Roho mbaya ndio hiii

Roho mbaya ndio hiii

Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. majuzi umesema umeoa miaka minne iliyopita tena mkeo na hawara yako wamezaa watoto wana miezi minne. hayo ya mke wa miaka ya tisini wapi tena.
 
Judgement ngoja na mimi nikupe ya kwangu.

Miaka ya tisini wakati NGO's zinaanza kuingia Tanzania mke wangu alibahatika kwenda China, kwenye maswala yao ya ki Beijing.
Aliporudi akanipangia zamu ya kuosha vyombo, kupika, kupakua, na mazagazaga mengine ambayo mimi nikiyafanya yeye na hausi geli wetu wanakuwa sebuleni wakiangalia mkanda wa Rambo wakisubiri niwaivishie.
Kwenye ka NGO kao yeye alikuwa ndio bosi, hivyo akawa anawaonyesha wwenzake wakija nyumbani kuwa eti ule mkutano alioendaga Beijing unafanya kazi, na usawa unaanzia nyumbani kwake, kwa mimi kufanya mijikazi ya kike.Kila kukicha mambo ni hayohayo, mume wangu leo nenda sokoni, kanunue ndizi, nyanya chungu, nazi na bamia,. Ukifika nyumbani kuna nanzi kisha osha vyombo vile nilivyovibakiza kwenye sinki jana usiku (mind u, hapo nyumbani house gal alikuwepo, eti tumegawiwa kazi)
Siku zikaenda weee, huku nikifikiria nitoke vipi?
Nikapata wazo, nikaanzisha urafiki na mateja, huku niwapa bukubuku za hapa na pale.
Siku moja nikawaambia mateja waje nyumbani kwangu saa nane za usiku , nikawahakikishia usalama kisha nikawapa elfu ishirini.
Nikawaambia wafanye kama wanataka kuing'oa milango na madirisha kwa vurugu.
Basi kweli bwana, usiku wasela wakatimba, wakaangusha songo mbingo la kufa mtu hadi mimi mwenyewe nikaogopa lakini nikajikaza, nikajidai kama sisikiii vile.
Mume wangu mume wangu, amka majambazi wamekuja, amka bwana tutakufa leo... Nilimsikia bibie akiongea kwa unyonge na hali ya kukata tamaaa.
Nikaaamka na mizuka ya Bruce Lee kama ile ya sosoliso, nikaita mastaaaa hu haaa, nani nyie hebu poitea, nikatoka nje na kijipanga changu cha kizushi, masela wakakimbia.
Urafiki wangu na mateja uliendelea kama kawaida,
huku nyumbani nikiendelea kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwa mke wangu FP .
Baada ya wiki mbili nikawaambia masela waje tena kuleta vagi home.
Safari hii walikuja na mikwala ya kufa mtu kama wale machalii wa Arushaone.
Nikamwambia , wife, mama leo zamu yako, panga hilo hapo nenda kapambane.
Mume wangu Bujibuji nenda, hili ni swala la kiume, mimi mtoto wa kike nitaanzia wapi??
Nikasema siku hizi ni usawa tu, hamna cha mtoto wa kike wala wa kiume, wote kazi moja. Nenda.
Akajiapiza kuwa hatoridia tena kunipa kazi za kike za kuosha vyombo na kupiga deki.
Nikaenda nikawatoa nduki makachala wangu wakatoka nduki ile mbaya. Kipaji Halisi pia alikuwepo kwenye lile crew.
Mbona baada ya hapo mama watoto kanyoooka

CC:- Ukitaka Ubaya..., Paloma, amu, MadameX, ladyfurahia, Zion Daughter, mwaJ, Mwita Maranya, majany, Asprin
Ulichukua muda mrefu na njia ndefu sana kujikomboa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom