Ingawa siungi mkono kitendo cha kupandisha bendera ya nchi nyingine,lakini serikali ya Tanzania ndiyo imewafanya wananchi wakafikia huko.Sukari imezuiliwa Himo bila kujali kuna Eneo lingine la Tanzania mbele ya Himo linaloitwa Rombo.
Rombo inastahili haki zote kama wananchi wa maeneo mengine.Kwa muda mrefu rombo imekuwa ikikandamizwa na kudharauliwa na watawala wetu,sijui ni kwa nini hasa.
Mkuu wa mkoa ameshindwa kuweka mkakati wa kutosha kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma hii wakati huo huo akidhibiti magendo.Ni kwa nini maeneo mengine yaliyopakana na nchi jirani wameweza kudhibiti hali hii bila kubughudhi wananchi ndani ya territory yake halafu mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ashindwe.Madiwani wa CCM ndiyo wanaoongoza halmashauri hivi kweli wanashindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kuweka ukaguzi katika usambazaji wa sukari kuanzia Himo,Mwika,Mamsera,Mkuu,Mashati,Useri na Tarakea? ni kwanini tusiweke logistics katika level yenye uwajibikaji wa kisiasa kama kata kisha nadharia ya monitoring and evaluation ikatumika?
Wananchi wa Rombo hata katika ugawaji wa Mahindi ya misaada madiwani wa CCM na wenyeviti wa vitongoji walitaka watu waonyeshe vitambulisho kwanza yaani kadi za CCM ndiyo wagawiwe.Nina ushahidi wa majina ya watu wasiojiweza kabisa hawakupewa mahindi,na pia hujuma iliyotumika kudhulumu watu waliostahili kupewa mahindi hawakupewa.Nimeorodhesha malalamiko na ushahidi wote ukajadiliwe kwenye vikao vya baraza la madiwani walifanyie kazi watoe ripoti kwa wananchi wa Rombo
Wananchi wa rombo wanatia huruma kwa jinsi wanavyobambikiwa kesi na watendaji wa serikali,ni ukandamizaji uliopitiliza.Kulikuwa hakuna vituo vya polisi na hata vilivyopatikana vinatumika kama tools za kutisha raia na kujipatia hela.Mojawapo ni kesi iliyomuhusu mwananchi mmoja anaitwa Aristariki Kimaryo aliyewekwa mahabusu na mtoto wake pamoja na mkwe wake kituo cha polisi Mashati kisa hawajatoa hongo ya kumnusuru mtoto wake,hivyo polisi wakaamua kuwasweka mahabusu.Tulipowahoji polisi sababu ni nini wakaishia kutoa vitisho hadi tulipotishia kutumia nguvu ndipo walipowaachia
Tembo wanaotoka nchi jirani wamekuwa wakivamia mashamba ya wananchi,wakiharibu na hata kuuwa watu lakini hakuna fidia ya maana iliyofanyika.Wanachi wa Rombo sasa inabidi kwa ruthless,wanyama wanaoingia kwenye mashamba inabidi wauwa na hakuna kutoa taarifa kwa idara ya maliasili,wauawe na pembe ziuzwe hela iingizwe kwenye akaunti maalumu ya kufidia walioathiriwa na wanyama hao
Leo hii watu wanawalaumu watu wa Rombo kwa kujiskia sehemu ya kenya bila kufikiria saikolojia iliyowaathiri ya muda mrefu.Huduma za kijamii na kiuchumi zimekuwa attached na wakenya.Hata Radio ya Taifa TBC haifiki kule badala yake KBC ndiyo inasikika sijui kama watu walioko Tunduma,Songea na kigoma wanasikiliza redio za Zambia,malawi,msumbiji au DRC kuliko TBC au ni Rombo peke yake?
Sasa serikali itende haki,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,madiwani pamoja na Mbunge wa Rombo simamieni maslahi ya wananchi wa Rombo.Serikali iache vitisho,iache kuwatisha wananchi wa Rombo.