Utu ni jambo la msingi. Busara ni pamoja na kujua kila jambo lina mahali pake na kila mahali pana jambo lake.
Uungwana ni sifa njema. Kinyume chake ni sifa mbaya.
Kutofautiana kwa waungwana kuna mipaka yake.
Utamaduni wa mwafrika una mzizi mrefu sana ktk Uungwana wa kumfariji mwenye msiba. Misiba kwetu hupatanisha walokosana na majirani ndugu jamaa na marafiki. Wake waliondoka hurudi n.k.
Hata hivo, Kama wanadamu tujitathmini pia km na sisi ni wasafi kiasi gani. Kwa level zetu tuna matatizo mengi hasa kukosa uaminifu na uadilifu kwa familia, ukoo, mahala pa kazi, na jamii.
Vipi tukianza kubezwa tunapopatwa na misiba?
Uungwana ni tabia njema.