RPC Mtwara hatakiwi kuwa kazini kwa uzembe aliofanya

Kumbe move aliyofanya RPC ni baada ya vigogo kukomalia ishu, basi hiyo syndicate nzima inabidi waingizwe..........inasikitisha sana polisi kuwa sehemu ya uhalifu kwenye jamii. Nilishasema humu, reform kubwa ifanyike jeshi la polisi kwa kuanza na recruitment ya graduates wenye first degree ili kujenga zaidi weledi wa kiutendaji...........saa hivi graduates wenye first degree wamejaa mtaani hawana ajira, kwa nini tusiwachuke hawa wapate mafunzo ya uaskari.
Mkuu huko Polisi wapo wenye degree na ni wapumbavu wakubwa tu. Transformation ni zaidi ya kuwa na graduates. Tunahitaji kuundwe chombo huru kitachoisimamia Polisi, pia wapunguziwe majukumu. Fikiria Polisi huyohuyo akamate, achunguze, atoe ushahida. Kuna kitabu nimekisahau jina, kilitoa mapendekezo mazuri mno juu ya mageuzi ya Jeshi la Polisi nchini. Bahati mbaya si taifa la watu wenye kusoma, kuanzia watawala wenyewe na watawaliwa.
 
RPC aunganishwe kwenye kesi, Waziri na IGP waachie ofisini na wasipofanya hivyo, Mama anapaswa kuwatumbua...tuache kulea uzembe.
 
Hatuna majeshi ndugu zangu, sio polisi, uhamiaji, jw nk Ni vile tu hatujawahi pata changamoto za kiusalama kama wenzetu Kenya na Uganda.
Usiombee changamoto za kiusalama ziwe kama za wenzetu ila kumbuka kuwa serikali inatumia gharama kubwa kuilinda amani hii iliyopo na haya mambo wanayofanya baadhi ya watumishi wa idara hizo yasikupelekee ww kutoa kauli nzito na tata kuhusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.Kila kitu kinacho fanyika hapa ni kwa sababu ya amani iliyopo,kuwa mzalendo sana kwa nchi yako,hayo mambo yanayo tokea ni changamoto tu za kiutendaji tu
 
Moja ya kituko jeshi la polisi ni kua RPC alikua anashiriki kuwaokoa wauaji lakini mbele ya safari watu wakubwa nchini wakakomalia issue na kwa aibu akapiga U turn.

Yule RPC kimaadili hatakiwi kuendelea kuwa RPC hata kwa dakika tano maana nae ni mtuhumiwa na uchunguzi ufanyike haraka apate stahiki yake.

Jeshi la polisi hasa IGP inabidi uchukue hatua kali dhidi ya msaidizi wako huyo wa mkoani Mtwara ili haki itendeke.

Kuna askari waadilifu kwenye jeshi la polisi lakini kuna askari ni majambazi wakubwa ndani ya jeshi la polisi yaani kula rushwa wanaona haitoshi wanaamua kuteka na kuua raia wema.

Kama walinzi wanaiba hii ndio mwanzo wa hali mbaya ya usalama nchini.

Pia soma
Acha jazba, tulia kabla ya kupost.
 
ZOMBE yupo mahali anacheka tuu........inatia hasira.......na huyu chui JIKE yuko ziarani kuvishwa U-Chief.....kweli wanasema pata fedha au pandishwa cheo tujue TABIA zako........hawa polisi hawa inabidi tuanze kuwafyatua kimya kimya....
 
Yule RPC kimaadili hatakiwi kuendelea kuwa RPC hata kwa dakika tano maana nae ni mtuhumiwa na uchunguzi ufanyike haraka apate stahiki yake.
 
Back
Top Bottom