Rostam: Kisutu, viongozi wakipiga simu hupati haki

Rostam: Kisutu, viongozi wakipiga simu hupati haki

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
752
Reaction score
1,259
Leo nawiwa kutoa ushauri kwa watanzania wenzangu kuhusu hali ya utoaji haki nchini. Kwakuwa jambo lenyewe ni nyeti na lina uzito wa kipekee nitajenga maoni yangu kupitia kauli ya Ndugu Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga 1994-2011, Katibu uchumi na fedha CCM 2005-2007, na Mjumbe wa kamati kuu CCM 2006-2011 unayoweza kuipata hapo chini.

Katika maelezo yake, ndugu Rostam alieleza mahakama ya kisutu kiongozi akipiga simu, hupati haki yako. Sina hakika sana na uzoefu wa Ndugu Rostam na mahakama zetu, mathalani kwenye eneo la haki jinai, kwasababu sijawahi kusikia ameshtakiwa kwa makosa ya kijinai. Kwa maoni yangu, tafiti kama hii isingekamilika, angalau kwenye eneo la haki jinai, bila kumsikiliza Mbowe, mtu aliyekaa lupango miezi nane akituhumiwa kuwa gaidi na Lissu, aliyekaa lupango zaidi ya miezi mitatu akituhumiwa kuwa mhaini.

Mifano hii miwili inatoa ujumbe madhubuti kuwa, inawezekana kabisa ukashitakiwa kwanza halafu ndio upelelezi na taratibu zingine zikafuata, inawezekana kabisa ukashitakiwa na mashahidi dhidi yako wakafichwa, ukituhumiwa tu kwa kosa lenye adhabu ya kifo, utafungiwa deathrow hata kama hujahukumiwa bado, ukishawekwa lupango washitaki wako wataendelea kuahirishwa kesi yako kila siku huku wakikudhihaki kuwa unaomba huruma ya mahakama.

Nimeyaandika haya, kuwausieni wasomaji wangu, na kuiusia nafsi yangu kuwa, yakikufika yakukufika haki jinai ni nadharia isiyotekelezeka haswa swala lako linapokuwa linagusa maslahi ya wakubwa. Maandiko matakatifu yanatuasa kuwa, "mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia" Mithali 27:12


View: https://vm.tiktok.com/ZMSGEkm8j/
 
Oppressor mkubwa kwenye nchi yeyote ile ni serikali yenyewe.
 
Walewale Wala keki Bora ungetolea MFANO MTU mwingine kaka umeharibu sana kwa HUYO MTU tunamjua makandokando yake
 
Back
Top Bottom