Routes za daladala zilizoleta mapinduzi DSM

Routes za daladala zilizoleta mapinduzi DSM

Bado zimebaki nyengine ambazo zilikuwa sumbufu angalau sikuhizi naona kidogo afadhali
MBAGALA - UBUNGO
MBAGALA - G/MBOTO
MBAGALA - GEREZANI VIA KILWA ROAD
Hizo route zote asubuhi au jion asee hazishikiki....
 
Mambo ya route kuanzishwa nmemkumbuka mwaibula
Sjui huyu mwamba yuko wapi sahvi

Ova

Huyu ndie aliboresha ruti kwa ubunifu wa hali ya juu. Zamani ilikuwa lazima uende Kariakoo au Posta ili ufike unapotaka
 
Ndio nani huyo mkuu??
Mkuu Kama sio under 21 basi ulikuwa kijijini na mjini hauna muda.

Anyway Mzee David Mwaibula alikuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya leseni za usafiri was daladala Dar es salaam (DTLA) kabla kuundwa SUMATRA. Alibuni ruti nyingi za pembeni pamoja na upakaji rangi mistari ya ruti.

Mzee aliboresha Sana usafiri wa daladala hapa mjini. Kabla ruti zote zilielekea Posta na Kariakoo.

m7.jpg
 
Jamani Tufufue hii mada, mtusaidie sisi wageni wa huu mji kuelewa baadhi ya ruti maana siku mbili hizi nimesimama zaidi ya masaa mawili kila kituo kusubiria gari za kutoka sehemu moja kwenda ingine kisa sijui kama kuna ruti ingine inayoweza kufanya nifike niendako hata kama itakuwa ni gari zaidi ya mbili
 
Ungesema unaenda wapi na umesimama wapi upewe mwongozo
Smart911
 
Ungesema unaenda wapi na umesimama wapi upewe mwongozo
Smart911
Natokea kivule shuleni naenda ubalozi wa marekani, njia nayotumiaga ni kivule banana kwa bajaji then banana nasubiri gari za kawe au masaki, but naona hii inanifanya kilasiku nikae banana karibu lisaa na zaidi kwani gari zinapita zimejaa na hazisimami
 
Hapo Banana panda zinazoenda Gerezani au Mnazi mmoja...
Kariakoo zipo za Masaki unashukia Namanga unaelekea Ubolozi wa marekani...

Posta unapanda za makumbusho au Tegeta, unashukia Mbuyuni au Morocco unatembea mpaka Ubolozi wa Marekani...
aise

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom