Kung'atuka ili kuinusuru CCM ni jambo la busara ila kung'atuka kabla ya kufanya marejesho ya pesa zetu haiwezekani. Kwanza wana JF mnaona jinsi mpango wa kususia simu za Vodacom unavyoanza kufanya kazi. Kazeni buti hata na wengine tususie biashara zao mpaka kieleweke. Huyu jama ni mwepesi kusoma alama za nyakati maana hapo ameona kuwa huko mbele ataambulia patupu ndio maana anaanza kutapatapa.