Rose Kamili Mke wa Dr. Slaa, amwaga mboga | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rose Kamili Mke wa Dr. Slaa, amwaga mboga

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Happycuit, Sep 5, 2015.

 1. H

  Happycuit JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2015
  Joined: Aug 18, 2013
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  AZIZA MASOUD NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM KWA vijana wa mjini, wanaweza kusema kwamba alichofanya Dk. Willibrod Slaa juzi kwa kuachana na siasa na kurusha tuhuma kwa chama chake, ni sawa na kumwaga ugali, na majibu aliyotoa mkewe wa kwanza, Rose Kamili jana, ni sawa na kumwaga mboga. Mke huyo aliyedai kutelekezwa na Dk. Slaa mwaka 2010 pamoja na watoto, alisema kiongozi huyo ni mwongo na ni dhaifu kwa wanawake.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rose alisema ameshtushwa na kauli zilizotolewa na Dk. Slaa, na hasa zile zilizoelekezwa kwake moja kwa moja na familia yake. Rose ambaye ni mke wa ndoa wa kiongozi huyo wa zamani wa Chadema, alisema kauli Dk. Slaa kuwa familia yake imekuwa ikishindia mihogo kwa sababu ya kuhangaikia na Chadema, ni kiashiria cha uongo wa wazi. “

  Siwezi kusema kwamba mihogo ni mibaya kuliwa, lakini napenda kukiri kwamba katika maisha yetu niliyokaa na Dk. Slaa kuanzia mwaka 1986, sikuwahi kushuhudia familia yetu ikila mihogo kwa sababu ya kukosa chakula kama alivyosema kwenye hotuba yake,” alisema. Aliongeza kuwa hata kauli yake kwamba Serikali ilimwekea pingamizi ili asifunge ndoa na mchumba aliye naye sasa, Josephine Mushumbusi, ni uongo kwani ni yeye ndiye aliyeweka pingamizi hilo kwa sababu ni mkewe rasmi wa ndoa. “Jambo la kujiuliza hapa ni kwamba tangu lini Serikali ikaweka pingamizi wakati aliyepinga ni mkewe.

  Ukweli ni kwamba mimi ndiye niliyeweka pingamizi hilo ili kunusuru kunyang’anywa nyumba na hatimaye kuhangaika na watoto,” alisema. Kuhusu kauli ya Dk. Slaa kwamba anamchukia Lowassa na hajazungumza naye kwa muda mrefu, Rose alisema waziri mkuu huyo wa zamani, ndiye aliyemshauri kuhamia Chadema mwaka 1995 na kugombea ubunge wa Karatu baada ya jina lake kukatwa na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM. “
  Nakumbuka wakati tukizungumzia suala hilo ilikuwa jioni na tulikwenda nyumbani kwa Lowassa, Monduli baada ya jina lake kukatwa na CCM, ndiyo akamshauri kuhamia chama kingine, sasa hizo chuki zinatoka wapi?” alisema na kuhoji. Kuhusu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Rose alisema pia ni uongo mwingine kwa sababu wawili hao walipigiana simu na kufanya mazungumzo wiki iliyopita. “Kwanini aonyeshe chuki na watu wakati sisi ametutelekeza kwa muda mrefu, lakini tumekuwa tukimlinda? Sasa inashangaza ni kwa nini padri huyu mstaafu anaonyesha chuki kwa wengine,” alisema. Aidha Rose pia alionyesha kusikitikia hatua ya mumewe kuzusha maneno ya uongo kwa viongozi wa dini, akiwatuhumu kuhongwa zaidi ya shilingi milioni 60 na Lowassa ili wamuunge mkono.

  Pia alisema kumuhusisha Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, kwamba ndiye alimleta Lowassa Chadema ni kichekesho kwa sababu muunganishaji mkubwa wa suala hilo ni yeye (Dk. Slaa) ambaye anasali katika kanisa hilo. Uongo mwingine alioutaja mkewe huyo wa ndoa ni kuhusu kukataa kwake kutojiandaa kuwania urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati inajulikana kuwa alikuwa akifanya maandalizi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya suala hilo. Rose aliendelea kubainisha kuwa tatizo kubwa la mumewe ni kuzungumza mambo kwa kukurupuka na kutokuvumilia, na hata kudiriki kutoa siri za viongozi wenzake waliokuwa wakimtaka arudi ofisini. “Aliniambia kwamba alikuwa akifuatwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyemuahidi kwamba iwapo atakaa kimya atateuliwa kuwa mbunge na baadaye kuwa waziri, akaniambia Rais Kikwete alimuahidi kumpatia ubalozi, ikiwamo na kuitwa na Kardinali Pengo ambaye hakusema walizungumza jambo gani. “

  Maneno hayo nimekuwa nikiyapata kutokana na tabia ya Dk. Slaa kwa kutokuwa na mdomo na ulimi usiokuwa na mfupa, hivyo kila jambo analoelezwa huwa analiweka wazi, na inawezekana safari aliyokwenda Afrika Kusini baada ya kumalizika kikao ndiyo kaelekea Ubalozi wa Afrika Kusini,” alisema Rose. Rose alipasha kwamba Dk. Slaa ambaye amekuwa akimfahamu, amekuwa tofauti na huyu aliyemsikia akizungumza kwenye mkutano ule na hilo limetokana na udhaifu mkubwa alionao kwa wanawake. “Dk. Slaa siye ninayemjua, anaonekana anaendeshwa na mwanamke aliye naye na ndiyo maana hata alikubali kumleta Lowassa kwa asilimia 80, lakini alipofika nyumbani alibadili msimamo baada ya kulazwa nje ya nyumba yake,” alisema.

  Rose ambaye ni mbunge wa viti maalumu (Chadema) aliyemaliza muda wake, alisema amekuwa akiwasiliana na mumewe huyo kwa muda mrefu, na hata alipopata taarifa za kugoma kwenda ofisi za Chadema, wanawe walikwenda nyumbani kwa Dk. Slaa kumjulia hali. “Cha kushangaza ni kwamba watoto walivyofika nyumbani kwake walibisha hodi, lakini walizuiliwa ndipo babu yao (baba yake Dk. Slaa) ndiye alitoka na kuzungumza nao nje ya geti huko JKT Mbweni,” alisema Rose aliyeambatana na watoto wake.
   
 2. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #21
  Sep 5, 2017
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,030
  Likes Received: 18,281
  Trophy Points: 280
  Dr.Willibroad P. Slaa
   
 3. Sky Eclat

  Sky Eclat JF-Expert Member

  #22
  Sep 5, 2017
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 20,846
  Likes Received: 52,216
  Trophy Points: 280
  Kulaaleki mama alimwaga radhi
   
 4. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #23
  Sep 5, 2017
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 45,500
  Likes Received: 27,038
  Trophy Points: 280
  Mimi simo bhana .
   
 5. Gide MK

  Gide MK JF-Expert Member

  #24
  Sep 5, 2017
  Joined: Oct 21, 2013
  Messages: 4,892
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Katerero haijawahi kumuacha mtu salama
   
 6. tweenty4seven

  tweenty4seven JF-Expert Member

  #25
  Sep 5, 2017
  Joined: Sep 21, 2013
  Messages: 6,439
  Likes Received: 3,783
  Trophy Points: 280
  Itakua RB N40 ndio inamoto wa kutosha kupiga pushups kma robot

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 7. Z

  Zola7 JF-Expert Member

  #26
  Sep 5, 2017
  Joined: Jun 23, 2015
  Messages: 358
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
 8. kajunjumele

  kajunjumele JF-Expert Member

  #27
  Sep 5, 2017
  Joined: Jul 5, 2014
  Messages: 1,664
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  ..Mbona kama chupi zimeanikwa kwa Jukwaa?
   
 9. MWALLA

  MWALLA JF-Expert Member

  #28
  Sep 5, 2017
  Joined: Dec 12, 2006
  Messages: 9,734
  Likes Received: 3,151
  Trophy Points: 280
  hahahaa umezisahau bikini zako hizo

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 10. jiwe angavu

  jiwe angavu JF-Expert Member

  #29
  Sep 5, 2017
  Joined: Aug 28, 2015
  Messages: 1,213
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa magu ana peacemaker kwenye moyo..ndiomana hutakuja sikia kapanda ndege yupo angani zaidi ya masaa matano..

  Halafu cha ajabu zaidi aliyetoa kibali cha kwenda india kutibiwa ni waziri mkuu mstaafu sumaye anaye mtia zengwe kisa kuhamia upinzani..

  Kweli dunia sio mbaya walimwengu wabaya.

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 11. data

  data JF-Expert Member

  #30
  Sep 5, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,919
  Likes Received: 6,683
  Trophy Points: 280
  Mmhh
   
 12. sayoo

  sayoo JF-Expert Member

  #31
  Sep 5, 2017
  Joined: Nov 19, 2014
  Messages: 1,296
  Likes Received: 1,027
  Trophy Points: 280
 13. data

  data JF-Expert Member

  #32
  Sep 5, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,919
  Likes Received: 6,683
  Trophy Points: 280
  Huyu Ni Nani!??

  Video ya lini hii!??
   
 14. KAMUGUNGA

  KAMUGUNGA JF-Expert Member

  #33
  Sep 5, 2017
  Joined: Mar 25, 2013
  Messages: 232
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
 15. S

  Siyabonga101 JF-Expert Member

  #34
  Sep 5, 2017
  Joined: Mar 8, 2016
  Messages: 2,437
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Acha chuki za ukabila ndugu. Hiyo kitu inaitwa Pacemaker na sio Peacemaker. Kwa mujibu wa uzandiki ulioandika hapo juu umetamka ya kwamba alienda kutibiwa India. Hapo hapo unatuambia ya kwamba hautakuja kusikia amepanda ndege yupo angani zaidi ya masaa matano. Unafahamu umbali wa kutoka India mpaka Tanzania kwa ndege!? Maana kama alienda India ni lazima alipanda ndege. Umbali wa kutoka India mpaka Tanzania ni masaa Sita na nusu mpaka masaa Saba. Ukiamua kuwa muongo ingia gharama ya kufanya utafiti kidogo itakusaidia huko mbeleni mkuu.
   
 16. ras jeff kapita

  ras jeff kapita JF-Expert Member

  #35
  Sep 5, 2017
  Joined: Jan 4, 2015
  Messages: 5,964
  Likes Received: 4,034
  Trophy Points: 280
  Wanawake hawajuagi kutunza vitu

  mioyoni.
   
 17. jiwe angavu

  jiwe angavu JF-Expert Member

  #36
  Sep 5, 2017
  Joined: Aug 28, 2015
  Messages: 1,213
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa kunisahihisha..kiingirishi hata mkuu kinampiga chenga..

  Ila suala la kupanda ndege..na kua angani zaidi ya masaa ma5 hutakuja kulisikia kitoka kwa mkulu..

  Nakuhusu baada ya matibabu..alirudi na ndege maalumu..

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 18. C

  Chintu JF-Expert Member

  #37
  Sep 5, 2017
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,516
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu bibi sie yule ambaye CCM walikuwa wanamkanyaga sehemu za siri kule Iringa wakati tunashindana na akina LOWASA?
  Mbona naye anasema "Mke wake"? sasa nani ni mke huyu au yule?
   
 19. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #38
  Sep 5, 2017
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Watu wanaanza kufunguka. Tutayasikia mengi, ajitahidi kuvumilia.
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #39
  Sep 5, 2017
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,140
  Likes Received: 5,129
  Trophy Points: 280
  +Shuntama, unatokaje hapo kwa mfano?
   
 21. MWALLA

  MWALLA JF-Expert Member

  #40
  Sep 5, 2017
  Joined: Dec 12, 2006
  Messages: 9,734
  Likes Received: 3,151
  Trophy Points: 280
  zile za kichinachina
   
Loading...