Tatizo hapa kwetu kila mtu anajichukulia haya mamlaka ya kudai kuwa fulani si raia, wakati ni wazi kuwa wenye hayo mamlaka ni uhamiaji. Tatizo hapa ni kuwa zaidi kwa watu wa bara mtu yeyote ambae si kabila lao basi si raia...vilevile kihistoria Tz tuna hii tabia ya kuzushiana hili suala ukianzia wakati wa miaka ya 60 Tanu ilipomzushia kuwa Kambona si Mtz naye alipohamia London akadai kuwa nyerere si Mtz vilevile...
Tukaona kila Ulimwengu, yule mbunge wa kigoma jina nimesahau, haya leo hii kina Bashe, Rostam na Mkulo...hii inaonyesha wazi tuna uelewa mdogo wa elimu ya uraia na vilevile kuna loopholes kwenye suala zima la uraia wa nchi yetu.
Jee sheria inasemaje kama wazazi wako si raia na wee umezaliwa hapa?
Bashe ni wazi kuwa ni raia halali na ana ruhusa kugombea nafasi za uongozi kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hilo limethibitishwa na uhamiaji. Sasa Makamba anadai kwamba wao CCM wana vigezo tofauti kuhusu swala la uraia yaani tofauti na serikali yao, hapo mi sielewi...
Ingekuwa vyema kama nafasi zote za uongozi (vyama na serikali) watu wawe vetted na vyombo husika kuhusiana na umri, uraia n.k. kabla ya kutuletea haya madudu na sababu zisizo na msingi!
Makamba na CCM yako msitufanye umma wa watanzania kama wote ni mataahira, na kutuletea sababu za ajabuajabu...
Bashe hama CCM, simple as that