Abiria waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Pakistan (Pia) waliingiwa taharuki baada ya kugundua kuwa rubani wa ndege hiyo alikuwa ametoka katika chumba chake na kuelekea sehemu nyingine kulala.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 305 ikisafiri kutoka mji mkuu wa Pakistan, Islamabad kuelekea London, Uingereza.

Rubani huyo, Amir Akhtar Hashmi anadaiwa kumwacha rubani mwanafunzi katika chumba cha kuongezea ndege na kwenda katika moja ya sehemu za abiria ambako alijifunika blanketi na kulala.

Tukio hilo lilitokea muda mchache baada ya ndege hiyo kuanza kuruka.

SOURCE:MWANANCHI
 
kwa jinsi sheria za aviation zilivyo kali pamoja na sheria mbalimbali za makampuni ya ndege, huenda ukawa mwisho wa carrier ya huyu rubani...
upload_2017-5-11_17-38-0.jpeg
 
Atakuwa alikuwa na hangover,
nakumbuka hata mimi kipindi nakunywa pombe,
nilikuwa nikifika joob ile saa mbili asubuhi niko hangover mbaya,nafika napanga kazi naset wasimamizi kisha najifungia ofisini nauchapa usingizi,siamshwi mpaka waniamshe kupata supu,ama nitafutwe na bigboss au
ifike saa tano za asubuhi sasa ndo naanza kuchapakazi
 
Back
Top Bottom