Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Mkuu kuanza story mpya wakati nyingine haiendelei unachosha wa somaji na kukatisha tamaa kuwa nayo itaishia katikati ukweli sianzi kusoma maana nimechoka arosto
Imeanza ambayo ipo hivi sasa
 
Mkuu kuanza story mpya wakati nyingine haiendelei unachosha wa somaji na kukatisha tamaa kuwa nayo itaishia katikati ukweli sianzi kusoma maana nimechoka arosto
Kweli kabisa, jamaa anazingua
 
Ungemaliza hii ndio ulete nyingine, Sasa hii haujamaliza unatuhamasisha tuanze nyingine ambayo nayo uhakika wa kwamba itafika mwisho hatuna
Kwani sababu za kutoimalizia hii ni zipi? Kama anataka tumchangie aseme maana sisi wengine kusoma riwaya ndo starehe yetu. gilbert35
 
Kwani sababu za kutoimalizia hii ni zipi? Kama anataka tumchangie aseme maana sisi wengine kusoma riwaya ndo starehe yetu. gilbert35
Huko anakochota kisima kimekauka mpaka mvua inyeshe ndio tupate maji, maana wenzake huwa wanasema mapema Kama inauzwa
 
Huko anakochota kisima kimekauka mpaka mvua inyeshe ndio tupate maji, maana wenzake huwa wanasema mapema Kama inauzwa
Duh! Kweli hii ni HATARI, jina la kitabu limesadifu hadhira yake.
 
Kwani sababu za kutoimalizia hii ni zipi? Kama anataka tumchangie aseme maana sisi wengine kusoma riwaya ndo starehe yetu. gilbert35
Haijaendelea kutungwa. Ikitungwa itawajia. Hakuna jambo zuri kama kuwa mwelewa Mkuu. Ikitungwa itawekwa na utaisoma
 
Haijaendelea kutungwa. Ikitungwa itawajia. Hakuna jambo zuri kama kuwa mwelewa Mkuu. Ikitungwa itawekwa na utaisoma
Kumbe hadi itungwe ndo utuletee,kwanini hukusubiri ikamilike sasa, ulikua na haraka ya nini
 
Kumbe hadi itungwe ndo utuletee,kwanini hukusubiri ikamilike sasa, ulikua na haraka ya nini
Nawe kwanini ulikimbilia kuisoma bila kuuliza? Je ni waandishi wote hutuma riwaya huku ikiwa tayari? Muda wote utakuwa huru kuandika? Fikiri kabla ya kuandika
 
HALFANI SUDY anaandika HATARI

Sehemu ya 14

Ilipoishia...

Fikra za Martin Hisia zilikuwa maili nyingi sana kutoka pale sebuleni. Fikra zake kwa sasa zilikuwa zimefika Mikocheni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa Daniel Mwaseba. Alikuwa hajui kitatokea nini endapo Daniel akigundua kama ameusaliti upande wake, alikuwa hajui Daniel atachukua hatua gani akijua kuwa Martin amefanya kitendo hiko kibaya kabisa cha usaliti. Kubwa zaidi, alikuwa anafikiria kazi ngumu iliyopo mbele yake, kazi ya kwenda kutega kamera ya siri katika chumba cha Rais Mark Mwazilindi, lakini, alikuwa tayari kwa chochote kile kitakachotokea, kwakuwa alikuwa ana ni ya dhati ya kutaka kumwokoa ndugu yake wa damu, Nato.

Songa Nayo...
DANIEL MWASEBA aliamka saa kumi na moja asubuhi. Alienda bafuni kupiga mswaki, alirudi chumbani kwake na kuvaa nguo za mazoezi. Moja kwa moja alielekea katika chumba cha mazoezi, alimkuta Hannan akifanya mazoezi ya kukimbia katika mashine maalum ya kukimbilia.

“Martin yuko wapi?” Daniel alimuuliza hata kabla ya salamu.

“Hata mimi nimeshangaa sana leo, sijamkuta Martin, labda amepitiwa na usingizi” Hannan alisema huku akiendelea kufanya lile zoezi la kukimbia katika mashine. Jasho lilikuwa linamtoka ishara kwamba alianza kufanya yale mazoezi kwa muda mrefu kidogo.

