Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,891
- Thread starter
- #21
Kitabu Tsh 10,000/=
Softcopy Tsh 3,000/=
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
Mzigo upo wa kutosha.
>>>>>>>>>>>>>>> Episode 05 <<<<<<<<<<<<<<<
>>>>>>>>>>>>>>> Episode 06 <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
>>>>>>> Episode 07 <<<<<<<<<<<<
>>>>>>> Episode 08 <<<<<<<<<<<<
>>>> Episode 09 <<<<<<<<<<
>>>>>>>>>> Episode 10 <<<<<<<<<<<<<<<
>>>>>>>>>> Episode 11 <<<<<<<<<<<<<<<<<
MLIO WA RISASI HARUSINI (Episode 11)
Mtunzi: Robert Heriel
WhatsApp 0693322300
ILIPOISHIA
Sajenti Warioba alifoka akimtingisha tingisha Omary ambaye muda huo alikuwa yupo uchi wa mbuzi mee.
"Umeniona mimi mchafu si ndio?"
Hapa Sajenti aliongea akimning'iniza Omary juu kwa kumkaba shingoni. Omary alipiga ukelele kwa maumivu aliyokuwa anayapata.
"Samahani braa..zaa! Mimi napenda sana mchezo huu. Nimeathirika kisaikolojia. Nisamehe! Utaniua kaka"
Omary aliongea huku sauti yake ikitoka kwa tabu kutokana na kukabwa na Sajenti Warioba.
ENDELEA
*************************************************Tayari ilikuwa imefika saa tatu na nusu asubuhi. Njaa ilipamba moto katika matumbo yao. "Braza ngoja mimi nikakuletee chakula. Tukikaa humu tutakufa njaa. Tutafika bandari ya Durban, afrika kusini baada ya siku saba na nusu"
Omary aliongea huku akipiga piga miayo ya njaa. Sajenti hakuwa na ubishi wowote licha ya kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa huenda Omary anaweza akaenda alafu akarudi na wale watu wabaya. Hilo lilimfanya akose amani. Lakini angefanya nini. Achague njaa au afe na wasiwasi wake. Omary akamuacha Sajenti mule ndani akaenda kuleta chakula. Sajenti alibaki mule ndani akitafakari mwenendo wa uchunguzi wake. Mpaka muda ule aliona yupo nje kabisa ya malengo ya uchunguzi wake. Yeye alikuwa anafanya uchunguzi wa uhalifu uliotokea siku ya harusi ya Adele na Robert. Alitakiwa arudishe majibu ya ni akina nani waliovuruga harusi ile. Ni kina nani waliomuua Ramla aliyekuwa mshenga wa Adele. Sasa yote hayo ameyaacha anachunguza mambo ambayo hakuyapanga wala hakutumwa. Hii ilitosha kumuambia kwamba ameshafeli. Ikapita nusu saa hivi. Hii ikampa kidogo mashaka. Mbona Omary harudi. Nini kimetokea huko alipoenda. Au kakamatwa. Au wanapanga namna ya kunikamata, machale yakaanza kumcheza. Akaamka akaenda kufungua ule mlango wa bati wenye kutu waliojia na aliotokea Omary kwenda kuleta chakula. Akajaribu kuufungua lakini ulikuwa umefungwa kwa nje. Ubaridi wa woga ulimpitia kwenye mishipa yake ya damu. Akajua tayari kakamatika kirahisi kama kuku wa kisasa. Akaenda kwenye ule mlango mwingine mfupi. Nao ulikuwa umefungwa na kufuli lakini kwa ndani. Punde akasikia mlango wa bati ukiguswa na mtu anayetaka kuufungua. Hakujua ni nani. Akaenda mpaka mlangoni akaweka sikio kwenye mlango kusikiliza mienendo ya upande wa pili. Aligundua kuwa aliyekuwa akiufungua ule mlango alikuwa yupo pekee yake.
"Omary!" Sajenti akaita kwa sauti ya chini kama mtu anayenong'ona.
“Braza ni Mimi" Omary aliitikia huku akiwa anaufungua mlango. Omary Aliingia akiwa kabeba mfuko wa karatasi. Wakarudishia mlango wakarudi kwenye godoro kukaa. Omary alimkabidhi Sajenti Warioba ule mfuko wa karatasi wa kaki ambao ndani yake kulikuwa na nyama choma na ndizi zilizokaangwa pamoja na chupa moja ya vodka.
"Mimi nimeshakula huko. Kula tuu braza" Omary aliongea akiwa ameanza mchezo wake mbaya wa kulegeza macho na kujilamba lamba. Mchezo huo ulikuwa unamkera sana Sajenti. Alitamani amwambie aache lakini alikumba msemo usemao mtumikie kafiri upate mradi.
"basi kula walau nyama" Sajenti aliongea akimbembeleza Omary ambaye muda huo alikuwa amelala kwa mapozi ya kike.
"Wewe kaka embu kuwa muelewa basi. Nimekuambia nimekula"
Omary aliongea kwa sauti ya kike kabisa. Huku akibetua betua midomo yake. Kitendo cha Omary kukataa kula chakula kilimfanya Sajenti aingiwe na wasiwasi. Alihisi huenda kile chakula kimewekewa madawa ya kulevya ambayo akila atasinzia. hivyo itawarahisisha kazi ya kumkamata. Akakumbuka zile kete mbili za heroine alizozikuta kule kwenye kile chumba cha mbrazili.
"Kama huli hata kipande kimoja cha nyama nami sitakula chakula chako" Sajenti akasema huku akikifunga kile chakula kwenye ule mfuko wa kaki. Alifanya hivyo kumjaribu Omary ingawaje alikuwa na njaa na alikitamani sana. Omary kuona Sajenti amesusa kula. Ilibidi aamke akaenda kuchukua kipande kimoja cha nyama na ndizi.
"Haya mume nawe amka ule. Najua huwezi kula wakati mkeo sili. Haya amka sasa" Omary alisema akiwa ameilegeza sauti yake. Sajenti alikasirika sana. Maneno ya Omary yalimkera kupita kiasi."Wewe ni fala nini. Usiniletee upuuzi hapa" Sajenti aligomba kwa sauti hali iliyomfanya Omary amuonyeshee ishara kuwa anapiga kelele.
"Shiiii! Acha kupiga kelele sasa. Mdomo uliponza kichwa shauri yako. Unadhani upo kwako humu" Sajenti alinyamaza hasira zikitingisha mashavu na midomo yake. Alitamani ampige hata makofi mawili lakini akakumbuka alipokuwa jeshini alivyofundishwa na mwalimu wake kuwa mwanajeshi mzuri ni yule anayeweza kuzuia mihemko yake. Akameza fumba la mate kisha akaanza kula. Ilikuwa ni nyama ya mbuzi iliyorostiwa kwa ufundi wa hali ya juu. Sajenti alikula haraka haraka mate yakimtoka mdomoni kwa utamu. Kwa kweli alifurahia mlo ule. Alimaliza kula wakawa wanapiga stori mbili tatu na Omary. Omary alianza kusimulia sababu iliyomfanya mpaka akajiingiza kwenye ushoga.
"Stori ndefu sana braza. Yaani sitaki hata kukumbuka" Omary alisema akiwa ametulia. Muda huu alionyesha uhalisia zaidi. Huzuni na simanzi ziliufunika uso wake. Machozi yalianza kumlengalenga. Nani ambaye asingeelewa kile ambacho anataka kuhadithia kuwa ni hadithi ya kusikitisha. Hadithi iliyojawa na visa vyenye simanzi na vilio. Sajenti Warioba kwa utulivu na ushawishi akazungumza.
"Omary! Kila hadithi inamsomaji. Kila ngoma inawachezaji. Tafadhali naomba unisimulie kwa ufupi" Omari alimtazama Sajenti Warioba kwa uso wa uchovu wa huzuni. Kisha akayakunja macho yake kama mtu anayekumbuka mbali.
"Nilimaliza shule ya msingi kwa msisi handeni. Nilikuwa naishi na bibi yangu mzaa Mama. Mama yangu alikuwa akiishi Dar es salaam maeneo ya mtoni mtongani ya temeke. Hakuwa akiishi na baba yangu kwani baba alikataa mimba yangu. Hivyo Mama akaamua kunilea yeye kama yeye" Omary aliweka kituo kwa kumeza fumba la mate. Alihadithia kwa utulivu sana. Sauti yake haikuwa ile yakishoga kama awali. Hata yale macho ya kurembua sasa yalikuwa hayarembui. Zaidi ya kuzingirwa na machozi. Omary akaendelea kusimulia.
"Mimba aliipatia huko huko Dar es salaam. Kama unavyojua mimba inahitaji uangalizi na malezi. Na Mama hakuwa na kazi ya maana zaidi ya uMama ntilie. Pesa zote alizopata ziliishia kwenye kodi. Hivyo mimba ilivyokuwa maisha ya Dar yakamshinda. Akaamua kurudi kwa bibi mpaka akajifungua mtoto wa kiume. Akamuita Omary matatizo" Uso wa Omary ulibadilika. Mdomo wake ulianza kutetemeka. Machozi yalitiririka kama mifereji katika mashavu yake. Alianza kulia.
"Sijawahi kumuona baba yangu tokea kuzaliwa. Sijui yupo wapi. Mama aliamua kumuita baba yangu matatizo. Matatizo! Matatizo! Ati matatizo ndio baba yangu. Omary matatizo. Hiiiiihiii" Omary alizidisha kulia kama yupo msibani. Hali iliyomfanya Sajenti ambembeleze. "Jikaze Omary. Wewe ni mwanaume. Usilie Omary"
" Ati mimi ni mwanaume. Omary mwanaume. Nilitoka handeni kama mwanaume nikiwa Darasa la saba. Nilikuwa na miaka kumi na mbili. Nikafika Dar es salaam alipokuwa akiishi Mama na mume wake mpya ambaye ni baba wa kambo" Omary aliweka kituo kisha akavuta makamasi mepesi yaliyokuwa yananing'inia puani. Alijipangusa machozi machoni kisha akaendelea.
"Mama alikuwa muuza bar moja pale mjini. Alikuwa akiondoka saa tisa jioni na kurudi saa tano za usiku. Hapo alikuwa amepika chakula cha usiku. Baba yangu wa kambo akirudi tulikuwa tunakula naye. Baba alikuwa ni konda wa daladala zilizokuwa zinatoka Mbagala rangitatu kwenda makumbusho" Alimeza fumba la mate kisha akamtazama Sajenti Warioba aliyeonekana kunogewa na stori hiyo ya kusisimua.
"Eehe ikawaje sasa?" Sajenti aliuliza.
"Maisha ya pale mtongani nilianza kuyazoea. Pale nyumbani nilipaona kama nyumbani. Japokuwa sikupendezwa na tabia ya Mama kurudi akiwa amelewa lakini sikuwa na lakufanya. Mama alikuwa akilewa sana. Kila mara akirudi nyumbani alikuwa akimtukana baba" machozi yalianza kutiririka tena katika uso wa Omary. Na kila alipokuwa akifanya hivi Sajenti alijua kuna jambo baya anaenda kulisimulia. Hii ilimfanya azidishe utulivu.
" Mama alikuwa akimfukuza baba chumbani ati akalale sebuleni. Siku moja baba alikuja chumbani kwangu akagonga mlango. Nilimfungulia. Akanambia amekuja kulala na mimi. Nilijua tuu kafukuzwa na Mama. Alafu pale sebuleni kuna mbu. Hivyo alichoka kung'atwa na mbu" akameza fumba la mate na kuvuta makamasi puani. Kisha akaanza kulia kwa sauti ya kutetema. "Huruma zangu zikaniponza braza. Huruma! Huruma ni mbaya jamani!
Akapanda kitandani tukalala wote. Mara usiku nikiwa nimelala nikasikia mtu akinikumbatia mwili wangu. Nilitaka kujinasua lakini sauti nzito ikaniambia nisihofu. Ni baba. Nikabaki nimetulia tuu. Alinishika sehemu zangu za siri. Kisha akaniingilia. Nilisikia maumivu makali sana. Sitakaa nisahau siku ile".
Kufikia hapa Omary alilia mfululizo akiwa anatingishwa kichwa chake kama mtu anayekataa kuamini historia yake. Sajenti Warioba alibaki amemtizama Omary kwa huruma. Alimuona ni kijana mdogo asiyestahili madhila yote yale.
"Baba wa kambo akanipa elfu ishirini na kuniambia nisiseme. Niliiona ni pesa nyingi. Tokea hapo ikawa ndio tabia yangu kuingiliwa na baba. Wewe ulisema mimi ni mwanaume lakini mume wa Mama yangu alinigeuza mwanamke wake kwa miaka mitatu" Omary aliendelea kulia ikafikia hawezi kusimulia tena. Sajenti Warioba alimkumbatia akawa anambembeleza mpaka usingizi ulipompitia Omary.
Sajenti aliitafakari historia mbaya ya Omary aliyohadithiwa. Ilikuwa ni historia ya kikatili sana. Alitamani amjue huyo baba yake Omary wa kambo. Ili amfungulie mashtaka. Ona sasa kijana wa watu anapata tabu. Ona sasa amegeuzwa mwanamke huku katika meli za maharamia watu wenye roho za kuua. Sajenti aliwaza mambo yote hayo. Sajenti alipitiwa na usingizi bila kujua wote wakawa wamelala. Wakwanza kuamka alikuwa ni Omary. Omary aliamka na moja kwa moja alitoka kwenye kile chumba. Punde alirejea akiwa na mwanamke na mwanaume mmoja wa kireno. Omary alishangaa kutokumkuta Sajenti Warioba kwenye kile chumba.
"Nilimuacha amelala hapa" Omary aliongea akimtazama yule mwanamke.
" Wewe usituchezee akili. Yupo wapi huyo mtu" yule mwanamke alisema kwa hasira huku akimtazama.
"Alikuwa hapa kweli. Alikaa hapa akiwa anakula kile chakula mlichonipa" Omary akasema akiwa anaangaza macho yake huku na huko. Ni kweli Omary alimuacha Sajenti pale akiwa amelala. Sasa kaenda wapi. Hilo ndilo lililomchanganya. Omary alijua kuwa yule mwanamke siyo mtu wa mchezo. Kitendo cha kutokumkuta Sajenti Warioba pale chumbani kinaweza kuhatarisha uhai wake.
"Wee mbwa naona umeanza kunizoea. Sasa leo utambua mimi ni nani" yule mwanamke alionsema kwa sauti ya kibabe yenye dalili zote za shari.
"Ommy huenda yupo sahihi. Si unaona ule mlango umefunguliwa" yule mreno akasema kwa kiswahili kibovu kama kanjibai. Wote walitazama kwenye ule mlango mfupi wa futi nne. Walishangaa kutokuona kufuli pale. Waliusogelea ule mlango mfupi ambao haukua na kufuli. Waliamini aliyeiondoa kufuli ile ni Sajenti. Kama paka anavyonyata kunyemelea panya ndivyo walivyokuwa wakinyata kuusogelea ule mlango. Waliufikia. Yule mreno akaushika ili kuufungua. Aliushika akamtazama yule mwanamke aliyekuja naye. Yule mwanamke akamtingishia kichwa kama ishara ya kumruhusu aufungue ule mlango. Wakati huo yule mwanamke alijiweka tayari kufanya shambulio kwa hatari itakayo jitokeza. Waliufungua ghafla yule mreno alipigwa usoni hali iliyomfanya yule mwanamke apige risasi hovyo. Looh! Kumbe ilikuwa ni kipepeo kikubwa cheusi ndicho kilichompiga usoni.
"Hoiii!" yule mreno alishusha pumzi nzito akiwa kaanguka chini kwa hofu. Wote walikitukana kipepeo cha watu kilichokuwa kinaendelea kuruka ruka mule ndani. Wakaingia upande wa pili ambapo kulikuwa na mabomba na vipuri vikuukuu vya meli. Walidhani kuwa ndipo alipokuwa amekimbilia Sajenti. Hata hivyo walikuwa sahihi. Sajenti hakuwa na njia nyingine ya kutokea zaidi ya ule mlango mfupi wa futi nne. Kulikuwa na giza sana. Kilichowasaidia ni tochi ya simu aliyokuwa ameishika yule mwanamke. Walimulika kila sehemu lakini hawakuweza kumuona Sajenti. Mule ndani kulikuwa na tando nyingi za buibui. Hii iliwafanya kila mara kupangusa nyuso zao pindi ziliposhikwa na utando wa buibui. Wakatembea mule ndani kumsaka Sajenti lakini hapakuwa na dalili ya mtu . Omary yeye alikuwa amebeba taa yake ya chemli. Alihisi huenda Sajenti Warioba ni mzimu kama siyo jini. Inawezekanaje amuache akiwa amelala kwa dakika zisizozidi mbili alafu arudi amkose. Haya hata kama kakimbia basi amekimbilia wapi maana kama ni msako wameufanya mpaka wamechoka. Ile meli wanaijua ndani nje. Wanajua njia zote za kutorokea na kujifichia. Iweje mgeni awatoroke kienyeji kiasi kile.
Moja kwa moja Omary alijua kuwa ataonekana ni muongo. Na uongo ni kosa kubwa katika kundi la Ambagon. Kosa ambalo hukumu yake ni kifo. Omary akajuta. Aliona ni bora asingeenda kumshtaki Sajenti kwa wale watu wabaya. Punde walisikia kwa mbele kitu kikichakura chakura. Hima walinyoshea bastola zao upande ule waliosikia sauti hiyo. Yule mwanamke akamulika tochi kuelekea upande waliosikia sauti. Aliishia kusonya baada ya kumuona panya akiwa anakula fupa la nyama. Kwa hasira alimpiga panya yule risasi aliyekuwa akisheherekea msosi wake. Walishusha pumzi kupunguza hofu iliyosababishwa na panya ambaye walidhani ni Sajenti. Baada ya kutafuta kwa muda mrefu kama lisaa limoja na nusu. Wakachoka.
"Leo utatutambua. Huwezi kutudanganya kama watoto wadogo" yule mwanamke aliongea kwa ukali kama mtu aliyeaibishwa.
"Dadaangu! Nilikuwa naye. Kwa nini nidanganye..."
" Wee koma! Mimi siyo dadaako. Mbwa wewe leo utanijua mimi ni nani" Yule mwanamke alimkatiza Omary akamkunja tai shingoni na kumsogelea usoni. Nyuso zao zikiwa zimekaribiana zero distance.
"Nisamehe dadaangu"
"Nimekuambia mimi siyo dadaako. Kaa kimya nguruwe wee!"
alimkemea na kumchapa kofi kali la shavuni. Waliondoka kule chini wakafunga kile kimlango kwa nje ili kama kweli Sajenti aliingia mule ndani asiweze kutoka. Muda wote huo Sajenti Warioba alikuwa amejificha ndani ya bomba moja kubwa ambalo alilifungua kwa kulisogeza. Maneno yote waliyoyaongea aliyasikia. Alimlaumu sana Omary kwa kitendo cha kumsaliti. Sajenti alikuwa tayari kumsaidia Omary kutoka mule ndani ya meli. Alipanga kuwa kama angefanikiwa kumtorosha kutoka mule melini angeenda kumsomesha ili naye awe na maisha yake. Lakini kumbe Omary alikuwa ni mtu mbaya asiyefaa hata kwa mkopo. Sajenti aliona hata ile hadithi aliyosimuliwa na Omary huenda ilikuwa ni danganya toto. Hakuiamini tena. Zaidi ya yote alishukuru kwa kuwa salama mpaka muda ule. Akatoka kwenye lile bomba akiwa hoi kwa kujikunja mule bombani. Akajinyoosha kuviweka sawa viungo vyake huku akivuta pumzi kufidia pumzi aliyoikosa alipokuwa ndani ya lile bomba. Kutokana na kukaa muda mrefu kwenye bomba macho yake yalikuwa yameshazoea giza. Aliona kiasi cha kumfanya atembee bila kujikwaa. Alikaa kule chini siku mbili mfululizo bila kula. Njaa ilimuuma sana. Akafanya mbinu zote alizozijua na alizofunzwa ili atoke kule chini lakini ilishindikana. Alikiona kifo kwa mbali kikimkonyeza kwa dhihaka. Alibaki anakitazama tuu asijue afanye nini wala akiambie nini. Akatembea tembea kule chini kuona kama atapata upenyo wowote wa kutoka lakini hakuona dalili yoyote ya kuwepo kwa upenyo. Punde akafika sehemu ambayo alisikia harufu kali ya kitu kilichooza. Itakuwa ni harufu ya nini hii. Sajenti alijiuliza huku akiifuata harufu inapotokea. "fuuuh! Mmmh!" alishika pua yake. Aliona mzoga wa panya ukiwa unafunza. Ni yule panya aliyeuawa kwa risasi na yule mwanamke mwenye roho mbaya. Sajenti Warioba awali aliwahi kusikia kuwa hakuna kifo kibaya kama kifo cha moto. Pia aliwahi kusikia kuwa hakuna kifo cha kikatili kama kifo cha maji. Kama kuna vifo alivyowahi kuviona ni vya kikatili basi ni kifo cha kuchinjwa na kisu au panga. Lakini leo mawazo yake yalibadilika. Alibadilisha mtazamo kuhusu kifo kibaya na cha kikatili kama siyo mateso. Leo hii kama angeulizwa ataje kifo kibaya basi angesema bila hata kufikiri kuwa kifo cha njaa ndio kifo cha kikatili chenye maumivu makali yasiyosemeka. Usicheze na njaa. Hata wahenga walikwisha sema kuwa adui yako mwombee njaa. Njaa ni habari nyingine kabisa. Sajenti nguvu zilimuisha kabisa. Aliona akitembea anapepesuka. Aliishika bastola yake. Akaitazama.
" Leo nataka uniue rafiki yangu. Umenisaidia sana rafiki yangu. Leo nami nataka uniue" Sajenti aliiambia bastola yake iliyokuwa ikimtazama bila kujibu chochote. Akaibusu kama ishara ya mapendo. Sajenti alikuwa katika hatua ya mwisho ya kufanya maamuzi ya kujiua. Aliona ni bora ajiue kuliko mateso aliyokuwa anayapata. Aliona ni heri mateso ya risasi yatakayodumu kwa sekunde chache kuliko mateso ya njaa yanayomtesa kwa muda wote ule.
Akaingiza kidole kwenye kilimi cha bastola yake. Kijasho chepesi cha njaa na hofu kikamtoka. Alipumua kwa nguvu. Hofu ya kifo ilimshika. Akaanza kuhesabu. Moja, mbili... Kabla hajafika tatu alishtuka kusikia kitu kinatembea tembea upande wake wakulia. Akageuka upesi kutazama. Huuh! Kumbe alikuwa panya. Alimpiga yule panya risasi ambayo ilimchakaza kichwani. Akamchukua yule panya. Mate yalimtoka mdomoni ungedhani aliona nyama choma. Lakini haikuwa nyama choma bali panya buku jike aliyenona. Alijua kabisa kuwa panya haliwi lakini atafanya nini ikiwa hakukuwa na kitu kingine cha yeye kula. Alianzia iliposhingo yake iliyokuwa inavuja damu. Hakika alijisikia kinyaa lakini kinyaa hakikuzidi njaa yake. Alimaliza kula panya wote kasoro mkia wake. Hahaha! Alijicheka kwa kula panya. Sajenti alipata nguvu mpya. Akahisi ahueni kidogo. Sasa hakutaka azidiwe tena na njaa mpaka ashindwe kufikiri vizuri namna ya kutoroka. Aliwahi kuambiwa na mwalimu wake jeshini kuwa njaa humfanya mtu asifikiri vizuri. Pia njaa humfanya mtu akubali jambo lolote lile bila kujali kuwa jambo hilo ni zuri au baya. Ndio maana adui ukimkamata unamnyima kwanza chakula. Hapo lazima utapata unachokihitaji. Alienda kwenye ule mlango mfupi ambao ulifungwa kwa upande wa pili. Alijaribu tena kuufungua lakini haukufunguka. Alipata wazo kuwa aitumie bastola yake kufungua mlango ule. Wazo hili aliliona ni jema na linafaa kabisa. Aliichukua bastola yake akaiweka usawa wa ilipokufuli iliyopo upande wa pili. Akafyatua risasi paa! Akapiga ingine paa! Akasikia kufuli likidondoka chini upande wa pili. Hapo akajua kazi imekwisha. Alifungua mlango. Akakuta lile godoro likiwa vilevile alivyoliacha. Akaondoka kwenda kwenye mlango wa bati wenye kutu. Nao ulikuwa umefungwa kwa nje. Aliichukua bastola yake akapiga sehemu aliyohisi inakomeo lililofunga mlango ule. Nao ukafunguka.
*************************************************
Siku saba zilipita meli ikatia nanga katiba bandari ya Durban iliyopo afrika ya kusini. Safari ya kueleke brazil ilianza. Kutoka bandari ya Durban mpaka bandari ya santos nchini brazil ni siku zaidi ya ishirini ukiwa baharini. Umbali kutoka Durban mpaka bandari ya santos ni
4838 nautical miles. Nautical mile ni kipimo kinachotumika kupima umbali katika safari za angani na majini. Sajenti Warioba bado aliendelea kuishi kwa ujanja ujanja mule ndani kama mjusi wa ukutani. Alikuwa akiiba makombo ya wale mabaharia pindi walipokuwa wanayatupa kwenye vyombo vya takataka. Siku kumi na tano zilimfanya aizoee ile meli. Tayari alikuwa naye ni miongoni mwa mabaharia katika meli ile. Ingawaje yeye alikuwa baharia wakujificha.
Siku ya ishirini na tisa meli ya Ambagon ilitia nanga katika kisiwa cha ilhal montao de trigo ambacho kipo karibu kabisa na bandari kubwa ya santos iliyopo Brazil. Walifika usiku wa saa sita. Kulikuwa na giza anga lote likiwa limetawaliwa na nyota. Sajenti alianza kufanya harakati za kutoroka. Alipanda mpaka vyumba vya juu bila ya kuonekana. Akafika kwenye korido moja ndefu kiasi ambapo kulikuwa na milango miwili upande na upande. Akaufuata mlango mmoja akachungulia. Alishangaa kuona Hall kubwa lenye watu wa rangi tofauti tofauti wakifanya starehe. Lilikuwa ni kasino la ile meli. Moyoni alijisemea kumbe hii meli inawatu wengi kiasi hiki. Wale watu katika lile kasino walikaa kwa mzunguko kufuatana na mpangilio wa viti na meza. Juu ya meza zao kulikuwa na vinywaji mbalimbali vya gharama. Vinywaji vingi vilikuwa ni pombe kali. Sajenti aliendelea kuchungulia akichunguza mule ndani. Lakini ghafla alihisi kitu kigumu kikigusa kichogo chake. Bila kupoteza muda Sajenti Warioba akageuka na pigo moja takatifu la kiwiko cha mkono kilichompata yule mtu aliyemuwekea bastola kwa nyuma. Yule mtu aligugumia bastola ikiwa imeanguka sakafuni. Sajenti aligeuka. Hamadi! Alikutana na jitu kubwa kama licheza mieleka. Bila shaka lilikuwa mlinzi wa lile kasino. Lilikuwa jitu kubwa la miraba minne. Jeusi tii lililonyoa kipara kichwani. Kifuani lilikuwa na maziwa liliyokuwa likiyachezesha chezesha kibabe kumtisha Sajenti Warioba. Sajenti hakuwahi kuona mtu wa namna ile tokea kuzaliwa. Watu wa namna hii aliwahi kuwaona tuu kwenye video hasa mchezo wa mieleka.
Sajenti akalisogelea lile jitu ambalo aliliita Umaga. Wakawa wanazunguka zunguka kila mmoja akimtafutia mwenzake nafasi ya kumshambulia. Umaga akarusha ngumi. ikapita pembeni ya sikio la Sajenti. Upepo aliousikia Sajenti uliingia sikio hili ukatokea sikio la pili. Ilikuwa ngumi ambayo kama ingempata Sajenti basi ingemsababishia madhara ikiwezekana kifo. Sajenti alijua kuwa ili alipige lile jitu alihitajika atumie mbinu ya kupigana akiwa mbali kidogo. Kwa kuhofia kukamatwa na jitu lile jeusi ambalo uso wake ulihifadhi ukatili wa kila namna. Sajenti akarusha ngumi ikalipiga kwenye tumbo. Lile jitu likacheka. Likamuamuru apige zaidi na zaidi. Sajenti akaona sasa hii dharau. Akaifunga ngumi yake kisha akaitupa tena kwa nguvu zake zote. Lakini ilitua kama mzaha katika tumbo la lile jitu na kudunda kama kitenesi. Lile jitu lilicheka kwa dharau. Likajitutumua likikaza kifua chake. Sajenti aliingiwa na woga. Akarudi nyuma polepole lile jitu likimfuata huku likinguruma kama simba. Likarusha ngumi nzito Sajenti akaikwepa. Likarusha ngumi ya pili Sajenti akainama ikapita kama panga boya lkikata upepo. Sajenti akamrukia na kumpiga kichwa cha kidevu. Lile jitu uso wake ukainuka juu huku jino moja likiruka juu. Lilikuwa pigo takatifu ambalo kama angepigwa mtu mwenye afya mgogoro angekufa papohapo lakini lile jitu lilipandisha maruhani. Likamfata Sajenti Warioba kama mbogo aliyejeruhiwa huku mdomoni likivuja damu. Sajenti alirudi nyumanyuma mpaka akafikia ukutani. Lilirusha ngumi ikapiga bega la Sajenti, akagugumia kwa maumivu makali. Ni bega lile lile aliloshambuliwa na risasi kipindi kile akiwa kwenye hospitali ya Ambagon.
Lile jitu likampiga teke la tumbo Sajenti akadondoka chini karibu na ile bastola ya lile jitu. Kwa kweli Sajenti hakuwa tayari kupokea pigo jingine. Aliichukua ile bastola na kumpiga risasi ya kichwa lile dubwana likamuangukia kwa juu. Dooh! Lilikuwa zito kama gunia la kahawa. Akalisukuma kwa pembeni kisha akaliburuza mpaka mafichoni. Alilipekua katika mifuko ya suruali yake akakuta kadi iliyowekwa nembo ya Ambagon ambayo ni herufi A. Akarudi kwenye ule mlango akaufungua kisha akatoma ndani ya kasino. Hakuna aliyekuwa na habari na mtu. Kila mtu alikuwa yupo bize kujipa raha za dunia. Kwa mbele aliona jukwaa kubwa ambapo aliwaona malaya wakiwa uchi wa mnyama wakicheza kwa madoido na ushankupe. Aliwaona wazungu, waafrika na waarabu. Karibu mataifa yote aliwaona wawakilishi wao kwenye lile jukwaa. Alitembea akijifanya mwenyeji ili asije akashtukiwa. Alipigana vikumbo na wanawake malaya waliokuwa wamesimama kwa kukosa wanaume wa kukaa nao. Kila meza alikuwa amekaa mwanaume na mwanamke. Wanaume wengine walikuwa wanavuta sigara wakiwa vifua wazi. Wengine walikuwa wamevaa suti kali za gharama. Wengi wao umri wao ulikuwa kati ya miaka thelasini na nane mpaka sabini.
Sajenti alikaa meza moja iliyokuwa na mzee mmoja mwenye asili ya kihindi aliyevaa miwani nyeusi na kofia kama la cowboy wa kimexico. Hakumsalimia akakaa tuu na kujifanya yupo bize kuangalia lilipojukwaa walipokuwa wanacheza wale Malaya wakifuata mdundo wa muziki uliokuwa ukipiga. Sekunde haikuisha alikuja mwanamke mweupe mwenye asili ya kibrazil.
"suas notícias bom irmão" mwanamke aliyekuja alimsalimia Sajenti. Sajenti aligeuka kumtazama na kumjibu.
"ola'" Sajenti alijibu kwa kifupi. Akimaanisha sijambo. Kwani alisalimiwa 'habari yako kaka'. "Wewe ni mswahili. Mbona unaongea kama Mtanzania" yule mwanamke aliongea kiswahili kibovu sana. Sajenti alishangaa kusikia yule mwanamke akiongea kiswahili. Kwa haraka akajibu.
"Hapana mimi ni mkenya. "
"Ahaa! Ulipandia mombasa?"
"Ndio! Nawe ulipandia wapi?" Sajenti alijibu haraka alafu naye akamtupia swali.
" Mimi mwenyeji wa mji wa Juquei. Ilipofukwe nzuri za Juquei. Huwa nakuja kwenye hii meli kwa kazi hii" yule mwanamke alisema akitingisha tingisha nywele zake ndefu zisiingie machoni. Akapeleka glass mdomoni aliyokuwa ameishika mkononi.
"Ahaa! Sawasawa!" Sajenti aliitikia akihitaji maelezo ya ziada.
"Nipo hapa kwa ajili ya kuwapa wanaume raha. Wafikapo katika kisiwa hiki cha montao de trigo kila mrembo humu hujichukulia mteja wake" yule mwanamke alisema.. Sajenti aligundua kuwa yule mwanamke alikuwa anaitwa Fernanda da silva kutokana na kitambulisho kilichokuwa kinaning'inia shingoni mwake.
"Utanilipa bei gani. Ninasehemu nzuri ya kulala tukitoka humu" Fernanda akasema akiyashika mabega ya Sajenti Warioba akiwa kamzunguka mgongoni. Hapa Sajenti akili yake ikamuambia kuwa hii ndio ilikuwa nafasi yake ya mwisho kutoka mule ndani. Aligundua kuwa kumbe ile meli licha ya kuwa inasafirisha miili na viungo vya watu lakini pia kulikuwa na matajiri waliokuwa wakizunguka dunia nzima wakiponda raha na wanawake malaya huku wakinywa na kula. Bila shaka wengi wa wasafiri mule ndani ya ile meli hawakujua kuwa meli ile pia ilikuwa inasafirisha bidhaa za magendo. Kama wangelijua huenda hata wasingethubu kuingia humo.
Muda wa kutoka melini ukawadia. Ilikuwa ni asubuhi tulivu kabisa katika kisiwa cha montao de trigo. Sajenti na Fernanda walikuwa kwenye msururu mrefu wa watu wanaotoka nje ya meli. Walipofika mlango wa kutokea walitakiwa wakabidhi vile vitambulisho. Fernanda alitoa kitambulisho chake wakati Sajenti Warioba akihaha kwa wasiwasi. Sajenti naye alitoa kile kitambulisho cha lile jitu alilopigana nalo kule ndani. Yule mkaguzi alikikagua kile kitambulisho kwa muda kidogo tofauti na alivyofanya kwa Fernanda. Moyo wa Sajenti alipwita pwita kama ringi la gari. Aliomba kimoyo moyo wasije wakamshtukia. Yule mkaguzi alimtazama usoni Sajenti Warioba kama ataona tashwishi yoyote lakini Sajenti alitabasamu kirafiki kumuondoa hofu. Yule mkaguzi naye alitabasamu na kumruhusu. Sajenti alishusha pumzi akiwa haamini. Chezea Ambagon wewe. Moto wa Ambagon siyo wa kitoto. Wakatoka; Fernanda akiwa amemshika kiuno chake. Punde alimuona yule mwanamke aliyemuona akifanya mapenzi kule katika meli, aliyetoka kupokea simu wakati Sajenti akiwa kajificha upande wa pili wa mlango. Ndio huyohuyo mwanamke aliyekuja na mwanaume wakireno aliyekuwa akimfokea Omary. Sajenti akamtazama kwa jicho la kuiba iba. Punde yule mwanamke aligeukia kule alipokuwepo Sajenti Warioba. Wakagongana macho lakini Sajenti akayaondoa macho yake na kumtazama Fernanda. Yule mwanamke aliingiwa wasiwasi kwa kitendo cha kumuona Sajenti Warioba. Hata hivyo alimpuuzia. Walitembea mpaka zilipo teksi za uber. Wakapanda na moja kwa moja wakaelekea upande wa pili wa ufukwe. Hapo Fernanda akamuambia Sajenti Warioba kuwa watapanda boat ya kuelekea ilipo beach ya Juquei ambapo ndio nyumbani kwake, Fernanda. Wakapakia boat na ndani ya nusu saa walikuwa wamefika fukwe ya Juquei.
Fukwe ya Juquei ilikuwa na mchanga mzuri mweupe. Maji yake yalikuwa meupe ambayo ukiyatazama unaweza kuona samaki anayepita chini kabisa. Pia ni fukwe ambayo ilikuwa na milima yenye kijani cha kupendeza. Ilikuwa ni saa mbili asubuhi lakini watu walikuwa wengi. Hasa watalii waliokuja kufanya utalii. Sajenti alivutiwa na mandhari ya fukwe ile. Walitembea kwa miguu mwendo wa dakika kumi wakiiacha fukwe ya Juquei wakikatiza mitaa na kona ya mji mdogo wa Juquei. Punde walisimama mbele ya geti jeusi ambapo Fernanda alienda kulifungua kisha wakaingia ndani. Sajenti alistaajabu mandhari ya mule ndani. Akaona bustani zenye maua ya kupendeza ya kila rangi. Aliona pia swimming pool la kuogelea ambapo pembeni yake kulikuwa na viti na vitanda maalumu vya kulalia. Mbele yake alitazamana na jumba kubwa la kifahari lenye madirisha ya aluminium na vioo vya gharama. Juu ya jumba lile kulikuwa na vigae vya rangi ya damu ya mzee ambavyo ndio vilikuwa paa la jumba lile. Fernanda alimkaribisha ndani Sajenti Warioba ambaye macho yake yalikuwa yakistaajabu kila alichokuwa anakiona.
"Hapa ni wapi Fernanda?" swali lilimponyoka Sajenti huku wakiwa wameshaingia sebuleni.
"Hapa ni kwangu mume wangu” Fernanda alijibu akijitahidi kuongea kiswahili kilichonyooka.
Mpaka muda huo Fernanda hakujua Sajenti alikuwa anaitwa nani. Wala Sajenti hakumuuliza Fernanda jina lake. Kama unakumbuka Sajenti alijua jina la huyu mwanamke wa kibrazil baada ya kusoma kitambulisho alichokuwa amekivaa kule kwenye kasino wakiwa melini.
Ni kawaida kwa malaya kutokuuliza majina ya wateja wao. Unajua kwa nini. Labda na wewe unaweza kujua ni kwasababu gani. Ila sababu kubwa ni kuwa watauliza majina ya wateja wangapi, kwa maana wao hulala na watu wengi. Hicho ndicho kinawafanya wasiulize majina ya wateja wao labda wawe wateja wa kudumu. Sajenti Warioba alipitisha macho yake kukagua sebule ya nyumba ile. Aliona picha kubwa ikiwa ukutani ikimuonyesha Fernanda akiwa amevaa gauni jeupe la harusi. Pembeni yake kulikuwa na picha nyingine ndogo ikimuonyesha Fernanda akiwa na Mama wa makamo ambaye moja kwa moja Sajenti alijua atakuwa ni Mama yake na Fernanda kutokana na kufanana.
Fernanda alikuwa kaingia ndani akiwa kamuacha Sajenti pale sebuleni. Sajenti aligundua sebule ile ilikuwa na kamera za siri za cctv zilizotegwa kwenye feni iliyokuwa juu ikizunguka upande huu na upande huu waliyoikuta ikiwa hivyohivyo inazunguka. Kamera nyingine ilikuwa imetegwa kwenye kinyago cha dragon kilichokuwa juu kabisa ya kabati la vyombo lililokuwa kwenye sebule ya kulia chakula. Ni elimu na mbinu za kijeshi ndizo zilizomsaidia Sajenti Warioba kujua kuwa mule ndani kulikuwa na kamera. Mtu wa kawaida wala asingeweza kujua jambo hili.
Hofu na mashaka vilibisha hodi katika moyo wake. Iweje Fernanda aweke kamera humu ndani. Fernanda ni nani hasa. Je ni kazi hiihii ya umalaya ndio mpaka nyumba hii ifungwe kamera. Au kuna kazi ingine anayoifanya Fernanda. Hata hivyo Sajenti hakutaka kumuamini sana Fernanda. Atawezaje kumuamini ikiwa walikutana kwenye meli hatari ya Ambagon. Sajenti aliamini kuwa mtu yeyote aliyekuwa kwenye ile meli hakupaswa kuaminiwa. Aliwaona watu wote mule ndani ni watu hatari na wauaji. Punde Fernanda alitoka chumbani akiwa kavaa taulo la kuogea. Alitembea kwa madaha kama mlimbwende anayetumbuiza jukwaani. Alilegeza macho yake ya kijivu na kuzirusha rusha nywele zake mbele na nyuma kumchanganya zaidi Sajenti. Sajenti alipagawa akajisemea kuwa leo amekamatika. Leo napewa mapenzi ya kimataifa. Yeye si alizoea mapenzi ya kibongo bongo leo kakutana na Fernanda malaya aliyebobea katika tasnia ya ukahaba. Fernanda akatembea kimanjonjo mpaka ilipo home thietre kubwa ya muziki. Kisha akawasha muziki wa kibrazili. Kisha akabenjuka na kumtazama Sajenti na macho ya uchu. Fernanda ndio kaanza hivyo. Sijui kama Sajenti atasalimika na mahaba ya kibrazil.
Akapeleka kidole mdomoni akaking'ata kisha akafumba macho yake kwa madaha na kuyafumbua polepole yakiwa yanarembua. Muda wote alikuwa akifanya hivi huku akimtazama Sajenti aliyekuwa kasimama kama sanamu la michelin. Muziki ulianza kuchanganya. Fernanda alihakikisha mapigo ya muziki hayamuachi. Alikata mauno muziki ulipohitaji akate mauno. Alitingisha matako muziki ulivyomuamrisha kufanya hivyo. Akainama chini na kuanza kutambaa kama mtoto kumfuata Sajenti ambaye muda huo alikuwa hajielewi. Kisha akasimama upesi akiwa amemkaribia Sajenti kama hatua moja. Wakiwa wanatazamana huku muziki ukiimba kama filamu ya kihindi. Fernanda akashika lile taulo lake akalirusha juu likanata kwenye feni. Feni ikawa inazunguka na lile taulo. Fernanda akabaki uchi kama alivyozaliwa huku cheni ya dhahabu ikiwa kiunoni na pete ikiwa kitovuni. Kitendo cha Fernanda kulirusha taulo juu ya feni Sajenti alikielewa. Alijua kuwa Fernanda kafanya vile makusudi kuziba kamera ili isiwachukue video wala kuwapiga picha. Sajenti akanyanyua uso wake juu kulitazama lile taulo. Alishangaa kuliona likiwa limeiziba kwa ufasaha ile kamera. Moyoni alimuona Fernanda kama mwanamke mwenye shabaha sana. Mtu mwingine asingeweza kurusha vile tena bila ya kuangalia juu.
Muda huo Fernanda hakujua kuwa Sajenti kaelewa mchezo mzima. Fernanda akamshika Sajenti shingoni na kumnyonya mdomo wake. Walinyonyana ndimi kwa dakika tano mfululizo huku Fernanda akimchojoa Sajenti nguo zake. Dakika kumi wote walikuwa wapo uchi wakipumua kama bata dume. Walifanya mapenzi palepale sebuleni kila mmoja akionyesha utundu wake. Hii ilikuwa kama finali ya kombe la dunia la mapenzi. Timu ya brazil ikiwakilishwa na Fernanda na timu ya Tanzania ikiwakilishwa na Sajenti. Mechi ilikuwa ni kali kila mmoja akijaribu kushambulia. Mpaka dakika ya tisini walikuwa wamefungana mbili mbili. Mechi ilienda matuta ambapo kwa mara ya kwanza kombe la dunia likaenda Tanzania. Walienda kuoga wakarudi kitandani kupumzika. Fernanda hakuamini kwamba kuna mwanaume anaweza kufanya mapenzi kwa kiwango kile mpaka aridhike. Amefanya mapenzi na wanaume wengi lakini wote hakuna aliyewahi kumfikisha katika pepo ya mahaba. Leo hii kwa mara ya kwanza alionja pepo pasipokifo akiwa na Sajenti Warioba.
"Wewe hata usiponilipa. Kiukweli umenifurahisha. Tutapumzika alafu jioni tutafanya tena" Fernanda alisema akiwa kalala kifuani mwa Sajenti akisikiliza mapigo ya moyo wa Sajenti yakikimbia.
ITAENDELEA
Jipatie simulizi yote ya MLIO WA RISASI HARUSINI Softcopy kwa Tsh 3,000/= Kitabu Tsh 10,000/=
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
ILIPOISHIA>>>>>>>>>>>>> Episode 12 <<<<<<<<<<<<
Safi sana Mkuu…Kazi nzuri
Mkuu hii kitu inazidi kuwa tamu shukran sana
Achia mkwaju mkuu nipo kwa watu huku burudani zako zinanifanya kuwa happy na kuona nipo home landMkuu shukrani sana
`kaa mkao wa kula, kuna simulizi mpya nimepost, inaitwa kaburi la mwanamuzikiAchia mkwaju mkuu nipo kwa watu huku burudani zako zinanifanya kuwa happy na kuona nipo home land
Achia mkwaju mkuu nipo kwa watu huku burudani zako zinanifanya kuwa happy na kuona nipo home land