Rostam sasa awaita akina Selelii "wapuuzi" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam sasa awaita akina Selelii "wapuuzi"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Nov 20, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 10,894
  Likes Received: 3,275
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz (CCM) ameeleza kusikitishwa na kushtushwa na hatua ya kundi la wabunge kupinga hatua yake ya kutaka tume huru au majaji kufanya uchunguzi upya kuhusu sakata la Richmond.

  Hatua hiyo ya Rostam imekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya wabunge watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupinga hoja yake inayoonekana kutaka kuingilia maamuzi ya Bunge.

  ‘‘Hawa ni wapuuzi, wanasukumwa na chuki,” alisema Rostam alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli za wabunge hao; Aloyce Kimaro (Vunjo), Lucas Selelii (Nzega) na James Lembeli (Kahama).

  Mbali ya hilo, mbunge huyo wa Igunga ambaye jina lake lilitajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata wa mkataba kati ya Shirika la Umeme (TANESCO) na Kampuni ya Richmond Development Company LCC alisema hoja zinazomhusisha yeye na umiliki wa mitambo ya Dowans ndizo zilizoliingiza taifa katika tatizo la giza leo hii.

  “Kwa hali ya kawaida miye si wa kujibizana na watu wa aina ya Kimaro... ni kudhani kwao Dowans ni yangu ndo kumepeleka nchi kuingia gizani. Aibu,” alisema Rostam ambaye alilieleza Tanzania Daima kuwa alikuwa yuko nje ya nchi.

  Rostam ambaye kwa mara ya kwanza aliwasilisha hoja ya kutaka kuundwa kwa tume huru au ya majaji ndani ya kikao cha maridhiano kati ya wabunge wa CCM na kamati inayoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alisema baadhi ya wabunge wanaomshambulia wanafanya hivyo si kwa matakwa yao bali kwa kutumwa na mtu ambaye hata hivyo hakumtaja.

  Katika hatua nyingine, Rostam ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alieleza kushangazwa na hatua ya wabunge hao kuonekana wakihofia kuundwa kwa tume huru wakati huo huo wakitamba kuwa ripoti ya kamati ya Bunge ya Richmond ilikuwa ni sahihi.

  Alisema iwapo ni kweli wanakiamini wanachokipigania, basi ilikuwa ni vyema waruhusu tume ya majaji ifanye uchunguzi upya na wa haki, na ambao iwapo ungebaini wao kuhusika katika kadhia hii, wafikishwe mbele ya vyombo vya kisheria.

  ‘‘Kama wanaona kweli ripoti ni sahihi si ndo watapata kutuona tunachukuliwa hatua na azma yao dhidi yetu kukamilika? Haiingii akilini kuogopa,” alisema.

  Akimzungumzia Kimaro, mbunge huyo wa Igunga alieleza kushangazwa na hatua yake ya kuwa mstari wa mbele kushutumu wenzake ilhali ukweli ukionyesha kwamba alikuwa ameshindwa kuliongoza jimbo lake la Vunjo, ambalo lilikaribia kuchukuliwa na chama cha upinzani cha TLP.

  ‘‘Jimbo alilopewa na wananchi limemshinda na kidogo tupokonywe na TLP kwa sababu ya kushindwa kuliongoza,” alisema Rostam.

  Katika mahojiano ya simu ya jana, Rostam alirejea kauli yake aliyopata kuisema siku zilizopita kwamba, iwapo angekuwa ndiye mmiliki wa Dowans, asingeona aibu kulisema hilo kwani, huo ni mradi mkubwa ambao hauwezi kumilikiwa na Mtanzania yeyote binafsi.

  Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti juzi, Selelii, Lembeli na Kimaro, walipinga hatua ya Rostam kutaka kuundwa kwa tume huru wakisema kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha kanuni na wajibu wa Bunge.

  Wabunge hao ambao siku zote wamekuwa na msimamo mkali kuhusu sakata la Richmond na masuala mengine yanayohusu tuhuma za ufisadi, walimtaka Rostam kuzisoma kanuni za Bunge na wakasisitiza mbunge mwenzao huyo hakuonewa katika maamuzi yaliyofikiwa.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,002
  Likes Received: 12,612
  Trophy Points: 280
  Kama unahisi kutotendewa haki mahali popote, unatinga mbele ya sheria, hakuna aliye juu ya sheria, kama rais mwenyewe ndiye mwenye kinga ya kushitakiwa na bado anashitakiwa litakuwa Bunge.

  Jamani RA kama anawashauri zaidi ya wale wapambe wake, mshaurini mwenzenu ajifunze kukaa kimya ...oh haya heri mimi sijasema kitakachomkuta... msije kusema hakushauriwa and by then it might be too late...
   
 3. m

  mkulu Member

  #3
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  "Kwa hali ya kawaida miye si wa kujibizana na watu wa aina ya Kimaro... ni kudhani kwao Dowans ni yangu ndo kumepeleka nchi kuingia gizani. Aibu,"

  hapa kuna namna .... kwahiyo hili giza ni kutukomoa kwa kumshtukia kwamba ni yake ama?
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,417
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Some unintended revelations..!
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Anachotukumbusha RA ni KINGA NZITO kupita kiasi ililonalo BUNGE letu ambayo maamuzi yake hayahojiwi na MAMLAKA nyingine yoyote. Tulijadili hili kwa kina badala ya kupoteza muda mwingi kumjadili yeye ambaye hata hivyo amekwisha jadiliwa sana humu.
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 9,570
  Likes Received: 1,485
  Trophy Points: 280
  Kwi kwi kwi!
  Alijuaje kwamba hauwezi kumilikiwa na Mbongo yeyote? Ina maana anajua details zake.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wewe una mashaka au kutopendezwa na hilo?

  For my case, kwa vile bunge halikurupuki kupitisha maamuzi, na linakaa ki`wapiga-kura zaidi kuliko kiserikali na chama(japo wanapenyeza vidole huko) naona ni sawa kwake kuwa na supremacy hiyo.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Checks and balances lazima ziwepo hata kama ni maamuzi ya kitaasisi kama BUNGE. Bunge letu limewahi kupitisha maamuzi ya ajabu kabisa yakiwemo takrima, hoja ya mgombea binafsi, juzi Zitto alijaribu kutoa hoja Wabunge waondoke kwenye bodi za taasisi za umma wakakataa,....
  Bunge kama hili la kwetu halipaswi kuwa na kinga hii. Bado ni la CHAMA kimoja.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,056
  Likes Received: 3,416
  Trophy Points: 280
  kimzungumzia Kimaro, mbunge huyo wa Igunga alieleza kushangazwa na hatua yake ya kuwa mstari wa mbele kushutumu wenzake ilhali ukweli ukionyesha kwamba alikuwa ameshindwa kuliongoza jimbo lake la Vunjo, ambalo lilikaribia kuchukuliwa na chama cha upinzani cha TLP.

  '‘Jimbo alilopewa na wananchi limemshinda na kidogo tupokonywe na TLP kwa sababu ya kushindwa kuliongoza," alisema Rostam.

  Jimbo la Vunjo lazima litachukuliwa na TLP si kwasababu Mheshimiwa Kimaro ameshindwa kufanyakazi bali wakaazi wengi wa Vunjo bado wanamkubali Bwana L A Mrema.
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 10,434
  Likes Received: 2,686
  Trophy Points: 280
  Hao akina Selelii si wampeleke mahakamani, kama kweli ni viongozi wazuri?
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 4,852
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  Rostam kama anataka majaji kuchunguza tuhuma zake ni jambo linalowezekana ila sii kwa namna anavyotaka yeye. Anachotakiwa kufanya ni kuiomba ofisi ya DPP imfungulie kesi ya kuikana kampuni yake ya kitapeli na huko mahakami atakutana na jopo la majaji watatu anaowataka na watamhukumu kwa uhuru na kwa haki kabisa!!
   
 12. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Bottom line Tanzania hakuna kiongozi msafi. Ni sawa na kauli aliyowahi kutoa Bob Mugabe kwamba kiongozi yoyote wa Afrika anayehisi kwamba yeye amechukua madaraka kimabavu na awe wa kwanza kumnyooshea kidole. Twende mbele turudi nyuma ili tuweze kuwa wasafi inabidi watanzania wenyewe waseme sasa INATOSHA.
   
 13. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,299
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hii ya Mugabe nasikia wapambe wote mkutanoni walishikwa na ganzi! na haikuwahi kutolewa magazetini sijui wewe nawe ulikuwamo?
   
 14. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie ningekuwa wewe rostamu nisingeendelea kukaa katika nchi ambayo wabunge wake ni waapuuzi! wakati nina kwetu kwa wenye akili.
  Kama unadhani chuki tu ndio zinasababisha haya yote si urudi tu kwenu ....unanga'nga'nia nini hapa! ulikotoka umeua? mcheza kwao hutunzwa hapa hautunziki tena!!!! rudi kwenu tuachie nchi yetu bwana

  Unajua nakumbuka wakati nakimbia mchaka mchaka kuna wimbo tuliimba " tanzania tanzani nchi yenye mali nyingi watu wengi wa ulaya wanaililia sana" kashamba ka bibi
  ooooh mie ponjoro mwenye asili ya tanzania! mmmh mnatufanya sisi wajinga ndio waliwao....kizazi kipya kinakuja na hata sasa kipo haturuhusu kukaa jamvi moja na watu wa aina hiiii! nimesema mwisho wenu haupo mbali,....tumechoka.
   
 15. R

  Rwechu Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wenzake wakati wakipinga uchunguzi mpya walinukuu kanuni za bunge kuwa, kinachopitishwa bunge hakiwezi kuundiwa tume na mhimili mwingine wa dola.
  Yeye mbona hasemi kanuni za bunge zinasemaje mtu akihisi hatatendewa haki?
  Chaajabu maazimio 18 kati ya 20 yametekelezwa sasa hiyo tume itaundwa kuchunguza hayo yaliyosalia au itabatlisha ripoti yote ya awali? Kwanini linalo mhusu R.A ndo liwe la uongo mengine sawa? HANA JIPYA
   
 16. R

  Rwechu Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wenzake wakati wakipinga uchunguzi mpya walinukuu kanuni za bunge kuwa:- kinachopitishwa na bunge hakiwezi kuundiwa tume na mhimili mwingine wa dola.
  Yeye mbona hasemi kanuni za bunge zinasemaje mtu akihisi hajatendewa haki?

  Chaajabu maazimio 18 kati ya 23 yametekelezwa sasa hiyo tume itaundwa kuchunguza hayo yaliyosalia au itabatlisha ripoti yote ya awali? Kwanini linalo mhusu R.A ndo liwe la uongo mengine sawa? HANA JIPYA
   
 17. R

  Rwechu Member

  #17
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kanuni haziruhusu ajenda iliyokwisha fungwa na bunge kuhojiwa na mhimili mwingine wa dola. Kama anataka tume mbona hatwambii kanuni zinasemaje?

  Maazimio 18 kati ya 23 yamekwisha tekelezwa sasa hiyo tume ya majaji itachunguza hayo matano yaliyobaki? Au hata hayo mengine ni ya uongo?
  R.A huna jipya umechemsha
   
 18. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 1,952
  Trophy Points: 280
  Watu wengine wana raha sana duniani mfano rostam, yaani anatuchezea tu vichwa vyetu.kutuibia katuibia sana huyu huyu anasababisha tunashindwa kujadili mambo ya muhimu tunamjadili yeye tumemchoka nae huyu muasia arudi tu uarabuni tujue moja.............anatupotezea tu muda wetu...
   
 19. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,341
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Meno ya Mbwa hayaumani.
   
 20. m

  mpuguso Member

  #20
  Nov 20, 2009
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RA ishakula kwake akae atulie, Dili lao la kuleta Richmond na kutaka kuuza mitambo mibovu ya dowans wenzao wamewazidi akili.
   
Loading...