Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

hapo si mwisho wao. wafikishwe mahakamani wataifishiwe mali zao. upuuzi mtupu watu wanakula pesa yau umma kisha kujiuzulu nyadhifa ndo iwe basi !!
 
ili kuwa fundisho kwa wote watakao kuja hawa wafilisiwe mali zao na pesa wapewe tanesco
 
Wakati bei ya Umeme imefikia kiasi kisicho kuwa cha kawaida naona bado kuna watu wanaleta mzaa.

Yaani watu wanasaini mikataba ya kutuuuza wananchi.

Mimi nafikiri kwa kuwa wabunge wametumwa na wananchi baada ya hapo wote waliohusika wafikishwe polisi mara moja wakiongozwa na Mkuu wao.

Huko ndiko waanze kusema jinsi wanavyoonewa.

Pia na wote walioimba wimbo ni wakati sasa wa kuwaita tena na kuwauliza kulikoni wimbo.

Nafikiri kamati ya Dr. Mwakyembe bado iendelee na Msabaa amesema atatoa ushirikiano nafikiri autoe Polisi.

Tunataka kujua milioni 152 analipwa nani?

Asije akawa analipwa Msabaa, Karamagi na Luwasa wakatuletea Mungiki-Tanzania.
 
Caspian Mininga > Richmond > Dowans Holdings!!!

Na kwa nini yeye kama mmoja wa watu waliokuwa implicated hakuweza kuonyesha roho ya kizalendo na kurudi nchini kwa ajili ya kutoa ushahidi!!!
 
Caspian Mininga > Richmond > Dowans Holdings!!!

Na kwa nini yeye kama mmoja wa watu waliokuwa implicated hakuweza kuonyesha roho ya kizalendo na kurudi nchini kwa ajili ya kutoa ushahidi!!!

Mkuu

Ukipewa Mtoto Umulee akakushinda unamrudisha kwao tu.

Huyu jamaa amepata faida nyingi amelelewa vizuri Tanzania mimi nafikiri amechoka.

Sasa anaanza kuanzisha makampuni ya kutuibia wananchi wa kawaida, dawa yake ni moja tu, inafaa kurudishwa kwao.

Vinginevyo afuate sheria za nchi, UFISADI atafute sehemu za kuufanyia na siyo Tanzania.
 
Hivi kama kina Rostam ndo wako CC ya CCM tutegemee nini toka chama hiki? na hiyo Sirikali yao Je!
 
Hivi kama kina Rostam ndo wako CC ya CCM tutegemee nini toka chama hiki? na hiyo Sirikali yao Je!

Ulichosema ni sahihi kabisa. CCM ni chama chenye sera moja tu kubwa ingawa haiko wazi "Kubakia madarakani".Wanafanya hivi kwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja kuitumia Katiba kuwa-favour wao, Tume ya Uchaguzi,Vyombo vya Dola na kibaya zaidi kuwakumbatia majambazi ambao ndo wanawasaidia kupata pesa wanazozihitaji. Bila kujali hizo pesa zinapatikana kwa gharama ya Maisha duni,Umasikini na Huduma duni kwa watanzania wao wanapokea na kufumba macho.Sidhani kama JK hajua nia na shughuli za RA,AB Gulamali na wafanyabiashara wengine wa madawa ya kulevya na baadhi ya waliokuwa Mawaziri wake na EL.Anawafumbia macho kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa CCM na chama kinahitaji pesa na hao ndo wanaprovida pesa kwa Chama.
 
Hamna kitu huyo....ni kutapatapa tu..yeye anachotakiwa kujibu ni yale yaliyomo kwenye ripoti. Na kama amejidai kununua hayo magazeti siyo rahisi kwamba atanunua yote....

Cha muhimu atuelezee kati yaliyoandikwa kwenye ripoti yapi sahihi...aweke bayana kwamba ana uhusiano wowote na hiyo Rich--mondu.

Muda wa ubabaishaji umekwisha....tufanye kazi zetu kwa umakini.
 
Hapa amejibu mapigo gani ama ndiyo aina ya waandishi njaa wa TZ wa kuuza magazeti .Hapa ni JF andika kichwa cha habari kulingana na uhalisia ndugu .
 
Rostam na wenzie wengi hapa ndo wamevuka mstari. Walichoilimbikizia hapa na nje ambacho tuna uwezo wa kukifikia vitaifishwe na Fisadi apewe masaa ya kuondoka nchini. Na serikali iangalie upya sheria zetu zinazowabana wazawa na kuwabeba wakuja hadi wanafikia kutudharau kiasi hiki. Tupo tunamsubiri JK aanze rasmi kumuenzi Nyerere kwa vitendo.
Kisingov
 
Rostam na wenzie wengi hapa ndo wamevuka mstari. Walichoilimbikizia hapa na nje ambacho tuna uwezo wa kukifikia vitaifishwe na Fisadi apewe masaa ya kuondoka nchini. Na serikali iangalie upya sheria zetu zinazowabana wazawa na kuwabeba wakuja hadi wanafikia kutudharau kiasi hiki. Tupo tunamsubiri JK aanze rasmi kumuenzi Nyerere kwa vitendo.
Kisingov

RA ni businessman ambaye ni ruthless kama kawaida ya business man yeyote ambapo popote penye opportunity atachukua...hata wewe ungefanya hivyo.

RA ni mtanzania ingawaje mwenye asili ya ki asia...ukiangalia historia kila mbogo ni wa kuja wengine walitoka south wengine north.....let us not play the race card here.

Wa kuwalaumu ni hawo viongozi waliopewa kazi ya kututumikia instead wamejiingiza business na kujilimbikizia mabilioni yetu
 
Hamna kitu huyo....ni kutapatapa tu..yeye anachotakiwa kujibu ni yale yaliyomo kwenye ripoti. Na kama amejidai kununua hayo magazeti siyo rahisi kwamba atanunua yote....

Cha muhimu atuelezee kati yaliyoandikwa kwenye ripoti yapi sahihi...aweke bayana kwamba ana uhusiano wowote na hiyo Rich--mondu.

Muda wa ubabaishaji umekwisha....tufanye kazi zetu kwa umakini.


JF kwa vichwa bwana, yaaani sina hamu maana haya maneno yameandikwa na kichwa, heshima mbele mkuu Babelwa1971
 
Mkapa alizua zengwe dhidi ya Jenerali Ulimwengu kuhusu uraia wake pale (Makapa) alipoona jamaa anamwandama sana kwenye magazeti yake.Tunajua Rostam ni Mtanzania "wa kuchonga",sasa dawa ya watu kama huyu ni kumvua urai kisha kumtimua haraka sana,hata kama kwa kufanya hivyo ataishia kuwa stateless.
 
JF kwa vichwa bwana, yaaani sina hamu maana haya maneno yameandikwa na kichwa, heshima mbele mkuu Babelwa1971


Tena Vichwa hasa, kwani hata mie nimesoma pahala mwanae Lowassa katimkia south africa juzi kukimbia kibano. Anaitwa RICHARD - anatoka MONDULI - kampuni ilisajiliwa kisanii ya RichMond(RICHARDMONDULI)! hapa Lowassa na Rostam ni Mabilionea kama Biligate! imagine mahela yote hayo kilasiku yanaingia kwenye account zao tuuuuu!
 
Haya tayari tuna Mh.Pinda ndani ya house, tunataka sasa ile kasi mpya iliyo kuwa ikihubiriwa kwenye majukwaa ya siasa ifanye kazi. Hii ni last chance kwa Mh.JK kutekeleza ila falsafa ya maisha bora kwa kila mtanzania. Imani kwa JK ilishuka toka kipindi kile Karamagi aliposign buzwagi contract, ihali akijua president alisha toa order kuwa usisigniwe mkataba mpya unless hii iliyopo imepitiwa kwa undani. Japo agizo la Raisi lilikiukwa ajabu JK hakuchukua hatua dhidi ya waziri mhusika, Je ni washirika au kuna nini nyuma ya pazia? Nini kitafuata baada ya riport ya Dr.Mwake? Ku-resign ni wajibu wao wali si ishu ya kuanza kupongezana hapa. Je watu hawa wanatofauti gani na jambazi? RA ni mfanyabiashara mjanja maana aliwapata partiners mazuzu, anyway viongozi ndo wakulaumiwa zaidi juu ya hili bcoz RA asingepenya ikiwa haja alikwa. Wote wenye kutoa support ya kifedha kwenye Chama Chao Maarufu deal zao za hatari na zinalete umasiki kwa watanzania tulio wengi.

Kaka K.
 
wengine wanaochangia kuiharibu nchi hii ni baadhi ya wahariri na waandishi wa habari!

Kimsingi rostam ni mtu mdogo sana, he s merely no body!!! lkn vyombo vya habari alivyovinunua vinampamba as if yuko maalum sana, tajiri sana nk, rostam ni dalali wa kawaida tu!! wala hana ujanja au elimu yoyote ya biashara!! tatizo ni wale anaokutana nao, they r very cheap!! ht lowassa na wengine wote!!

Mtu anapokosa integrity na kua cheap, ni jambo la kawaida kwake hata kunyang'anywa mke!! na asiseme lolote!!hana msimamo!!fedha haiwezi kukufanya uwe cheap! ni bora upotelee mbali, kabla mambo kukurudia.kama ilivyokuwa kwenye hili sakata la richmond.

Tuache bla bla tuwasaidie watu wa igunga, jimbo maskini kabisa ktk nchi hii, namna ya wao kumtoa rostam kwenye wadhifa alionao!! hapo tutajenga nchi, sio upuuzi huu tunaojadili hapa!
 
“Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond na Dowans Holdings S.A, baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo.

“Aidha, alitakiwa aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd, ilitumiwa na Dowans.”

Lakini alipoulizwa na Mtanzania jana, Rostam alisema yeye ana kampuni ya ukandarasi na amekuwa akifanya kazi na makampuni mbalimbali bila kujali mambo ya kisiasa.

“Mimi ni mkandarasi, nimefanya kazi na nitaendelea kufanya kazi na makampuni mengi, sina la kuficha katika hilo, kwani kila mtu anajua kampuni yangu,” alisema.

Kama kawaida yake anakimbilia magazeti yake kujisafisha bila kujua kuwa magazeti ya mtanzania yameisha credibitility kabisa!

Anatapatapa na hajui cha kufanya, kila mti unateleza... tik tak tik tak tik tak......
 
Back
Top Bottom