Rose Kamili Mke wa Dr. Slaa, amwaga mboga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rose Kamili Mke wa Dr. Slaa, amwaga mboga

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Happycuit, Sep 5, 2015.

 1. H

  Happycuit JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2015
  Joined: Aug 18, 2013
  Messages: 280
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  AZIZA MASOUD NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM KWA vijana wa mjini, wanaweza kusema kwamba alichofanya Dk. Willibrod Slaa juzi kwa kuachana na siasa na kurusha tuhuma kwa chama chake, ni sawa na kumwaga ugali, na majibu aliyotoa mkewe wa kwanza, Rose Kamili jana, ni sawa na kumwaga mboga. Mke huyo aliyedai kutelekezwa na Dk. Slaa mwaka 2010 pamoja na watoto, alisema kiongozi huyo ni mwongo na ni dhaifu kwa wanawake.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rose alisema ameshtushwa na kauli zilizotolewa na Dk. Slaa, na hasa zile zilizoelekezwa kwake moja kwa moja na familia yake. Rose ambaye ni mke wa ndoa wa kiongozi huyo wa zamani wa Chadema, alisema kauli Dk. Slaa kuwa familia yake imekuwa ikishindia mihogo kwa sababu ya kuhangaikia na Chadema, ni kiashiria cha uongo wa wazi. “

  Siwezi kusema kwamba mihogo ni mibaya kuliwa, lakini napenda kukiri kwamba katika maisha yetu niliyokaa na Dk. Slaa kuanzia mwaka 1986, sikuwahi kushuhudia familia yetu ikila mihogo kwa sababu ya kukosa chakula kama alivyosema kwenye hotuba yake,” alisema. Aliongeza kuwa hata kauli yake kwamba Serikali ilimwekea pingamizi ili asifunge ndoa na mchumba aliye naye sasa, Josephine Mushumbusi, ni uongo kwani ni yeye ndiye aliyeweka pingamizi hilo kwa sababu ni mkewe rasmi wa ndoa. “Jambo la kujiuliza hapa ni kwamba tangu lini Serikali ikaweka pingamizi wakati aliyepinga ni mkewe.

  Ukweli ni kwamba mimi ndiye niliyeweka pingamizi hilo ili kunusuru kunyang’anywa nyumba na hatimaye kuhangaika na watoto,” alisema. Kuhusu kauli ya Dk. Slaa kwamba anamchukia Lowassa na hajazungumza naye kwa muda mrefu, Rose alisema waziri mkuu huyo wa zamani, ndiye aliyemshauri kuhamia Chadema mwaka 1995 na kugombea ubunge wa Karatu baada ya jina lake kukatwa na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM. “
  Nakumbuka wakati tukizungumzia suala hilo ilikuwa jioni na tulikwenda nyumbani kwa Lowassa, Monduli baada ya jina lake kukatwa na CCM, ndiyo akamshauri kuhamia chama kingine, sasa hizo chuki zinatoka wapi?” alisema na kuhoji. Kuhusu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Rose alisema pia ni uongo mwingine kwa sababu wawili hao walipigiana simu na kufanya mazungumzo wiki iliyopita. “Kwanini aonyeshe chuki na watu wakati sisi ametutelekeza kwa muda mrefu, lakini tumekuwa tukimlinda? Sasa inashangaza ni kwa nini padri huyu mstaafu anaonyesha chuki kwa wengine,” alisema. Aidha Rose pia alionyesha kusikitikia hatua ya mumewe kuzusha maneno ya uongo kwa viongozi wa dini, akiwatuhumu kuhongwa zaidi ya shilingi milioni 60 na Lowassa ili wamuunge mkono.

  Pia alisema kumuhusisha Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, kwamba ndiye alimleta Lowassa Chadema ni kichekesho kwa sababu muunganishaji mkubwa wa suala hilo ni yeye (Dk. Slaa) ambaye anasali katika kanisa hilo. Uongo mwingine alioutaja mkewe huyo wa ndoa ni kuhusu kukataa kwake kutojiandaa kuwania urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati inajulikana kuwa alikuwa akifanya maandalizi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya suala hilo. Rose aliendelea kubainisha kuwa tatizo kubwa la mumewe ni kuzungumza mambo kwa kukurupuka na kutokuvumilia, na hata kudiriki kutoa siri za viongozi wenzake waliokuwa wakimtaka arudi ofisini. “Aliniambia kwamba alikuwa akifuatwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyemuahidi kwamba iwapo atakaa kimya atateuliwa kuwa mbunge na baadaye kuwa waziri, akaniambia Rais Kikwete alimuahidi kumpatia ubalozi, ikiwamo na kuitwa na Kardinali Pengo ambaye hakusema walizungumza jambo gani. “

  Maneno hayo nimekuwa nikiyapata kutokana na tabia ya Dk. Slaa kwa kutokuwa na mdomo na ulimi usiokuwa na mfupa, hivyo kila jambo analoelezwa huwa analiweka wazi, na inawezekana safari aliyokwenda Afrika Kusini baada ya kumalizika kikao ndiyo kaelekea Ubalozi wa Afrika Kusini,” alisema Rose. Rose alipasha kwamba Dk. Slaa ambaye amekuwa akimfahamu, amekuwa tofauti na huyu aliyemsikia akizungumza kwenye mkutano ule na hilo limetokana na udhaifu mkubwa alionao kwa wanawake. “Dk. Slaa siye ninayemjua, anaonekana anaendeshwa na mwanamke aliye naye na ndiyo maana hata alikubali kumleta Lowassa kwa asilimia 80, lakini alipofika nyumbani alibadili msimamo baada ya kulazwa nje ya nyumba yake,” alisema.

  Rose ambaye ni mbunge wa viti maalumu (Chadema) aliyemaliza muda wake, alisema amekuwa akiwasiliana na mumewe huyo kwa muda mrefu, na hata alipopata taarifa za kugoma kwenda ofisi za Chadema, wanawe walikwenda nyumbani kwa Dk. Slaa kumjulia hali. “Cha kushangaza ni kwamba watoto walivyofika nyumbani kwake walibisha hodi, lakini walizuiliwa ndipo babu yao (baba yake Dk. Slaa) ndiye alitoka na kuzungumza nao nje ya geti huko JKT Mbweni,” alisema Rose aliyeambatana na watoto wake.
   
 2. a

  akilikubwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2015
  Joined: May 11, 2015
  Messages: 595
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nikiona watu wenye umri kama wa baba na mama yangu kuhibishana kwenye vyombo vya habari kiasi hiko..mimi napata AIBU sana
   
 3. H

  Happycuit JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2015
  Joined: Aug 18, 2013
  Messages: 280
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hamna namna nyingine sasa
   
 4. M

  Makele mbele JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 283
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Kusema kweli Dr amejiaibisha sana. Nahii dhambi itamsumbua maisha yake yote.

  Hata anavoongea anababaika sana maskini. Anaonekana yuko under pressure. Anaonekana kabisa anaongea asichoamini.

  Nadhani madhara yake ataanza kuyaona baada yauchaguzi. Atajikuta pekeyake asione mtu wakumliwaza. Mtu aliyezoea kupata heshima kutoka kila sehem, atajikuta sasa anapuuzwa nakila mtu.

  Ajiandae tu kisaikolojia kupokea hiyo hali lasivo itamuathili sana. Asidhani hata hao wanaomtumia leo baada yauchaguzi wataendelea kumthamini tena. Naowatampuuza tu, Chadema na Ukawa kwaujumla nao kwakuwa ameshanyea kambi yao, nao watampuuza tu.

  Kanisani nako ambako labda angeweza kukimbilia apate msaada wakiroho nako haaminiki tena kutokana na uchafu aliowatupia. Sijui kachanganyikiwa huyu mzee jamani? Nadhani ana tatizo si bule.

  Kiujumla mimi binafsi namuonea huruma.
   
 5. MWALLA

  MWALLA JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2017
  Joined: Dec 12, 2006
  Messages: 10,590
  Likes Received: 3,729
  Trophy Points: 280
   
 6. MWALLA

  MWALLA JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2017
  Joined: Dec 12, 2006
  Messages: 10,590
  Likes Received: 3,729
  Trophy Points: 280
 7. Lello199

  Lello199 JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2017
  Joined: Aug 26, 2016
  Messages: 584
  Likes Received: 1,540
  Trophy Points: 180
  Mhhhh
   
 8. MWALLA

  MWALLA JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2017
  Joined: Dec 12, 2006
  Messages: 10,590
  Likes Received: 3,729
  Trophy Points: 280
  KUMBE! anatumia betri akipiga pushapu betri zinausukuma!!
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,322
  Likes Received: 12,828
  Trophy Points: 280
  Hatari mura!
   
 10. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,584
  Trophy Points: 280
 11. Shindu Namwaka

  Shindu Namwaka JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2017
  Joined: Sep 22, 2014
  Messages: 4,825
  Likes Received: 2,936
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye battery sasa sijui ni Panasonic au national special.

  Post by Shindu Namwaka.
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2017
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,516
  Likes Received: 7,266
  Trophy Points: 280
  Naona ni mwendo wa kufukua Makaburi tu

  Sasa Membe alijua yeye ndio atapita?, naona alijiandaa sana sana, maana inasemekana eti hata ule mpinga ulioshikwa Dodoma na yule muhindi ulikuwa ni wa timu yake

  Sasa naamini kila Mtu ana bei yake, Mpaka Slaa kanunuliwa?
   
 13. Gyole

  Gyole JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2017
  Joined: Sep 20, 2013
  Messages: 3,218
  Likes Received: 2,722
  Trophy Points: 280
 14. k

  kindafu JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2017
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,139
  Likes Received: 929
  Trophy Points: 280
  Hii kali, kumbe bei ya Slaa ilipangwa na mke/hawara Josephine? Ama kweli kila zama na kina Dellilah wake!
   
 15. TAWA

  TAWA JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2017
  Joined: Jun 23, 2013
  Messages: 3,542
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
 16. Pablo Blanco

  Pablo Blanco JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2017
  Joined: Dec 20, 2016
  Messages: 1,622
  Likes Received: 918
  Trophy Points: 280
  Huyo mama anaitwa nani?
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2017
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,977
  Likes Received: 5,802
  Trophy Points: 280

  Dr. ni tajiri sana, kwa Membe alivuta B2, sasa huko lumumba si atakuwa amevuta zaidi ya B 10, ndiyo maana anazidi kuonekana kijana, kweli pesa sabuni ya roho siyo lile propesa uchwara lilipewa kiduchu sasa zimeisha linakubali kutumika kijinga kabisa.
   
 18. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2017
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Mke Wa kwanza Wa Dr Slaa ni mbunge viti maalumu chadema Bi Rose Kamili
   
 19. Replica

  Replica JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2017
  Joined: Aug 28, 2017
  Messages: 318
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 180
  Siasa za jukwaani, kwa hio Slaa kateuliwa mbunge na waziri?
   
 20. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2017
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,651
  Likes Received: 19,858
  Trophy Points: 280
  Noma
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...