Rizone Kikwete: Suala la elimu ya Mnyika

Rizone Kikwete: Suala la elimu ya Mnyika

Status
Not open for further replies.
Rizone kapasua jipu kumbe alimuacha mnyika chuo kikuu sasa ubishi wa nini amueleze nape ambaye anasema elimu ya mnyika form six.
 
Why presenting it in english, while his first post was in Kiswahili? My friend positions held by him in both law firms were just privileges because of his father's position. And for your information, from very reputable sources, the guy is terribly and profoundly bogus/TABURA LASA in law (at IMMMA, he never practised law, he was just like a messenger instead. where do you find his administrative and technical skills here? worse still he failed his masters in the UK, and you know what, in Europe when you fail a PhD or Masters degrees, you are given its immediate lower degree, the worst for r1, he was given a diploma, what a mercy! Education level ant nothing but INTELLECT!
sounds quite strange!!!
kwamba alienda kusoma kule akiwa tayari na Bachelor Degree kama 'entry requirement' then akawa demoted to diploma!? Ina maana ingekuwa seminary za wakati huo wangelikuja ku-nullify hiyo degree ya awali maana inakuwa na utata.

tunaongea haya yote but the guy has money, I tell you.

 
Riz1 Kikwete kapost hvi facebook kuhusu Mnyika..

Hivi juzi bwana Nape Nnauye alijitokeza hadharani akisema juu ya uhakika alionao kuhusiana na elimu ya bwana Mnyika (mb) kuwa ameishia form Six. nikaguna kidogo hasa nikiangalia mambo mengi sana.

Mie nimepata nafasi ya kukaa na Mnyika pale chuoni na nikaona hata uhodari wake katika kuchochea migogoro. ninamkumbuka katika sakata la Mikopo ya wanafunzi na jinsi alivyoshauri wanafunzi waandamane waende IKULU kwa miguu.sasa swali au maswali ambayo sina jibu nayo ni kama haya

1. Nini kilitokea mNYIKA (MB) baada ya sisi kuondoka CHUONI? maana kumbukumbu zinaonyesha nilikuacha ukiendelea na masomo.

2. lini ulimaliza chuo pale mlimani?

3. unakumbuka habari ya Bw.Kihiyo wa jimbo la Temeke na ushuhuda wa ELIMU ambayo hakuwa nayo.

JITOKEZE HADHARANI TANABAISHA JUU YA UFAHAMU WAKO . MAANA WENGINE WAMEANZA SEMA ..................... NDIYO MAAANA KUMBE.!!!!!

My take.
HUYU JAMAA KUMBE NI MBUMBUMBU KAMA MDINGI WAKE,JE MNYIKA AKITAJA ELIMU YAKE NINI KITABADILIKA TZ..

Mnyika ni kijana hodari sana na mwenye weledi wa hali ya juu sana pale chadema. Hakuna haja ya kuleta mada kama hii hapa ndani. Ulitakiwa kupuuza haya maswali ya rizone. Muache riziwani ajifurahishe nafsi yake. Lakini usimuite Mbumbumbu. Rizone amesoma LLB.
 
Hii vita ya elimu ya Mnyika ingemalizwa kwa kuwafumba mdomo wote wanaochonga, na Mnyika kuweka hadharani elimu yake.

Mtu anaweka elimu yake hadharani kwa matendo na maneno yake. Mnyika kashafanya hivyo.

Usichanganye "vyeti" na "elimu".

Viwili hivi si kitu kimoja.
 
Hivi elimu ya J. Zuma wanaijua au ya prf. Majimarefu kwa kuwa yuko ccm basi aachwe ila mnyika asulubiwe.
 
Mtakumbuka ni hawahawa waliokuja na hoja kuwa Dr. Slaa ana kadi ya ccm kwa hiyo bado ni mwana-ccm. Sasa baada ya kujua Slaa ana kadi ya CCM tukapata nini? Ilimfanya aache harakati zake za kuwatetea wananchi? Leo Wanaleta hoja za kijinga namna hii ili watu dhaifu wajadili mambo dhaifu na kusahau hoja za maana na zenye mashiko kwa jamii ya watanzania. Tukishajua kuwa Mnyika ana elimu ya form vi kisha? Watz anzeni sasa kuwa critical thinkers. kuna mamia ya watu wenye elimu kubwa ambao wametumika tu kufisadi nchi hii. Suala hapa siyo elimu ya Mnyika, ni Mnyika anafanya nini jimboni mwake na kwa nchi yake. Mmeelewa wajukuu zangu eeeh! Kumbukeni Nape ndiye mwanzilishi wa hoja nyepesinyepesi akiwatumia watu kama Mtela Mwampamba na Juliana Shoza. Ukikubali kununuliwa unakuwa mtumwa wa aliyekununua. Sasa mnaona wanawatumia vijana wale wawili kuzunguka kuzungumza yasiyo na mashiko kwa taifa letu. Sioni ccm walichokifanya kule Temeke. Wamesahau wajibu wao kama chama tawala wa kuisimamia serikali ilete hali bora kwa wananchi, sasa wanahubiri Chadema. Sioni mahubiri yao dhidi ya Chadema yatawapeleka wapi. I surely pity them!

Great. Short and clear. Nimekugongea 'like'.
Tafadhali sambaza ujumbe huu mfupi na unaojitosheleza kwa vijana wote wanaopenda kuona mabadiliko ya kweli.
Afadahali kuwa na mbuge au mtawala mwenye elimu ya Form VI anayetetea maslahi ya wengi kuliko kuwa na Profesa anayeFISADI. Na serikali yetu imejaa maprofesa na ma-Dr waliotufikisha hapa!!!!
 
sounds quite strange!!!
kwamba alienda kusoma kule akiwa tayari na Bachelor Degree kama 'entry requirement' then akawa demoted to diploma!? Ina maana ingekuwa seminary za wakati huo wangelikuja ku-nullify hiyo degree ya awali maana inakuwa na utata.

tunaongea haya yote but the guy has money, I tell you.


Katoa wapi?
 
Unajua hoja nyingine huletwa hapa ili kupotezeana uelekeo na muda wa kufikiri mambo ya kulijenga taifa.
Mnyika big up sana. Endelea kuwacha magamba na kuwaonyesha hata kama wana vyeti vya chuma lakini vichwa mbumbumbu.
Hata kama Nape anajikusanya na magamba yote, kwa hoja hawakuwezi.
 
Aliyesomeshwa na CCM na kutumia nguvu kubwa ya ubalozi wa Tanzania India kupata Admission Acharya university-Bangalore,India ana Termerity ya kuhoji elimu ya Mnyika?


Na huyu mwingine aliyedandia akiambiwa alete Tasnifu(thesis) yake ya shada ya uzamili kwenye sheria LLM kule hulls university ataleta? Mnyika hajawahi kuwa na taaluma Fake kama huko CCM ambako mtu yeyote anaweza kujiita professa (mganga wa kienyeji na mfuga majini) au Doctor kisha baadae anarudi kusoma shule kuusomea udaktari ambao ameshajipa title.TCU imeshathibitisha makada wengi wa CCM wenye shahada fake

-Hebu turudi katika hoja za msingi na sio story za kutunga za vijiweni.Katibu wa itikadi na uenezi anaongea trivial issues?

nimepitia tovuti ya bunge upande wa elimu, mnyika hajajaziwa chochote. hoja ya kutokua na shahada inaweza kuwa na ukweli lkn hata hivyo uwezo wa mnyika ni mkubwa sana. namkubali
 
Biashara ya kadi ya Dr Slaa aliyofungua kwa ubia na akina Shonza imemuingiza hasara mpaka masalia wametafuta pa kutokea. Sasa wanatafuta mradi mpya, lakini huu nadhani hauna hata pa kuanzia ila unaweza kumpandisha Mnyika, ila najiuliza mpaka wapi? maana tayari yuko juu kupitiliza
 
Mbona nayeye alikuwa akinunua Mitihani ya sheria kwa kutumia nguvu ya baba yake..!!! Pia Law School ameiba mitihani kupindukia na sisi tumenyamaza.....Hana hoja huyo.

Mmmmmmmmmmmmh ww nawe acha uongo na ushabiki uliopitiliza duuuuuuuuuh??law school ipi aliyosoma ridhiwani??kama huna data just keep uiet or else unajiaibisha
 
Kaka sikiliza simulizi za alfa ulellah.......

Mr. Kikwete is a young and dynamic legal practitioner with 5 years experience in legal practice having worked with reputable law firms in and outside Tanzania.Before joining GRK Advocates as a partner Mr. Kikwete worked with IMMA Advocates holding different challenging positions from January 2005 to December 2010.


During the same period Mr. Kikwete was attached to DLA Piper in London, one of ten largest law firms in the world where he was exposed to high level legal practice in the area of project financing. Both at IMMA Advocates and DLA Piper Mr. Kikwete was involved in various areas of modern day legal practice ranging from legal drafting to major aspects of project financing including due diligence inquiries, loan negotiations, consortium building and mortgage financing. His five years period of his legal practice saw him moving within the ranks of the law firms from legal officer to a partner level. Mr. Kikwete is therefore equipped with sufficient administrative as well as technical skills required for running a successful law practice.


Mr. Kikwete was admitted to the bar of advocates in 2009. He is also handling commercial and corporate litigation matters at all levels of court system and quasi- judicial tribunals. At GRK Advocates Mr. Kikwete is a partner in charge of Administration and Business Development.


He is a member of Tanganyika and East Africa Law Societies. Apart from the law degree Mr. Kikwete holds Postgraduate Certificate in Business Development from the Hull University (UK)

sasa huu naona uswahili. ungethibitisha kwanza elimu ya mnyika ya chuo kikuu au useme kuwa hajamaliza chuo...... kuliko kuleta mada nyingine. huwa naheshimu michango yako lkn hapa umechemsha.
 
biashara ya kadi ya dr slaa aliyofungua kwa ubia na akina shonza imemuingiza hasara mpaka masalia wametafuta pa kutokea. Sasa wanatafuta mradi mpya, lakini huu nadhani hauna hata pa kuanzia ila unaweza kumpandisha mnyika, ila najiuliza mpaka wapi? Maana tayari yuko juu kupitiliza




hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa !


Kwa hivyo this week manifesto ya ccm kitaifa ni elimu? Tulipotaka kujadili elimu agenda ilikuwa kanuni za bunge na mamlaka ya spika, sasa agenda ya wazalendo ni maji dar, tuko kwenye degree. Kuna siku tutaka mtu fulani atwambie honary degree wanazopewa udom na kenyatta university ni za nini kama sio rushwa za kisiasa. Na kama bwana vuvuzela leo kakumbuka kuhoji elimu ya mnyika basi kawatoa jasho kiukweli. Lakini huyu professor magembe haponi kwa hili. Hawa washabiki kina riz one wepesi sana!!! Hakuna kitu has an opinion on everything but nothing substantial apart from wanting to know he is a waned kikwete dynasty. Afu vuvuzela mjanja anadhani tumesahau kuwa yeye ndiye moja ya wale waliokuwa wanaeneza siasa za udini leo wanayakimbia matunda ya siasa zao.
 
PIA TUSISAHAU KUWA KINGINE KINACHOKWEPWA NA VUVUZELA NI KIKOSI CHAKE NI HILO HAPO CHINI


UVCCM waumana
• Aliyefukuzwa adai hakuna spika bora kama Sitta

na Edson Kamukara




SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis kumvua ujumbe wa Baraza Kuu la umoja huo, aliyekuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa, Paul Makonda, utata mkubwa umetanda kuhusu uamuzi huo.

Makonda alivuliwa wadhifa huo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, muda mfupi tangu ateuliwe na Sadifa Oktoba mwaka jana, baada ya kushindwa na Mboni Mhita katika uchaguzi wa UVCCM.

Hata hivyo, wadadisi wa masuala ya kisiasa wanalitafsiri suala hilo kama msuguano wa makundi yanayotajwa kusaka urais wa 2015 kupitia CCM, kwani Makonda anatajwa kuwa mfuasi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wakati Sadifa anadaiwa kumuunga mkono Edward Lowassa.

Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu kuenguliwa kwake, Makonda alidai ni mapema sana kulizungumzia, kwani bado anajipanga ili kutoa taarifa kamili, lakini akamshtumu mwenyekiti wake Sadifa kuwa ana uelewa mdogo, wala si suala la makundi.

"Mimi nilipoteuliwa sikutaka kukubali uteuzi huo haraka, bali nilijipa muda kwanza nitafakari na kupooza hasira za makundi yaliyokuwa yakituunga mkono. Leo kama naondolewa kwa sababu hiyo nikiitwa mtovu wa nidhamu itakuwa ni ajabu," alisema.

Makonda ambaye alizungumza kwa tahadhari ya kutotaka kujiingiza kwenye malumbano kwa sasa, aliongeza kuwa aliteuliwa kupitia mkutano mkuu, na hivyo mwenye mamlaka ya kumwengua ni mkutano huo.

"Huyu kaniita mwenyewe Dodoma, nikalipwa posho halafu naingia kwenye kikao naambiwa nimevuliwa wadhifa wangu. Nimeamua kuondoka zangu kabisa Dodoma ili nisije kuonekana nina mkono katika mivutano inayoendelea ndani ya UVCCM," alisema.

Alifafanua kuwa hadi jana mchana wajumbe wa Baraza la UVCCM walikuwa wakivutana na mwenyekiti wao tangu asubuhi, lakini akasisitiza kuwa msimamo wake ni kwamba "mwenye haki akifedheheshwa, mbingu husimama nyuma yake".

Makonda aliongeza kuwa, CCM haina makundi bali kuna magenge yanayotumia nafasi ya mbio za urais kujionesha kuwa kuna makundi yenye malengo fulani kumbe ni ajenda zao binafsi.

Kuhusu kuhusishwa kwake na kundi la Sitta katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, Makonda alitumia mifano zaidi kumsifu mwanasiasa huyo, na kuhoji ni nani asiyetambua umahiri na uwezo wake katika uongozi.

Alisema kuwa Sitta aliliongoza Bunge la Tanzania na kulipatia sifa kubwa iliyotukuka katika mabunge ya Jumuiya ya Madola, huku akihoji kuna ubaya gani kwake kujivunia mtu kama huyo?

"Hivi hao wanaosema kuna makundi, na kudai mimi namuunga mkono Sitta, ni kwanini wasitambue kuwa anabebwa na sifa na utendaji wake uliotukuka katika kuliongoza Bunge la Tisa? Mimi kujivunia mtu kama huyo kuna tatizo gani?" alihoji.

Makonda alikwenda mbele zaidi na kuwataja Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na yule wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuwa uchapakazi na uadilifu wao hakuna asiyefurahishwa nao, huku akihoji kuwa, watu wanataka waendelee kujivunia nini katika ufisadi wa Richmond?
 
nimepitia tovuti ya bunge upande wa elimu, mnyika hajajaziwa chochote. hoja ya kutokua na shahada inaweza kuwa na ukweli lkn hata hivyo uwezo wa mnyika ni mkubwa sana. namkubali

Asante kwa kuverify.

Ridhiwani hawezi hata kusema Mnyika kadanganya kwamba ana degree kwenye official records. Kitu ambacho kingeweza ku validate scrutiny.

Kwa hiyo Ridhiwani anasema nini? Hakuna watu wenye uwezo bila degree kina Bill Gates na Lula Da Silva?

Ridhiwani anaelewa tofauti ya elimu na elimu rasmi? Na kwamba kupata cheti si kuelimika? Kuelimika kunapimwa na kazi.

Na katika mizani yangu, kwa kuangalia hiyo Facebook post, kati ya Mnyika na Ridhiwani, Ridhiwani ndiye anaonekana hajaelimika.

Limbukeni wa elimu asiyejua tofauti ya cheti na elimu.
 
Mbona nayeye alikuwa akinunua Mitihani ya sheria kwa kutumia nguvu ya baba yake..!!! Pia Law School ameiba mitihani kupindukia na sisi tumenyamaza.....Hana hoja huyo.

Aibe mitihani kwa minajili gani? Manake sheria wala haina ugumu wowote kama ambavyo watu wanaifanya ionekane...
 
By the way, who are you ? Mpambe wa Ritz au ndo muendelezo wa kujipendekeza ili upate nafasi za uteuzi? Ritz tumesoma nae tunamfahamu kuliko unavyo fikiria, na hii siyo siri tena Ritz ni kilazest. Elewa mtoto wa nyoka ni nyoka tu na huo ndo ukweli.

Unatakiwa kuwa na akili nyingi kumuelewa Safari ni Safari, kwa vilaza kama nyie ngumu kumuelewa Safari ni Safari.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom