Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Dah mkuu mbona kakipande kaduchu leo,, ila shukrani Sana pia
 
Halfani Sudy anaandika HATARI
Mawasiliano 0652 212391
Mahali Mafinga, Iringa

“Siwezi kumchagua Daniel Mwaseba ukiniwekea pamoja na Nato. Usiku ninaufungua ukurasa mpya wa uadui wa mimi na Daniel Mwaseba! Itakuwa ni vita vya tatu vya dunia. Hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe, lakini nina uhakika ninaenda kumshinda Daniel Mwaseba. Martin alisema kwa sauti kubwa na kurejea kitandani akiwa kaishikilia ile chupa ya K-Vant.
Kisha akalala tena chali.

Hii ni Sehemu ya Kumi na Moja

NI SAA SITA na dakika thelethini na nne usiku. Pikipiki aina ya boxer BM 125 ilikuwa inaegeshwa upande wa nyuma wa nyumba ya Mrombo. Dereva wa boxer aliangalia huku na kule kabla ya kushuka. Alikuwa amevaa nguo nyeusi tii, zilizofanya iwe ni ngumu sana kumtofautisha yeye na lile giza la saa sita na dakika thelathini na nne usiku. Usoni, alikuwa amejivika barakoa nyeusi ambayo ilifanya iwe ngumu sana kumtambua yeye ni nani?. Akajipekua upande wake wa kushoto wa kiuno, alitoa bastola ndogo nyeusi yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Alinyata gizani mithili ya paka mjamzito akielekea katika nyumba ya Mrombo. Alipofika karibu na ukuta alisita kidogo, kisha kwa umakini mkubwa aliangalia pande zote nne za dunia. Aliangalia mashariki, akageuka magharibi, kisha akamallizia kusini na kaskazini, akaona hakuna tatizo lolote litakalomzuia kufanya alichokusudia kufanya. Alianza kuuparamia ukuta kwa namna ya ajabu sana, ilikuwa kama ana gundi mwilini mwake ikiyomnasisha yeye na ukuta, akafika kileleni akiwa amelalia tumbo. Kwa ustadi mkubwa akajitupa ndani ya nyumba ya Mrombo bila kutoa ukelele hata kidogo, ilikuwa ni kama usufi mdogo ulidondokea mle ndani ya nyumba. Kwa bahati nzuri upande aliodondokea hakukuwa na taa za nzuri, hivyo giza lilikuwa upande wake kumsaidia kufanya alichokusudia kufanya.

Akiwa mle ndani ya nyumba, aliangalia tena pande zote nne za dunia, kisha akaangalia juu na chini. Bastola ikiwa imetangulia kifua chake, akapiga hatua ya kwanza kwa mguu wake wa kulia, mguu ulitua taratibu ardhini mithili anakanyaga sinia la mayai. Akapiga hatua ya pili kwa mguu wake wa kushoto, mguu wa kushoto nao ulifika ardhini salama. Macho yakiwa mbele, masikio yakiwa wazi kusikia lolote lile litakalomsaidia, huku ubongo wake ukiwa kazini. Akataka kupiga hatua ya tatu ili asonge mbele kwa kutumia tena mguu wake wa kulia. Hatua hii hakufanikiwa kupiga hatua. Hakufanikiwa!

Taratibu, alihisi akiguswa na kitu cha baridi shingoni mwake. Kwakuwa alikuwa mzoefu alijua kwamba ubaridi ule shingoni mwake ulikuwa ni ubaridi wa mdomo wa bastola. Sekunde tatu baada ya kuguswa na ule ubaridi, alisikia sauti nzito ikiunguruma nyuma yake.

“Tupa bastola yako chini, na kisha nyoosha mikono yako juu!” Sauti nzito ilisema kwa kujiamini.

Jamaa hakuwa na namna yoyote ile ya kufanya, taratibu aliinama na kuweka bastola yake chini. Aliamua kujipa nafasi ya kusubiri kwa maana hakujua adui aliye nyuma yake alikuwa amejipanga vipi na ana silaha aina gani?.

“Karibu sana Martin Hisia. Tulijua utakuja tu…” Sauti nzito ilisema nyuma yake kwa majigambo. Martin Hisia alistuka sana, hakujua kwa namna gani yule jamaa amejua kwamba ni yeye, pia hakujua kwa namna gani amelijua jina lake. Wote walikuwa katikati ya kiza kinene, huku Martin Hisia akiwa ameiziba sura yake kwa barakoa nyeusi.

“Martin, Umemfuata kaka yako eeeh, ” Sauti nzito ilisema kwa kejeri huku ikiusukuma mgongo wa Martin kwa mdomo wa bastola yake. Martin akaelewa anachopaswa kufanya, alianza kusonga mbele huku mikono yake ikiwa juu. Bado alikuwa anapiga mahesabu ya kumuonesha yule jamaa yeye ni nani? Lakini bado mahesabu yake yalikuwa hayajaleta majibu chanya. Jamaa hakufanya kosa lolote ambalo Martin Hisia angelitumia kama faida kwake. Moja kwa moja, walielekea katika nyumba kubwa iliyokuwa mbali kidogo na ule ukuta. Kila walivyokuwa wanakaribia ile nyumba, ndipo ubongo wa Martin ulianza kuelewa kwamba ulikuwa amefanya makosa. Hisia za Martin Hisia zilimwambia kwamba ameingia kwenye mtego, tena mtego hatari sana, lakini bado mawazo ya kwamba Mrombo alikuwa ni ndugu yake wa damu ilimpa imani kwamba alikuwa amefanya jambo sahihi.

Njiani, wakati wakielekea katika ile nyumba, walipishana na walinzi wengi sana wenye silaha huku wakiwa wamevaa sare nyeusi. Kwa hesabu zake za harakaharaka aliona walinzi zaidi ya hamsini wakiwa wanailinda ile nyumba kwa upande ule. Hisia kwamba hakuwa amefanya jambo sahihi kwenda peke yake katika lile jumba lile zikamjia. Akajua kwamba watu wale walikuwa wamejipanga sana kiulinzi kiasi kwamba asingeweza kumfikia Mrombo kwa namna aliyopanga. Wakiwa njiani, hamu ya kutaka kujua watu wale ni kina nani na wanafanya nini ilimjia, lakini hamu ya kukutana na ndugu yake Nato iliizima hamu hiyo.

Yule jamaa alimuongoza Martin hadi sebuleni katika hilo jumba. Martin alikaribishwa sofani. Pale sebuleni, waliwakuta wanawake watatu wakiwa wamekaa katika sofa moja la watu watatu. Wanawake wazuri sana wenye umri usiozidi miaka ishirini. Walikuwa wamekaa kihasarahasara sofani. Sehemu kubwa za miili yao zikiwa wazi, lakini hata hawakujishughulisha kuzificha. Aibu iliondoka usoni kwao, soni zilipotea katika nyuso zao.

“Karibu sana Martin Hisia,” Yule jamaa aliyemteka Martin Hisia alisema akiwa amesimama mbele ya Martin aliyekuwa amekaa sofani.

“Ninaitwa John Masalu, ni mlinzi mkuu hapa, na pia ni mlinzi mkuu wa Mfalme Mrombo. Wewe hauna haja ya kujitambulisha kwangu. Tulikuwa tunajua kwamba utakuja, pia tulikuwa tunajua kwamba utapitia upande ule ndio maana tukazima taa. Ninajua unaitwa Martin Hisia. Ninajua kuwa wewe ni mpelelezi wa kujitegemea ambaye unafanya kazi zako kwa kushirikiana na kijana mpumbavu anayeitwa Daniel Mwaseba. Sasa kama wewe ni mpelelezi wa kujitegemea naamini utajitegemea leo, badala ya kila siku kumtegemea yule kijana Mpumbavu. Dakika tano zijazo, atakuja Mfalme Mrombo mbele yako, utamsikiliza kwa umakini kila atakachokwambia, narudia tena, utamsikiliza kwa umakini kila atakachokwambia na utatekeleza maagizo yake yote bila kuuliza swali. Ujue kwamba, huruhusiwi kuuliza swali lolote lile mbele ya Mfalme Mrombo. Kwa maana, hapa kuna mgawanyo wa majukumu, jukumu letu kukupa maelekezo, jukumu lako ni kutekeleza maelekezo yetu. Kinyume na hapo ni sawa na kukisaka kifo chako mwenyewe kwa makusudi!” Mrombo alisema huku akimlingishia kwa madaha bastola usoni.

Hiyo ilikuwa ni saa sita na dakika arobaini na tano usiku.

Martin Hisia ametokaje nyumbani kwa Daniel Mwaseba? Je kina Daniel wamegundua hila za Martin Hisia? Daniel mwaseba atafanya nini akigundua hiki kitendo alichokifanya rafiki yake? Dakika tano zijazo, Martin na Mrombo wanaenda kukutana uso kwa uso, nini kitatokea?

LAKO JICHO!
 
Mbona kipande kinajirudia mkuu.
 
Halfani Sudy anaandika HATARI
Mawasiliano 0652 212391
Mahali Mafinga-Iringa

Hii ni Sehemu ya Kumi na Mbili

Martin Hisia alimsikiliza John Masalu, lakini moyoni mwake alipatwa na hamu kubwa sana ya kuonana na Mrombo, ambaye yeye alijua kuwa ni ndugu yake wa damu, Nato.

“Martin, kauli ya kwanza ya Mfalme Mrombo baada ya kuvuta funda la kwanza la sigara ni amri, nakushauri itekeleze! Usipoitekeleza litakalokutokea tusilaumiane!” John Masalu alisema maneno hayo kwa msisitizo.

Hapo ndipo Martin alikumbuka hadithi za Babu Ogutu kuhusu Mrombo walipoenda kuvamia gari la abiria, na hiyo ndio ilikuwa tabia ya ndugu yake Nato, hivyo alitamani huyo Mrombo aje haraka ili amwone ndugu yake.

Mara, mlango wa kuelekea vyumbani ulifunguliwa, wale madada watatu ambao walikuwa wakimwangalia tu Martin tangu alipoingia pale sebuleni walisimama wima na kuelekea mlangoni. Mara akatoka mtu wa kwanza, alikuwa ni mzee Maloto, kisha akafuata mtu wa pili, yeye alikuwa mtu mfupi na mwenye rangi nyeusi ya kukoza. Ilichukua dakika zipatazo kumi ndipo mtu watatu alipotokea pale mlangoni. wakatu wale watu waliotoka awali Mzee Maloto na mwenzie wakiwa wamesimama kila upande wa mlango, mzee Maloto upande wa kushoto na yule ntu mfupi mwenye rangi nyeusi ya kukoza alisimama upande wa kulia wa mlango. Na mtu watatu aliyetoka ndiye alikuwa Mrombo, Mrombo Hisia!
Wale wanawake watatu walifuata nyuma ya Mrombo, wakati Mrombo akielekea kukaa sofani taratibu. Alipokaa, mwanamke mmoja alisimama upande wake wa kushoto, huku kimahaba akilichua bega lake la kushoto na yule mwanamke mwengine alikaa upande wake wa kulia wa Mrombo, naye akilichua bega lake la kulia kwa madaha, na yule mwanamke wa wtatu alisimama alisimama nyuma ya Mrombo, akiichua shingo yake.

Wakati hayo yakifanyika, kulikuwa na mshangao mkubwa sana katika sura ya Martin Hisia. Macho yake yalikuwa yamemtoka pima, mdomo wake ulibaki wazi, huku mikono yake yote miwili ikimtetemeka. Alijua kwamba, mtu alikuwa mbele yake, ndiye mtu aliyekuja kumpa maelekezo lakini yeye hakuruhusiwa kumuuliza swali. Ndio, alikuwa Mrombo Hisia lakini kwa bahati mabaya sana hakuwa mtu aliyemfikiria, hakuwa ndugu yake wa damu, hakuwa Nato. Hata kama watu hubadilika, lakini Nato asingeweza kubadilika kwa namna ile na kuwa katika umbo la Mrombo. Swali kuu lililopita katika kichwa chake ni, huyu Mrombo ni nani? Na kwanini ana tabia kama za ndugu yake Nato? Hayo maswali yalipita kichwani kwake harakaharaka lakini kumbuka alikuwa haruhusiwi kuuliza maswali, kama alivyosema John Masalu hapo awali, jukumu lake lilikuwa ni kufuata maelekezo ya Mrombo na sio kumuuliza maswali Mrombo.

“Karibu sana Martin Hisia, mbele yako, unayemwangalia kwa macho yako ni Mfalme Mrombo, Mfalme Mrombo alikuwa na shida sana na wewe ama Daniel Mwaseba, kwa bahati nzuri sana umeanza kufika wewe kabla ya Daniel Mwaseba. Najua Daniel yupo njiani kuja hapa, na utaungana naye muda si mrefu. Kuna maelekezo machache tu ambayo Mfalme Mrombo atakupa, na jukumu lako ni moja tu, kuyatekeleza, kama nilivyokwambia awali hapa hakuna nafasi ya wewe kuuliza swali” John Masalu alisema taratibu akimwangalia Martin Hisia.

“Martin….” Sauti nzito ya Mfalme Mrombo ilisema, kisha akaingiza mkono wake wa kulia kwenye mfuko wa shati, akatoa pakiti la sigara, akaligonga kwa juu na kutoa sigara moja iliyochomoza kwa juu. Alipoitoa na kuiiweka mdomoni tu, John Masalu alikuwa ameshafika na kuwasha kiberiti cha gesi, Mrombo akapiga funda la kwanza la sigara na kusema

“Washa runinga,”

John Masalu alikimbia mbio kuwahi kuiwasha runinga, runinga ikawaka, video fupi ikaanza kuonekana. Ilikuwa ni video iliyochukua dakika moja tu, ikamalizika, narudia tena, video ilichukua dakika moja tu, ikaisha, lakini ilimuuumiza sana Martin Hisia kuliko wakati wowote ule katika maisha yake.

“Nato,” Martin alishindwa kuvumilia na kujikuta akiita baada ya dakika moja ya ile video kuisha. Mashavu yake yalikuwa yameloa machozi. Mwili wote ulikuwa unamtetema kwa hasira. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yanapiga kwa kasi kubwa sana haijawahi kutokea hapa duniani.

“Umemwona ndugu yako Nato? Nato yupo katika mateso makali sana. Yupo katika chumba cha mateso ambacho si rahisi kwa mtu wa kawaida kujua kilipo. Uhai wa ndugu yako upo mdomoni mwangu. Mimi ni Mungu wake kwasasa, nikishika simu yangu na kupiga chumba cha mateso, nikasema tu Nato afe, basi anakufa sekunde hiyohiyo. Sasa mimi sitaki uhai wa Nato uwe mdomoni mwangu, nataka uhai wa Nato uwe mikononi mwako. Nitakupa kazi, ukiitelekeza kazi hiyo, Nato aanaenda kuwa huru. Nato anatoka katika chumba cha mateso na kurudi duniani…..”

“Kwanini mmetesa ndugu yangu kiasi kile?, ni watu gani ninyi msio na huruma hata kidogo? amewafanya nini ndugu yangu?” Martin alisema huku akibubujikwa na machozi.

“Martin, wewe ni mwanaume, sijawahi kufikiria kama unaweza kumwaga chozi namna hiyo kama mtoto wa kike. Wewe ni kijana jasiri sana. Hupaswi kulia hata kidogo, kama nilivyokwambia awali, uhai wa Nato upo mikononi mwako, una nafasi ya kuchagua, Nato aishi ama afe?” Mrombo alisema kwa sauti yake ya taratibu huku akimwangalia Daniel Mwaseba.

“Una kazi ndogo tu Martin, kazi ndogo sana. Najua kwamba, wewe na Daniel Mwaseba mna nafasi ya kwenda ikulu kwa Rais Mark Mwazilindi wakati wowote ule mtakapohitaji, pia mna uwezo wa kuonana na Rais Mark Mwazilindi hata chumbani kwake. Sasa huko chumbani kwa Rais Mark Mwazilindi ndipo tunapokutaka sisi. Tutakupa kamera ya siri uende ukaiweke kwa siri chumbani kwa Rais Mark Mwazilindi. Endapo tukianza kuona picha za chumba cha Rais Mark Mwazilindi hapa sebuleni kwetu, basi ndugu yako Nato atakuwa huru” Mrombo alimwangalia kwa umakini Martin kuhakikisha kama maneno yake yamemwingia Martin.

Mrombo anampa kazi ngumu sana Martin ya kwenda kuweka kamera ya siri katika chumba cha Rais Mark Mwazilindi. Je Martin atakubali kwenda kuweka? Kwanini Mrombo anataka kamera ya siri ikawekwe katika chumba cha Rais?

LAKO JICHO!
 
Naona hii ngoma imekata…..

Au mshatumiwa mesej pm za kuchangia ndo utumiwe story….
 
Hiki kigongo hakika ni hatari, nimesoma misheni nyingi za Daniel Mwaseba na mafanikio yake lakini hii mwanzo mwa kazi tu inaonesha atakutana na upinzani mkali sana.
 
Martin Hisia ameingia choo Cha kike, na amepoteza uaminifu Kwa kundi lake hata akijirudi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom