Zambotti
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 1,983
- 3,669
Kwa wale watumiaji wa usafiri wa daladala wenzangu mtakuwa pamoja nami, hususani wale ambao harakati nyingi na mizunguko ya hapa na pale katika kutafuta tonge la siku zinategemea matumizi ya usafiri huu.
Wakati fulani kuna maeneo usafiri wa daladala ulikuwa mtihani kabisa katika baadhi ya maeneo, yalikuwa hayafikiki kwanza kwasababu ya miundombinu yake lakini pia umbali wake kutoka katikati ya mji.
Kwangu mimi routes zifuatazo zimeleta mabadiliko makubwa na kulifanya jiji la DSM kuwa jepesi kufikika kutoka eneo moja kwenyda jengine lakini pia kutoka katikati ya mji kwenda maeneo husika.
1.GEREZANI TO KISEMVULE VIA KILWA ROAD
Route hii ya daladala imerahisisha usafiri wa kutoka mjini kuelekea ndanindani ya maeneo ya mbagala kuanzia mbande, maji matitu mpaka huko kisemvule.
2.TEMEKE TO MBEZI VIA BUZA, KINYEREZI MPAKA MARAMBA.
Ebhana hili ni bonge la route ambalo kwanza ni linaua tabu ya usafiri wa maeneo kama vile malamba mawili na huko kinyerezi nauli yake ni 750, aliyebuni hii njia roue yuko vizuri sana.
3. CHANIKA TO SEGEREA
Hii route tangu niione haijawahi kuwa rahisi kila niionape magari yake yako mtiti maana yake kipengele hiko kilikuwa na uhitaji mkubwa wa usafiri.
4. TEMEKE STEREO TO TOANGOMA VIA KONGOWE
5. T/NYUKI - KKOO
6. MBEZI TO M/MBUSHO VIA GOBA
Duhh siku ya kwanza kupanda hizi daladala sikuamini kama zitapita eneo nnalolitaka maana ziko complicated kidogo lakini ndo maendeleo yenyewe, wako vizuri eti.
Hizi kwangu ni route za daladala ambazo kwa namna moja ama nyengine zimekuja kuondoa kero ya adha ya usafiri DSM.
UNAWEZA ONGEZA ZA KWAKO MKUU, KUSIFIA SI JAMBO BAYA..MAENDELEO HAYANA CHAMA..