RPC Mbeya, Kamanda Msangi azuia maandamano ya kumpokea Lowassa

RPC Mbeya, Kamanda Msangi azuia maandamano ya kumpokea Lowassa

kama vip wana nchi wajipange pembeni mwa barabara ili wamuone rais wao lowassa!!
 
Asante kamanda Msangi...mwenye kusikia na amtaarifu mwingine

Ccm mafuriko yamewafika shingoni mapema sana hadi mmepanic.
Team ya Bensuda imetumbua macho inatazama kila ukiukwaji unaofanywa na serikali ya ccm inayodondoka.
 
Kwani nani kamwambia tunaandamana?
 
Mbona Magufuli hakuwekewa utaratibu wa aina hii? haya mambo ndiyo yanalalamikiwa kila siku. Jeshi la polisi haliwezi kuwa na double standard kiasi hicho kisha likaaminiwa. Ni wiki mbili tu tangu mgombea wa CCM amezunguka mikoani huku akilakiwa kwa maandamano makubwa, lakini hatukusikia yote haya. Leo wamesikia EL anafanya hivyo vikwazo tayari kila mahali! Tuweke uwanja sawa kwa wagombea wote si kumpendelea mgombea mmoja.
 
Magufuli akiwa anaandamana kwenye hizo barabara inamaana watumiaji wa hizo barabara wanakua wamelala au?
Je mnajua kuwa Msangi hichi cheo amepewa kina husiana na Ulimboka saga?
 
Intelligence ya Tanzania Police ipo juu sana katika suala la maandamano. Nahisi world wide tutakuwa top 3
 
Hawa WATANZANIA wanaolalamika kuwa maandamano yanawazuia kufanya shughuli zao ni wa nchi ipi? Nadhani ni wale wanaofanyia kazi zao ikulu? Sasa camping zikianza itakuwaje?
 
Mwenye kuelewa na kusikia siddhan Kama ataacha shughuli zake kisha aende kufikinya macho,tunashukuru jeshi la Polisi inadvance kumbe dola mpo macho,kwani siasa zisiharibu Amani kisa ati Watu waandamane tu tanzania bado twajitambua hatujafikia huko
 
Wamekwisha hao, hata watu wakienda mkutanoni wataonekana wanaandamana mana watakua wengi, cjui nini dhana ya maandamano.
Labda wanapelekewa helikopta za kuwashusha uwanjani moja kwa moja uliza vizuri ujulishwe
 
Tusishangae polisi wakizuia mikutano na maandamano wakati wa kampeni. Tanzania ni yetu sote,polisi tekelezeni wajibu wenu kisheria,acheni kujipendekeza kuwafurahisha CCM
Kweli kabisa tanzzania yetu sote hata wanaopata taby na kusimamisha shughuli zao sababu ya maandamano ni watanzania poa
 
Jipangeni pembezoni mwa barabara tu kumpokea mgeni wenu. Wengine nendeni uwanjani kwenye mkutano.
 
In short, MENTALLY STUNT.

Nampongeza kamanda Msangi.Misafara ya kisiasa ya maandamano barabarani inazuia shughuli za kuchumi.Jana mabasi toka Moshi,Arusha na Nairobi kwenda Dar es SALAAM yamechelewa kufika sababu ya msafara wa maandamano wa LOWASA na maboda boda yake ya kukodi yaliyokuwa yametanda barabara zima.Mabasi yalikuwa hayawezi ku-overtake YANAZOMEWA na vibaka wa BODA BODA waliokuwa msafara wa Lowasa.

Kamanda msangi ana hoja barabara ziachwe wazi zifanye shughuli za kiuchumi watu waende huko kwenye mikutano yao ya kisiasa waache watu waendelee na shughuli za kiuchumi.Anayependa kwenda mkutanoni aende na anayependa kuendelea na shughuli zake kama za daladala nk aendelee na kazi zake bila bughudha kutoka kwa waandamaji kwenye barabara.

Ombi langu ni kuwa wanaporudi pia kwenye hiyo mikutano wasirudi na maandamano tena ya kuleta siasa mabarabarani na kuanza kupora watu na maduka.Mihemuko yao ya kisiasa iishie huko huko mikutanoni kwao wasianze kurudi kimakundi na michaka michaka na kufanya vurugu na kupuliza mahoni ya bajaji nk.Wamalize mikutano yao kwa amani watawanyike kwa amani waende kama ni boda boda warudi sehemu zao za kazi waendelee na maisha yao.

Hongera kamanda Msangi
 
Back
Top Bottom