Roho mbaya ndio hiii

Roho mbaya ndio hiii

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,036
Reaction score
168,674
Jamaa watatu wamefanikiwa kufika
kwenye kisiwa kisicho na watu wala
kisichojulikana baada ya boti yao
kuvunjwa na upepo mkali baharini.
Ghafla wakaokota nyupa, ile chupa
ikatoa sauti: "Kila mmoja wenu
aombe chochote atakacho, kimoja
tu na atapewa."! Jamaa
wakashtuka. Wa kwanza akaanza:
mimi naomba nijikute niko
nyumbani na familia yangu!
Akatoweka akajikuta kwake. Wa pili
akasema: mimi naomba nijikute
kwetu naendelea na biashara
zangu. Ghafla akatoweka akajikuta
home anaendelea na bizinezi zake.
Wa tatu akasema: mimi najiskia
upweke hapa kisiwani naomba wale
wenzangu wawili warudi niwe nao.
Ghafla wakarudishwa wakajikuta
wote watatu kisiwani.
 
Kastory kaswiti ! Kuna ubaya nikupe na ka'kwangu?
Nway ni hivi :-
Miongo ddahari iliyopita maisha ya kanuni ktk utawala wa kifamilia Mama ndiye alikua mtawala mkuu mwenye sauti.
Kifanyike nini, na nini kiachwe kwa watoto, kilitegemea amri ya mama.
Ikatokea siku Baba akiwa shamba huku nyumbani mtoto mtundu wa kutambaa akaungua na maji ya moto.
Baba aliporudi hom kabla hajaingia ndani, akasikia mkewe akilia .
"Jamani jamani hata sijui nitakuja kumwambia nini mwenye mtoto akija!? Na hivi ametoka na panga mkononi , si atanikatakata huyu m'baba?!"
Na ni kweli Baba wkt huo panga lilikua mkononi.
Ndipo akili yake na fikra vilipozinduka!
"kumbe mie Baba ninaogopeka kiasi hiki?!"
Aliingia ndani na mkwara usio wa polepole!
Huku akilipungapunga panga lake hewani.
"Yaani umekalia uzembeuzembe hadi mwanangu ameungua kiasi hichi ?!"
Mama akamjibu "nisamehe mume wangu huyu mwanao kazidi utundu"
Tangu siku hiyo hadi sasa madaraka na utawala ukahamia kwa Baba rasmi, na anaulinda kwa gharama yeyote ile!
Btw mama wala hakurubuniwa kuuhamisha utawala toka kwake! Aliugawa mwenyewe.
 
Jamaa watatu wamefanikiwa kufika
kwenye kisiwa kisicho na watu wala
kisichojulikana baada ya boti yao
kuvunjwa na upepo mkali baharini.
Ghafla wakaokota nyupa, ile chupa
ikatoa sauti: "Kila mmoja wenu
aombe chochote atakacho, kimoja
tu na atapewa."! Jamaa
wakashtuka. Wa kwanza akaanza:
mimi naomba nijikute niko
nyumbani na familia yangu!
Akatoweka akajikuta kwake. Wa pili
akasema: mimi naomba nijikute
kwetu naendelea na biashara
zangu. Ghafla akatoweka akajikuta
home anaendelea na bizinezi zake.
Wa tatu akasema: mimi najiskia
upweke hapa kisiwani naomba wale
wenzangu wawili warudi niwe nao.
Ghafla wakarudishwa wakajikuta
wote watatu kisiwani.

Ina maana yeye hakuwa na pakwenda hadi awatie wenzi manza ya kurudi kisiawni? Kweli roho ya kwa nini....hata kwetu wapo
 
Judgement ngoja na mimi nikupe ya kwangu.

Miaka ya tisini wakati NGO's zinaanza kuingia Tanzania mke wangu alibahatika kwenda China, kwenye maswala yao ya ki Beijing.
Aliporudi akanipangia zamu ya kuosha vyombo, kupika, kupakua, na mazagazaga mengine ambayo mimi nikiyafanya yeye na hausi geli wetu wanakuwa sebuleni wakiangalia mkanda wa Rambo wakisubiri niwaivishie.
Kwenye ka NGO kao yeye alikuwa ndio bosi, hivyo akawa anawaonyesha wwenzake wakija nyumbani kuwa eti ule mkutano alioendaga Beijing unafanya kazi, na usawa unaanzia nyumbani kwake, kwa mimi kufanya mijikazi ya kike.Kila kukicha mambo ni hayohayo, mume wangu leo nenda sokoni, kanunue ndizi, nyanya chungu, nazi na bamia,. Ukifika nyumbani kuna nanzi kisha osha vyombo vile nilivyovibakiza kwenye sinki jana usiku (mind u, hapo nyumbani house gal alikuwepo, eti tumegawiwa kazi)
Siku zikaenda weee, huku nikifikiria nitoke vipi?
Nikapata wazo, nikaanzisha urafiki na mateja, huku niwapa bukubuku za hapa na pale.
Siku moja nikawaambia mateja waje nyumbani kwangu saa nane za usiku , nikawahakikishia usalama kisha nikawapa elfu ishirini.
Nikawaambia wafanye kama wanataka kuing'oa milango na madirisha kwa vurugu.
Basi kweli bwana, usiku wasela wakatimba, wakaangusha songo mbingo la kufa mtu hadi mimi mwenyewe nikaogopa lakini nikajikaza, nikajidai kama sisikiii vile.
Mume wangu mume wangu, amka majambazi wamekuja, amka bwana tutakufa leo... Nilimsikia bibie akiongea kwa unyonge na hali ya kukata tamaaa.
Nikaaamka na mizuka ya Bruce Lee kama ile ya sosoliso, nikaita mastaaaa hu haaa, nani nyie hebu poitea, nikatoka nje na kijipanga changu cha kizushi, masela wakakimbia.
Urafiki wangu na mateja uliendelea kama kawaida,
huku nyumbani nikiendelea kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwa mke wangu FP .
Baada ya wiki mbili nikawaambia masela waje tena kuleta vagi home.
Safari hii walikuja na mikwala ya kufa mtu kama wale machalii wa Arushaone.
Nikamwambia , wife, mama leo zamu yako, panga hilo hapo nenda kapambane.
Mume wangu Bujibuji nenda, hili ni swala la kiume, mimi mtoto wa kike nitaanzia wapi??
Nikasema siku hizi ni usawa tu, hamna cha mtoto wa kike wala wa kiume, wote kazi moja. Nenda.
Akajiapiza kuwa hatoridia tena kunipa kazi za kike za kuosha vyombo na kupiga deki.
Nikaenda nikawatoa nduki makachala wangu wakatoka nduki ile mbaya. Kipaji Halisi pia alikuwepo kwenye lile crew.
Mbona baada ya hapo mama watoto kanyoooka
Kastory kaswiti ! Kuna ubaya nikupe na ka'kwangu?
Nway ni hivi :-
Miongo ddahari iliyopita maisha ya kanuni ktk utawala wa kifamilia Mama ndiye alikua mtawala mkuu mwenye sauti.
Kifanyike nini, na nini kiachwe kwa watoto, kilitegemea amri ya mama.
Ikatokea siku Baba akiwa shamba huku nyumbani mtoto mtundu wa kutambaa akaungua na maji ya moto.
Baba aliporudi hom kabla hajaingia ndani, akasikia mkewe akilia .
"Jamani jamani hata sijui nitakuja kumwambia nini mwenye mtoto akija!? Na hivi ametoka na panga mkononi , si atanikatakata huyu m'baba?!"
Na ni kweli Baba wkt huo panga lilikua mkononi.
Ndipo akili yake na fikra vilipozinduka!
"kumbe mie Baba ninaogopeka kiasi hiki?!"
Aliingia ndani na mkwara usio wa polepole!
Huku akilipungapunga panga lake hewani.
"Yaani umekalia uzembeuzembe hadi mwanangu ameungua kiasi hichi ?!"
Mama akamjibu "nisamehe mume wangu huyu mwanao kazidi utundu"
Tangu siku hiyo hadi sasa madaraka na utawala ukahamia kwa Baba rasmi, na anaulinda kwa gharama yeyote ile!
Btw mama wala hakurubuniwa kuuhamisha utawala toka kwake! Aliugawa mwenyewe.

CC:- Ukitaka Ubaya..., Paloma, amu, MadameX, ladyfurahia, Zion Daughter, mwaJ, Mwita Maranya, majany, Asprin
 
Last edited by a moderator:
Bujibuji mi vitu vireeeeeeeeefu kama hivi siwezi kusoma bana chukua like
 
Last edited by a moderator:
Naona wivu tu na roho ya kwanini inamaana hakuonachakuomba mpaka awarudishe nyuma wenziwe.
 
Bujibuji yani kwenye ka ngo ketu tulikuwa tunaona mkeo ni bonge ya maza, na wewe ni bonge la bwana!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom