Huu ujinga tunaouendekeza utakuja kutuponza, na hapa ndio huwa nauona ukweli wa nadhatia ya doctor watson, akili za mtu mweusi ziko chini kupita maelezo, hivi hawa maRPC wameahidiwa nn kiasi kwamba wanashawishika kutoa amri za kijinga kama hizi?! Si mgombea wa ccm tumemuona huko mikoani akitambulishwa na shamra shamra hizo kupambwa na maandamano?! Tena kwa ulinzi mzito wa polisi! Sasa kuzuia upande wa pili wananaana gani?! Ukitaka kufuga ngombe lazima ukubali kushughulika na kinyesi chake!
Huu ni ushahidi tosha wa uelewa mdogo wa watu wanaopewa dhamana katika ofisi mbalimbali! Sijui sheria za kipolisi but common sense inaonesha kabisa hili si jambo jema na linaweza kuleta vurugu zisizokuwa za lazima, kwann tusiwe wavumilivu na kusubiri sanduku la kula liamue mambo?! Hivi hatujifunzi kwa nchi za jirani?!
Wewe unayetoa order kama hizi ebu fungua macho na uone umbali mrefu zaidi ya urefu wa pua yako, tukiingia katika machafuko uwe na uhakika kuna jamaa wengi tu wa ukoo wako kama sio familia ambao watadhurika ma machafuko hayo! Ebu tuache ubinafsi na tuvifikirie vizazi vilivyo chini yetu, watoto wetu, wajukuu wetu....waliopo na ambao hawajazaliwa bado!
Kuandamana ni haki ya kikatiba ya watanzania wote, watanzania hawa wameshajeruhiwa saana na ugumu wa maisha, tafadhari! Msiache mwaka huu watanzania waumalize kwa kufungua kwa sura ya machafuko na mahangaiko ambayo yako ndani ya uwezo kuyatatua. Taifa kwanza!
Ujumbe kwa maRPC wote, akili itumike ili mje mjiachie legacy siku za mbeleni.