Road Safety: Stika za Nenda kwa Usalama ni wizi, tuungane kuupinga

Wadau habari..

Naomba kujua hili zoezi la usalama barabarani la kubandika stika limeanza tarehe ngapi na linaisha lini maana leo nimekamatwa na trafic kwakosa la kutokua na stika na akataka anitoze faini elfu 30 kwakosa hilo..ila nimejieleza na thanksGod amenielewa bila chochote..ila alikua anaelekea kwenye kutoa chochote.

Je ni haki kukamatwa kwa kosa hilo..maana kanambia zoezi limeanza sijui October. .ss mbona October haijaisha..mwenye uelewa anieleweshe..na nimekagua magari mengi njiani hayana stika mpya.

Msaada ili nisije kamatwa tena
 
Huu uchangiaji wa miradi ya watu mi inanikera kweli, watu wanajibunia miradi ya kijinga jinga tu, juzi nilikamatwa na askari alikuwa anaulizia stika hiyo hiyo, stika zenyewe wameanza kuzitoa wiki ilopita wanategemea kila mtu atakuwa nayo kwenye gari yake!
 
Wapuuzi tu hawa...mimi pia nimekamatwa leo pale science kwenye mataa kwa kosa hilo la kutobandika sticker! Bahati nzuri huyu wakala/askari kanikuta nimempa lifti mtu mzima ningemmalizia kisirani changu chote cha asubuhi
 
Wadau habari..naomba kujua hili zoezi la usalama barabarani la kubandika stika limeanza tarehe ngapI na linaisha lini maana leo nimekamatwa na trafic kwakosa la kutokua na stika na akataka anitoze faini elfu 30 kwakosa hilo..ila nimejieleza na thanksGod amenielewa bila chochote..ila alikua anaelekea kwenye kutoa chochote..je ni haki kukamatwa kwa kosa hilo..maana kanambia zoezi limeanza sijui October. .ss mbona October haijaisha..mwenye uelewa anieleweshe..na nimekagua magari mengi njiani hayana stika mpya..msaada ili nisije kamatwa tena

Wiki ya Nenda kwa Usalama ilishamalizika tokea mwezi wa tisa mwishoni, na maadhimisho yake kama sikosei yalifanyika Mwanza...

Hiyo stika kwa kawaida huwa inatakiwa kutolewa kwa tozo ndogo baada ya polisi wa usalama barabarani kufanya ukaguzi wa chombo cha moto...

Ukaguzi wa stika hizo huwa ni wa mwaka mzima maana humaanisha kuwa gari lako limekaguliwa na ni salama kuendeshwa barabarani...

Hayo magari uliyoyaona hayana stika njiani sio kwamba wamiliki wake wapo sahihi nadhani tu hawajabananishwa...

NB:
Binafsi huwa nahisi haka kazoezi ni kamradi fulani maana zile stika hutolewa kwa udhamnini wa makampuni ambayo kwa mwaka huu ni Be Foward, Airtel Tanzania na PUMA Energy Tanzania...sasa sijui zile pesa tunazolipia huwa zinatozwa kwa ajili ya nini...

picture+4.jpg


Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti wa kwanza kushoto akifatiwa na mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando kwa pamoja wakimkabidhi Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga stika za usalama barabarani kwa mwaka huu. Airtel, Puma pamoja na Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu.
 
Mbaya zaidi nikamuuliza ok sawa afande hizo stika unazo hapo..akanijibu hapana mpk vituoni ss kwann wasiwe nazo..huko vituoni wanategemea twende tukajazane..me nakumbuka last year afande alinisimamisha akanielewesha kisha akanibandikia stika na hakunikagua sababu gari ilikua ndo ina mwezi tu akasema nenda..though stika inauzwa 3000.nilimpa 5000 hakurudisha change
 
Ni mwaka wa nne sasa, huwa nashuhudia ikitangazwa wiki ya nenda kwa usalama ikiambatana na kuuzwa kwa stika za wiki ya nenda kwa usalama, binafsi huwa nanunua kuanzia 5,000 mpaka 10,000 inategemea na muuzaji. na nikishanunua tu basi ugomvi wangu na Polisi umeisha bila kujali gari langu lipo katika hali gani. Huu uhuni utaendelea mpaka lini?

1. Hivi hiki ni kitu gani kwa Serikali mbona naona ni uhuni uliopata Baraka zote za Rais au IGP?
2. Je ni kweli ukishauza stika nchi nzima ndo kutakuwa na usalama barabarani?
3. Hivi usalama wa Taifa hawajastukia huu uhuni unaofanyika nchi nzima?

Wadau naombeni tujadiri hili mimi nataka safari hii nisinunue hizi stika barabarani nataka gari yangu ikaguliwe ndo nipewe stika kuonyesha gari ipo salama au lah, nadhani sisi Watanzania wenyewe tunaipa ushirikiano Serikali kufanya uhuni huu alafu ajari zinapokithiri tunalaumu, mimi naanza sasa kuiwajibisha Serikali nataka waikagaue gari yangu hata kama hawakuzoea utaratibu huo.

Kama kuna mtu gari yake ilishawahi kukaguliwa na Polisi kabla hajapewa Stika anipe uzoefu pia
 
Ni mwaka wa nne sasa,
huwa nashuhudia ikitangazwa wiki ya nenda kwa usalama ikiambatana na
kuuzwa kwa stika za wiki ya nenda kwa usalama, binafsi huwa nanunua
kuanzia 5,000 mpaka 10,000 inategemea na muuzaji. na nikishanunua tu
basi ugomvi wangu na Polisi umeisha bila kujali gari langu lipo katika
hali gani. Huu uhuni utaendelea mpaka lini?

1. Hivi hiki ni kitu gani kwa Serikali mbona naona ni uhuni uliopata
Baraka zote za Rais au IGP?
2. Je ni kweli ukishauza stika nchi nzima ndo kutakuwa na usalama
barabarani?
3. Hivi usalama wa Taifa hawajastukia huu uhuni unaofanyika nchi nzima?

Wadau naombeni tujadiri hili mimi nataka safari hii nisinunue hizi stika
barabarani nataka gari yangu ikaguliwe ndo nipewe stika kuonyesha gari
ipo salama au lah, nadhani sisi Watanzania wenyewe tunaipa ushirikiano
Serikali kufanya uhuni huu alafu ajari zinapokithiri tunalaumu, mimi
naanza sasa kuiwajibisha Serikali nataka waikagaue gari yangu hata kama
hawakuzoea utaratibu huo.

Kama kuna mtu gari yake ilishawahi kukaguliwa na Polisi kabla hajapewa
Stika anipe uzoefu pia

kibongo bongo
 
Khaaa... Juzi kati nilisimamishwa na traffick alikagua gari nzima hakuona kosa. Akaniuliza mbona haina Sticker za usalama? Kwa bahati nzuri wakati wa Wiki ya nenda kwa usalama hapa Jijini Mwanza nilikwenda kwenye maonesho wakasema zimekwisha na aliyesema ni huyo huyo Traffick, nikamwambia kuwa si mlisema zimekwisha??

Ndo akanambia zimeshakuja nenda ukachukue, hiyo ndo ilikuwa ponapons yangu....

Binafsi sijui maana ya hiyo Sticker make siku hiyo niliona watu wananunua tu kama bidhaa bila magari yao kufanyiwa ukaguzi!
 
Mbaya zaidi stika za mwaka huu hazijaandikwa bei, ukiingia vibaya unalambwa msimbazi..!
 
Khaaa... Juzi kati nilisimamishwa na traffick alikagua gari nzima hakuona kosa. Akaniuliza mbona haina Sticker za usalama? Kwa bahati nzuri wakati wa Wiki ya nenda kwa usalama hapa Jijini Mwanza nilikwenda kwenye maonesho wakasema zimekwisha na aliyesema ni huyo huyo Traffick, nikamwambia kuwa si mlisema zimekwisha??

Ndo akanambia zimeshakuja nenda ukachukue, hiyo ndo ilikuwa ponapons yangu....

Binafsi sijui maana ya hiyo Sticker make siku hiyo niliona watu wananunua tu kama bidhaa bila magari yao kufanyiwa ukaguzi!

Umeona ee mimi sielewi elewi, nataka safari hii nisinunue mpaka mwisho na nikikamatwa sitoi rushwa nata nione hili shauri litakaaje mahakamani, watasema sijanunua stika au watafungua shauri la kutokukaguliwa?
 
Umeona ee mimi sielewi elewi, nataka safari hii nisinunue mpaka mwisho na nikikamatwa sitoi rushwa nata nione hili shauri litakaaje mahakamani, watasema sijanunua stika au watafungua shauri la kutokukaguliwa?

Hahahaaaaa.... Usinishwishi nami nifanye hivyo!
 
Umeona ee mimi sielewi elewi, nataka safari hii nisinunue mpaka mwisho na nikikamatwa sitoi rushwa nata nione hili shauri litakaaje mahakamani, watasema sijanunua stika au watafungua shauri la kutokukaguliwa?
Mashtaka yote mawili uliyotaja yatakukabili, pia tarajia mengine ya nyongeza yatayotategemea ufundi wa kubambika makosa wa yule atakaye kukamata. Utakomajeee!
 
Back
Top Bottom