Wala huhitaji mtaalamu wa kugushi kwa mtu mwenye akili timamu kugundua kwamba hiyo email hapo juu ni feki...tena huna hata haja ya kusoma maudhui yenyewe yaliyoandikwa unajua ni feki. Kwanini nasema hivi?
1) Mtu kutumia email address ya kazini kuomba rushwa, na tena kutaja kiwango chenyewe cha hiyo rushwa haiingii akilini, sembuse tu kuandika kuhusu mambo binafsi tena ya kimapenzi. Ungetegemea kama ni kweli mtu huyu asingeacha "paper trail" ya aina yoyote.
2) Karatasi yake inaonekana imekunjwa-kunjwa, lakini maandishi yake yamebandikwa juu ya karatasi bila ya maandishi yenyewe kukunjika. Maneno yanaonekana kabisa kwamba yana kimvuli fulani ambacho kinatokana na jitihada za ku-copy and paste, au ku-fotokopi.
3) Formatting ya email inaashiria kabisa kwamba imekuwa typed kwenye Word document. Tazama indentation kwanzo kabisa wa email ambapo sentensi imeanzia kati kati, na mwisho kwenye sahihi ambapo jina limekuwa centred. Hii formatting haipo katika email etiquette wala katika programs kama MS Outlook au Lotus Notes.
4) Ukiprint email kawaida inatokea mistari fulani juu pamoja na jina la mwenye account, vitu ambavyo havipo hapa.