Roma bado inatawala dunia

KIUFUPI KABISA KITABU CHA DANIELI
Kitabu hiki kinakadiriwa kuwakilinadikwa
mwaka 165 K.K. kipindi ambacho Waisraeli
kutoka ufalme wa Yuda walikuwa wakitawaliwa
na Wagiriki waliotawala kutoka 333-63 K.K.
Mwandishi akiwa mtu kutoka ufalme wa Yuda
aliandika kitabu chake hususani sura ya 7 kwa
kuzingatia historia ya utawala wa ufalme huo
wa Yuda.
Hivyo mwandishi anawafariji watu waliokuwa
katika enzi ya madhulumu yaliyofanywa na
__ Wababeli kutoka mwaka 587-539 K.K.
___ Wamedi 539 K.K. (Isa 13:17).
___ Waajemi 538-333 K.K.
___ Wagiriki 333-63 K.K.
SASA NAOMBA NIJARIBU KUKUELEZEA
BAADHI YA AYA AMBAZO HUTOLEWA TAFSIRI
POTOFO NA BAADHI YA WATU
Mwandishi katika sura ya 7:1-12 anatumia
wanyama wanne ili kuwasilisha ujumbe wake.
Ukweli huu tunapata tunaposoma Dan 7:1-12; “
Danieli akanena, akisema: naliona katika maono
yangu wakati wa usiku, na tazama, hizo pepo
nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya
bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne
wakatoka baharini, wote wanamna
mbalimbali.” (Dan 7:2-3).
Na ukisoma Dan 7:15-28 mwandishi anatoa
tafsiri ya maono aua ndoto inayosimuliwa
kutoka Dan 7:1-14.
Wanyama hao wanne ni wafalme wa falme nne
zilizotokea duniani. (rej. Dan 7:17). Mnyama wa
kwanza alikuwa kama simba (7:4); mnyama
huyu anasimama badala ya ufalme wababeli
ambao walikuwa wa kwanza kuwatawala
Waisraeli walioishi ufalme wa kusini – ufalme
waYuda – kutoka587- 539 K.K.
Mnyama wa pili alikuwa kama dubu (7:5).
Mwandishi alimtumia mnyama huyu (dubu)
kama jina bndia la ufalme wa Wamedi
waliotawala kwa muda mfupi sana – yaani 539
K.K.
Mnyama wa tatu ni chui (7:6). Chui anasimama
badala ya ufalme wa Waajemi lililokuwa taifa la
tatu kuwatawala Waisraeli walioishi katika
ufalme wa Yuda. Waajemi walitawala kutoka
ufalme 538-333 K.K.
Mnyama wa nne anayeelezwa katika Dan 7:7-8
na ambaye hatajwi jina lake ; na ambaye
anaonekana kuwa ni mwenye kutisha sana, ni
ufalme wa Wagiriki ambao ulikuwa ufalme
shupavu uliowatawala Waisraeli kutoka 333-63
K.K.
Katika kitabu cha Dan 7:7-8 tunasoma hivi: “…
mnyama wa nne mwenye kutisha, mwenye
nguvu, mwenye uwezo mwingi, nayw alikuwa na
mwno ya chuma, makubwa sana; alikula na
kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga
mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa
mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa
na pembe kumi, nikaziangalia sana pembe
zake, na tazama, pembe nyingine ikazika kati
yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbgele yake
pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa
kabisa; na tazam, katika pembe hiyo moikuwa
na macho kama macho ya mwanadamu, na
kinywa kilikuwa kikinena mneno makuu.” (rej
Dan 7:7-8).
Pembe 10 ni wafalme 10 ambao wataondoka
katika ufalme huo. (Dan 7:24a). na Dan 7:24b
panasomeka hivi; “na mwngine ataondoka
baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa
kwanza, naye atawashusha wafalme watatu.’
Mfalme anayedokezwa katika Dan 7:24b ni
mfalme Antioko Epifani ndiye anayesemwa
kuwa atawashusha wafalme watatu. Ni mfalme
aliyeziangamiza falme tatu zilizokuwepo nyakati
zake. Na wafalme wa falme hizo tatu
walioshushwa ni: mfalme Ptolemy VI
Philometor mnamo mwaka 169 K.K.; mfalme
Ptolemy VII Euergete mwaka 169 K.K.; na
mfalme Artakias wa Armenia katika mwaka
166 K.K.
Ukisoma Dan 7:25, naadokezwa mfalme
ambaye atanena maneno kinyume chake Aliye
juu,naye atawadhoofisha watakatifu wake Ailye
juu. Mfalme huyo pia ni Antioko Epifani
ambaye aliwalazimisha Wayahudi (walioishi
Palestina) kufuata utamaduni wa Kiyunani aua
Kigiriki kwa kuiacha dini yao katika Mungu wa
kweli na kufuata dini ya Kipagani kama
tusomavyo 1Macc 1:41-64. Ili kufanikisha
lengo lake la kukomesha dini ya Kiyahudi na
kueneza utamaduni wa Kigiriki aliamuru hekalu
la Zeus – mungu wa kipagani; pia alipiga
marufuki kwa Wayahudi kutahiriwa kama
Torati ilivyodiwa.
Kadiei ya Wayahudi kuiabudu miungu ya
kipagani ilikuwa ni kuvunja amri ya Mungu ya
kutoabudu miungu wengine. (Kut 20:3; 34:14
Kumb 5:7). Na kupiga marufuku kutahiri ilikuwa
ni kupingana na agizo la Mungu kuwa kila
mwanaume atahiriwe kma ishara ya agano
alilofanya Mungu na taifa
 
la Israeli. Rej. Mwa
17:10-11 “Hili ndilo agano langu utakalolidhika,
kati ya nini na wewe, na uzao wako baada
yako: kila mwanaume wa kwenu atatahiriwa.
Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo
hilo litakuwa ishara ya nini na ninyi.”Mwa
17;10-11l.
Kutahiriwa kulimfanya mmoja kuwa mali ya
Mungu. Na kutotahiriwa kulimfanya mmoja
kuwa malia ya Mungu. Na kutotahiriwa
kulimfanya mmoja kutengwa na jamii ya taifa la
Mungu.
kadiri ya maelezo hayo na kadiri ya tafsiri
iliyotolewa katika Dan 7:15-27 juu ya maono
yaliyoandikwa katika Dan 7:1-14, pembe ndogo
nayotajwa katika Dan 7:8
Kusema kwamba pembe hiyo ndogo ni kanisa
katoliki sijui ni papa AU MAREKANI kunaonesha
kuwa Biblia hawaisomi ipasavyo; wameamua
kuinyofoa aya hiyo ya 8 katika sura ya 7 ya
kitabu cha Danieli na kuipa tafsiri isiyo na
ukweli ndani mwake. Nimesema wameamua
kuinyofoa aya hiyo moja bila kusoma angalau
sura yote ya saba ya kitabu cha Danieli kwa
sababu maono yaliyoandikwa katika Danieli
7:1-8 yamefuatiwa na tafsiri yake aya chache
tu baadaye.
pembe ndogo inayoelezwa katika Dan 7:8 ni
mfalme Antioko Epifani aliyeongoza ufalme wa
Wagiriki. Mfalme Antioko Epifani anaitwa
pembe ndogo kwa sababu, kati ya wafalme
wote wadola ya Kigiriki, ni yeye peke yake
aliyeshindwa kumudu vizuri utawala wake.
KIUFUPI KITABU CHA UFUNUO
Kitabu cha ufunuo ni kitabu kilicho andikwa kwa
kificho kwa lugha yakufichaficha ili wale
wahusika waliokuwa wakiendesha mateso na
unyanyasaji kwa Wakristo wasiweze kugundua.
Kitabu cha Ufunuo kinaandikwa kipindi Wakristo
wapo kwenye mateso makali. Hakika kilikuwa ni
kipindi ambacho Mungu alikuwa haja waadhibu
watesaji na kutoa ushindi mnono kwa Kanisa
kama Kristo mwenyewe alivyo ahidi “nitakuwa
nanyi mpaka ukamilifu wa dahali” (Mt. 28:20).
Na hivyo kulikuwa hakuna kitu cha kuogopa
tena. Hakika ni kitabu cha ushindi wa kanisa
lililoteswa na kinabaki kuwa kitabu
kinachoonesha kilele cha matumaini ya
Wakristo.
hivi sasa naomba tuone kwa pamoja nani ni
mwandishi hasa wa kitabu hiki cha Ufunuo.
Ukisoma kitabu hicho cha Ufunuo wa Yohane
sura 1:9 mwandishi anajiita Yohane nanukuu
“Mimi Yohane, ndugu yenu na mwenye kushiriki
pamoja nanyi katika mateso na ufalme na
subira ya Yesu Kristo”. Ingawa baadaye
kunamiono mbalimbali kuhusu nani hasa
mwandishi wa kitabu hiki haya yanatokea
baada ya watu kusoma na kupenda kufanya
uchunguzi hiki siyo kitu kibaya na yafaa
kiendelee ili tuzidi kulielewa zaidi neno la
Mungu.
Kuhusu tarehe ya kitabu kuandikwa kuna
miono miwil i, muono wa kwanza unasema
kitabu kiliandikwa 81-96 mwishoni mwa utawala
wa Domisiari. Ambaye alikuwa ni katili na watu
walimfananisha na mfalme Nero. Mtazamo wa
pili ni huu kwamba kitabu kiliandikwa miaka ya
nyuma zaidi yaani miaka ya 64 wakati wa
mateso yaliyoendeshwa na mfalme Nero.
(58-68)
Natena kuhusu sehemu au mahali kitabu kitabu
kilipoandikwa tunapata jibu kutoka kwenye
kitabu hicho hicho. Sura 1 aya 9 “Nalikuwa
katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya
neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. nikipindi
ambacho Yohane alikuwa uhamishoni kwa ajili
ya neno la Mungu.
Baada ya kuona nani mwandishi na tarehe ya
kuandikwa, sasa ni vema na haki kabisa tuone
nani alikuwa mlengwa wa kitabu hik i.,
walengwa hasa wa kitabu hiki ni makanisa
saba yaliyokuwa Asia ndogo. Makanisa hayo ni
Thyatira, Pergamum, Smrna,Sardis, Philadelphia,
Epheso na Laodicea. Ambapo makanisa haya
leo hii yapo magharibi mwa Uturuki.
sababu kubwa iliyopelekea kitabu hiki cha
Ufunuo wa Yohane kuandikwa ni mateso
makali (Rej Uf. 2:10, 12:7) hivyo mwandishi
alitaka:- Mosi, kuwafariji watu waliokuwa katika
mateso makali, Mbili , kuwaambia wabaki katika
nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu wao.
kama nilivyosema pale mwanzoni kuwa kitabu
hiki siyo rahisi hivyo kueleweka kwani
kiliandikwa kwa lugha ya kificho ili wahusika tu
wapate kuelewa bila maadui zao kuambulia
chochote. Hivyo nawaomba kwa pamoja tuanze
kuchambua sura na haya zenye maneno
magumu tukianzia na sura ya kwanza mpaka
ya mwisho ili tuweze kuelewa vyema maana
hasa ya kitabu hiki. L
 
Lengo kubwa hasa likiwa ni
kuondoa tafsiri zisizo sahihi kuhusu kitabu hiki.
Ndugu biblia sio gazeti la udaku au mwananchi
tunapotafuta ukweli wa kibiblia unapaswa kujua
vifuatavvyo
elimu juu ya mazingira ya uandishi, historia,
utamaduni wa jamii za wakati Biblia
inaandikwa, jiogarafia ya nchi za Biblia,fani na
miundo ya vitubu vya Biblia; lugha ya Biblia na
mikazo ya kiteolojia: utaweza kuupata na
kuujua ujumbe aua maana sahihi ya Maandiko
Matakatifu
BASI NDUGU YANGU UKIONA MTU AU
MUHUBIRI ANAKOMAA KUKUELEZEA NA
KUKUTAFSIRIA ICHO KITABU CHA UFUNUO NA
DANIELI KILEO LEO MUANGALIE MTU HUYO
MARA MBILI MBILI NA KUWA MAKINI NAE
 
ndugu sikukatalii madai yako ila ningependa tu
kukwambia kwamba moja ya vitabu vigumu na
vilivyoandikwa kwa ufundi mkubwa ni DANIELI
NA UFUNUO
naomba ujue na kutambua wazi kuwa kitabu
hiki cha Ufunuo na danieli ni sawa na ndimu
au chungwa ambalo kabla ya kulila lazima
ulimenye kwanza
Kwa kifupi ni kwamba wengi wetu hatukijui kwa
undani kitabu hiki kwa sababu ya mafumbo
yake na hivyo kujaribu kutoa tafsiri ambazo
tunajisikia.
Ukinifuatilia vizuri utagundua kuwa wengi
walijaribu kutoa tafsri juu ya kitabu hiki lakini
mpaka sasa hakuna kilichofanikiwa kutokea na
hivyo tafsiri zao kukosa mashiko kabisa.
tatizo kubwa walilonalo baadhi ya wakristo
hasa ndugu zetu wasabato ni kwamba
wanalazimisha kuvitafsiri hivyo vitabu kileoleo
kana kwamba viliandikwa leo au jana au
vimeandikwa katika karne yetu hii ya 20
ukiitaji nikupe mifano ya baadhi ya tafsiri za
kisabato naweza kukupatia
tena kwa ile ambayo ilishindwa kutimia
na matarajio yao ya baadae kuhusu baadhi ya
aya za ufunuo na danie li
angalia mfano mmoja hapa chini
wasabato wengi waliamini kuwa kipindi
ambacho “Euro” ilipoanza kutumika kama fedha
ya umoja wa nchi za Ulaya ungekuwa mwisho
wa dunia wakilinganisha na kitabu cha Ufunuo.
Yote hayo hayakutokea
na ajabu ni kwamba wengi wanazidi kuamini
wakati huu kwamba ipo siku eti marekani
atalazimisha duniani kote kila mmoja kusali
JUMAPILI kama alama ya mnyama wa kitabu
cha ufunuoni ni kitambo tangu utabiri huo
kuonekana hauna maana kwa watu wenye akili
timamu.
na zaidi ukuomaa kuvitafsiri kana kwamba sisi
watu wa karne yahii ishirini ndio walengwa wa
kwanza kabisa wa ivo vitabu,
akati ndugu yangu kuna watu mahususi kabisa
kama walengwa wa kwanza wa ivo vitabu vya
danieli na ufunuo AMBAO WAO KUTOKANA NA
MAZINGIRA FULANI WALIOKUWA NAYO
WAKATI HUO NDIO ILIWABIDI HAO WAJUMBE
WA MUNGU KUVIANDIKA IVO VITABU kwa
malengo maalumu kwa ajili ya watu hao
usihamaki sijasema ivo vitabu au neno la
Mungu havitusu sisi kabisa la hasha ILA SISI,
MIMI NA WEWE TUNAWEZA KUINGIA NA
KUHUSIKA NA VITABU KAMA VYA UFUNUO NA
DANIELI IWAPO TU KATIKA UTUME WETU NA
KUMTANGAZA KRISTO TUTAKUMBANA NA
MAZINGIRA KAMA YA HAO WAHUSIKA WA
KWANZA WA IVO VITABU VYA UFUNUO NA
DANIELI
Na mwishoni, mwenzetu anatuuliza, “Nini hasa
fundisho la kitabu hiki? Kwa ujumla kitabu hiki
kina mafundisho mengi sana. Kwanza kinaeleza
manyanyaso waliyopata wazee wetu walioamua
kumfuata Kristo, kama haitoshi kinatupa
changamoto kuwa kumfuata Kristo ni jambo
linalo hitaji sadaka na masumbuo mengine
mengi.
AU TUNAWEZA KUJIFUNZA YAFUATAYO
KUTOKA KWENYE IVO VITABU
kitabu cha Ufunuo NA danieli kinatuhimiza
waamini tuvumilie mateso yetu kwa vile hata
Yesu mwenyewe alipitia njia ya mateso ili
kupata ushindi.
najua kwa hayo maelezo yangu hapo juu ,
ungeniuliza swali kuwa lakini ivo vitabu vya
danieli na ufunuo si vya UNABII
ni kweli ni vitabu vya unabii sikatai ila ni
kwamba UNABII UNAOZUNGUMZWA HUMO
NDANI YA IVO VITABU ULISHATIMIA ZAMANI
SANA KIASI KWAMBA HATA WAHUSIKA
WENYEWE (walengwa wa kwanza) WA IVO
VITABU WALISHA SAHAU KITAMBO SANA
na kama unabisha kuwa utabiri
unaozungumzwa humo kwenye ivo vitabu
HAUJATIMIA BADO nenda sasa ivi kule
wanakoishi wayahudi islaeli (koloni la wagiriki
kipindi icho kitabu cha danieli kinaandikwa )
ukawaambie eti kuna baadhi ya aya za unabii
wa danieli haujatimia bado, ndugu yangu
watakushangaa sana na utaishia kuchekwa tu
au enda sasa ivi kule wanakoishi wayahudi
islaeli (koloni la wagiriki kipindi icho kitabu
cha danieli kinaandikwa ) ukawaambie eti
MNYAMA ANAYEZUNGUMZIWA KITABU CHA
DANIELI SIJUI NI PAPA, SIJUI NI TRUMP AU
MAREKANI huone utakachojibiwa
yaani nakuhakikishia wewe mwenyewe ukirudi
utakuwa shahidi yangu
NDUGU NARUDIA KWA WATU WANAOFAHAMU
VYEMA MAZINGIRA YA IVO VITABU , SABABU
YA KUANDIKWA KWAKE NA HISTORI YA TAIFA
LA ISLAELI NA UKRISTO KATIKA KARNE ZA
KWANZA WATAKUAMBIA KUWA UNABII WA
UFUNUO NA DANIELI ULISHATIMIA KITAMBO
SANA KIASI KWAMBA HATA WAHUSIKA
WENYEWE WALISHA SAHAU NA IMEBAKI
HISTORIA TU
ndugu wahenga walishasema AKUTUKANAYE
AKUCHAGULII TUSI
 
Aliyekwambia jumapili ni siku ya kusali ni nan?
Wapi kwenye biblia imeandikwa?
Kwanini tunaweka sanamu kanisani?
Je zile picha zilizo kanisani ni za yesu? sura halisi ya yesu imehifadhiwa wapi?
Kwanii kwenye Salamu.Maria tunakiri kuwa Ni mama wa Mungu
Je mungu anazaliwa?
Ikiwa yeye ni mungu kwanin wakati anabatizwa na Yohane sauti inasikika ikitoka juu ikisema huyu ndiye mwanangu mpendwa nliye pendezwa naye...
Je huoni yupo mwenye mamlaka mkuu zaidi yake?
Je isingefaa iwe Mama wa mwana wa Mungu?
he he he ...NONDO hizi ""!!?
 
Bila shaka ndugu wewe ni msomaji wa vitabu vya Danieli na Ufunuo!
Ukisoma vizuri Danieli 9:20-27, utaelewa kwamba utawala wa Roma utatawala juma la 70 (wiki 1). Kinabii wiki 1 = miaka 7. Kipindi hicho kitaanza baada ya unyakuo wa kanisa (waliompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao walipokuwa duniani). Wakati huo serikali zote duniani zitakuwa chini ya serikali kuu moja zikipokea amri za kiutawala kutoka kwa mkuu mmoja ambaye ni serikali ya Roma (mfano wa utawala huo ni kama Raisi Magulifuli alivyo na mamlaka kwa wakuu wote wa mikoa yote ya Tanzania). Huyo Rumi (Kaisari) atatawala kwa kushirikiana na mataifa mengine 10 (rejea Danieli 2:33, 41 - sanamu aliyoota Nebukadreza). Wakati huo hakuna atakayekiuka amri hata moja ya mtawala huyo yaani Rumi. Huyo Rumi (Kaisari) atakuwa na nguvu sana, na ndiye Mpinga Kristo.
Tujiulize, kama Roma ndiyo inatawala dunia kwa sasa je, kila serikali iliyoko duniani inatii kila amri kutoka kwa huyo mkuu (Kaisari=mpinga kristo)? Je hizo serikali zinatekeleza policy za huyo Mrumi? Jibu ni hapana. Kipindi hicho bado hakijafika ila hakiko mbali (2Thesolanike 2:1-10). Wateule kuweni macho!
Sawa
 
Kwanza niseme kwamba mimi siyo Msabato. Mimi ni mkristo ninasali kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).
Umande fungua Biblia yako kitabu cha Danieli 2:29-45.
Aya hizi zinaonesha dola kuu ambazo zimetawala dunia tangu wakati huo (Nebukadreza alipoota ndoto hiyo) na zitakazotawala duniani hadi dunia hii itakapoondolewa. Falme hizi (dola kuu) zilikuwa na mamlaka kamili dunia nzima (serikali zote duniani zikiwa zinafuata amri kutoka dola hizo kuu). Ikumbukwe kwamba kabla ya Nebukadreza (Babeli) kulikuwa na falme kuu 2 zilizokuwa zimetawala dunia hii, nazo ni Misri na Ashuru. Ukisoma aya hizo utaona kwamba zenyewe hazikuzungumzwa:
Hizo dola kuu 4 tangu ndoto ya Nebukadreza zilizoitawala dunia yote ni kama ifuatavyo:
1. Dola ya Babeli - Kichwa cha dhahabu (Danieli 2:36-38) tangu mwaka 612KK hadi 539KK (Kabla ya kuzaliwa Kristo - KK)
2. Dola ya Umedi na Uajemi - Kifua na mikono ya fedha (Danieli 2:39) tangu mwaka 539KK - 333KK
3. Dola ya Uyunani - Tumbo la shaba (Danieli 2:39) tangu mwaka 333KK hadi 146KK
4. Dola ya Rumi - Miguu miwili ya chuma (Danieli 2:33, 40) tangu mwaka 146KK
Utawala wa dola ya Rumi uligawanyika sehemu mbili:
a. Rumi ya magharibi (Western Roman Empire) ambayo mji wake mkuu ulikuwa Roma (tangu mwaka 146KK hadi 476BK - (BK-Baada ya kuzaliwa Kristo)
b. Rumi ya Mashariki, mji wake mkuu ulikuwa Constantinople (tangu mwaka 146KK hadi 1453BK)

Dola 4 tayari zimekwisha itawala dunia yote, bado dola ya 5 ambayo ni "nyayo" (Danieli 2:33, 42,43). Dola hii ya 5 itakuja kuondolewa na ufalme mwingine utakaotawala milele na milele ambao mtawala wake hatakuwa mwanadamu (Danieli 2:44-45).
Swali; dola ya 5 ni mfalme wa dola gani?
Huyo mfalme atakayeondoa utawala wa dola ya 5 kisha kutawala milele na milele ni
nani?
Tutumie Biblia kudadavua hii mada muhimu! Karibuni.
UPADRE UNAKUHUSU AISEE
 
Hapa alieandika biblia alikuwa na IQ kubwa mpaka watu mnabishana kwa stor za kusadikika kutojielewa sisi ni kitu gani ndo kunasababisha kuwepo kwa sintofahamu kama hizi za mleta uzi
Kuna hasara kubwa walioturetea hawa watu hadi hatuwezi kujadili kujihusu sisi badala tunapigania assumption zao sisi zetu zi nalala
Hivi kwann mmelala kiasi hicho kwann amfikirii chochote zaidi kariri za vitabu kwann lakini
Mna macho hamuoni mna masikio hamsikii mna pua hamnusi kila mlango wa fahamu hamtumiii
Badilikeni badilikeni khaaaa. Sio siri mnakera
hasara. ...sana Hawa watu "" wameshindwa kustick kwenye mada" wanaanza kushambuliana kiimani...jinga kabisa.." Mara sijui petro ..Mara sijui Mudy"" wakati hao watu wanaowataja wala hawawajui....na hawana Uhakika kama niwatu kweli ambao walikuwepo tu duniani...au ni anonymous kama MAJINA YA KIPEPE NA MADENGE
 
Ndugu Mackie, tumia Biblia kujibu kwani mada hii ni ya kibiblia.
Enzi (dola) hizi ni za binadamu yaani watawala halisi ni wanadamu siyo roboti kama ulivyosema! Soma Danieli 2:43-44

Vipi huo ufalme utakaotawala milele na milele baada ya dola ya 5 ni ufalme gani?
Nadhani ufalme wa 5 utamalizwa na kiama then mungu mwenyewe atachukua usukani
 
Ni kweli!; ndio sababu waisilamu wanasali ijumaa wakisherehekea kwamba Yesu kafa...wasabato wanasali jumamosi wakifurahia Yesu yupo kaburini...Wakristo tunasali JPili tunasherehekea Bwana wa Mabwana kashinda kifo ni limbuko letu
Una uhakika na ulichokiandika hapa????
 
Ndio ume-post nini kila kitu kina makusudi yake, kama hujui umuhimu wa makalio kalia kichwa kama huzipendi emoji jidunge ndoba usepe
Emoji zinaendana na nini unaandika kwa mlengwa wa kipi kinamfikia.

Siyo kuzitumia tumia bila kujua umuhmu wake.

Sijaona umuhmu wa emoji pale zaidi kukariri kisa zipo.

Nafunga mjadala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom