Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,379
PowerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrPiiiiipooooooozzzzzz
PowerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrPiiiiipooooooozzzzzz
Breaking news!!!
Mr. Paul Matemu katibu wa fedha na mchumi wa Ccm mkoa wa Kilimanjaro na Mr. Fredrick Mushi Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro. Wamejiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama kwa kutoridhishwa na utendaji mbovu wa CCm. Na kujiunga rasmi na CHADEMA. Wakiungwa mkono na wanachama 200. Received
Haya bwana, sasa Lowasa kaanza kuwatisha hata kabla ya kuanza campaign.
Bado police kupiga marufuku live broadcasting ya mikutano ya siasa kwenye Tv
Miye natoa kaushauri kadogo tu:
Kwa kuwa, hata siku zilizotolewa kupiga kampeini ni chache saana, na kwa kuwa, hatutaweza kupiga kameni kimya kimya bila watu kufika kwenye viwanja na kuondoka kwenye viwanja kwa makundi.
Na kwa kuwa, hawa viongozi na haswa wa upinzani wanaungwa mkono na hao watu ambao policcm wanawaona kwenye intelijensia yao kuwa ni vibaka wote, na kwa kuwa hao vibaka tu ndo wanaenda kwenye hiyo mikutano ya upinzani
Nashauri; Mikutano ya kampeni ikome tupewe nafasi kwenda kupiga kura kesho asubuhi bila kameni.
Aruhusiwe raisi aliyeko madarakani kuamua hili jambo aitishe uchaguzi HARAKA TENA BILA KUCHELEWA. Aksanteni kama mtaunga mkono
sasa hao watu wakati wa kwenda au kutoka kwenye mkutano watatembea vipi?maana watu ni wengi kwa mfano pale Arusha barabara ya kwenda kwenye mkutano ni moja sasa watawezaje kujitenga isionekane kama ni maandamano? polisi waeleze wazi jinsi watu watakavyotembea wakati wa kwenda na kutoka kwenye huo mkutano
Wamekwisha hao, hata watu wakienda mkutanoni wataonekana wanaandamana mana watakua wengi, cjui nini dhana ya maandamano.
Hapa Arusha kukataza maandamano Lowasa atakapokuja ni sawa na bure labda wamkataze asije
Huu ujinga tunaouendekeza utakuja kutuponza, na hapa ndio huwa nauona ukweli wa nadhatia ya doctor watson, akili za mtu mweusi ziko chini kupita maelezo, hivi hawa maRPC wameahidiwa nn kiasi kwamba wanashawishika kutoa amri za kijinga kama hizi?! Si mgombea wa ccm tumemuona huko mikoani akitambulishwa na shamra shamra hizo kupambwa na maandamano?! Tena kwa ulinzi mzito wa polisi! Sasa kuzuia upande wa pili wananaana gani?! Ukitaka kufuga ngombe lazima ukubali kushughulika na kinyesi chake!
Huu ni ushahidi tosha wa uelewa mdogo wa watu wanaopewa dhamana katika ofisi mbalimbali! Sijui sheria za kipolisi but common sense inaonesha kabisa hili si jambo jema na linaweza kuleta vurugu zisizokuwa za lazima, kwann tusiwe wavumilivu na kusubiri sanduku la kula liamue mambo?! Hivi hatujifunzi kwa nchi za jirani?!
Wewe unayetoa order kama hizi ebu fungua macho na uone umbali mrefu zaidi ya urefu wa pua yako, tukiingia katika machafuko uwe na uhakika kuna jamaa wengi tu wa ukoo wako kama sio familia ambao watadhurika ma machafuko hayo! Ebu tuache ubinafsi na tuvifikirie vizazi vilivyo chini yetu, watoto wetu, wajukuu wetu....waliopo na ambao hawajazaliwa bado!
Kuandamana ni haki ya kikatiba ya watanzania wote, watanzania hawa wameshajeruhiwa saana na ugumu wa maisha, tafadhari! Msiache mwaka huu watanzania waumalize kwa kufungua kwa sura ya machafuko na mahangaiko ambayo yako ndani ya uwezo kuyatatua. Taifa kwanza!
Ujumbe kwa maRPC wote, akili itumike ili mje mjiachie legacy siku za mbeleni.
Nampongeza kamanda Msangi.Misafara ya kisiasa ya maandamano barabarani inazuia shughuli za kuchumi.Jana mabasi toka Moshi,Arusha na Nairobi kwenda Dar es SALAAM yamechelewa kufika sababu ya msafara wa maandamano wa LOWASA na maboda boda yake ya kukodi yaliyokuwa yametanda barabara zima.Mabasi yalikuwa hayawezi ku-overtake YANAZOMEWA na vibaka wa BODA BODA waliokuwa msafara wa Lowasa.
Kamanda msangi ana hoja barabara ziachwe wazi zifanye shughuli za kiuchumi watu waende huko kwenye mikutano yao ya kisiasa waache watu waendelee na shughuli za kiuchumi.Anayependa kwenda mkutanoni aende na anayependa kuendelea na shughuli zake kama za daladala nk aendelee na kazi zake bila bughudha kutoka kwa waandamaji kwenye barabara.
Ombi langu ni kuwa wanaporudi pia kwenye hiyo mikutano wasirudi na maandamano tena ya kuleta siasa mabarabarani na kuanza kupora watu na maduka.Mihemuko yao ya kisiasa iishie huko huko mikutanoni kwao wasianze kurudi kimakundi na michaka michaka na kufanya vurugu na kupuliza mahoni ya bajaji nk.Wamalize mikutano yao kwa amani watawanyike kwa amani waende kama ni boda boda warudi sehemu zao za kazi waendelee na maisha yao.
Hongera kamanda Msangi
Ni moja kati ya mawili.....hujawahi kukaa kwenye foleni ya kupisha misafara ya viongozi. Au mahaba yamekupofua fikra. Kikwete hata hajatua airport, huku barabara zote zimeshafungwa. Hiyo theory yako ya 'dakika tu' una-derive toka wapi? Walisemaga wahenga....''mapenzi ni upofu''. Punguza mahaba mkuu.Wacha uongo.Yule ni kiongozi wa nchi.Anatanguliwa na pikipiki moja.Sio boda boda 300 AU kama lowasa.Msafara wake unaende spidi ya kuua mtu KIASI KUWA DAKIKA TU NJIA INAKUWA NJEUPE.Hauendi taratibu kama wa Lowasa ambao kutoka biguruni tu hadi posta mpya kufika unatumia masaa matano mazima!!!!.