Roma bado inatawala dunia

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,501
28,703
Roma bado inatawala dunia: ingawa ilianguka mwaka 476 AD ila athari zake zilikula dunia yote, ndo maana primary tulisoma no. za Kirumi na hata saa na Kalenda tunatumia za Kirumi na mataifa mengi yana sheria za Roma mpaka lugha zao tunazitumia. Roma haikuanguka kama inavyosemwa bali ilisambaratika na kuwa nchi za Ulaya ambazo zilikuja kuwa zenye nguvu na kutawala karibu dunia yote na kusambaza utamaduni wao.

Mfano Uingereza imetawala bara Asia mpaka bara Arabu, hata ufalme wa Yordan, Saudia, Qatar zimewekwa na Uingereza. Kwaiyo ukisikia jumuiya ya madola tambua hizo ni nchi zilizotawaliwa na the greater Britain. Na Ufaransa, Spain, Portugal nazo hivo hivyo.

Ulaya(Roma ya zamani) bado ina mkono mkubwa juu ya nchi za dunia hii. Ndo maana wameweka mahakama yenye sheria za Roma(The hague) ambayo daima ikiwahukumu viongozi wa nchi maskini, utake usitake ukiitwa hapo utaenda tu, na ukibisha utatolewa kwa bunduki.

Nabii Daniel alisema hivi juu ya Roma.
23 Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. Daniel 7
Huu utawala wa Roma utadumu mpk Kuja kwa Yesu. Roma imeathiri dunia kisiasa, kidini, kisheria na kitamaduni na nchi yeyote inayokataa hoja za Roma lazima iangamizwe. Sadamu, Gadafi waliangamizwa sababu walipingana na utawala wa Roma, na sahivi Assad anakinywea kisha # Iran itapotezwa. Nabii aliona jinsi wana wa Ishmael(waarabu) wanavyopinduliwa na Roma maana hao waliifukuza Roma karne ya 7 na Roma ikajirudi tena kwa namna ya kuwaweka vibaraka wao ktk falme za Kiarabu kama ufalme wa Saudia, Qatari, UEA na Jordan hao wote ni puppet wa Roma. Na wote watakao pinga watafanyiwa hivi:-
Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Daniel 11:42
Utawala wa Roma utaziangusha nchi zote pinzani zikiwemo nchi za Kiarabu na dunia itamstajabiwa mnyama yule(ufalme huo) na kuufata. Ufunuo 13:3 NIV

ROMA itatengeneza utawala wa dini na kulazimisha dunia yote kufata dini hiyo na watakao pinga watauawa.
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Ufunuo 13:5
Roma haitaangushwa na wanadamu......
......wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Ufunuo 13:4

Roma itaangushwa na Mungu tu.
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. Ufunuo 18:8
Take care usije anguka na Roma

a1175df048e7c5de0a0fe3db44ef801f.jpg
 
Bila shaka ndugu wewe ni msomaji wa vitabu vya Danieli na Ufunuo!
Ukisoma vizuri Danieli 9:20-27, utaelewa kwamba utawala wa Roma utatawala juma la 70 (wiki 1). Kinabii wiki 1 = miaka 7. Kipindi hicho kitaanza baada ya unyakuo wa kanisa (waliompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao walipokuwa duniani).

Wakati huo serikali zote duniani zitakuwa chini ya serikali kuu moja zikipokea amri za kiutawala kutoka kwa mkuu mmoja ambaye ni serikali ya Roma (mfano wa utawala huo ni kama Rais Maguli alivyo na mamlaka kwa wakuu wote wa mikoa yote ya Tanzania). Huyo Rumi (Kaisari) atatawala kwa kushirikiana na mataifa mengine 10 (rejea Danieli 2:33, 41 - sanamu aliyoota Nebukadreza). Wakati huo hakuna atakayekiuka amri hata moja ya mtawala huyo yaani Rumi. Huyo Rumi (Kaisari) atakuwa na nguvu sana, na ndiye Mpinga Kristo.

Tujiulize, kama Roma ndiyo inatawala dunia kwa sasa je, kila serikali iliyoko duniani inatii kila amri kutoka kwa huyo mkuu (Kaisari=mpinga kristo)? Je hizo serikali zinatekeleza policy za huyo Mrumi? Jibu ni hapana. Kipindi hicho bado hakijafika ila hakiko mbali (2Thesolanike 2:1-10). Wateule kuweni macho!
 
Roma bado inatawala dunia: ingawa ilianguka mwaka 476 AD ila athari zake zilikula dunia yote, ndo maana primary tulisoma no. za Kirumi na hata saa na Kalenda tunatumia za Kirumi na mataifa mengi yana sheria za Roma mpaka lugha zao tunazitumia. Roma haikuanguka kama inavyosemwa bali ilisambaratika na kuwa nchi za Ulaya ambazo zilikuja kuwa zenye nguvu na kutawala karibu dunia yote na kusambaza utamaduni wao. Mfano Uingereza imetawala bara Asia mpaka bara Arabu, hata ufalme wa Yordan, Saudia, Qatar zimewekwa na Uingereza. Kwaiyo ukisikia jumuiya ya madola tambua hizo ni nchi zilizotawaliwa na the greater Britain. Na Ufaransa, Spain, Portugal nazo hivo hivo.
Ulaya(Roma ya zamani) bado ina mkono mkubwa juu ya nchi za dunia hii. Ndo maana wameweka mahakama yenye sheria za Roma(The hague) ambayo daima ikiwahukumu viongozi wa nchi maskini, utake usitake ukiitwa hapo utaenda tu, na ukibisha utatolewa kwa bunduki.
Nabii Daniel alisema hivi juu ya Roma.
23 Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. Daniel 7
Huu utawala wa Roma utadumu mpk Kuja kwa Yesu. Roma imeathiri dunia kisiasa, kidini, kisheria na kitamaduni na nchi yeyote inayokataa hoja za Roma lazima iangamizwe. Sadamu, Gadafi waliangamizwa sababu walipingana na utawala wa Roma, na sahivi Assad anakinywea kisha # Iran itapotezwa. Nabii aliona jinsi wana wa Ishmael(waarabu) wanavyopinduliwa na Roma maana hao waliifukuza Roma karne ya 7 na Roma ikajirudi tena kwa namna ya kuwaweka vibaraka wao ktk falme za Kiarabu kama ufalme wa Saudia, Qatari, UEA na Jordan hao wote ni puppet wa Roma. Na wote watakao pinga watafanyiwa hivi:-
Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Daniel 11:42
Utawala wa Roma utaziangusha nchi zote pinzani zikiwemo nchi za Kiarabu na dunia itamstajabiwa mnyama yule(ufalme huo) na kuufata. Ufunuo 13:3 NIV
ROMA itatengeneza utawala wa dini na kulazimisha dunia yote kufata dini hiyo na watakao pinga watauawa.
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Ufunuo 13:5
Roma haitaangushwa na wanadamu......
......wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Ufunuo 13:4
Roma itaangushwa na Mungu tu.
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. Ufunuo 18:8
Take care usije anguka na Roma

a1175df048e7c5de0a0fe3db44ef801f.jpg
Hiyo Ufu:13 ni muham mad ibn abd allah..
 
Ilipoandikwa MNYAMA WA NNE , UFALME WA NNE. hizo nne zinamaanisha nini?. yaani 1,2,3 ni wakina nani hadi kufikia roma 4? Tuanzie hapo
 
Umande, nitakujibu swali lako nikipata nafasi japokuwa mleta mada ndiye anapaswa kufanya hivyo!
 
Hii mada ni ngumu kuielewa. Mimi nachojua ni kuwa to fall for one empire is to rise for another. Kwa sasa tawala inayotawala dunia ni America. Kwa maana ya marekani. Wao ndio dola kuu kwa sasa hapa dunia. Hata pesa yao ndio turufu kwa maana ndio pesa ya kufanyia biashara. Yaani kila bidhaa kwenye sako la kimataifa inapewa thamani in terms of $.
 
Tunajadili hii mada kwa mujibu wa Biblia inavyosema. Biblia inaposema nchi fulani kuwa dola kuu inamaanisha kwamba hiyo nchi ndiyo inatawala ulimwengu mzima, yaani amri zake ndizo zinatekelezwa na ulimwengu mzima (serikali zote duniani) kwa lazima!
 
Ilipoandikwa MNYAMA WA NNE , UFALME WA NNE. hizo nne zinamaanisha nini?. yaani 1,2,3 ni wakina nani hadi kufikia roma 4 ? Tuanzie hapo
Kwanza niseme kwamba mimi siyo Msabato. Mimi ni mkristo ninasali kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).
Umande fungua Biblia yako kitabu cha Danieli 2:29-45.
Aya hizi zinaonesha dola kuu ambazo zimetawala dunia tangu wakati huo (Nebukadreza alipoota ndoto hiyo) na zitakazotawala duniani hadi dunia hii itakapoondolewa. Falme hizi (dola kuu) zilikuwa na mamlaka kamili dunia nzima (serikali zote duniani zikiwa zinafuata amri kutoka dola hizo kuu). Ikumbukwe kwamba kabla ya Nebukadreza (Babeli) kulikuwa na falme kuu 2 zilizokuwa zimetawala dunia hii, nazo ni Misri na Ashuru. Ukisoma aya hizo utaona kwamba zenyewe hazikuzungumzwa:
Hizo dola kuu 4 tangu ndoto ya Nebukadreza zilizoitawala dunia yote ni kama ifuatavyo:
1. Dola ya Babeli - Kichwa cha dhahabu (Danieli 2:36-38) tangu mwaka 612KK hadi 539KK (Kabla ya kuzaliwa Kristo - KK)
2. Dola ya Umedi na Uajemi - Kifua na mikono ya fedha (Danieli 2:39) tangu mwaka 539KK - 333KK
3. Dola ya Uyunani - Tumbo la shaba (Danieli 2:39) tangu mwaka 333KK hadi 146KK
4. Dola ya Rumi - Miguu miwili ya chuma (Danieli 2:33, 40) tangu mwaka 146KK
Utawala wa dola ya Rumi uligawanyika sehemu mbili:
a. Rumi ya magharibi (Western Roman Empire) ambayo mji wake mkuu ulikuwa Roma (tangu mwaka 146KK hadi 476BK - (BK-Baada ya kuzaliwa Kristo)
b. Rumi ya Mashariki, mji wake mkuu ulikuwa Constantinople (tangu mwaka 146KK hadi 1453BK)

Dola 4 tayari zimekwisha itawala dunia yote, bado dola ya 5 ambayo ni "nyayo" (Danieli 2:33, 42,43). Dola hii ya 5 itakuja kuondolewa na ufalme mwingine utakaotawala milele na milele ambao mtawala wake hatakuwa mwanadamu (Danieli 2:44-45).
Swali; dola ya 5 ni mfalme wa dola gani?
Huyo mfalme atakayeondoa utawala wa dola ya 5 kisha kutawala milele na milele ni
nani?
Tutumie Biblia kudadavua hii mada muhimu! Karibuni.
 
utawala wa nyayo ni utawa wa humanoid under alliens ...

alliens wameshaanza kutengeneza human hybrid ambao ni half human na halfu alliens na hao ndo wanakuja kumonopolise this universe...ndo mana Nchi kibwa kama japan,america,uingereza na zingine zimeanza kutengeneza robot wenye ngozi kama binadamu kabsa na hao robot wana uwezo wa kupiga stori na mwanafamu wa kawaida kabsa bila kumshtukia ...
kwa hiyo binadamu wa kawaida have to be perished away kwa kasi ya ajabu snaa ili kuacha universe hii ndani ya mikono ya wengine....
inshot ndo mana sumu nyibgi zinatengenezwa ili kufupisha life span ya mwnadamu halisi....

it is a battle btn God and satarn let' s enjoy it...hakika wanajuana malengo yao ni nini sio sisi tunaochezeshwa kama mazombi....
 
Weka hizo aya hapa. Kwani Biblia yote inazungumzia habari za Mudi? Mnajidanganya bure, hakuna hata chembe ya habari inayomhusu Mudi kwenye Biblia!
nimekwambia soma Biblia yoote.. au hukunielewa nikuongoze kidogo tu kwa mujibu wa uf.13 maana ya joka, mnyama, bahari, pembe ni ipi
 
Ndugu Mackie, tumia Biblia kujibu kwani mada hii ni ya kibiblia.
Enzi (dola) hizi ni za binadamu yaani watawala halisi ni wanadamu siyo roboti kama ulivyosema! Soma Danieli 2:43-44

Vipi huo ufalme utakaotawala milele na milele baada ya dola ya 5 ni ufalme gani?
 
Biblia sio Neno pekee la Mwenyezi
 
Back
Top Bottom