“Hii sio kawaida ya Martin. Siku zote yeye huwa wa kwanza kufika katika chumba cha mazoezi, hadi sisi tunapoingia tunamkuta ameshafanya mazoezi zaidi ya saa moja. Ngoja nikamwangalie chumbani kwake.” Daniel alisema huku akitoka nje ya chumba cha mazoezi na kuelekea kilipo chumba cha Martin. Alipigwa na butwaa baada ya kugundua kwamba mlango wa chumba cha Martin ulikuwa wazi. Alipoingia ndani, hisia zake zilikuwa sahihi, kweli haikuwa kawaida ya Martin. Martin hakuwepo chumbani!.
Moja kwa moja alirudi katika chumba cha mazoezi.

“Hannan, Martin hayupo chumbani kwake!” Daniel alisema mara tu baada yakuingia katika chumba cha mazoezi.

“Acha utani Daniel, Martin hayupo chumbani kwake?, kaenda wapi? au ameenda kupumzika bustanini?” Hannan alishangaa huku akitupa maswali mfululizo kwa Daniel.

“Ni kweli, inawezekana Martin yupo bustanini, ngoja nikamwangalie” Daniel alisema na kutoka tena nje ya chumba cha mazoezi. Alienda hadi bustanini, lakini Martin hakuwepo, akatafuta kila mahala ndani na nje ya nyumba yake, lakini bado hakumwona. Hali ya uwoga ikaanza kumpanda juu ya usalama wake, na kitu cha kwanza alichofikiria kichwani kwake ni Okello. Lazima Okello anahusika na kupotea kwa Martin.

“Okello hanijui vizuri mimi!” Daniel alisema kwa ghadhabu. alikuwa ameshakasirika. Moja kwa moja alielekea tena katika chumba cha mazoezi, alimkuta Hannan akimaliza kufanya mazoezi.

“Martin hayupo sehemu zote, nina wasiwasi na Okello!” Daniel alisema kwa hasira huku akiangalia darini.

“Inawezekana ukawa sahihi, lakini ngoja tukaangalie kwenye kamera zetu, zitatuonesha wapi alipo Martin?, au kama alitoka humu ndani pia tutaona” Hannan alitoa ushauri uliokubaliwa na Daniel.

Moja kwa moja walielekea katika chumba maalum cha mawasilino. Humo kulikuwa na kompyuta nne, runinga tatu, simu za mezani mbili na vifaa mbalimbali vya mawasiliano. Hannan alikaa mbele ya kompyuta moja na kuanza kuangalia matukio yaliyotokea tangu walipoenda kulala ule usiku. Kompyuta ilionesha kila tukio, hadi ilipofika asubuhi, lakini haikuonesha chochote kile juu ya upotevu wa Martin.

“Kitu gani kimetokea? kamera za ulinzi hazijanasa chochote kuhusu Martin!” Hannan alisema kwa mshangao mkubwa.

“Twende chumbani kwa Okello” Daniel alisema huku sauti yake ikionesha kwamba alikuwa amekasirika.

Bila ya kusita Hannan alifuata nyuma kuelekea chumbani kwa Okello. Walikuta mlango wa chumba cha Okello ukiwa umefungwa kwa ndani. Daniel aligonga taratibu, lakini hakuna aliyejibu. Akagonga tena, ikawa kimya tena.

Akagonga,

Akagonga,

Akagonga huku akiliita jina la Okello, bado kulikuwa kimya. Hakukuwa na dalili zozote zile za kuitikiwa.

“Nisubiri,” Daniel alisema huku akielekea chumbani kwake. Alirudi baada ya dakika tatu na rundo la funguo mkononi. Akauchagua funguo mmoja baada ya kuchagua kati ya funguo alizobeba. Akauingiza kitasani na kuuzungusha.

Mlango ukafunguka.

Wote wawili waliingia ndani wakiwa na shauku kubwa sana ya kujua watakutana na nini mle ndani. Lakini shauku zao zilipigwa na bumbuwazi zito sana, kwani mbele yao walikuwa hawamtazami Okello, bali walikuwa wanautazama mwili wa Okello ukiwa umelala hovyo sakafuni, michirizi myembamba ya damu ilikuwa imeelekea chini ya kitanda. Dalili zote zilionesha kwamba Okello alikuwa ameuwawa!.

Daniel aliusogelea mwili wa Okello akiwa hayaamini kabisa macho yake, kwa maana na tukio hili pia hawakuliona katika kamera zao licha ya kwamba kulikuwa na kamera za siri pia katika chumba cha Okello.

“Okello ameuwawa!” Daniel alisema baada ya kuuinamia kwa karibu mwili wa Okello. Aliona alama za kunyongwa shingoni kwake na mpini wa kisu ukiwa umepotelea kifuani mwake. Huku sura ya maiti ya Okello ikionesha kuwa ilipitia katika maumivu makali sana kabla haijakata roho. Swali jipya likaibuka,

“Ni nani aliyemuua Okello ndani ya nyumba ya Daniel Mwaseba?” Hili lilikuwa swali jepesi sana lakini lenye majibu magumu na tata kuliko unavyoweza kufikiria.

“Kwanini kamera za ulinzi hazikunasa matukio haya?” Hili lilikuwa swali kutoka katika mdomo wa Hannan ambalo aliliuliza kwa nguvu. Kitu ambacho alikuwa hakijui ni kwamba yeye hakupaswa kuuliza swali hilo, yeye ndiye alipaswa kutoa majibu endapo angeulizwa na Daniel , kwakuwa yeye alikuwa ni Mchawi wa Kompyuta. Pengine kwasasa alilisahau hilo kwa kwakuwa alikuwa amechanganyikiwa.

“Hannan kuna mambo hayapo sawa, kuanzia kupotea kwa Martin, kuuwawa kwa Okello na kamera zetu kutorikodi tukio lolote kati ya hayo, hii sio kawaida. Yatupasa tuchukue hatua za haraka sana kujua ni kitu gani kimetokea?” Daniel aliuliza huku akiuangalia mwili wa Okello uliolala sakafuni.
 
Halfani Sudy anaandika HATARI
Mawasiliano 0652 212391
Mahali Mafinga, Iringa

“Una kazi ndogo tu Martin, kazi ndogo sana. Najua kwamba, wewe na Daniel Mwaseba mna nafasi ya kwenda ikulu kwa Rais Mark Mwazilindi wakati wowote ule mtakapohitaji, pia mna uwezo wa kuonana na Rais Mark Mwazilindi hata chumbani kwake. Sasa huko chumbani kwa Rais Mark Mwazilindi ndipo tunapokutaka sisi. Tutakupa kamera ya siri uende ukaiweke kwa siri chumbani kwa Rais Mark Mwazilindi. Endapo tukianza kuona picha za chumba cha Rais Mark Mwazilindi hapa sebuleni kwetu, basi ndugu yako Nato atakuwa huru” Mrombo alimwangalia kwa umakini Martin kuhakikisha kama maneno yake yamemwingia Martin.

Hii ni sehemu ya Kumi na Tatu

Martin alibaki katika mshangao mkubwa sana, kitu alichokuwa anakitaka Mrombo alikuwa ana uwezo wa kukifanya, lakini ilimpa ukakasi kwakuwa hakujua nia ya kina Mrombo ni nini hadi kutaka afanye hiyo kazi ya kwenda kufunga kamera katika chumba cha rais Mark Mwazilindi.

“Hilo ndio jukumu lako Martin, na tunaamini unaweza kulitekeleza kwa uaminifu mkubwa ili ufanikiwe, ila tu ni kama unataka thamani ya machozi yako ya kumlilia Nato yasiende bure” Mrombo alisema huku akimwangalia Martin kwa dharau.

“Kwanini mnataka nikaweke kamera ya siri katika chumba cha Rais Mark? Mna shida gani na chumba cha Rais? Kitu gani mnataka mkione anachokifanya Rais akiwa chumbani kwake?” Martin aliuliza maswali mfululizo akiwa katikati ya majonzi.

“John! Hivi hukumpa maelekezo huyu mbwa?” Mrombo aliuliza swali kwa hasira huku akimwangila John Masalu.

“Nilimpa maelekezo yote Mfalme Mrombo. Martin, nilikwambia kuwa huruhusiwi kuuliza swali lolote kwa Mfalme Mrombo. Jukumu lako hapa, ni kutekeleza hicho alichokisema Mfalme wa wafalme” John Masalu alisema kwa sauti ya uwoga.

“Mrombo, jambo ulilonambia kwenda kulifanya kama njia ya kumwokoa Nato sio rahisi kama unavyofikiria, ni jambo gumu na la hatari sana. Najua mnajua ugumu na uhatari wake ndiomaana mkatutaka mimi au Daniel Mwaseba tukaifanye kazi hiyo. Mimi nina nia ya kweli ya kuhakikisha Nato anakuwa huru kwa kutekeleza hicho mlichonituma, lakini nahitaji kujua, nia yenu ni nini pengine ninaweza kuwapa njia ya rahisi zaidi ya kufanya hilo jambo mnalolitaka kuliona chumbani kwa Rais Mark?” Martin Hisia alieza kwa kirefu.

“Nia yetu ni moja tu Martin, kamera yetu ya siri ichukue picha moja kwa moja kutoka katika chumba cha Rais Mark Mwazilindi na kuzileta hapa sebuleni kwetu. Hatutaki jambo lengine lolote zaidi ya hilo” Kwa mara ya kwanza, Mrombo alijibu swali kutoka kwa Martin Hisia.

“Halafu?” Martin aliuliza tena huku akimwangalia Mrombo kwa macho ya mshangao.

“Picha zote za chumba cha Rais Mark Mwazilindi tuzione tukiwa hapa sebuleni” Kwa mara nyingine tena, Mrombo alijibu swali la Martin Hisia.

“Halafu?” Martin aliuliza tena huku akimtazama Mrombo machoni.

“Tutamwachia huru ndugu yako, Nato” Mrombo alisema wakati akinyanyuka sofani, moja kwa moja alielekea chumbani kwake bila ya kumuaga mtu yeyote. Na wale watu wawili aliokuja nao walimfuata kwa nyuma.

Martin alibaki sofani akiwa hajui ni kitu gani sahihi cha kufanya? Atekeleze maelekezo ya Mrombo kama alivyoahidi ili ndugu yake awe huru ama sitekeleze maagizo ya Mrombo na ndugu yake asiwe huru. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake kufanya maamuzi katika maisha yake.

“Nitaenda kuyafanya haya yote kwa ajili yako Nato. Kama nimeweza kumsaliti Daniel Mwaseba, kwanini nisifanye hiki ambacho Mrombo amekitaka. Nitaenda kuifanya kazi hii kwakuwa maji nishayavulia nguo ni sharti niyaoge. Natamani tungekuwa na Daniel Mwaseba hapa. Namjua vizuri sana Daniel Mwaseba, lazima angefanya kitu na tungetoka katika hiki kisanga. Lakini, hawa watu ni kina nani? Wana nia gani na Rais Mark baada ya kuweka kamera ya siri katika chumba chake? Hivi kwanini Mrombo ana tabia zote za Nato? Nato alikutwa na nini hadi kukamatwa na hawa watu na kuteswa namna ile? Maswali ni mengi sana, na kwa bahati mbaya sana watu wa kunijibu maswali yangu hawataki maswali.” Martin aliwaza peke yake akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Nimekubali kuifanya hiyo kazi” Ghafla Martin alisema kwa nguvu huku akinyanyua sura yake na kumwangalia John Masalu aliyekuwa mbele yake.

“Hongera sana Martin, ninaenda kumwelekeza Mfalme Mrombo kuwa umekubali tuone atatupa maelekezo gani? Gharama za vifaa vyote utakavyovihitaji kufanikisha jambo hili zitakuwa juu yetu” John Masalu alisema huku akinyanyuka sofani kuelekea alipoelekea Mrombo.

John Masalu alivyotoka tu sebuleni, wale wanawake watatu aliowakuta Martin wakati akiingia walinyanyuka kwa pamoja, ilikuwa ni kama wote walikuwa wameambiana au kupeana ishara. Wakaenda hadi katika sofa dogo alilokuwa Martin Hisia. Walijigawa mithili walivyojigawa kwa Mrombo, wakaanza kumfanyia mithili walivyofanya kwa Mrombo.

Kiasili, Martin ni mtoto wa mjini, ni bishoo na mpenda starehe sana licha ya uwezo wake wa ajabu sana katika uchunguzi na mapigano. Leo hii, Martin alikuwa anastareheshwa na wanawake watatu kwa mpigo, lakini katu, hakuisikia starehe. Ingawa hakuwakataza wale wanawake watatu kufanya wanachomfanyia, lakini hakuhisi ladha yoyote ile wakati wakimchua kimahaba huku wakitoa miguno mitamu ya kimapenzi.

Fikra za Martin Hisia zilikuwa maili nyingi sana kutoka pale sebuleni. Fikra zake kwa sasa zilikuwa zimefika Mikocheni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa Daniel Mwaseba. Alikuwa hajui kitatokea nini endapo Daniel akigundua kama ameusaliti upande wake, alikuwa hajui Daniel atachukua hatua gani akijua kuwa Martin amefanya kitendo hiko kibaya kabisa cha usaliti. Kubwa zaidi, alikuwa anafikiria kazi ngumu iliyopo mbele yake, kazi ya kwenda kutega kamera ya siri katika chumba cha Rais Mark Mwazilindi, lakini, alikuwa tayari kwa chochote kile kitakachotokea, kwakuwa alikuwa ana ni ya dhati ya kutaka kumwokoa ndugu yake wa damu, Nato.

JE NINI KITATOKEA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom