Roman Abramovich: Utajiri wa Damu, Risasi na Umafia

Kapwil

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Messages
862
Points
1,000

Kapwil

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2018
862 1,000
Hakuna story ambayo haiishi kwenye group. Kule premium so lazima upate vitu Premium.

Mfano hii ya Abramovich kule ishaisha.
Ujasusi Sebuleni kwetu ishaisha.
The Richest Man tuko Episode 9
Leo hii tunamalizia makala inayohusu Utata wa Watoto wa Mtawala wa Dubai aliowafunga ndani ya jela kwenye kasri la Zabeel. (Undani wa kwanini mkewe ametoroka miezi miwili iliyopita)
Vipeoeo Weusi season 2 tuko Episode 71
Pia tuna Simulizi mpya inaitwa Shah Tazamon iko sehemu ya Tano.

Hii ndio shughuli yangu mkuu. Naandika, nalala, naamka, naandika tena. Kila siku, mwaka mzima, miaka yote.

And elfu tano ni ndogo sana chief, kuanzia tarehe 1 January nitaongeza kiduchu.
Naomba namba ya kujiunga ya watsap
 
Joined
Aug 27, 2018
Messages
76
Points
125
Joined Aug 27, 2018
76 125
Kaka mkubwa The Bold kama sijakosea wakati unaanza kuitoa hii story hapa ulituahidi kwamba hii story itaisha pia ulituambia kwamba kwenye group lako la wasap imeshaisha sasa kama ni hivyo kwanin usitubwagie mzigo wote hapa sisi tupambane nao kuliko kuwa unatuletea vipande then unapotea kama story unayo yote wew tuwekee tusome au kama unataka tuilipie pia utuambie. Samahani kama ntakukwaza
 

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,439
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,439 2,000
Shukrani mkuu.

Nimekuelewa vyema. Nitazingatia..
2008 BADO UKO HIGH SCHOOL, basi ww ni kijana mdogo na unafanya kazi nzuri katika uandishi, ila nakushauri swala moja. Kama umeamua kutoa stori kwa watu ili wajifunze humu ndani jitaidi tu uikamilishe isije ishia njiani.

Pia ili umakini wako usitie shaka weka siku moja ya kudondosha episode za stori hii hata kama ni kila baada ya siku 7, 14 ama hata mara moja kwa mwezi litakuwa limekupa credit kubwa mnoo zaidi ya hivi kwenda zigzag.

Lakini pia kazi ya uandishi ni ngumu kama stori zako unaamua zisipatikane for free mwanzo wa story zako toa taarifa utaratibu wa kuipata story husika ili wenye nia ya kuipata waweze ipata kwa utaratibu wako kuliko kuanza ikifika kati ndo unaaanzisha inshu hizo.

Baada ya kuanza kusoma hii story nikaamua kusoma na story zingine ulizoandika ni nzuri na zenye mafunzo kwa wenye kutaka kujifunza ila nimegundua huwatendei haki wasomaji wako kwani kuna baadhi nimeona zimeishia kati.

ALL IN ALL unafanya kazi nzuri tena sana. Ni ushauri tu unaweza ufanyia kazi ama la.
 

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,439
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,439 2,000
Stori itaisha chief... mimi ni mtu wa kusimamia neno langu.
Hivi mpaka tumefika sehemu ya kumi bado kuna mtu anadhani tunaishia njiani??? Smh

Yani tumeanza sehemu ya 1, 2, 3, 4, 5....... 10
Bado kuna mtu ana mashaka. C'mon
Kaka mkubwa The Bold kama sijakosea wakati unaanza kuitoa hii story hapa ulituahidi kwamba hii story itaisha pia ulituambia kwamba kwenye group lako la wasap imeshaisha sasa kama ni hivyo kwanin usitubwagie mzigo wote hapa sisi tupambane nao kuliko kuwa unatuletea vipande then unapotea kama story unayo yote wew tuwekee tusome au kama unataka tuilipie pia utuambie. Samahani kama ntakukwaza
 

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,439
Points
2,000

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,439 2,000
Asante sana mkuu..
Kuna vi mtu vinakuja na sera uchwara oooh mara anayatoa mtandaoni mara watu wavivu wa kujisomea, we unahisi kufukunyua habar na kuziunganisha zikaleta radha ni kazi ndogo? Shwain kasomen nanyie mtuletee kama mnaweza .....manna. Big up King of articles in JF "Bold"
 

mbutamaseko

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Messages
382
Points
500

mbutamaseko

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2018
382 500
ROMAN ABRAMOVICH: UTAJIRI EA DAMU, RISASI NA UMAFIA


SEHEMU YA KUMI


(Wale wote waliojipa mission ya kunitukana na kunikashifu kwenye comments nina neno moja kwenu… nyinyi ni wana wa Mungu na kwa sababu hiyo nawapenda sana)


Nilisema nitaeleza kidogo kuhusu Deripaska ambaye Abramovich alitambulishwa kwake na Berezovsky. Deripaska ni aina ya wasomi ambao wametumia taaluma yao vyema kujichumia utajiri. Tangu akiwa bado kijana mdogo tu Deripaska alikuwa na shauku kubwa mno ya kujisomea na kitu angalinacho hata sasa. Huyu bwana hata sasa ukifika ofisni kwake makau makuu ya Basic Elements jijini Moscow kwenye jengo hilo kuna kuta nyingi ambazo zina shelves za vitabu kuanzia chini mpaka juu. Deripaska alikuwa na kipawa kikubwa cha hisabati tangia utoto. Mwaka 1993 alihitimu chuo kikuu ‘with honors’ shahada ya fizikia kutoka Moscow State University. Miaka miwili baadae alihitimu shahada ya uzamili katika uchumi kutoka Plekhanov University of Economics.

Ndoto ya awali Deripaska ilikuwa ni kuwa msomi mbobezi kama ‘Theoretical physicist’. Lakini utakumbuka kwamba kipindi hiki ndicho ambacho Soviet Union ilidondoka. Hapo awali wanafunzi wote walikuwa wanasoma kwa udhamini wa serikali lakini baada ya Soviet Union kudondoka elimu ikawa ghali na serikali kuacha kugharamia masomo ya wanafunzi. Kwa hiyo kwa kijana kama Deripaska ambaye mwenyewe anasema kwamba hata hela ya kula ilikuwa ni tatizo kwake kipindi hicho hakukuwa na uhalisia wa yeye kuweza kugharamia masomo yake mwenyewe.

Lakini pia kipindi hiki kama tulivyoona awali kilikuwa ni kipindi chenye fursa nzuri kwa mtu kujilimbikizia utajiri. Kwa hiyo Deripaska akiwa na miaka 25 tu alishawishi wanasayasi wengine kadhaa manguli wa hesabu, fizikia na hata rocket science kuungana naye kuanzisha kampuni ya ‘ku-trade’ metals. Kampuni hii waliita VTK, na Deripaska ndiye alikuwa mwanahisa mkubwa kuzidi wenzake. Deripaska alikuwa ni moja ya watu wa mwanzo kabisa nchini Russia kutumia mifumo ya kisayansi na ‘systematics’ katika kutrade commodities. Unaweza kujiuliza namna gani anatumia sayansi kutrade commodities… binafsi huwa natrade currencies na huwa nawaambia watu ‘trading’ ni science and mathematics na ndio maana watu wengi hawako successful wakitaka kuwa traders… kwa nini? Kwa sababu sayanasi na hisabati sio kitu chepesi.
Uzuri ni kwamba Deripaska alikuwa ni nguli wa hisabati kwa hiyo VTK ilikuwa kwa haraka sana. Deripaska alikuwa ananunua commodities kwa bei ya chini ndani ya Urusi na kwenda kuziuza kwa bei ya juu kwenye soko la dunia.

Kwenye sehemu za mwanzo kabisa za makala hii nilieleza kwamba kipindi serikali ya Russia inabinafsisha viwanda na makampuni ya umma waligawa voucher kwa wananchi ili watumie voucher hizo kununua hisa kwenye makampuni ambayo yalikuwa yanabinafsishwa. Nilieleza kwamba kila mwananchi alipewa voucher ya Rubble 10,000 za Urusi. Kama ambavyo ilitokea hapa kwetu Tanzania wakulima walivyouza vocha za pembejeo za kilimo ndivyo ambavyo pia Warusi walivyouza voucher zao kwa matajiri. Deripaska ni moja ya matajiri hawa ambao waliwekeza hela ya kutosha kununua voucher kwa wananchi.

Kama mwaka mmoja tu baadae Deripaska alitumia voucher zote na faida yote aliyoipata kwenye kutrade commodities kununua hisa kwenye kiwanda cha Sayanogorsk Aluminium Smelter. Hiki ndicho kilikuwa kiwanda kikubwa zaidi cha uzalishanji aluminium nchini Rusia. Uwekezaji wake huu mkubwa ulimpatia hisa 20% za kiwanda hiki. Kwa wingi huu wa hisa ulimfanya Deripaska kuwa mwanahisa mkubwa zaidi nyuma ya serikali kwenye kiwanda hiki. Yaani mwenye hisa nyingi zaidi alikuwa serikali na yeye alikuwa namba mbili.

Kutokana na ushawishi huo mkubwa aliokuwa nao kwenye kiwanda cha Sayanogorsk Aluminium Smelter kwa sababu ya kuwa na hisa nyingi kuzidi mtu yeyote binafsi, mwaka 1994 Deripaska alifanya ushawishi kwa wanahisa wengine na kupewa Ukurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo. Nikukumbushe tu kwamba mwaka huo 1994 wakati anapewa ukurugenzi mkuu wa smelter kubwa zaidi nchini Russia alikuwa ana miaka 26 tu.

Miaka mitatu baadae yani mwaka 1997 Deripaska alianzisha Sibirsky Aluminium Group ambayo aliitumia kama kampuni mama ‘kuhold’ kampuni zake zote nyingine na shares zake zote kwenye makampuni mengine.

Kwa hiyo huyu ndiye mtu wa pili ambaye Berozovsky alimtambulisha Abramovich kwake.

Naweza kusema kwamba huyu pengine ndio alikuwa mtu muhimu zaidi kwa Abramovich kumfahamu labda nyuma ya Berozosky tu pekee. Licha ya umuhimu wake mkubwa ambao tutauona hivi punde lakini pia bwana huyu walikuwa na mengi ya kufanana. Ukipiga hesabu yako sawasawa utaona kwamba Abramovich alikuwa anamzidi mwaka mmoja tu Deripaska. Yaani kipindi kile Abrampvich anapewa Baraka na Putin kuingia kwenye biashara ya Aluminium akiwa na miaka 33, Deripaska alikuwa na miaka 32.

Wote wawili walikuwa ni vijana wadogo sana. Wote wawili wametokea kwenye maisha ya hali ya chini sana. Wote wawili wanajua namna ya kuishi kimkakati. Wote wawili walikuwa na ushawishi mkubwa sana. Abramovich kwenye system ya serikali na Deripaska kwenye ulimwengu hatari wa biashara ya Aluminium.
Wenye unyoya wa kufanana… huruka pamoja.

Nilieleza kwamba mwaka huo alipopewa Baraka na Putin kuingia kwenye biashara ya Aluminium, Abramovich alifungua kampuni iliyoitwa Millhouse Capital ambayo ilisajiliwa nchini Uingereza. Kampuni hii ilikuwa inatrade commodities. Tufahamu kwamba mpaka muda huu kampuni hii haikuwa lolote wala chochote. Haikuwa na ‘volumes’ kubwa kwenye kutrade hizo commodities wala assets za maana. Thamani pekee ya kampuni hii iliyokuwa nayo ni ile u kwamba inamilikiwa na Roman Abramovich.

Abramovich alipotambulishwa kwa Deripeska alikuwa na ombi moja tu kwake… waunganishe kampuni zao Millhouse Capital ya Abramovich na Sibirsky Aluminium Group ya Deripaska na iwe kampuni moja. Kwa umombo dili kama hii wanaita ‘merger’.
Unaweza kuona kwamba ombi hili lilikuwa ni la kijinga… Sibirsky Aluminium Group ilikuwa kwa muda huo ni kampuni kubwa sana ndani ya Russia inayomiliki smelters kadhaa kubwa kubwa ndani ya Russia na pia ilikuwa kampuni mama ya trading companies kama vile ile VTK ambayo deripaska aliinzisha na wanasayansi wenzake. Wakati ambapo Millhouse Capital ya Abramovich ilikuwa kama ni kampuni jina tu yenye ofisini bila mali kubwa kubwa kulinganisha na Sibirsky Aluminium Group.

Ajabu ni kwamba Deripaska hakusita hata kwa sekunde kukubali ombi hilo. Alikubali mara moja waunganishe kampuni hizo mbili kuwa moja ambayo watakuwa wanaimiliki wote.
Kwa nini akubali kirahisi hivi? Wendawazimu?... hapana, kama ilivyo kwa Abramovich ndivyo hivyo hivyo pia ilivyo kwa Deripaska… ni mtu wa mikakati. Anaiona miaka ishirini ijayo leo.

Kuna mambo mawili…

Thamani halisi ya kitu haitokani na hali yake ya sasa bali thamani yake ni ile ‘potential’ iliyonayo kuleta mafanikio huko mbeleni. Yaani kwamba tukiwaza kibiashara… kwa mfano utajiri au umasikini wa mtu haupimwi kwa kile alichonacho sasa bali ‘potential’ aliyonayo kupoteza zaidi au kuingiza zaidi kwa siku na miaka ijayo. Unaweza kuwa na milioni mia moja leo hii lakini kuna mtu akikuangalia anakuona masikini. Labda kwa namna fulani amegundua ndani ya miezi michache tu utazipoteza zote. Na unaweza kuwa na elufu kumi tu mfukoni na mtu mwingine akakuona tajiri kwa sababu anahisi potential uliyonayo mwakani tu unaweza kuwa na bilioni umelaza benki.

Napenda mifano hai, nitoe mfano mfupi halisi…
Mwaka 2008 nilikuwa na rafiki yangu tulikuwa darasa moja Tambaza High school. Huyu kwao walikuwa na haueni sana. Mzee wake alikuwa afisa mwandamizi wa serikali kwenye kitengo fulani. Alikuwa na safari za mara kwa mara nje ya nchi. Kuna safari moja aliporejea alimletea zawadi ya simu ya iPhone. Hiyo ni mwaka 2008 ambapo unaweza kutembea mjini kutwa nzima bila kuona mtu hata mmoja mwenye simu aina ya iPhone. Unaweza kupata picha ni kiasi gani yeye mwenyewe na sisi 'washkaji' zake tulikuwa ‘tunavimba’ shuleni… ndio hata sisi wapambe wake tulikuwa tunajiona kama simu yetu. Loooh.!!
Basi tukaanza ‘uzungu uzungu’ hivi… kutaka kujua mambo ambayo yanatrend huko duniani. Mara tukafahamu kuhusu facebook… hu ni mwaka 2008… sikumbuki kuwahi kumsikia mtu yeyote kabla akitaja facebook. Kilikuwa ni kitu kipya ambacho hapa nchini kilikuwa hakijulikani kabisa kabisa. Kipindi kile ‘chat rooms’ ndio zilikuwa maarufu sana hapa nchini. Pale shuleni kwetu ni ‘genge’ letu tu nadhani ndio ambao tulikuwa na akaunti za facebook na hata sisi ni baada ya kusikia ni kitu ‘hot’ huko duniani.

Kutokana na udadisi sikuishia tu kuitumia facebook bali nikaanza kuichimba. Ndio nikafahamu kuhusu mmiliki wake bwana Mark Zuckerberg na kipindi kile akisemwa kuwa ndio Bilionea kijana zaidi duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 2.4 akiwa na umri wa miaka 26 tu. Nikawa najiuliza sana… huyu mtu anawezaje kuwa tajiri mkubwa kiasi hicho wakati huduma hiyo tunaitumia bure? Kipindi kile facebook haikuwa na matangazo kama sasa na ilikuwq sehemu ya sera yao kutokuweka matangazo kwenye mtandao wao… hakukuwa na tangazo hata moja na wala walikuwa hawapokei matangazo. Na pia wala walikuwa hawajafanya ile IPO… ile kuirodhesha kwenye soko la hisa na kuanza kuuza shares kwa umma. Kipindi kile hata financial documents za kampuni zilikuwa zinaonyesha kwamba kwa mwaka wanapata zero revenue? Inakuwaje huyu mtu awe tajiri hivi? Hizi hela zinatoka wapi? Hawa wazungu wanatuzuga na uongo au nini?

Wewe unadhani hela za Mark zilikuwa zinatoka wapi kipindi kile? Kwa nini kipindi kile waseme ana utajiri wa dola bilioni 2.4?

Jawabu ni 'Speculation'… ‘potential’ ambayo watu wanaiona kwa kitu hicho kutengeneza faida kubwa kwa wakati ujao. Sikumbuki sawasawa lakini nadhani kipindi kile Facebook ilikuwa na watumiaji kama milioni 300 hivi duniani. Kwa hiyo kulikuwa na speculation kubwa kwamba hii kampuni siku yoyote ile ‘ita-boom’ na kuleta fedha nyingi. Na hii ndio ilikuwa inafanya thamani ya kampuni ya facebook kuwa kubwa na kumfanya Mark kuwa na utajiri wote ule. Lakini kiuhalisia kwa kipindi kile hawakuwa wanaingiza revenue hata kipande ukiachaa hela za investors.

Sasa hiki ndicho ambacho Deripaska alikuwa anakiona kwa Abramovich… potential. Potential gani? Abramovich alikuwa ni ‘mtoto’ pendwa wa Putin. Putin alikuwa anamuamini Abramovich kuzidi mtu yeyote yule. Kwa hiyo kama akiwa mmiliki mwenza wa kampuni moja na Abramovich, basi hakuna anga ambalo litawashinda kulivuka na wanaweza kutengeneza moja ya kampuni tajiri zaidi duniani.

Nilisema kuna mambo mawili… hiyo ilikuwa sababu ya kwanza. Sababu ya pili ilikuwa ya busara zaidi. Isingelikuwa busara kwake kumkatalia Abramovich kwasababu, ‘If Roman wants something… Roman gets something.!” Kama angemkatalia ofa hiyo Abramovich, basi Abramovich angetafuta namna nyingine ya kukipata kiwanda hicho na njia hiyo nyingine ingekuwa hasara kwa Deripaska. Abramovich ni aina ya watu ambao lazima wapate wanachokitaka… hakuna kiunzi ambacho atashindwa kukiruka.

Kwa hiyo wakaunganisha kampuni zao, Millhouse Capital na Sibirsky Aluminium Group na kuunda kampuni mpya inayoitwa RUSAL (siku hizi inaitwa United Company RUSAL).

RUSAL ilikuwa kwa haraka sana. Walichokuwa wanakifanya… walikuwa wananunua viwanda vingine na migodi ya boksiti ndani ya Russia na nchi jirani. Maoligarch ambao walikuwa wanamiliki viwanda hivyo na migodi ilikuwa ni eidha uwauzie RUSAL kiwanda chako kwa hiari au wakichukue kwa lazima. Ukikubali kuwauzia wanakulipa hela… ukikataa kuwauzia kesho kutwa tunaokota mwili wako jalalani.
Kuna ‘transcript’ za mahakamani kutoka Uingereza za mwaka 2010 ambapo Abramovich aliitwa kutoa ushahidi kwenye kesi fulani, anakiri kwamba hizi aluminium wars zilikuwa moto kweli kweli kiasi kwamba yeye binafsi anakumbuka kwa miaka ya 2000 na 2001 kwa wastani wa kila baada ya siku tatu ulikuwa unasikia mwii wa oligarch fulani umeokotwa.

Na hapa ndipo ambapo ulikuja umuhimu wa Badri Patarkatsishvili yule jamaa wa kwanza aliyetambulishhwa na Berezovsky. Unapojihusisha na sekta ambayo kila kukicha unasikia wenzako wanakufa lazima uwe na tahadhali makini haswa. Huyu Badri nilieleza kwamba alikuwa anajua kudili na Mafia.
Unapomwaga damu za wenzako lazima kuna marafiki zao na ndugu zao na hata wale wengine wanajihisi nao siku utawamaliza, wote hawa watajihami kwa kutaka kukumaliza wewe. Ilifika kipindi ndani ya Russia Abramovich alikuwa hawezi hata kuonekana hadharani… kila oligarch aliyekuwa bado hai alikuwa ameweka vijana kumuwinda na kutaka kumuua. Ndio hapa ambapo Abramovich ilimbidi kulipa zaidi ya dola milioni 500 kupitia kwa Badri kwenda kuhonga kila kikundi cha mafia ndani ya Russia ambacho kilitumwa kumuua yeye na kisha kuwapa agizo jipya wakawamalize wale ambao waliwatuma awali.

Nchi ilichafuka haswa kwa vifo vya maoligarch… lakini RUSAL ilizidi kupaa. Ndani ya miaka miwili tu walikuwa wana-control karibia migodi yote muhimu ya boksiti na viwanda vyote vikubwa vya Aluminium ndani ya Russia na nchi jirani. Kuanzia viwanda vya Armenal foil mill nchini Armenia mpaka Belaya Kalitva Metallurgical plant na Novokuznetsk aluminium smelter nchini Russia. Uje migodi ya boksiti ya Friguia bauxite na Alumina complex mpaka Kindia Company. RUSAL ilipaa juu kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji wa aluminium duniani. Lakini hapana… Abramovich hakutaka kuwa ‘moja ya’ kampuni kubwa duniani. Alitaka kuwa kampuni kubwa zaidi duniani ya uzalishaji aluminium.

Afanyeje? Kulikuwa na ‘terget’ ya mwisho… Krasnoyarsk.

Kipindi hicho jimbo la Krasnoyarsk ndilo lilikuwa na hifadhi kubwa zaidi ya migodi ya boksiti. Sasa pale Krasnoyarsk kulikuwa na kiwanda cha aluminium kinachoitwa Krasnoyarsk Aluminium Smelter. Kiwanda hiki kilikuwa kinamilikiwa na oligarch anaitwa Anatoly Bykov. Huyu oligarch alikuwa ni kijana kama wao akina Abramovich japo alimzidi Abramovich miaka miwili kwa kuzaliwa. Kampuni yake ambayo ndiyo ilikuwa inamiliki Krasnoyarsk Aluminium Smelter kwa kipindi hicho iikuwa inashika nafasi ya pili nyuma ya RUSAL kwa uzalishaji Aluminium. Abramovich tayari alikuwa amemfuata na kumpa ofa mara kadhaa kuwauzia kampuni lakini Bykov alikataa. Mpaka muda huo alikuwa amefanikiwa kukwepa majaribio 26 ya kumuua.

Kwa hiyo huyu oligarch biashara alikuwa anaijua kama wao na uhuni wa kimafia pia alikuwa anaujua.

Kama Abramovich akifanikiwa kuchukua kiwanda hiki cha Krasnoyarsk Aluminium Smelter maana yake ni kwamba atafanikiwa kuifanya RUSAL kuwa kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji aluminium duniani.

Lakini Bykov alikuwa amejiapiza kutowauzia kiwanda chake na majaribio ya kumtoa roho yalishindikana mara 26.
Abramovich si mtu wa kukubali kushindwa vita… “Roman wants something… Roman gets something.”

Alikuwa anahitaji mbinu mpya… Abramovich alijiapiza kuwa hataki tu kuwa na ‘moja ya’ kampuni kubwa zaidi duniani ya kuzalisha aluminium...alitaka kuwa na kampuni kubwa zaidi duniani ya kuzalisha aluminium.

Alikuwa anahitaji ‘kuchemsha muarobaini’ mpya wa kumnywesha Bykov.


Bold… Nitarejea.

To Infinty and Beyond
Mkuu epuka uongo. umesema unawapa neno moja wanaokutukana, lakini umewapa maneno kumi na moja. Huoni kama umedanganya mara kumi zaidi. Punguza uongo kidogo Itakusaidia
 

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2016
Messages
611
Points
500

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2016
611 500
kazi ya uandishi jamen si nyepesi nyepesi ka kusoma unaweza soma Gazeti kwa nusu saa story ambazo zieandaliwa kwa masaa mengi pamoja na mlolongo wa uhariri tuwe na tabia ya kujiuliza muda anaotumia kuandika Simulizi hizo na kuzitafuta kuzichambua anaupata wapi

pia ye Kabuni wazo la kumpatia kipato cha ziada we niuamuzi wako kukaa na stress zako ukamalize unakojua au baki na debe tupu ukapige kelele uko.

nawe buni chako just unaweza mfanyia exploitaions ukalipia wewe 5000 ukaenda bandika kwa blog yako kwa stail hiyo hiyo uvutie users kuja kila siku ukarudisha pesa yako with extra coins

internet ni soko unaloweza uza nothing na hakuna lawama buy or not buy its belong to your pocket or rocket your heart
 

Pacbig

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2017
Messages
243
Points
500

Pacbig

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2017
243 500
kazi ya uandishi jamen si nyepesi nyepesi ka kusoma unaweza soma Gazeti kwa nusu saa story ambazo zieandaliwa kwa masaa mengi pamoja na mlolongo wa uhariri tuwe na tabia ya kujiuliza muda anaotumia kuandika Simulizi hizo na kuzitafuta kuzichambua anaupata wapi

pia ye Kabuni wazo la kumpatia kipato cha ziada we niuamuzi wako kukaa na stress zako ukamalize unakojua au baki na debe tupu ukapige kelele uko.

nawe buni chako just unaweza mfanyia exploitaions ukalipia wewe 5000 ukaenda bandika kwa blog yako kwa stail hiyo hiyo uvutie users kuja kila siku ukarudisha pesa yako with extra coins

internet ni soko unaloweza uza nothing na hakuna lawama buy or not buy its belong to your pocket or rocket your heart
Unashauri wizi?
 

Beberu

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Messages
832
Points
1,000

Beberu

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2017
832 1,000
Mkuu the bold mm naomba nikupe ushauri wa kibiashara

Kwa kuwa sometime kuitoa buku tano ni ngumu na wengine hawapendi magroup mengi ya watsap bas jaribu kuuza story moja moja

Mfano kama hii ulipo fikia sehemu ya tano ungeweza kutangaza anaeitaka yote atume hata 1000 au 500 atumiwe watsap mmalizane moja kwa moja


Nitashukuru ukisoma hapa na kujibu pia kama itawezekana
 

Forum statistics

Threads 1,343,297
Members 515,007
Posts 32,779,645
Top