Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Halfani Sudy anasimulia HATARI
Mawasiliano 0629 360357
Mahali Getho

“Hatupendi kuwafanyia hiki tunachoenda kuwafanyia, lakini hatuna namna nyingine sahihi ya kufanya zaidi ya kufanya hivi, mmejifanya wakaidi, na siku zote hivi ndivyo tuwafanyavyo wakaidi” Daniel alisema kwa sauti ndogo wakati akimfuata yule aliyejiita mwenyekiti.

Hii ni Sehemu ya Tano
Mwenyekiti alimwangalia usoni Daniel, aliiona dhamira halisi ya kufanyiwa jambo baya katika sura ya Daniel Mwaseba.

“Msituue, msituue, msituue….” Mwenyekiti alisema kwa sauti ndogo huku akimwangalia Daniel kwa macho ya huruma.

“Hatuwaui, ila tutakachowafanya ni bora tungewaua” Daniel alisema wakati akiwasha jiko la umeme lilikuwa pembeni ya kiti alichofungiwa Mwenyekiti. Jiko lilipotengeneza miale ya moto, akakiweka kile chuma alichokitoa kabatini, kikaanza kupata moto. Kulingana na moto ulivyokuwa mkali ilichukua dakika zipatazo tano kile chuma kubadilika rangi na kuwa chekundu.

“Ninawapa nafasi ya mwisho ya kuwasikiliza, hamtaipata nafasi hii tena katika maisha yenu endapo nikianza kuwatesa. Nitazipasha korodani zenu kwa kile chuma cha moto! Hamtaweza kupata watoto tena. Niwaahidi tu, sitakuwa na huruma nanyi tena!” Daniel alisema akimsogelea Mwenyekiti.

“Sisi tumetumwa, tumetumwa tu, tumetumwa tu sisi…” Mwenyekiti alisema kwa sauti ya uwoga huku akimwangalia Daniel Mwaseba.

“Mmetumwa na nani?” Martin aliuliza swali akimtazama Mwenyekiti.

“Jamani, kwa kifupi sisi ni vibaka tu wa mtaani, mimi ninaitwa Babu Ogutu, yule mwenzangu anaitwa Okello. Kazi zinayotuweka hapa mjini ni kazi haramu. Mara kadhaa tunakodiwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kuwafanyia kazi zao haramu. Wiki moja iliyopita tukiwa kijiweni kwetu alikuja kijana mmoja wa makamo. Alijitambulisha kuwa anaitwa John Masalu, alituita pembeni na kutuambia kwamba kuna kazi ya kufanya ambayo ingetuingizia pesa nyingi sana, tulikubali bila kujiuliza kwakuwa ndio kazi zetu. Alitupakia kwenye gari yake na kutupeleka katika jumba moja maeneo ya Oysterbay. Ndani ya hilo jumba ndimo tulipokutana na Mrombo”

“Mrombo ni nani?” Daniel Mwaseba alimkatisha Babu Ogutu na kuuliza swali. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulisikia hilo jina.

“Mrombo, Mrombo ni jambazi anayeogopeka sana hapa jijini Dar es salaam. Wizi mwingi mkubwa unaofanyika hapa jijini kunakuwa na mkono wwa Mrombo. Kwa mfano uvamizi wa benki ya LDB pale Mlimani city uliofanyika wiki moja iliyopiata ilikuwa ni kazi ya genge la Mrombo. Uvamizi wa Juso Supermarket uliofanyika juzi kule Mikocheni pia ulifanywa na genge la Mrombo. Pia uvamizi wa vituo mbalimbali vya mafuta vinakuwa na mkono wa Mrombo”

“Eeeh endelea, milivyokutana na Mrombo?” Daniel alimkatisha Babu Ogutu.

“Mrombo ndiye aliyetupa majukumu ya kazi ile, mimi nijifanye kuwa mwenyekiti wa mtaa na Okello ajifanye kuwa mjumbe. Ilikuwa ni kazi ndogo sana lakini ingetuingizia shilingi milioni mbili. Mimi na mwenzangu tulikubali bila kujifikiria mara mbili. Jana, John Masalu alitufuata kijiweni kwetu na kutuambia kuwa leo ndio ilikuwa siku ya kazi. Na ilipofika leo asubuhi, John Masalu alitupitia na gari yake, ndani ya gari tuliwakuta wale askari na moja kwa moja tukaja ofisini kwako” Babu Ogutu alielezea kwa kirefu.

“Huyo John Masalu yeye yupo wapi?” Daniel aliuliza swali.

“John Masalu ndio yule askari aliyejitambulisha kwako kama Inspeta Hayman. Yule sio askari, ila ana urafiki na maaskari wengi hapa jijini, ambao anawatumia katika madili yake mbalimbali” Babu Ogutu alisema.

“Unaweza kutupeleka katika nyumba anayoishi Huyo Mrombo?” Daniel Mwaseba alimuuliza tena Babu Ogutu, aliamini kila alichosema.

“Atatuua, Mrombo atatuua…” Okello alisema huku sauti yake ikimaanisha alichokuwa anakisema. Walikuwa wanamuogopa Mrombo.

“Kwani mnajua sisi tutawafanya nini endapo msipotupeleka?” Daniel aliuliza swali huku akimwangalia Okello.
Okello alikaa kimya.

“Babu Ogutu, mtatupeleka nyumbani kwa Mrombo, kwa njia yoyote ile lazima tumpate Mrombo ili tujue malengo ya watu hawa” Daniel alisema akimwangalia Babu Ogutu.
Babu Ogutu aliitikia kwa kutikisa kichwa.

“Tutakuja hapa baada ya nusu saa, tukija moja kwa moja tutaelekea nyumbani kwa Mrombo. Nawaonya, msijaribu kufanya ujanja wa aina yoyote ile wa kutuhadaa, utagharimu maisha yenu!” Daniel alisema wakati akitoka nje, Martin Hisia naye alifata kwa nyuma.

Walipofika sebuleni walimkuta Hannan akiwa amekaa sofani, ameipakata tarakilishi yake akiwasubiri kwa hamu. Daniel Mwaseba alichukua nafasi ya kumueleza Hannan kila kitu kilichotokea katika chumba cha mateso. Mara kadhaa Hannan alikuwa anaitikia kwa kutikisa kichwa wakati Daniel akimsimulia na kuuliza sehemu asipoelewa vizuri.

“Hayo ndio yetu Hannan kutoka katika chumba cha mateso. Kikubwa tumeondoka na jina moja tu, Mrombo, eeeh tuambie wewe umepata nini juu ya zile kazi mbili tulizokupa za kufatilia namba ya Msamaria mwema na yule mtu aliyenipigia kunipa vitisho tukiwa hapa?” Daniel alisema huku akimwangalia Hannan.
Hannan alikohoa kidogo kuitengeneza sauti yake sawa, macho yake yakaelekea kwenye tarakilishi yake huku akiongea, “Msamaria mwema, imenifanya nitumie program maalum kuweza kuingia katika kanzidata ya mawasiliano ya jeshi la Polisi, sio kazi ndogo hata kidogo, sio tu yahitaji uwe na program maalum ambayo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuwa nayo lakini pia inabidi uwe mtaalam wa hadhi ya juu sana kuweza kucheza na kompyuta. Nimeyasikiliza mawasiliano yote ya Polisi ya leo asubuhi katika kanzidata yao, hakuna simu iliyopigwa kutoka kwa mtu anayejiita Msamaria mwema, na hiyo inamaanisha kwamba yote aliyoyasema Babu Ogutu ni kweli, Inspekta Hayman alikuwa Polisi feki, yeye alikuwa mwenyekiti feki, na wenzie wote hawakuwa halisi kwa maana ya neno halisi linavyomaanisha. Baada ya kutopata lolote kutoka katika kanzidata ya mawasiliano ya jeshi la Polisi nikahamia kwa huyu mtu aliyekupigia simu ya vitisho hivi punde. Baada ya kuichunguza namba ile, nimegundua kwamba namba imesajiliwa kwa jina la Witness Msombe. Nilianza kumchunguza huyo Witness Msombe ni nani, majibu niliyoyapata ni kwamba Witness Msombe ni mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Dar es salaam, Witness yupo mwaka wa pili akisomea hiyo shahada ya sheria. Hayo ndio niliyoyagundua juu ya zile namba mbili ulizonipa” Hannan alisema huku akiinyanyua sura yake iliyokuwa imeiinamia tarakilishi yake iliyokuwa juu ya mapaja yake.

“Safi sana Hannan, umefanya kazi kubwa sana, sasa tumepapata pa kuanzia ili kujua hawa watu wana mpango ndani ya nchi hii. Kwanza lazima tukamchukue Mrombo nyumbani kwake na kumleta hapa, ni yeye ndiye atakayetuambia anashirikiana na kina nani? Na wana mpango gani? Pili lazima tuende chuo kikuu cha Dar es salaam kuonana na huyo Witness Msombe. Lazima atuambie iweje namba yake itumike kunitishia, na bila shaka yeye atakuwa anajua mahali alipowekwa Dokta Tawakal” Daniel Mwaseba alisema kwa kirefu.

“Upo sahihi Daniel, lazima tuyafanye hayo uliyosema, lakini tutaweza kweli peke yetu kufanya mambo yote hayo, ninashauri tuongeze nguvukazi ya kutusaidia ili tufanikishe uchunguzi wetu” Martin alitoa ushauri wake.

“Upo sahihi Martin, tunahitaji nguvukazi ili kukamilisha uchunguzi wetu kwa wakati, pengine kabla ya mimi na Hannan hatujamaliza likizo zetu. Lakini niseme tu uchunguzi huu utafanywa na watu watano tuliomo humu ndani. Nitamwambia Chifu juu ya mpango wa watu hawa tukikamilisha au itakapobidi. Safari hii nataka niwaoneshe mimi ni nani hawa wapuuzi walionikatisha safari yangu ya kwenda Dubai kula starehe” Daniel alisema akimwangalia Martin Hisia.

“Daniel, unasemaje tupo watano wakati tupo watatu tu, mimi, wewe na Hannan, hao watu wawili wengine wapo wapi?” Martin aliuliza huku akimwangalia Daniel kwa mshangao.

“Sijakosea Martin, tupo watano humu ndani, Tutawatumia Babu Ogutu na Okello katika uchunguzi wetu, wale ndio watakamilisha idadi ya hao watu watano” Daniel alisema kwa kujiamini.

“Khhaaaa Daniel, umeshawaamini wale majambazi?” Martin na Hannan walijikuta wakiuliza kwa pamoja.

“Ninawaamini, ni shida tu ndizo zilizowafanya wachague upande ule haramu, tutawapa nafasi ya kubadilika na kusahihisha makosa waliyoyafanya hapa duniani. Babu Ogutu jinsi anavyoongea anaonesha kabisa hafurahii alichokuwa anakifanya, bila shaka ugumu wa maisha umemfanya aichague njia ile. Nitaenda kuongea nao, na bila shaka watakubali kuungana na sisi katika uchunguzi wetu” Daniel alisema kwa kirefu.

“Daniel, wewe ni kiongozi wangu katika operesheni nyingi sana, operesheni zilizoisha kwa mafanikio makubwa na kuiokoa nchi yetu katika hatari kutokana na uongozi wako madhubuti, lakini kwa mara ya kwanza leo napingana na wewe, sikubaliani na mpango wako wa kuwatumia wahalifu katika uchunguzi wa suala hili. Wale ni nyoka wenye sumu kali na sisi ni binadamu wa kawaida, Daniel, hakujawahi kutokea urafiki wa dhati kati ya nyoka wenye sumu kali na binadamu wa kawaida hata siku moja” Martin alionesha msimamo wake kwa kukataa mpango wa Daniel Mwaseba.

“Martin najua hisia zako zinapokupeleka, lakini naomba ukubali mpango wangu huu, hata hao wakina David unaoweza kushauri tuwatumie walikuwa katika upande sawa na kina Babu Ogutu. Hata wewe mwenyewe ulikuwa upande ule kabla hujahamia upande huu. Ni imani yangu kwako ndio iliyotuleta pamoja leo hii. Naomba unikubalie tufanye kazi na wale watu, kuna faida kubwa sana tukiwaonesha kuwa tumewaamini” Daniel Mwaseba naye alisimamia msimamo wake.

“Moja…..” Hannan alianza kuhesabu huku akinyoosha kiganja chake kwa mbele.

“Mbili…..” Martin akadakia, akanyoosha kiganja chake na kugusanisha juu ya kiganja cha Hannan.

“Tatu……” Daniel Mwaseba alimalizia huku naye akikigusisha kiganja chake juu ya mikono ya Hannan na Martin.

“Mojaaaa, mbiliiiiii, tatuuuuuu…………” Wote watatu, walihesabu kwa pamoja kwa sauti kubwa huku viganja vyao vikiwa vimeshikana.

“Tunaishi pamoja…”Daniel Mwaseba alisema….
“…na tutakufa pamoja!” Hannan Halfani na Martin Hisia waliitikia.

Walikuwa wameelewana, na walikuwa tayari kuanza kazi.
*****
Je nini kitatokea?
LAKO JICHO.
 
Achia vitu ndg
 
Tunaishi pamoja…”Daniel Mwaseba alisema….
“…na tutakufa pamoja!” Hannan Halfani na Martin Hisia waliitikia.

Walikuwa wameelewana, na walikuwa tayari kuanza kazi.

Kazi gani hiyo? Twende sawa
 
  • Thanks
Reactions: ADK
Halfani Sudy anasimulia HATARI
Mawasliano 0629 360357
Mahali Getho

“Moja…..” Hannan alianza kuhesabu huku akinyoosha kiganja chake kwa mbele.
“Mbili…..” Martin akadakia, akanyoosha kiganja chake na kugusanisha juu ya kiganja cha Hannan.
“Tatu……” Daniel Mwaseba alimalizia huku naye akikigusisha kiganja chake juu ya mikono ya Hannan na Martin.
“Mojaaaa, mbiliiiiii, tatuuuuuu…………” Wote watatu, walihesabu kwa pamoja kwa sauti kubwa huku viganja vyao vikiwa vimeshikana.
“Tunaishi pamoja…”Daniel Mwaseba alisema….
“…na tutakufa pamoja!” Hannan Halfani na Martin Hisia waliitikia.
Walikuwa wameelewana, na walikuwa tayari kuanza kazi

Na hii ni Sehemu ya Sita

SAA moja baadae, Daniel Mwaseba, Martin Hisia, Hannan Halfani, Babu Ogutu na Okello walikuwa ndani ya gari moja, Toyota x-trail ya rangi ya kijivu. Gari ilikuwa inaendeshwa na Martin Hisia kwa mwendo wa wastani kuelekea Ubungo maji, mahali kilipo chuo kikuu cha Dar es salaam. Baada ya kina Daniel kuelewana, Daniel alienda kuwaelekeza wakina Babu Ogutu juu ya mpango wao wa kuwashirikisha katika uchunguzi wao.

Okello alikubali palepale ila Babu Ogutu aliomba muda wa kutafakari, saa moja baadae naye alikubali. Sasa walikuwa wanaelekea chuo kikuu cha Dar es salam kwa tahadhari kubwa sana, kwa maana taarifa za kutafutwa kwa Daniel Mwaseba kwa kosa la kufanya mauaji ya mzee Maloto zilikuwa zimeshasambaa jijini Dar es salaam.

Saa moja baadae, walifika karibu chuo kikuu cha Dar es saalam, mahali ambapo walipanga kwenda kumsaka mwanamke anayeitwa Witness Msombe, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sheria ambaye laini yake ya simu ilitumika kumpa vitisho Daniel Mwaseba, na bila shaka huyo Witness alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anajua Dokta Tawakal yupo wapi?

Na hii ndio sababu iliyowafanya waanze kumfuata Witness badala ya Mrombo, lengo lilikuwa ni kumwokoa Dokta Tawakal kwanza, kisha ndo waende kwa Mrombo. “Hannan, utaenda kuulizia taarifa za Witness Msombe ofisini kwa Mshauri wa chuo, utajitambulisha kama ndugu yake, sisi tutakusubiri ndani ya gari. Maana tukienda kumuulizia wote watano tunaweza kuzua taharuki isiyo na sababu” Daniel Mwaseba alisema akimgeukia Hannan aliyekuwa amekaa katika siti za kati sambamba na kina Babu Ogutu.
“Sawa Daniel, hakuna tatizo” Hannan alikubali.

Dereva, Martin Hisia aliiegesha gari barabarani, usawa wa chuo cha maji Ubungo, Hannan alishuka ndani ya gari na kuelekea kilipo chuo kikuu cha Dar es salaam. Njiani hakupata tatizo lolote lile, umbo lake, urembo wake, mavazi yake, alikuwa anafanana na wanafunzi wengi aliokuwa anapishana nao katika viungo vya chuo, tofauti yake na wao ni bastola ndogo aliyoifutika kiunoni mwake, bastola ambayo isingeweza kuonwa na macho ya kawaida. Hakumuuliza mtu, alisoma vibao hadi akafika katika ofisi ambacho juu ya mlango kulikuwa na kibao kilichoandikwa kwa wino mweusi ‘Dean of Students”. Hannan alipiga hodi na kuingia ndani baada ya kukaribishwa.

“Habari za hapa Madam?” Hannan alisalimia baada ya kukaribishwa kitini na mwanamke wa makamo aliyemkuta mle ndani.
“Nzuri, karibu sana binti yangu, naitwa Madam Consolata, ni mshauri wa wanafunzi hapa, sijui wewe ni nani mwenzangu? Na ungependa nikusaidie nini?” Madam Consolata alisema huku akilifunuafunua faili moja lililokuwa juu ya meza yake. Macho ya kipelelezi yalifanikiwa kusoma jina la faili lile, lilikuwa ni faili la Witness Msombe, mtu aliyemfanya awe pale.

“Ahsante sana Madam Consolata, kwa majina ninaitwa Rose, Rose Msombe…” Hannan alivyojitambulisha tu jina lake yule mama aliacha kufunua lile faili la Witness Msombe na kumwangalia Hannan kwa uwoga, hali hiyo ilionwa pia na macho ya Hannan, lakini aliendelea kuongea,” ………nimekuja kumwangalia ndugu yangu, anasoma mwaka wa pili shahada ya sheria, anaitwa Witness Msombe”

“Witness Msombe……” Madam Consolata alisema kwa sauti ndogo, sauti iliyokosa ujasiri ilipolitamka jina hilo, kisha akasema kwa sauti ndogo sana lakini iliyosikiwa na masikio yote masikio yote mawili ya Hannan, “Witness Msombe ameuwawa…”
“Unasemaje Madam?” Hannan aliuliza kwa nguvu huku akiinuka kitini.
“Naomba kaa chini binti yangu,” Madam Consolata alisema kwa sauti ya upole.

“Siwezi kukaa chini hadi uniambie kuwa taarifa kwamba Witness Msombe ameuwawa sio za kweli!” Hannan alisema kwa nguvu akiwa bado amesimama.
“Binti yangu, ni kweli Witness Msombe ameuwawa saa chache zilizopita, kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa mwanafunzi anayeishi nae chumba kimoja katika hosteli zao, ni kwamba, saa mbili zilizopita Witness alikuja kutembelewa na rafiki yake wa kiume. Yeye, alitoka nje ili kuwapa nafasi ya kuongea vizuri. Lakini aliporudi chumbani kwake baada ya saa moja hakumkuta Witness Msombe, aliukuta mwili wa Witness Msombe ukiwa umelala kitandani huku mpini mwekundu wa kisu ukisimama imara kifuani mwake. Kwakweli hii imekuwa taarifa iliyotustua sana, ni tukio la kwanza kutokea hapa chuoni kwetu” Madam Consolata alisema huku akimwangalia Hannan.

“Haiwezekani, haiwezekani, nasema haiwezekani, haiwezi kuwa…” Hannan alisema huku akipigapiga mapaja yake mawili kwa mikono yake. “Huyo rafiki wa kiume wa Witness anaitwa nani?”
“Safina, ambaye ndiye mwanafunzi aliyekuwa anakaa na Witness Msombe chumba kimoja, alisema analijua jina moja tu la huyo rafiki wa kiume wa Witness, ana…….”

“Naomba uniambie anaitwa nani huyo Muuaji?” Hannan alimkatisha Madam Consolata huku akiuliza kwa hasira.
“Anaitwa Mrombo!” Yule mama alisema kwa sauti iliyosikiwa vyema na masikio yote mawili ya Hannan.
Mstuko uliompata Hannan haukuwa na mfano. Katika majina yote ya hapa duniani, katu hakulitegemea jina la Mrombo. Jina hili lilikuwa shabaha yao ya pili kuifuata, baada ya kutoka kuonana na Witness Msombe.

Kumbe watu hao walikuwa na uhusiano, kumbe watu hao walikuwa wanajuana, kumbe watu hao walikuwa wapenzi. Bila shaka kuna siri kubwa kati ya Witness Msombe na Mrombo, na siri hiyo Mrombo anajaribu kuificha, na ndiomaana kamua Witness Msombempenzi wake. Sasa, ni siri gani hiyo?

“Madam Consolata kusema kweli nimechanganyikiwa sana na taarifa za kuuwawa kwa ndugu yangu. Naomba nikuage kwa sasa, nitarudi, nitarudi tena…..” Hannan alisema huku akitoka nje. Madam Consolata alibaki akiushangaa mgongo wa Hannan ukitokomea mlangoni. Moja kwa moja, Hannan alienda mahali alipowaacha wakina Daniel Mwaseba, aliwakuta wote wakiwa garini wakimsubiri. Alichukua nafasi ya kuwasimulia makutano yake na Madam Consolata yalivyokuwa. Wote walishangaa sana waliposikia kwamba Mrombo ndiye alikuwa pia mtuhumiwa katika kifo cha Witness Msombe.

“Nakuja kwako sasa Mrombo! Nakuapia kwa Mungu, utanieleza hata nisichokuuliza!” Daniel Mwaseba alisema kwa kwa nguvu. Martin na Hannan walijua kwamba Daniel alikuwa amekasirika sana. Martin aliwasha gari, safari ya kuelekea Oysterbay nyumbani kwa Mrombo ilianza. Ndani ya gari ilikuwa kimya, kila mmoja akitafakari lake kichwani mwake. Iliwachukua zaidi ya saa moja kufika Oysterbay. Martin aliegesha gari upande wa pili wa barabara likiiangalia nyumba ya Mrombo kama walivyoelekezwa na kina Babu Ogutu.

“Martin na Babu Ogutu mtaenda kugonga geti, Babu Ogutu tunakutegemea wewe kutuwezesha kuingia ndani ya ile nyumba. Wewe wanakutambua mle ndani, kwahiyo….” Daniel Mwaseba hakumaliza maelekezo yake. Kwani geti kubwa la nyumba ya Mrombo lilifunguliwa, gari mpya aina ya Range rover vogue nyeusi toleo la kisasa lilikuwa linatoka.

“Ile ni gari anayotembelea Mrombo…” Babu Ogutu alisema huku akiionesha kwa kidole ile Range rover vogue nyeusi.
Gari ilipofika usawa wa geti kioo cha upande wa kushoto ulifunguliwa. Walimwona mlinzi wa getini akikimbilia pale dirishani bila shaka ili kupewa maelekezo. Baada ya kama dakika mbili za maelekezo ile gari ilianza kuondoka, dereva alielekea upande wa kulia, wakati huo yule mtu aliyekuwa anampa maelekezo yule mlinzi ndo alikuwa anapandisha kioo chake.

Kioo kilijifunga, lakini macho ya Daniel Mwaseba yaliwahi kumwona yule mtu. Daniel alibaki katika mshangao mkuu wakati ile gari ikiingia barabarani. Watu wote ndani ya gari walikuwa kimya kusubiri maelekezo ya Daniel Mwaseba, Daniel mwenyewe alikuwa katika mshangao mkuu, kwa mara nyingine tena, leo hii Daniel Mwaseba hakuyaamini macho yake, kwa maana alikuwa anamfahamu mtu aliyekuwa anaendesha ile gari, ni mtu ambaye walionana kwa mara ya kwanza asubuhi ya leo akiwa mahututi, na pia alimkuta akiwa amekatwa vipande vidogovidogo alipoenda kununua mfuko wa nailoni katika duka la zana za kilimo.

Aliyemwona Daniel Mwaseba akifunga kioo cha gari alikuwa ni mzee Maloto. Mtu anayemfanya asitembee kwa uhuru kwa maana alikuwa anatuhumiwa na jeshi la Polisi kuwa alimuua.
Hivi ni nini kinatokea hapa?
LAKO JICHO!
 
Halfani Sudy anasimulia HATARI
Mawasliano 0629 360357
Mahali Getho

“Moja…..” Hannan alianza kuhesabu huku akinyoosha kiganja chake kwa mbele.
“Mbili…..” Martin akadakia, akanyoosha kiganja chake na kugusanisha juu ya kiganja cha Hannan.
“Tatu……” Daniel Mwaseba alimalizia huku naye akikigusisha kiganja chake juu ya mikono ya Hannan na Martin.
“Mojaaaa, mbiliiiiii, tatuuuuuu…………” Wote watatu, walihesabu kwa pamoja kwa sauti kubwa huku viganja vyao vikiwa vimeshikana.
“Tunaishi pamoja…”Daniel Mwaseba alisema….
“…na tutakufa pamoja!” Hannan Halfani na Martin Hisia waliitikia.
Walikuwa wameelewana, na walikuwa tayari kuanza kazi

Na hii ni Sehemu ya Sita

SAA moja baadae, Daniel Mwaseba, Martin Hisia, Hannan Halfani, Babu Ogutu na Okello walikuwa ndani ya gari moja, Toyota x-trail ya rangi ya kijivu. Gari ilikuwa inaendeshwa na Martin Hisia kwa mwendo wa wastani kuelekea Ubungo maji, mahali kilipo chuo kikuu cha Dar es salaam. Baada ya kina Daniel kuelewana, Daniel alienda kuwaelekeza wakina Babu Ogutu juu ya mpango wao wa kuwashirikisha katika uchunguzi wao. Okello alikubali palepale ila Babu Ogutu aliomba muda wa kutafakari, saa moja baadae naye alikubali. Sasa walikuwa wanaelekea chuo kikuu cha Dar es salam kwa tahadhari kubwa sana, kwa maana taarifa za kutafutwa kwa Daniel Mwaseba kwa kosa la kufanya mauaji ya mzee Maloto zilikuwa zimeshasambaa jijini Dar es salaam.
Saa moja baadae, walifika karibu chuo kikuu cha Dar es saalam, mahali ambapo walipanga kwenda kumsaka mwanamke anayeitwa Witness Msombe, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sheria ambaye laini yake ya simu ilitumika kumpa vitisho Daniel Mwaseba, na bila shaka huyo Witness alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anajua Dokta Tawakal yupo wapi? Na hii ndio sababu iliyowafanya waanze kumfuata Witness badala ya Mrombo, lengo lilikuwa ni kumwokoa Dokta Tawakal kwanza, kisha ndo waende kwa Mrombo.
“Hannan, utaenda kuulizia taarifa za Witness Msombe ofisini kwa Mshauri wa chuo, utajitambulisha kama ndugu yake, sisi tutakusubiri ndani ya gari. Maana tukienda kumuulizia wote watano tunaweza kuzua taharuki isiyo na sababu” Daniel Mwaseba alisema akimgeukia Hannan aliyekuwa amekaa katika siti za kati sambamba na kina Babu Ogutu.
“Sawa Daniel, hakuna tatizo” Hannan alikubali.
Dereva, Martin Hisia aliiegesha gari barabarani, usawa wa chuo cha maji Ubungo, Hannan alishuka ndani ya gari na kuelekea kilipo chuo kikuu cha Dar es salaam. Njiani hakupata tatizo lolote lile, umbo lake, urembo wake, mavazi yake, alikuwa anafanana na wanafunzi wengi aliokuwa anapishana nao katika viungo vya chuo, tofauti yake na wao ni bastola ndogo aliyoifutika kiunoni mwake, bastola ambayo isingeweza kuonwa na macho ya kawaida. Hakumuuliza mtu, alisoma vibao hadi akafika katika ofisi ambacho juu ya mlango kulikuwa na kibao kilichoandikwa kwa wino mweusi ‘Dean of Students”. Hannan alipiga hodi na kuingia ndani baada ya kukaribishwa.
“Habari za hapa Madam?” Hannan alisalimia baada ya kukaribishwa kitini na mwanamke wa makamo aliyemkuta mle ndani.
“Nzuri, karibu sana binti yangu, naitwa Madam Consolata, ni mshauri wa wanafunzi hapa, sijui wewe ni nani mwenzangu? Na ungependa nikusaidie nini?” Madam Consolata alisema huku akilifunuafunua faili moja lililokuwa juu ya meza yake. Macho ya kipelelezi yalifanikiwa kusoma jina la faili lile, lilikuwa ni faili la Witness Msombe, mtu aliyemfanya awe pale.
“Ahsante sana Madam Consolata, kwa majina ninaitwa Rose, Rose Msombe…” Hannan alivyojitambulisha tu jina lake yule mama aliacha kufunua lile faili la Witness Msombe na kumwangalia Hannan kwa uwoga, hali hiyo ilionwa pia na macho ya Hannan, lakini aliendelea kuongea,” ………nimekuja kumwangalia ndugu yangu, anasoma mwaka wa pili shahada ya sheria, anaitwa Witness Msombe”
“Witness Msombe……” Madam Consolata alisema kwa sauti ndogo, sauti iliyokosa ujasiri ilipolitamka jina hilo, kisha akasema kwa sauti ndogo sana lakini iliyosikiwa na masikio yote masikio yote mawili ya Hannan, “Witness Msombe ameuwawa…”
“Unasemaje Madam?” Hannan aliuliza kwa nguvu huku akiinuka kitini.
“Naomba kaa chini binti yangu,” Madam Consolata alisema kwa sauti ya upole.
“Siwezi kukaa chini hadi uniambie kuwa taarifa kwamba Witness Msombe ameuwawa sio za kweli!” Hannan alisema kwa nguvu akiwa bado amesimama.
“Binti yangu, ni kweli Witness Msombe ameuwawa saa chache zilizopita, kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa mwanafunzi anayeishi nae chumba kimoja katika hosteli zao, ni kwamba, saa mbili zilizopita Witness alikuja kutembelewa na rafiki yake wa kiume. Yeye, alitoka nje ili kuwapa nafasi ya kuongea vizuri. Lakini aliporudi chumbani kwake baada ya saa moja hakumkuta Witness Msombe, aliukuta mwili wa Witness Msombe ukiwa umelala kitandani huku mpini mwekundu wa kisu ukisimama imara kifuani mwake. Kwakweli hii imekuwa taarifa iliyotustua sana, ni tukio la kwanza kutokea hapa chuoni kwetu” Madam Consolata alisema huku akimwangalia Hannan.
“Haiwezekani, haiwezekani, nasema haiwezekani, haiwezi kuwa…” Hannan alisema huku akipigapiga mapaja yake mawili kwa mikono yake. “Huyo rafiki wa kiume wa Witness anaitwa nani?”
“Safina, ambaye ndiye mwanafunzi aliyekuwa anakaa na Witness Msombe chumba kimoja, alisema analijua jina moja tu la huyo rafiki wa kiume wa Witness, ana…….”
“Naomba uniambie anaitwa nani huyo Muuaji?” Hannan alimkatisha Madam Consolata huku akiuliza kwa hasira.
“Anaitwa Mrombo!” Yule mama alisema kwa sauti iliyosikiwa vyema na masikio yote mawili ya Hannan.
Mstuko uliompata Hannan haukuwa na mfano. Katika majina yote ya hapa duniani, katu hakulitegemea jina la Mrombo. Jina hili lilikuwa shabaha yao ya pili kuifuata, baada ya kutoka kuonana na Witness Msombe. Kumbe watu hao walikuwa na uhusiano, kumbe watu hao walikuwa wanajuana, kumbe watu hao walikuwa wapenzi. Bila shaka kuna siri kubwa kati ya Witness Msombe na Mrombo, na siri hiyo Mrombo anajaribu kuificha, na ndiomaana kamua Witness Msombempenzi wake. Sasa, ni siri gani hiyo?
“Madam Consolata kusema kweli nimechanganyikiwa sana na taarifa za kuuwawa kwa ndugu yangu. Naomba nikuage kwa sasa, nitarudi, nitarudi tena…..” Hannan alisema huku akitoka nje. Madam Consolata alibaki akiushangaa mgongo wa Hannan ukitokomea mlangoni.
Moja kwa moja, Hannan alienda mahali alipowaacha wakina Daniel Mwaseba, aliwakuta wote wakiwa garini wakimsubiri. Alichukua nafasi ya kuwasimulia makutano yake na Madam Consolata yalivyokuwa. Wote walishangaa sana waliposikia kwamba Mrombo ndiye alikuwa pia mtuhumiwa katika kifo cha Witness Msombe.
“Nakuja kwako sasa Mrombo! Nakuapia kwa Mungu, utanieleza hata nisichokuuliza!” Daniel Mwaseba alisema kwa kwa nguvu. Martin na Hannan walijua kwamba Daniel alikuwa amekasirika sana.
Martin aliwasha gari, safari ya kuelekea Oysterbay nyumbani kwa Mrombo ilianza. Ndani ya gari ilikuwa kimya, kila mmoja akitafakari lake kichwani mwake. Iliwachukua zaidi ya saa moja kufika Oysterbay. Martin aliegesha gari upande wa pili wa barabara likiiangalia nyumba ya Mrombo kama walivyoelekezwa na kina Babu Ogutu.
“Martin na Babu Ogutu mtaenda kugonga geti, Babu Ogutu tunakutegemea wewe kutuwezesha kuingia ndani ya ile nyumba. Wewe wanakutambua mle ndani, kwahiyo….” Daniel Mwaseba hakumaliza maelekezo yake. Kwani geti kubwa la nyumba ya Mrombo lilifunguliwa, gari mpya aina ya Range rover vogue nyeusi toleo la kisasa lilikuwa linatoka.
“Ile ni gari anayotembelea Mrombo…” Babu Ogutu alisema huku akiionesha kwa kidole ile Range rover vogue nyeusi.
Gari ilipofika usawa wa geti kioo cha upande wa kushoto ulifunguliwa. Walimwona mlinzi wa getini akikimbilia pale dirishani bila shaka ili kupewa maelekezo. Baada ya kama dakika mbili za maelekezo ile gari ilianza kuondoka, dereva alielekea upande wa kulia, wakati huo yule mtu aliyekuwa anampa maelekezo yule mlinzi ndo alikuwa anapandisha kioo chake. Kioo kilijifunga, lakini macho ya Daniel Mwaseba yaliwahi kumwona yule mtu. Daniel alibaki katika mshangao mkuu wakati ile gari ikiingia barabarani. Watu wote ndani ya gari walikuwa kimya kusubiri maelekezo ya Daniel Mwaseba, Daniel mwenyewe alikuwa katika mshangao mkuu, kwa mara nyingine tena, leo hii Daniel Mwaseba hakuyaamini macho yake, kwa maana alikuwa anamfahamu mtu aliyekuwa anaendesha ile gari, ni mtu ambaye walionana kwa mara ya kwanza asubuhi ya leo akiwa mahututi, na pia alimkuta akiwa amekatwa vipande vidogovidogo alipoenda kununua mfuko wa nailoni katika duka la zana za kilimo. Aliyemwona Daniel Mwaseba akifunga kioo cha gari alikuwa ni mzee Maloto. Mtu anayemfanya asitembee kwa uhuru kwa maana alikuwa anatuhumiwa na jeshi la Polisi kuwa alimuua.
Hivi ni nini kinatokea hapa?
LAKO JICHO!
Noma sana
 
Halfani Sudy anasimulia HATARI
Mawasiliano 0629 360357
Mahali Getho

Gari ilipofika usawa wa geti kioo cha upande wa kushoto ulifunguliwa. Walimwona mlinzi wa getini akikimbilia pale dirishani bila shaka ili kupewa maelekezo. Baada ya kama dakika mbili za maelekezo ile gari ilianza kuondoka, dereva alielekea upande wa kulia, wakati huo yule mtu aliyekuwa anampa maelekezo yule mlinzi ndo alikuwa anapandisha kioo chake.

Kioo kilijifunga, lakini macho ya Daniel Mwaseba yaliwahi kumwona yule mtu. Daniel alibaki katika mshangao mkuu wakati ile gari ikiingia barabarani. Watu wote ndani ya gari walikuwa kimya kusubiri maelekezo ya Daniel Mwaseba, Daniel mwenyewe alikuwa katika mshangao mkuu, kwa mara nyingine tena, leo hii Daniel Mwaseba hakuyaamini macho yake, kwa maana alikuwa anamfahamu mtu aliyekuwa anaendesha ile gari, ni mtu ambaye walionana kwa mara ya kwanza asubuhi ya leo akiwa mahututi, na pia alimkuta akiwa amekatwa vipande vidogovidogo alipoenda kununua mfuko wa nailoni katika duka la zana za kilimo.

Aliyemwona Daniel Mwaseba akifunga kioo cha gari alikuwa ni mzee Maloto. Mtu anayemfanya asitembee kwa uhuru kwa maana alikuwa anatuhumiwa na jeshi la Polisi kuwa alimuua.

Na hii ni sehemu ya Saba.

“Ifuate ile gari Martin, tumia ujuzi wako wote wa kuwafatilia wahalifu kuhakikisha hawa jamaa hawajui kama wanafuatwa” Daniel alisema huku akilipiga bega la kushoto la Martin kwa mkono wake wa kulia. Bila ajizi, Martin alianza kuifukuzia ile gari ambayo ilikuwa imeshawaacha kwa umbali mkubwa kidogo. Dakika kumi zilitosha kwa gari la kina Martin kuikaribia ile range rover vogue nyeusi, sasa kulikuwa na utofauti wa magari kama matatu kati yao kulifikia.

“Babu Ogutu unamfahamu mzee Maloto?”Ghafla Daniel Mwaseba alirusha swali huku akiangalia mbele.

“Mhh ninaweza kusema ninamfahamu mzee Maloto ingawa sio sana, tumewahi kufanya kazi pamoja kama mara tatu au nne. Mzee Maloto ni mlinzi mkuu wa Mrombo” Babu Ogutu alijibu swali la Daniel Mwaseba.

“Mlinzi mkuu wa Mrombo, iweje Mrombo achague mlinzi mzee kama yule?” Daniel Mwaseba aliuliza swali kwa mshangao.

“Watu wengi hushangaa wakisikia kwamba yule mzee ndiye mlinzi mkuu wa Mrombo. Sikufichi Daniel, kwa mara ya kwanza hata mimi nilishangaa sana. Lakini, baada ya kufanya naye kazi, mshangao wangu wote uliisha. Yule mzee anastahili kuwa mlinzi wa Mrombo, ana uwezo wa ajabu sana ambao ni ngumu kupatikana katika kichwa na mwili wa binadamu wa kawaida” Babu Ogutu alisema kwa hisia sana.

“Mmmh yah inawezekana, kwa maana tukio nililolishuhudia leo limenipa maswali mengi sana juu ya huyu mtu, hamu ya kumshika mikononi mwangu ili ajibu maswali yangu inapanda kila mshale wa sekunde wa saa unaposogea. Bila shaka kumpata mzee Maloto utakuwa ufunguo kwetu katika kutatua kisa hiki cha utata. Natamani niote mbawa nipae na kwenda kutua katika ile gari na kumchomoa mzee Maloto” Daniel alisema kwa hisia. Wakati huo gari akiloendesha mzee Maloto lilipunguza mwendo, likawasha taa ya pembeni ya upande wa kushoto kisha kukata upande huo.

“Wewe pitiliza Martin, tutaenda kusimama pale kwa mbele” Daniel alimwambia Martin. Martin Hisia alifanya kama alivyoelekeza Daniel Mwaseba. Alipita pale mahali walipokata kina mzee Maloto na kwenda kusimama kwa mbele.

“Geuza sasa, tuwafuate” Daniel Mwaseba alisema baada ya kufika kwa mbele kidogo.

Martin alitikisa kichwa chake kukubaliana na Daniel Mwaseba. Akatafuta nafasi nzuri ya kugeuza gari na kuanza kuelekea ule upande walipokuwa wametoka. Walipokata ile kona, waliliona lile gari likiwa limeegeshwa mbele ya duka moja mita kama mia mbili hivi.

“Wameshagundua kama tunawafuata” Daniel Mwaseba alisema kwa uhakika mkubwa huku akiichomoa bastola yake kiunini.

“Mama weee! tutafanyaje sasa?” Okello aliuliza huku sauti yake ikionesha kuwa alikuwa katika uwoga mkubwa sana.

“Okello, sisi hatuna msamiati wa uwoga katika kamusi za ubongo wetu. Uwoga pekee tunaoweza kuufanya ni wa kuigiza ili tupate taarifa, lakini sio uwoga wa kumuogopa mtu au tukio. Sisi ndio tunapaswa kuogopwa sio sisi tuogope!” Hannan alisema akimtazama Okello.

Okello alijisikia vibaya sana kuambiwa maneno yale na mtoto wa kike. Alijiona dhaifu sana mbele ya wenzake. Alijiapia kimoyomoyo kwamba hatuonesha uwoga tena mbele ya wenzake.

“Okello nadhani umemwelewa Hannan, Martin endesha gari taratibu, lakini utaongeza kasi tukilikaribia lile gari lao. Bila shaka jamaa wamepanga kutushambulia, tatizo hatujui wapo wangapi garini na wamejipanga vipi? Tungefanya kitu. Jamani, kila mmoja awe tayari na silaha yake, lolote linaweza kutokea dakika chache zijazo” Daniel alisema huku akiichomoa kwa mkono wa kushoto bastola yake nyingine kiunoni mwake. Tayari alikuwa ameshachomoa bastola yake nyingine hapo awali. Sasa alikuwa na bastola mbili mikononi, tayari kwa lolote, muda wowote.
Wakina Hannan, Okello na Babu Ogutu kila mmoja alijiandaa kwa kuweka sawa silaha zao tayaritayari, wakati Martin, bila wasiwasi wowote akiwa makini na gia, breki na usukani wa gari. Alikuwa akifuata maelekezo ya Daniel Mwaseba.

Zilipofika mita kama mia kabla hawajalifikia lile Range rover vogue, Martin aliongeza kasi ya gari lao kwa namna ya ajabu sana, gari lilipata moto na kutimka mithili lilikuwa katika mashindano ya magari. Watu wote waliokuwa katika ile Range rover vogue nyeusi hakuna aliyeamini kwa kitendo kile cha ghafla kilichotokea. Wao, walikuwa na silaha zao tayari kulishambulia gari ambalo walihisi linawafuata. Ujio wa taratibu wa gari hilo uliwafanya wajipange vizuri ili walishambulie pindi litakapofika katika usawa waliosimama, lakini kuongezeka kwa ghafla kwa mwendokasi wa gari kuliwaacha mdomo wazi. Hakuna aliyejiandaa kwa tukio hilo hivyo walishindwa hata kulishambulia.

“Wamejua kama tuliwawekea mtego hapa” Mzee Maloto alisema kwa sauti ndogo.

“Ni kina nani wale lakini wanaojaribu kukifuata kifo chao!” Mrombo aliuliza kwa sauti yake nzito.

“Bila shaka wanaweza kuwa askari Polisi, pengine wamenusa uhusika wetu katika tukio tuliolifanya kule chuo kikuu cha Dar es salaam” John Masalu alisema akiwa ameketi katika siti za nyuma.

“Sidhani kama tukio la kumuua yule Malaya ndio limewafanya hawa manjagu watufuate, nina shaka sana na hilo, mzee Maloto geuza gari, nitampigia simu Nyoka kwamba tumeghairisha safari ya kwenda kwake baada ya kugundua kwamba kuna mkia unatufuata” Mrombo alisema.

Mzee Maloto aligeuza gari, na moja kwa moja walirejea nyumbani kwa Mrombo, ndani ya gari kulikuwa kimya, kila mmoja akiwaza lake kichwani, tukio la kufuatiliwa na wale jamaa liliwaumiza sana vichwa vyao.

“Yaani kuna watu wananijua mimi halafu mimi siwajui? Ni kina nani wale watu waliofikia hatua yana kunifuatilia?” Mrombo aliongea peke yake wakati wakiingia katika geti la nyumba yao.

“Usiwe na wasiwasi Mrombo, tunaenda kuwajua hivi punde wale jamaa, bila shaka jamaa wameanza kutufatilia kuanzia hapa nyumbani, bila shaka wanajua kama wewe unaishi hapa, lazima watarudi tu hapa baada ya kugundua kwamba tuligundua kuwa walikuwa wanatufatilia. Cha msingi ni kuongeza umakini na ulinzi hapa nyumbani, watakifuata tu kifo chao” John Masalu alisema.
Mrombo akatoa pakti la sigara aliloliweka katika mfuko wake wa shati jeupe.

Akatoa sigara moja na kuiweka mdomoni. Watu wote ndani ya gari walianza kutetemeka. Harakaharaka huku akitetemeka mzee Maloto akatoa kiberiti cha gesi kwenye droo, akakiwasha na kuiunguza ile sigara ya Mrombo pale mdomoni mwake. Mrombo akaivuta ile sigara, kisha akatoa moshi mwingi.

“Nataka wale watu wawe ndani ya himaya yangu ndani ya saa tatu!” Mrombo alisema baada ya kuitoa ile sigara mdomoni.
“Sawa mkuu!” John Masalu na watu wengine wote waliokuwa wamekaa katika siti za nyuma waliitikia kwa pamoja. Hili halikuwa ombi, ilikuwa ni amri, amri kutoka kwa Mrombo. Na amri hii huitoa siku zote baada ya kuvuta funda la kwanza la moshi wa sigara. Kushindwa kufanya akisemacho Mrombo, baada ya kuvuta funda la kwanza la sigara, ni sawa na kukataa kuendelea kuishi! Kwa hivyo, kwa jasho na damu, iliwapasa kuwapata wakina Daniel ndani ya saa tatu, kinyume na hapo, Mrombo huwapa adhabu nyepesi, na adhabu nyepesi kwa Mrombo, ni kukuuwa!

Mzee Maloto aliegesha gari, wakati Mrombo akishuka na kuelekea ndani, John Masalu alikusanya walinzi wote na kuwapa amri ya Mrombo. Walipewa saa tatu kuwasaka watu waliokuwa wanawafatilia na kuwakatisha safari yao ya kuelekea kwa Nyoka. Sekeseke kubwa sana liliibuka katika mitaa yote ya Oysterbay na jiji zima la Dar es salaam.

Je nini kitatokea?
LAKO JICHO!
 
Mrombo akatoa pakti la sigara aliloliweka katika mfuko wake wa shati jeupe. Akatoa sigara moja na kuiweka mdomoni. Watu wote ndani ya gari walianza kutetemeka. Harakaharaka huku akitetemeka mzee Maloto akatoa kiberiti cha gesi kwenye droo, akakiwasha na kuiunguza ile sigara ya Mrombo pale mdomoni mwake. Mrombo akaivuta ile sigara, kisha akatoa moshi mwingi.

“Nataka wale watu wawe ndani ya himaya yangu ndani ya saa tatu!” Mrombo alisema baada ya kuitoa ile sigara mdomoni.

Twende Sawa. Hii ni Sehemu Inayofuata
 
Halfani Sudy anaandika HATARI
Mawasiliano 0629 360357
Mahali Bliss Hotel, Nyali Kenya.

Mzee Maloto aliegesha gari, wakati Mrombo akishuka na kuelekea ndani, John Masalu alikusanya walinzi wote na kuwapa amri ya Mrombo. Walipewa saa tatu kuwasaka watu waliokuwa wanawafatilia na kuwakatisha safari yao ya kuelekea kwa Nyoka. Sekeseke kubwa sana liliibuka katika mitaa yote ya Oysterbay na jiji zima la Dar es salaam.

Na hii ni Sehemu ya Nane, Karibu.

WAKINA Daniel walikuwa wameshhafika Mikocheni, nyumbani kwa Daniel Mwaseba. Baada ya kugundua kwamba wakina mzee Maloto waligundua kwamba walikuwa wanawafuatilia, moja kwa moja walirejea katika maskani yao. Sasa walikuwa sebuleni wakichanga karata zao upya, kutafuta namna sahihi ya kumtia mikononi mwao Mrombo.

“Lakini waligunduaje kama tulikuwa tunawafuata? Unajua kugundua kwao kumenijulisha kwamba hawa jamaa ni watu hatari sana. Tuliacha gari zaidi ya tatu kati yetu na wao, na hata namna nikivyoendesha hakuna kiumbe ambacho kingegundua kwamba tulikuwa tunawafatilia wao. Wamenistaajabisha sana!” Martin Hisia alisema akishangaa kwa namna gari jamaa waligundua kama wanafatilia.

“Mrombo ni binadamu mwenye hisia kali zaidi hapa duniani. Ana uwezo wa kuihisi hatari ikiwa mbali hata kama itakuwa inamjia taratibu. Kama nilivyosema awali, sote hapa tunamjua Mrombo kwa jina moja tu, lakini wapo wanaomuongeza jina la pili, wanamwita Mrombo Hisia, kutokana na huo uwezo wake wa ajabu wa kuihisi hatari hata ikiwa mbali kwa kiasi gani?” Babu Ogutu alisema baada ya kuiweka mezani bilauri ya maji aliyokuwa anakunywa.
Macho manne ya Daniel na Hannan yalimwangalia Martin kwa kustaajabu, huku Martin yeye akionesha sura ya kutoamini maneno aliyokuwa anaongea Babu Ogutu.

“Mrombo Hisia……” Martin alilirudia hilo jina kwa sauti ndogo. Siku zote aliamini yeye ndiye binadamu mwenye hisia zaidi hapa duniani kama alivyoaminishwa na Daniel Mwaseba, leo hii, anaambiwa kwamba kuna watu duniani wanaamini kwamba Mrombo ndiye binadamu mwenye hisia zaidi hapa duniani. Hamu ya kumwona huyo Mrombo ilifika kileleni ndani ya mtima wa moyo wake.

“Daniel, lazima tukaivamie nyumba ya Mrombo usiku wa leo! Tuhakikishe tunampata na kumleta hapa huyo Mrombo kivyovyote vile!” Martin alisema kwa nguvu akimwangalia Daniel Mwaseba.
“Martin, kwa leo itakuwa ni ngumu sana kwenda nyumbani kwa Mrombo, kwa vyovyote vile ataimarisha ulinzi katika nyumba yake kwa kuhisi lazima usiku tutaenda kumwinda. Tumuache asahau kwanza kuhusu sisi kwa saa kadhaa ndipo tumfuate” Daniel alishauri akimtazama Daniel Mwaseba.

Martin alikaa kimya lakini macho yake yalionesha kuwa hakuridhika kabisa na uamuzi wa Daniel Mwaseba. Moyo wake ulitamani sana kukutana na huyo mtu anayeitwa Mrombo Hisia.
Baada ya saa moja Hannan alikuwa ameshaandaa chakula, wote walikula wali kwa nyama ya kuku, huku Babu Ogutu akichukua nafasi ya kuwasimulia matukio mbalimbali ya uporaji aliyowahi kuyafanya katika maisha yake ya ujambazi.

Alionesha kusikitika sana kwa matukio mabaya aliyowahi kuyafanya, huku mara kwa mara akimshukuru sana Daniel kwa kumtoa katika upande ambao yeye aliuita upande wa kishetani. Hadithi za matukio yao, zikwafikisha katika hadithi ambayo ilikuwa inamhusu Mrombo. Martin alikuwa makini sana aliposikia kuwa hadithi hiyo ilikuwa inamhusu Mrombo.

“…nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi….” Babu Ogutu alianza kuhadithia, “…..siku hiyo nilikuwa getho, sikuwa na mishe yoyote ile ya kufanya. Ndiposa, simu yangu ya mkononi iliita, niliitoa mfukoni simu yangu mfukoni na kuangalia jina la aliyekuwa ananipigia. Alikuwa ni John Masalu, yule mshirika wa karibu sana wa Mrombo. Nilipopokea, Masalu alinambia kwamba kuna kazi ya kwenda kuzichekesha gari za abiria huko Kibiti”

“Kuchekecha ndo nini?” Hannan aliuliza akiwa amelishikilia paja la kuku lilikuwa likichuruzika mchuzi.

“Kuchekecha ni kuwaibia abiria wa magari wanapokuwa safarini. Mnaenda kujitega porini na kutega gogo kubwa barabarani, magari yakifika hilo eneo lazima yasimame, yakisimama tu inakuwa wamefanya kosa watakalolijutia milele. Sisi huwa tumejificaha porini tukiwa na silaha, hujitokeza na kuwaibia kila kitu abiria. Sasa siku hiyo tulienda kufanya kazi hiyo na Mrombo mwenyewe.

Ilikuwa ni siku yangu ya kwanza kufanya kazi na Mrombo, nilikuwa makini sana kwakuwa Mrombo havumilii makosa kazini, naye kama kiongozi, kila neno lake aliongealo baada ya kuvuta funda la kwanza la sigara ni amri, usipoifuata basi utakifuata kifo. Tukajificha vizuri porini, gari la kwanza lililopata bahati mbaya kukutana na sisi lilikuwa Tazanja, gari lifanyalo safari zao kutoka Dar es salaam kuelekea Kilwa.

Gari ilikuwa katika mwendokasi mkubwa, lakini kwa bahati nzuri dereva aliweza kuliona gogo akiwa kwa mbali na kupunguza mwendo, akafanikiwa kusimama, aliposimama tu, kabla hajapata nafasi ya kutafakari nini cha kufanya, tulitoka porini na kulivamia lile basi. Tulikuwa kama watu kumi hivi, kila mmoja akiwa na bunduki yake mkononi. Tukaanza kuwachekesha abiria waliokuwepo katika lile gari. Kuna kijana mmoja, nakumbuka alikuwa anajiita Chura Kazini, ndiye aliyepewa kazi ya kukusanya pesa, simu na mali mbalimbali na kuweka kwenye viroba. Sasa Chura wakati akikusanya zile mali kwa bahati mbaya alikutana na mtu anayemfahamu…”

“Alikutana na nani?” Hannan aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua.
“Chura alikutana na mama yake mzazi, ingawa Chura alikuwa ameificha sura yake kwa kitambaa cheusi alichokitengeza kama vile wavaavyo Maninja, lakini kwa bahati mbaya sana mama yake alimtambua. Si unajua mtoto kwa mama. Kosa alilolifanya yule mama ni kujionesha kuwa amemtambua Chura, na kosa kubwa zaidi alilolifanya ni kujionesha kwamba Chura ni mwanawe mbele Mrombo. Mrombo alisikia, aliwatazama Chura na mama yake kwa sekunde kama tano, harakaharaka alitoa pakiti ya sigara na sigara na kutoa sigara moja, kwa kasi mzee Maloto alimfuata akiwa tayari amewasha kibiriti cha gesi, alikiweka kwenye ile sigara iliyokuwa katika papi za midomo za Mrombo, sigara ikaungua. Mrombo alivuta ile sigara, akatoa moshi mwingi hewani kisha akasema neno moja tu “Muuwe!”

“Khaaa yaani amuuwe mama yake?” Hannan aliuliza kwa mshangao.

“Ndivyo alivyosema Mrombo, na kumbuka kuwa Mrombo akisema neno baada ya kuvuta funda la kwanza la moshi wa sigara inakuwa ni amri. Kwahiyo Chura aliamrishwa amuuwe mama yake mzazi. Chura alisita kwa sekunde zisizozidi tatu, kwa sekunde hizo za kusita alikuwa tayari amekiuka amri ya Mrombo. Mrombo akamwamrisha John Masalu amchukue yule mama. Akamrisha pia mtu mwengine abebe vile vitu tulivyokuwa tumevipora, kisha tukatokomea porini. Njia nzima Chura alikuwa analia huku akimuombea msamaha mama yake, alikuwa tayari kufa yeye lakini mama yake mzazi aachwe hai. Maneno ambayo hayakutiliwa maanani kabisa na Mrombo. Yeye alikuwa kama hamsikii vile, anavuta sigara huku anatabasamu, pengine angekiuka amri ya Mrombo kabla hajavuta funda la kwanza la sigara angepata matokeo mengine, lakini sio baada ya Mrombo kuvuta funda la kwanza la sigara.

Tulipofika tu sebuleni, maskani kwetu, Mrombo alitoa sigara mpya, niliona watu wowote wakitetemeka, kumbe walikuwa wanajua kwamba baada ya kuvuta funda la kwanza kinachofuata ni amri ambayo ni lazima itekelezwe. Alipoiweka ile sigara mdomoni, kwa kasi mzee Maloto alisogea na kumuwashia kwa kiberiti cha gesi. Mrombo allivuta moshi wa sigara na kusema,

“Mvue nguo zote!” Mrombo alisema huku akiniangalia mimi. Sikuwa na namna, nilimfuata yule mama na kumvua nguo harakaharaka. Mama alibaki uchi wa mnyama!. Nililiona tabasamu kutoka kwa Mrombo akimwangalia yule mama mtu mzima akiwa uchi! Ulikuwa ni udhalilishaji wa kiwango cha juu. Mrombo aliitupa ile sigara ambayo aliivuta kidogo sana, akatoa sigara mpya kutoka katika mfuko wake wa shati, kama kawaida mzee Maloto alienda kumuwashia kwa kiberiti chake cha gesi, baada ya kuvuta fundo la kwanza, akasema,

“Mto####### mama yako!” alisema hiyo kauli hiyo kwa sauti kubwa huku akimwangalia Chura.
“Ni Nato!” Ghafla Martin Hisia alisema kwa nguvu huku akiipiga kofi meza ya kioo iliyokuwepo mbele yake.

“Nato? Ni nani Nato?” Daniel aliuliza huku akimwangalia Martin Hisia kwa mshangao.

“Hisia zangu zimekuwa sahihi, tangu niliposikia kuhusu Mrombo kuna hisia fulani hunijia kuwa namjua huyo mtu. Babu Ogutu aliposema kuwa Mrombo huwa anajiita yeye ni binadamu mwenye hisia zaidi duniani, nikaamini hisia zangu zilikuwa ni sahihi. Daniel, wewe huniita mimi kuwa ni binadamu mwenye hisia zaidi duniani, lakini Nato huwa anapenda kujiita hivyo yeye mwenyewe hivyo. Na Babu Ogutu aliposema kuwa miongoni mwa tabia za Mrombo ni kuwa,neno lake la kwanza baada ya kuvuta funda la kwanza la sigara huwa ni amri, hapo ndipo hisia zangu zilipokamilika. Mrombo Hisia ni Nato, kaka yangu, baba mmoja, mama mmoja!” Martin Hisia alisema kwa hisia kali sana.
Je nini kitatokea katika Hatari?
TUKUTATANE HAPA JUMAPILI..

Maoni ni muhimu sana. Toa maoni yako
 
Halfani Sudy anaandika HATARI
Mawasiliano 0629360357
Mahali Vikindu, Pwani

“Ni Nato!” Ghafla Martin Hisia alisema kwa nguvu huku akiipiga kofi meza ya kioo iliyokuwepo mbele yake.
“Nato? Ni nani Nato?” Daniel aliuliza huku akimwangalia Martin Hisia kwa mshangao.
“Hisia zangu zimekuwa sahihi. Maana tangu niliposikia kuhusu Mrombo kuna hisia fulani hunijia kuwa namjua huyo mtu. Sasa pale Babu Ogutu aliposema kuwa Mrombo huwa anajiita yeye ni binadamu mwenye hisia zaidi duniani, nikaamini hisia zangu zilikuwa ni sahihi. Daniel, mara kwa mara huniita mimi kuwa ni binadamu mwenye hisia zaidi duniani, lakini tofauti na mimi, Nato huwa anapenda kujiita hivyo yeye mwenyewe hivyo. Na Babu Ogutu aliposema kuwa miongoni mwa tabia za Mrombo ni kuwa, neno lake la kwanza baada ya kuvuta funda la kwanza la sigara huwa ni amri, hapo ndipo hisia zangu zilipokamilika. Mrombo Hisia ni Nato, kaka yangu, baba mmoja, mama mmoja!” Martin Hisia alisema kwa hisia kali sana.

Karibuni Mabibi na Mabwana, maana hii ni Sehemu ya Tisa.

“Mmmmh daaah, sikutegemea kama Mrombo atakuwa ndugu yako Martin, lakini ilikuwaje hadi Mrombo au Nato aliingia katika upande ule mbaya?” Daniel Mwaseba alimuuliza Martin, huku watu wote wakiwa katika mshangao mkuu mle ndani.

“Ni hadithi ndefu sana Daniel, lakini kwa kifupi tu, Nato ni ndugu yangu wa damu, na alikuwa mtata tangu zamani. Neno lake baada ya kuvuta funda lwa kwanza la sigara lilikuwa ni amri. Mimi nilijaribu kumshauri juu ya kuamini kwake hivyo lakini hakutaka kunisikia. Alipofikisha umri wa miaka kumi na nne, Nato alitoroka nyumbani. Na hakurudi tena hadi leo hii, ni miaka kumi na tisa sasa imepita. Kuondoka kwake kuliwaumiza sana baba na mama, unajua sisi tumezaliwa wawili tu, mimi na Nato, hivyo wazee waliona kwamba wamepoteza mmoja wa ubavu wao” Martin Hisia alisema.

“MMMMhhhh!” Daniel alipumua kwa nguvu, aliona kwamba misheni itakuwa ngumu na ya hatari sana tofauti kabisa na alivyofikiria awali. Ndani ya moyo wake, hakuamini kwamba Martin ataweza kufanya misheni hii kwa asilimia miamoja, kufanya misheni ya kumsaka ndugu yako wa damu ili apelekwe katika vyombo vya dola sio mas’hara. Yahitaji ujasiri mkubwa sana, yahitaji uzalendo usio na mfano na kujiamini kwa maana sahihi neno kujiamini linavyomaanisha.

“Babu Ogutu, vipi Chura alifanya mapenzi na mama yake?” Daniel aliuliza swali akimwangalia Babu Ogutu huku akijifanya hajastushwa sana na taarifa ya Martin Hisia.

“Hapana kaka Daniel, pamoja na ukichaa wote wa Chura lakini hilo hakuweza kulifanya katu, na siku ile ndio ilikuwa mwisho wa maisha ya Chura na mama yake katika ulimwengu huu. Mrombo aliwaua kwa kifo kibaya sana mtoto na mama yake. Nakumbuka alimwagiza John Masalu akageleke mafuta ya kula katika jiko la gesi, yalipopata moto hasa, aliwauwa mtu na mama yake mzazi kwa kuwamwagia yale mafuta ya moto mtu wakiwa uchi wa mnyama. Kilikuwa ni kiifo kibaya na chenye maummivu makali sana nilichowahi kukishuhudia!” Babu Ogutu alisema huku akionesha kuumia sana moyoni mwake.

“Ni ngumu sana mtu kumwingilia mama yake mzazi, tena mbele za watu, nah ii ni ngumu kama ilivyo ngumu kwa Martin kuhusika kwenye misheni ya kwenda kumkamata kaka yake” Daniel aliwaza mwenyewe kimoyomoyo.

“Martin Hisia, upo tayari kushiriki misheni hii ingawa umesikia kuwa mtuhumiwa mkubwa ni kaka yako wa damu?” Daniel aliuliza huku akimwangalia Martin Hisia.
Martin Hisia alikaa kimya, alibaki akifikiria kwa dakika kama sita. Ukumbi wote ulikuwa kimya ukisubiri jibu la Martin Hisia. Baada ya dakika sita za kufikiria, dakika ya akasema kwa sauti ndogo,

“Nipo tayari…..”
Ukumbi mzima ulipiga makofi kwa uamuzi wa kijasiri uliofanywa na Martin Hisia.

“Sawa Martin Hisia. Wewe ni mwanaume, mzalendo kwa nchi yako na unajiamini sana. Sasa kesho asubuhi tunaenda kuvamia katika ile nyumba ya Mrombo, najua watakuwa wameweka ulinzi mkubwa sana kuanzia sasahivi baada ya kugundua kuwa tumewafatilia. Sasa, mimi nataka tuwashangaze, tunaenda kuwavamia asubuhi kabla hawajanywa hata chai, na tunamchukua Mrombo na kuja naye hapa! Lazima atujibu maswali yetu!” Daniel alisema huku akimwangalia kila mmoja kwa wakati wake. “…..sasa ni muda wa mapumziko, tutakutana tena jioni, katika chumba cha mazoezi kabla ya kuja kula chakula cha usiku” Daniel alisema na kunyanyuka kuelekea chumbani kwake, na kila mmoja alielekea chumbani kwake kasoro Hannan.
Daniel alifikaa chumbani kwake, alianza kuvua kofia yake aina ya kapelo nyeusi iliyoandikwa neno Levi’s kwa mbele, kisha akavua fulana yake nyeusi. Akabaki kifua wazi, akaanza kulegeza mkanda ili aweze kuvua na suruali yake.

“Hannan, unataka kuona nini wewe mtoto wa kike?” Daniel aliuliza akiwa amegeukia mbele, lakini cha ajabu alimhisi mtu aliyeingia kimyakimya nyuma yake.

“Hivi Daniel, ni binadamu wa kawaida kweli wewe?, Umejuaje kama kuna mtu nyuma yako?, nimeingia kimyakimya kama tulivyofundishwa katika chuo cha upolisi kule Moshi. Nakumbuka katika wanafunzi mia tano tuliokuwa kozi mimi niliibuka namba moja katika zoezi la kumnyatia mtu bila ya kutoa sauti, na leo nimefanya kama nifanyavyo siku zote, lakini nimeshindwa kuthibitisha kama mimi ni namba moja mbele yako Daniel” Hannan alisema huku akiushangaa uwezo wa ajabu wa Daniel Mwaseba.

“Hannan acha sifa zako bwana, siku zote umekuwa ukinipa sifa zisizostahili. Mimi ni binadamu wa kawaida kabisa, kama huamini njoo kitandani hapa nikuoneshe” Daniel alisema kwa utani huku akimgeukia Hannan.

“Umeanza ujinga wako Daniel, unaiweza kazi yenyewe? Sio unaniita kitandani ili ulielie hapo hahaha” Hannan alisema huku akicheka.

“Hahaha tuache hayo Hannan, eeh niambie umegundua kitu gani baada ya kuzifatilia simu za kina Babu Ogutu na Okello?” Daniel aliuliza huku akikaa kwenye sofa dogo lilikuwepo mle chumbani.
“Kama siku zote unavyokuwa sahihi, na leo umekuwa sahihi Daniel, shaka yako imekuwa kweli. Hadi sasahivi hakuna tatizo lolote nililoliona kwa Babu Ogutu, yeye ameonesha nia ya dhati ya kuhamia upande huu. Tatizo lipo kwa yule Okello…” Hannan alisema akimwangalia Daniel.

“Kuna tatizo gani uliloligundua kwa Okello?” Daniel alimuuliza Hannan.

“Unajua nimetumia teknolojia ya juu sana kuunganisha simu zao na simu yangu. Kila wanachofanya katika simu zao kinanaswa moja kwa moja na simu hii. Sasa nikutaarifu tu, Okello ndiye alimwaambia Mrombo kama tunawafatilia! Nilitaka nikutumie ujumbe wa simu baada ya kuusoma ujumbe wa Okello kwenda kwa Mrombo, lakini nikakumbuka kuwa ulizima simu yako baada ya kupewa vitisho na ile namba ya Witness Msombe, ila ulinishangaza tena ulipogundua kwamba wale jamaa wamegundua kwamba tulikuwa tunawafatilia na wanajipanga kwa shambulizi” Hannan alimwelezea Daniel Mwaseba.

“Nilijua tu, nililijua hilo na ndiomaana nikawahadaa hawa jamaa kwa kuwaweka upande wetu. Najua watatufikisha mahala sahihi katika uchunguzi wetu. Endelea kuwafatilia tutagundua mengi sana kutoka kwao, na nina uhakika uchunguzi wetu utakuwa mwepesi sana kupitia wao” Daniel alisema.

“Ulikuwa sahihi Daniel, halafu kitu kingine Daniel, unaamini Martin atafanya misheni hii kwa asilimia mia moja?, Kugundua kwake kuwa Mrombo ni kaka yake kutamtesa sana safari hii. Nadhani tumpumzishe kwenye hii misheni, tuifanye sisi wenyewe, kama itahitajika kuongeza mtu, tumlete Adrian…” Hannan alitoa ushauri wake.

Hannan anatoa ushauri wake kuhusu uhusika wa Martin katika misheni ya HATARI, je ingekuwa ndio Daniel Mwaseba ungejibu nini? Martin Hisia IN or OUT of the mission?
 
Halfani Sudy anaandika HATARI
Mawasiliano 0652212391
Mahali Gehto

“Ulikuwa sahihi Daniel, halafu kitu kingine Daniel, unaamini Martin atafanya misheni hii kwa asilimia mia moja?, Kugundua kwake kuwa Mrombo ni kaka yake kutamtesa sana safari hii. Nadhani tumpumzishe kwenye hii misheni, tuifanye sisi wenyewe, kama itahitajika kuongeza mtu, tumlete Adrian…” Hannan alitoa ushauri wake.

Hii ni sehemu ya Kumi

“Hannan usiwe na shaka juu ya Martin hata kdogo. Namwamini sana Martin Hisia. Amini anaweza kufanya kazi hii kwa ufanisi wake kwa asilimia miamoja. Kumtumia Martin ni faida sana kwetu, tunahitaji sana kuzitumia hisia za Martin katika uchunguzi wetu kuliko wakati wowote ule. Kumtoa Martin katika kazi hii itakuwa hasara kubwa sana kwetu. Acha tumtumie tu” Daniel alikataa katakata kumtoa Martin Hisia katika misheni.

“Daah sawa Daniel, upo sahihi Martin lakini hii itakuwa ni kazi ngumu sana kwa Martin Hisia. Kila nikijaribu kufikiria sioni hata kidogo kama ataweza kufanya kazi hii ufanisi kama wa siku zote. Yani kama ishu hii ingekutokea wewe nisingekuwana shaka hata kidogo, lakini sijui Martin Hisia ataubeba vipi msalaba huu” Hannan aliendelea kusisitiza alichoamini.

“Hannan, mimi ninamwamini sana Martin Hisia. Umesema kwamba ningekuwa mimi usingekuwa na wasiwasi hata kidogo, ungeniamini. Umesema hivyo kwakuwa unanifahamu mimi vizuri sana. Sasa, mimi ninamfahamu Martin Hisia, na ninafahamu kwamba Martin hawezi kutuangusha katika kazi hii, cha msingi ni kumwamini tu” Daniel Mwaseba alisema.

Wakati wakina Daniel Mwaseba wakijadiliana kuhusu uhusika wa ndugu wa Martin katika uchunguzi wao, Martin mwenyewe alikuwa amekaa kitanda chake. Aliingia katika chumba chake dakika kumi na tano zilizopita. Alivua tshirt yake ya rangi ya bluu na kuitupa zuliani, alijitupa kitandani na kulala chali. Alidumu akiwa amelala chali kwa dakika zipatazo kumi, kisha akainuka na kukaa katika ncha ya kitandani. Mawazo yalimsafirisha mbali sana. Aliikumbuka siku ambayo baba yake mzazi alifariki. Aliyakumbuka pia maneno pekee aliyofanikiwa kuyatamka baba yake Martin kwenda kwa watoto wake wawili wa kiume wakati akikata roho. Aliongea maneno maneno mengi miongoni mwa maneno hayo ni

“ Wanangu naomba mpendane…”.

Martin aliweka mikono yake yote miwili usoni akiwa amefumba macho. Aliona giza, na fikra zake zilisafiri tena hadi ile siku ambayo haiwezi kufutika katika ubongo wake. Maneno aliyoongea baba yake yalikuwa yanajirudia katika ubongo wake mithili ya sinema nzuri aipendayo.

“…wanangu, mimi ninaoondoka katika sura ya dunia. Sioni namna yoyote ile kwamba ninaweza kupona ugonjwa huu. Ugonjwa umenitafuna sana, ila ninaendelea kuwasihi mpendane. Msiachane sikuzote, msaidiane kwa namna yoyote ile. Kama mnavyoona, kwa sasa mtakuwa hamna baba wala mama hapa duniani. Kwa bahati mbaya sana tumewaacha mkiwa na umri mdogo sana, lakini naomba mpendane, mkipendana hamtaiona athari ya kutokuwa na wazazi”

“Nato!” Ghafla Martin alisema kwa nguvu akikutanisha viganja vyake na kupiga kofi kubwa, “Kwanini lakini umechagua upande huo. Nato, hivi ni kweli wewe ni jambazi?, Nato kuwa jambazi sio tatizo lakini una bahati mbaya sana, kusakwa na Daniel Mwaseba ni bahati mbaya kwako!” Nato aliipandisha mikono yake kichwani na kushika kichwa, aliendelea kufikiria “ Nisipo fanya kitu, Daniel anaenda kumkamata na kumuua Nato. Sipo tayari hata kidogo kumwona Nato anauwawa, lazima nimwokoe ndugu yangu katika kisanga hiki! Ndio, Nato ni damu yangu!” Martin alisema huku akipiga ngumu ndogo katika kiganja chake cha mkono wa kushoto baada ya kuitoa ghafla mikono yake kichwani. Safari hii ninaenda kuwa kinyume na Daniel Mwaseba, lazima nihakikishe Daniel hamkaribii Nato! Najua Daniel atakasirika sana kwa kitendo change. Najua ataniona msaliti. Najua ataapa viapo vyote vya dunia na kunisaka popote duniani ili aniuwe, lakini sitojari hilo, ninachojari ni ndugu yangu atakuwa hai! Nitafafanyaje sasa kumwokoa Nato? Lazima nionane na Nato leo usiku!”

Martin aliinuka pale kitandani, alienda pembeni ya chumba ambapo kulikuwa na friji ndogo, akalifungua, akatoa chupa ambayo iliandikwa K-vant, akaifungua na kuimimina tumboni mithili anakunywa maji ya kunywa, hakuitoa mdomoni hadi kinywaji kilichokuwa katika ile chupa kilipofika nusu.

“Siwezi kumchagua DanielMwaseba ukiniwekea pamoja na Nato. Usiku ninaufungua ukurasa mpya wa uadui wa mimi na Daniel Mwaseba! Itakuwa ni vita vya tatu vya dunia. Hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe, lakini nina uhakika ninaenda kumshinda Daniel Mwaseba. Martin alisema kwa sauti kubwa na kurejea kitandani akiwa kaishikilia ile chupa ya K-Vant.

Kisha akalala tena chali.

HATARI! HATARI! HATARI!
NINI HIKI?
LAKO JICHO!!

Like, Toa maoni kisha share kwa wingi iwafikie wengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom