Riwaya ya Kijasusi Mabaduni wa serikali

Samahani kwa kukawia, lakini mzigo utashuka ndani ya wiki hii. Nina changamoto kidogo ya afya but hope nitakuwa sawa soon, Tutamalizia sehemu ya mwisho.
 
Ndio maana watu huwa wanapita kimya kimya. Tukishaanza kuwakubali tuu mnaanza kuugua mara kuwa busy
 
Mkuu mbona ulete muendelezo Hadi wiki imeisha

Sent from my A004SH using JamiiForums mobile app
Mkuu Joseph ma, kwa style hii tutaipua ugali mbichi Subiri niivishe cross dongo la kwenda ili likishuka mezani liwe linafuka tu moshi.
By the way niko jikoni ndani ya hii wiki yote. Ugonjwa uliingilia kati lakini kwa sasa niko njema, naburuza button kwa kwenda mbele, dropping soon.
 
Kijana wangu Sonko Bibo ,unataka mpaka nije mwenyewe ndio utasikia vijana wanachokuambia? Waelezee legacy yangu kama nilivyokupa copywights za kuiandika hapa😁
Hahahahaaaaa!!!
Huyo mwamba ndie kakukosha sana eti?
Hadi ukaamua kusepa na jina lake, Inapendeza sana, hongera pia.
 
Hahahahaaaaa!!!
Huyo mwamba ndie kakukosha sana eti?
Hadi ukaamua kusepa na jina lake, Inapendeza sana, hongera pia.
Ahahahah.kabisaa. ukiona kuna vijana machachari idarani bas ujue kuna mpishi matata anayewaandaa na kuwa groom, sasa mimi ndio godfather wa hao wote kina Seif na mabaduni wenzake. 😁
 
Ahahahah.kabisaa. ukiona kuna vijana machachari idarani bas ujue kuna mpishi matata anayewaandaa na kuwa groom, sasa mimi ndio godfather wa hao wote kina Seif na mabaduni wenzake. 😁
Shida ni kwamba umetengeneza mashetani mkuu, hawafai hawa viumbe.
 
Serikal zote za kiafrika zinahitaji watu kama hawa mambo yaende viongoz wanasiasa wawe na adabu
Hapana haya yanatokea Songomo tu. Lakini hata huko kwenye nchi zenu wananchi wakipata elimu bora mambo yatabadilika kwa kasi hadi mtashangaa, Tatizo kubwa la huko kwenu ni mitaala ya Elimu.
Jifunzeni kwa Songomo pengine mtayakabili yanayowasibu.
 
Wakuu poleni kwa kuwaweka sana bila muendelezo but jumatano tunamaliza hii Riwaya then tunaanza mzigo mpya.
Ninyi ndio wa kutoa maoni ni mzigo gani mngependa ufuate kati ya hii miwili.

1: Siri ya Meza Huu ni mzigo wa kijasusi, umesheheni mambo mengi sana yatakayowaanda vyema majasusi wapya kuukabili na kuuhimili ulimwengu wa kijasusi.
Humo tutaiangazia pia mbinu ya Avadra kwa undani zaidi kwa wale watamanio kuujua ulimwengu wa giza kwa kiasi chake.

2: Agano Jeusi Huu ni mzigo unaohusu mafungamano ya ulimwengu wa mali na ulimwengu wa ufukara, humu kuna watu tutachukiana hususani wale tunaofahamiana maana hawatapenda kuyasoma yale yanayowalenga wao ila hatuna namna.
Karibuni sana idadi ya kura kutoka kwenu ndio itaamua mzigo gani tuanze nao.
Sonko Bibo.
 
Final Episode Loading...................
MABADUNI WA SERIKALI 6.



Jiga Kinamba alikuwa kwenye gari yake akiiendesha taratibu katika viunga vya Homabay, huku wimbo mmoja maridadi ulioimbwa na msanii mmoja mahiri kutoka huko Afrika Mashariki ukiwa unatumbuiza. Hakika ni wimbo ulioonekana kuzisisimua sana hisia zake maana alikuwa akiusikiliza kwa umakini mkubwa huku tabasamu Fulani likiwa linajitengeneza usoni mwake.

Africa Liberte’(Le Bucheron) kazi ya Franklin Boukaka, akishirikiana vyema na Manu Dibango. Kutoka nchini Congo ni wimbo uliokuwa ukisikika vyema kwa sauti ya chini kidogo.

Kuonesha ni jinsi gani wimbo huu ulivyomshika alikuwa akiyafuatisha vyema mashairi ya wimbo huu.

Ndani ya huu wimbo Mwanamuziki huyu anasikika akiuzungumzia utawala wa nchi za Afrika akiushutumu kuwa ni utawala usiojali watu zaidi ya viongozi tu

Maana anasikika akisema “Nimewapa ujasiri watu ambao mawazo na hatma yao viko juu ya starehe na maisha ya kifahari, lakini ikikaribia kwenye uchaguzi wananikumbusha kuwa mimi ni mtu muhimu kwao. Na pia Mkoloni ameondoka ndani ya Afrika sasa nini kinafuata juu ya uhuru wako Afrika?”

Hiyo ni sehemu tu ya tafsiri juu ya wimbo huo wa Le bucheron.

Malone yeye akiwa ametulia kwenye siti ya nyuma alikuwa akimuangalia Jiga Kinamba ni kama alikuwa akisubiri huu wimbo ufike tamati ndio aongee jambo.

Basi baada ya wimbo huo kutamatika,Malone alimwambia Jiga Kinamba kuwa, “Hivi unajijua kuwa wewe ni hazina ya kipekee sana ndani ya Taifa hili na ulimwengu kwa ujumla?”

“Malone, are you kidding? Yaani ukitumwa hazina za taifa utanipeleka mimi kweli? Mi nadhani kuna watu wengi sana ambao wanastahili sifa hiyo ndani ya taifa hili kuliko mimi”
Alisema Jiga Kinamba.

“Miongoni mwao pia umo, na hata ndani ya taasisi yetu hii una nafasi ya muhimu sana ni vile tu hujui.” Alimalizia Malone.

“Wote tuna umuhimu na tunategemeana maana mimi siwezi kuongoza taasisi kama ilivyo kwako na Fanton Mahal wala kuendesha ndege ama gari kama afanyavyo Macka Shinea, nadhani unaweza kuona nafasi zenu zilivyo za msingi sana pengine kuliko mimi nilivyo” Alimalizia Jiga Kinamba.

“Ok tuachane na hayo, ujue kipindi kile mkuu wa hii taasisi alipotuma maombi kwako hakuna aliedhani kama utakubali kuungana na sisi, hivyo kitendo cha wewe kukubali kuungana nasi kilileta furaha kubwa sana kwetu maana hatukutaka kabisa uwe upande wa adui hiyo ingeleta shida katika kazi zetu” Alisema Malone.

“Na ni nini kilipelekea ninyi kuhisi kuwa mimi naweza kuwa katika upande wa adui?” Aliuliza Jiga Kinamba.

“Ni hisia tu maana mara nyingi watu wenye uwezo mkubwa huwindwa na watu wengi wakiwemo matajiri wenye malengo binafsi au watawala wenye nia ovu juu ya taifa.

Ujue hakuna mtawala yeyote hapa ulimwenguni anaependa kutawala taifa ambalo wananchi wake wanajiweza sana kiuchumi au kimaarifa ukiona imetokea hivyo basi ni vile tu wanakuwa hawana uwezo wa kuvuruga hayo maarifa au uchumi.”
Alitananbaisha Malone.

“Kwahiyo unamaanisha kuwa hata huu mfumo wanalenga kuvuruga uchumi wa vijana ili watengeneze taifa la masikini wengi ambao watakuwa wanaitikia kila wimbo unaoimbwa na watawala?” Aliuliza Jiga Kinamba.

“Na sio kuitikia tu bali na kucheza huku unatabasamu hata kama huo wimbo haukuburudishi. Yaani mfano ni pale mtu anapokuwa anakununulia pombe baa, akikuamuru uinuke ucheze wimbo wowote unakuwa huna namna tofauti na kufanya vile anavyotaka mdhamini wako.” Alihitimisha Malone.

Yalikuwa ni mazungumzo ya hapa na pale baina ya hawa watu wawili kisha yalikoma na gari ikaongezwa mwendo ikaenda kasi ya ajabu mpaka kwenye bandari ya Homa bay.

Katika Jengo moja lililokuwa likitumika kama stoo ya kuhifadhia mizigo ambayo wateja wake hawakuwa wamefika ama kuitolea taarifa ndimo kulihifadhiwa vifaa na zana mbali mbali kwaajili ya kazi zao maana mitambo iliyokuwa imewekwa humu ilitisha na ukweli ni kwamba hawa watu walikuwa wamejipanga sana ukizingatia mitambo mizito na ya kisasa ambayo ilikuwa imefungwa humu unaambiwa kuwa walikuwa na uwezo wa kuichunguza nchi nzima mpaka Ikulu kwa muda mfupi kupitia mitambo hii waliyokuwa wameifunga hapa ndani watu hawa wana uweredi mkubwa sana katika utendaji kazi wao na walikuwa wamedhamiria kuendeleza mizizi yao ya utawala ndani ya Songomo Kifupi wamewekeza sana katika kuhakikisha hawaikosi keki ya Taifa haijalishi ni nani ambae yuko madarakani kwa wakati husika.

Uwekezaji huu ulikuwa ni mzito sana kiasi kuwa ilikuwa ni vigumu kwa raia ama wanasiasa wa kawaida kuweza kuipinga nguvu hii. Watu walioshiba kiuchumi wanaoweza kununua hata jeshi na dola nzima kwaajili ya maslahi yao mapana.

Akili ya mwanadamu imejaa ubinafsi sana hasa linapokuja suala la mali, inahitaji kiwango kikubwa sana cha hekima na utu kuweza kuitawala tamaa hii juu ya mali.

Harakati hizi zilikuwa ni muendelezo wa kutengeneza taifa la wasakatonge hohe hahe wasiojiweza mifumo iliyolenga kumfanya mtoto wa maskini kubaki kuwa masikini kifupi uliruhusiwa kushika pesa ila sio kuimiliki.

Wananchi walihimizwa sana na kubembelezwa kupitia riba kiduchu ilimradi tu waweke pesa zao benki, maana benki ni moja ya mifumo inayozisaidia Serikali nyingi za Ulimwengu kuutawala uchumi wa wananchi ilihali watawala wao pesa zao wakizificha kwenye mahandaki katika mfumo wa vipande vya dhahabu ili kuficha taarifa kamili juu ya uchumi wao.

Baada ya ukaguzi huu wa siri uliochukua takribani lisaa lizima wanaume walitoka na kuzunguka maeneo haya wakitazama kama wanatafuta kitu lakini uhalisia haukuwa hivyo walikuwa wakiangalia upande wa majini kuona kama wangeona chochote

Ni kweli kwa umbali mkubwa sana waliweza kuona kama kimnara kikiwa kinachungulia kutoka usawa wa maji kuja juu kidogo ndipo wakaingia kwenye gari na kushuka huku gari hii wakiiacha kwenye yadi moja ya kulazia magari hapo.

Kisha wote wawili wakiwa wamevaa mashati makubwa na suruali pana ambazo hazijanyooshwa walitembea kuingia katika viunga vya bandari hiyo ungewaona ungedhani ni wasakatonge wa hapo bandarini vichwani kila mmoja aliweka wigi la nywele za kipilipili walifika sehemu ya kukodi boti wakamkodi jamaa mmoja ambae alidai alipwe kwanza ndipo awashe boti maana kwa kuwatazama tu ni wazi alipata mashaka ya kutokulipwa pindi hawa watu wakifika.

Hawakuonekana kujimudu kifedha.

Basi walilipa fedha kila mmoja kivyake kisha safari ikaanza hapa majini kulikuwa na boti nyingi zilizokuwa zikifanya safari za hapa na pale kubeba mizigo baadhi midogo hapa bandarini na kusambaza kwenda visiwa vya karibu hivyo boti zilikuwa nyingi huku wengine wakionekana na mashua wakijaribu kuvua samaki na mazao mengine ya bahari.

Safari iliendelea mpaka walipoukaribia ule mnara na wakaona kuwa ni jahazi moja kubwa na la kisasa kabisa lilikuwa limetia nanga karibu kabisa na kisiwa kimoja hapo.

Jiga Kinamba alimuamuru nahodha alisogelee lile jahazi lakini nahodha alisema walikuwa wamekatazwa kulisogelea hilo jahazi na maaskari wa majini.

Malone akamwambia “Wewe twende mpaka pale usihofu wakija tutajitetea,”

Nahodha akasema kuwa hawezi kwenda maana watamponza hii inaweza kupelekea kibali chake cha kufanya biashara kusitishwa.

Jiga Kinamba alimwambia asiwe na mashaka kama ni faini watalipa. Lakini, nahodha akiziangalia hizi sura haoni muunganiko wa haya wanayoyaongea na muonekano wao hivyo akawa anakataa.

Kitendo cha yeye kuendeleza mkazo kilipelekea ahisi kitu cha baridi shingoni mwake na baada ya kugeuka aliona ni bastola, akatulia huku akitetemeka, akiomba wasimuue maana ana watoto wadogo mapacha wanamtegemea hivyo wasimpore boti yake ndiyo nyenzo kuu kwake ya kuingizia kipato.

Wakamwambia aendeshe kuelekea ile boti lakini awamu hii bastola ilirudishwa kibindoni ili kumuweka sawa kiakili asiwe na wenge lililopitiliza.

Basi wakazidi kulisogelea lile jahazi lakini kitendo hiki kilifuatiwa na kitendo kingine cha boti moja ya wanausalama iliyokuwa inakuja kwa kasi sana kama vile inataka kuwagonga ubavuni kulia. Ilipowafikia iliwapisha kidogo tu na kuwazunguka kwa mbele huku maaskari wale wakitoa mitutu ya bunduki wakiwa wanafoka sana.

“ Ina maana ninyi ndio mnakaidi amri ya Serikali eti, hamjasikia kuwa hairuhusiwi kulikaribia lile jahazi? mnataka kufa sio? Hamjipendi?”

Watu hawa ambao walikuwa wamevaa sare za jeshi la wanamaji walikuwa wameweka sura za mbuzi haswa, wakionekana kuchukizwa na kitendo hiki vibaya mno.

Kwa namna hawa maaskari walivyokuwa wakitisha nahodha alijikuta akitetemeka kwa woga akawa anawatazama wateja wake kama anaetarajia waseme neno na roho yake ipone.

Lakini wateja wake walikuwa kimya tu hawaongei neno lolote licha ya hawa maaskari kuwa wanafoka na kuamrisha nahodha aendeshe boti uelekeo mwingine lakini wateja wake ndio kwanza hawakuwa wakisema chochote.

Baada ya kuona Nahodha anababaika sana Malone aliwaambia wale maaskari kwa kuwasihi sana kuwa hawana lengo la kwenda kwenye lile Jahazi bali wameona wakatishie pale ili iwe njia fupi kufika pale kisiwani.

“Kisiwa gani?” Akauliza askari mmoja alieonekana kuwa kiongozi wa kikosi hiki cha doria ya majini.

“Kile pale.” Alinyoosha kidole Malone akionyeshea kisiwa kile kilicho nyuma ya ile boti.

“Hata kule hamtakiwi kwenda mpaka pale Serikali itakapotoa tamko.” Alisema askari

“Lakini afande kule kuna mizigo yetu tunaifuata.” Aliongea Malone.

“Nimesema hivi hairuhusiwi mtu yeyote kwenda kule kama kuna mtu mwenye mzigo basi anatumia ule upande wa pili wa kisiwa kufuata mizigo na hairurhusiwi kuja upande wa huku wa ufukwe ndani ya kilomita mbili, Ni utaratibu, naomba hilo lizingatiwe.” Alikazia askari yule.

“Kwani afande ukituruhusu tukapita mara moja tu kitaharibika nini?” Aliuliza Jiga Kinamba.

“Naona mna vichwa vizito kiasi hamuwezi kuelewa maana ya amri, nahodha geuza boti twende kule maana ninyi inabidi tufundishane heshima kwanza.” Aliamrisha askari.

Nahodha kusikia hivyo alianza kuomba msamaha akiomba wamwachie tu maana yeye alishawaambia wateja wake lakini wao ndio wakasisitiza afanye hivyo.

Wakati wanazungumza haya tayari hizi boti zilikuwa zishagusana na zimesimama hivyo baadhi ya maaskari akiwemo mkuu wao walikuwa wamo kwenye hii boti waliyomo akina Malone.

“Hawa wateja wako ndio wanaendesha chombo chako au ni wewe?” Aliuliza askari mwingine.

“Ni mimi” Alijibu Nahodha. Alishitukia kofi zito limetua usoni.

Askari mmoja alianzisha kipigo kwa nahodha akataka kumpiga la pili lakini mkono wake ukadakwa na Malone.

“Afande habari za kuanza kupigana zinatoka wapi tena? Ni mambo tu ya kuongea na kuelewana sisi ndio tunaotaka kwenda kule sio huyu.” Aliongea Malone.

Namna ule mkono wa askari yule ulivyodakwa iliamsha hisia kwa kiongozi na baadhi ya maskari hao. Mkono ule ulidakwa kinyambilisi. Maana hakushikwa mkono ilimradi tu kashikwa bali alishikwa kwenye maungio ya mkono na kiganja huku akiminywa kwa nguvu sana kwenye kinundu cha maungio hayo na kupelekea askari huyo kuhisi maumivu makali. Akafoka kwa kelele za maumivu, “Niachie mkono wangu, mnataka kupigana na sisi au?” Hakujibiwa, wanaume waliendelea kukaa kimya tu.

Kiongozi wa hawa maaskari kuna jambo aliliona haliko sawa maana akiwasikiliza kwa umakini hawa watu ni kama anabaini uaskari katika maongezi yao.

lakini akitaka kuthibitisha hilo hawa watu wanamkwepa, akashituka kidogo akawa na tahadhari tofauti na hapo mwanzo maana wanasema machui hutambuana kwa harufu. Hapa wanajeshi wote watanielewa katika kipengele cha namna ya kuzungumza, kula na vile unavyotembea.

Ingawa akiwaangalia muonekano wao hauonyeshi kuwa ni wanajeshi maana wanaonekana walugha lugha tu.

Akawaza akaona ngoja atumie mbinu moja na atajua tu kama hawa watu ni wanajeshi, kwanza aliwatuliza vijana wake watulie na akamuomba radhi nahodha.

Huyu jamaa ni captain maana ana nyota tatu, kijeshi ni hivi unavyozidi kupanda cheo ndivyo kiwango cha makasiriko kinazidi kupungua maana unakuwa unakaa mbali na msitari wa utumishi.

(Hivyo nawasihi sana raia msiwachokoze hawa wanajeshi wenye vyeo vya chini.

Mkiwachokoza, kwanza huwa wanahisi mmewadharau sana hivyo hutibu majeraha yao ya mioyoni yanayotokana na kuhenyeshwa kuanzia kambini mpaka kwenye misheni mbali mbali. Hivyo hujipoza kupitia ninyi maana saikolojia yao hutaka mtambue uzito wa lile vazi walilolivaa kwa kuwapa adhabu nyingine ambazo huenda kinyume na utu.)

Captain alikaa kimya kwa muda wa kama dakika moja kisha ghafla alinyanyua mkono wake wa kulia haraka sana akapiga saluti, Malone alijikuta ni kama anataka kuitikia ile saluti kabla ya kujikumbuka kuwa yeye hapo ni nani na lengo la ile saluti ni nini maana mkono uliishia usawa wa mdomo.

Jiga Kinamba alijikuta akitabasamu huku akimuangalia Malone maana tayari ameuza mchezo.

Captain naye alitabasamu tu baada ya kuona mpango wake umezaa matunda akabaki akimuangalia Malone ambae nae alikuwa akitabasamu tu akiwa anaushusha mkono wake chini taratibu .

Baada ya kubaini hilo Captain aliwataka vijana wake waingie kwenye boti yao kisha yeye akabaki kwenye boti waliyokuwemo akina Malone, akamuambia nahodha wa boti hii kusogeza mbali kidogo na pale.

Nahodha hakuelewa maana ya kuambiwa vile basi Malone akamwambia aisogeze tu wala asiwe na wasi wasi ambapo alitekeleza zoezi hilo.

Wakiwa wamejitenga peke yao ndipo Captain alihitaji kutambuana vyema na hawa watu, basi utambulisho ulitolewa kwa ufupi tu kwamba watu hawa yaani Malone na Jiga Kinamba wanatoka shirika la SIA ( Songomo Intelligence Agency ) kitengo cha Foreign & Stratergic Intelligence, wakamuonesha na vitambulisho vyao akaridhika.

Malone akamwambia huyu Captain Inakuwaje wanapewa amri na kuitekeleza bila hata kuwa na shauku ni kwanini wamepewa ile amri? hivyo hii haina tofauti na kuwalinda maadui waliomo ndani wakiwa wanajadili namna ya kuliangamiza taifa bila wao kujua.

Kauli hii ilimshitua kidogo Captain na kujikuta akitaka maelezo zaidi ndipo wakamwambia kuwa wana mashaka na lile jahazi huenda likawa ni makao ya maadui wenye njama dhidi ya taifa lao.

Maneno haya yalionekana kumuingia vyema captain na kuibua shauku ndani yake ya kutaka kujua ukweli juu ya haya maneno.

Captain akaamuru boti zote ziendeshwe kwa tahadhari kuelekea kwenye lile jahazi kubwa, boti zote zikavuma kuelekea pale lakini wakiwa wamekaribia Jiga Kinamba alitoa ishara ya kutoendelea mbele zaidi kuna kitu alibaini ghafla.

Mita kama thelasini kutoka walipo aliweza kuona kama uzi wa bluu bahari mwembamba sana ukiwa umetoka katika kwenye lile jahazi kuelekea majini hivyo kutokana na rangi ya bahari hii iliufanya ule uzi uwe ni ngumu sana kuonekana.

Lakini Jiga Kinamba aliuona maana ni kama ni vitu alikuwa akiviwinda, muda wote macho yake yalikuwa makini sana kutazama huku na kule.

Huyu ni Jasusi wa kiwango cha juu sana hapa ulimwenguni, hivyo basi vitu kama hivi anajua ni kawaida kukutana navyo maana adui huandaa kingio kwanza kabla hajaanza mashambulizi.

Uzi huu ulikuwa umezama majini kisha kwa mbele kama mita kumi ukawa umetengeza duara lililolala juu ya maji kiasi ambacho kama meli au boti ingeufikia basi ni wazi sehemu ya mbele kwenye kitako cha chombo husika ingeunasa huo uzi na kuuvuta hivyo kufanya mtego husika kuteguka na kufanya kazi husika.

Jiga kinamba aliwaambia warudi nyuma zaidi ambapo walirudi kama mita hamsini hivi kisha Jiga Kinamba alitoa kifaa kidogo sana kwenye begi lake ukikiangalia kina upana wa inchi tatu na urefu wa inchi sita kina vitufe viwili tu upande mmoja na kwa mbele kina mdomo mwembamba kama wa chupa ya soda.

Akabonyeza kitufe kimojawapo ya vile viwili, kukachomoka kimshale kifupi cha urefu wa inchi tatu kikiwa na Kamba nyuma yake ambayo ilizidi kutanzuka kadri kile kimshale kilivyokuwa kikizidi kusonga kwenda mbali zaidi hatimae kile kimshale kiligota kwenye maji kwa juu nyuma kabisa kuupita ule uzi. Kisha akabofya kitufe cha pili ambapo Kamba ilianza kujivuta kwa kasi na kile kimshale kikaunasa ule uzi na kuuvuta.

Kilichotokea baada ya hapo ni kwamba lile eneo lote kuanzia mita thelasini mpaka karibu na jahazi lilipo kulizungukwa na mionzi ya kijani iliyokuwa ikizunguka eneo lote la ile boti kisha kukatokea mripuko mkubwa katika mwendo wa duara kulizunguka lile jahazi.

Mripuko huu mkubwa ulipelekea kuvurugika kwa nguvu ndani ya bahari na kusababisha mawimbi makubwa na msukumo mkubwa wa maji mpaka boti hizi mbili zikajikuta zimerushwa mbali zaidi nyuma kutoka pale walipokuwa na mpaka muda huo hakuna hata boti moja iliyokuwa na mtu ndani yake, wote walikuwa wakipiga mbizi kuziendea boti zao ambazo zilikuwa zimebinuliwa na kuchota maji.

Baada ya kuziweka sawa na dhoruba kutulia hawa watu wawili walizivua nguo zao ambazo zilikuwa zimelowa chapachapa!!

Ikawa ni shughuli ya kuchota maji kutoka kwenye boti zao

Hapa napo Captain alishuhudia vitu vya tofauti, ndio utofauti ulioonekana kwenye mavazi ya hawa watu wawili na mabegi yao aliona ubora wa vitu hivi. Ni kwamba nguo za hawa watu zilikuwa ni gwanda nyeusi zenye material magumu sana na yasiyoweza kupitisha maji.

Malone alitoa kitu mfano wa tochi ndogo akamulika kuelekea lile jahazi kubwa, mwanga uliotoka ni mwekundu sana huu mwanga ulikuwa ni maalumu kwaajili ya kutambua aina yoyote ya kilipuzi kinachoweza kuwepo eneo hilo kuanzia kwenye lile jahazi mpaka pale walipo ambapo taa ya kijani kwenye hii tochi iliwaka kuashiria kuwa eneo lilikuwa ni salama.

Wanaume wakajiweka tayari kikazi na kumuambia nahodha asogeze chombo pale ufukweni.

Captain akataka kuongozana nao wakamwambia aingie kwenye ile boti waliyokuja nayo yeye na vijana wake kisha waondoke eneo lile. Captain akataka kugoma akidai kuwa yeye ndie anatakiwa kuwa kiongozi wa lile zoezi maana wako katika eneo lake la kazi.

Wakamwambia akae nje ya hayo majukumu akapinga maana alikuwa bado hawaamini hawa watu. Lakini, ikageuka kuwa amri, tena amri nzito isiyokuwa na chembe ya utani.

Captain bado alionekana kuwa mkaidi akisema kuwa yeye alidhani kwamba watafanya kazi sambamba lakini kumbe ni tofauti na matarajio yake? Akasema kuwa kama ni hivyo basi anarudisha ule msimamo wake wa mwanzo kuwa hakuna mtu anaepaswa kwenda pale.

Lakini muda huu alijikuta akitazamana na bastola yenye mdomo mpana, Vijana wake walivyoona hivyo nao wakaziweka sawa silaha zao wakiwa tayari kushambulia.

Lakini captain alipotazama mkono wa Malone aliiona ile beji ya dhahabu ikiwa na muhuri wa moto akaduwaa sana na kuwatazama hawa watu. Akajikuta akihamaki kwa sauti bila kupenda “Ancient Guards!!”

Wanaume hawakuwa na muda wa kupoteza, zaidi walimsukumia kwenye maji akabaki anatoa ishara kwa vijana wake kuwa wasishambulie. Wanaume wakamuamuru nahodha wa boti achape mawimbi, wakaondoka kulielekea lile jahazi wakawaacha wanausalama wakihangaika na mkubwa wao kumuingiza kwenye boti yao ili waendelee na doria eneo lingine.

Hiki kitendo ndicho kilipelekea huyu captain kuandika kitabu kilichojulikana kama,“I met them”

Ndani ya hicho kitabu mwandishi anaelezea nguvu anayoihisi juu ya hilo kosi la damu, kutokana na yale machache tu aliyoyaona ile siku.

Mwishoni mwa hicho kitabu anamalizia kwa kusema

“To me, it was a fluke meeting them,it’s not a myth.”

Mwishoni kabisa upande wa kulia chini anamalizia na kimeme cha mtu akiwa anavua kofia.

Kijeshi hii ni heshima kuu kwa wahusika.

****** ******* ******* *******

Huko mashariki katika anga la bahari karibu na ufukwe wa Taiwan lilionekana chopa moja jeusi lenye bendera ya Marekani likiwa linasonga kuelekea Shanghai uelekeo wa kaskazini kutoka kwenye pwani ya Fuhzou, kwa mbali ilionekana meli kubwa ya umoja wa kujihami kutoka huko magharibi.

Hivyo kitendo cha chopa hilo kuonekana likiwa linaikaribia pwani ya china kilitafsiriwa moja kwa moja kuwa ni uchokozi wa marekani kwa China ambapo marekani imekuwa ikiutumia mzozo wa Taiwan kutaka kuivuruga china licha ya makubaliano ya nyuma yaliyosainiwa ya kuitambua Taiwan kama eneo la kimkakati la china ndani ya miaka hamsini.

Taarifa zilitumwa haraka kwenda Wilayani haidian ili ziweze kurudufiwa na Mamlaka za Beijing chini ya (MSS) Shirika la kijasusi la China.

Kitendo hiki kilipelekea mawasiliano ya haraka sana baina ya Viongozi wa MSS na wale wa CPC yaani viongozi wa Chama cha kikomunisti ndani ya China.

Haraka sana watu hawa walielekea huko Pwani katika moja ya bandari kubwa sana duniani, Shanghai.

Baada ya kufika huko walikuta meli kubwa ya MIB(Military Intelligence Bureau) ikiwa eneo lile na tayari chopa hili lilikwishakutua juu ya meli hii kubwa.

Kwasababu meli hii ilikuwa ni kutoka mamla za ndani ya Taiwan basi ni wazi kuwa waliokuwemo ndani ya chopa walikuwa wakisubiri viongozi kutoka China Mainland ama mamlaka kutoka Beijing.

Baada ya viongozi wa MSS na CPC kufika akiwemo minister of State Security na general Secretary wa CPC ambae ndie raisi wa China Bw. Bolin Chun waliingia ndani ya ile meli na kwenda moja kwa moja kwenye chemba ya mikutano ambapo sasa Waliokuwemo ndani lile chopa walitoka ambapo idadi yao ilikuwa ni watu watano wote wakiwa ni wazungu wenye nywele za usinga jamii ya watu wa Cherokee Indians wa huko marekani na Mexico mpaka Canada ila kwa sasa wakiwa wamesambaa maeneo mengi ya Bara la Ulaya lakini ndani ya Marekani wanapatikana kwa wingi ndani ya majimbo ya California, Carolina Kaskazini,Oklahoma na baadhi ya maeneo ya Kansas na Missouri.

Basi watu hawa waliingia ndani ya chemba ya mikutano ambapo walikutana na jopo kubwa la viongozi wa China wakiwasubiri humo huku kwa nje ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha.

Mkalimani wa kimataifa Chen Bao alikuwa ndani ya ukumbi tayari kwa mazungumzo na hawa watu hivyo baada ya kila mmoja kuwa ameketi sehemu yake, Bolin Chun aliwakaribisha hawa watu kwa mazungumzo ya amani yaliyolenga kwanza kujua lengo kuu la ujio wao.

Mmoja kati ya hawa wazungu alisema anaitwa John Chasse, na kuwa ujio wao ilikuwa ni kukutana na watu wawili ambao ni Xian Xing na Huang Feng.

Na dhima kuu ikiwa ni masuala ya kibiashara.

Walipohojiwa kuhusu uraia wao walikiri kuwa wao ni Raia wa Marekani wanaoishi nchini ufilipino wakiwa wanajishughulisha na shughuli za uvuvi baharini.

Wakaonyesha na nyaraka zao juu ya shughuli hizo wanazozifanya.

Ni kweli hawa watu ndio wamiliki wa Kampuni inayojishughulisha na uvuvi na uvunaji wa mazao bahari mengine.kampuni ya 8-Water Fisheries.

Ndani ya Chopa alibaki Rubani ambae ni mweusi akiwa ametulia kwenye siti yake huku macho kayaelekeza kwenye Pilot cockpit na panel. akiwa anangojea jambo Fulani litimie.

Wakati mazungumzo yakiendelea simu ya Bwana Chasse iliita akaipokea na kuzungumza kidogo kisha akaomba radhi na kusema amepokea simu ya dharura hivyo wanaondoka watarudi kwa mara nyingine kwaajili ya jambo hilo.

Kisha wote kwa pamoja wakainuka na kupanda floor ya juu na kuingia kwenye chopa na kuondoka upesi sana wakiwaacha wachina wakiwa katika sintofahamu.

Viongozi hawa wa china walijaribu kutafakari maana ya hawa wamarekani hata wasielewe lengo lao, wakahisi kwa namna yoyote ile hawa watu watakuwa ni watu kutoka CIA waliokuja kujaribu kunusa ili waweze kuipeleleza nguvu ya Beijing.

Lakini ajabu ni kwamba chopa lilipoukaribia mwambao wa Santa Cruz rubani aliwatosa wale wazungu kwenye maji baada ya kuona wako karibu na ufukwe hivyo watu hawa wangepata msaada kwa wepesi kutokana na majahazi na baadhi ya boti zilizokuwa zinaonekana kwa chini, hakuwa na lengo la kuwadhuru kabisa watu hao.

Yeye aliendelea na safari kwa chopa hilo mpaka alipoufikia mwambao wa Palawan, karibu na mji wa Rizal

Kisha kwa nyuma ilionekana speed boat moja ikija kwa kasi ya ajabu sana Boti hii na hili chopa vilikaribiana yaani zilikuwa zikitembea kwenye msitari mmoja wima, chopa likiwa juu umbali wa mita sabini. Kisha chopa likaongeza kasi na huku boti ikipunguza kasi hivyo chopa likawa limetangulia mbele kama mita thelasini.

Ndipo kukashuhudiwa kitendo cha ajabu kilichofanywa na Rubani wa lile chopa, rubani alijiachia kutoka kwenye lile chopa na kubaki akielea hewani akienda chini. lakini kabla ya kuyafikia maji alipitiwa na ile boti kama kipanga ambapo sasa ilikuwa kwenye mwendo usiomithilika.

Ndani ya boti walikuwemo watu wa kazi tu, na Safari iliendelea mpaka kwenye mwambao wa kisiwa cha Balabac Pawalan hapo walikuta jahazi moja kubwa na la kisasa lililotengenezwa na kampuni ya Moonrakers ya huko marekani Ina uwezo mkubwa sana wa 60knots, hivyo kasi yake ni kubwa sana ukilinganisha na majahazi mengine ambayo huishia 40knots mara nyingi. Na kwa juu kabisa likiwepo lile chopa walilokuja nalo toka kule Songomo.

Wanaume wakaingia ndani ya jahazi hilo ambapo lilianza safari huku likiwa na vijana wachache wa JISA, lakini haikuchukua muda ambapo lile chopa lilipaa likiwa na mabaduni watano pamoja na wale vijana wa JISA likiliacha jahazi hilo hapo hapo likiwa ni kama vile limetelekezwa.

***** ******** *********

Huko uchina Ndani ya jiji la Shanghai mjini Baoshan, kulitokea mlipuko mkubwa sana na ilidaiwa kuwa eneo ambalo lilikuwa kitovu cha shambulio hilo ni yanapopatikana Makao makuu ya magenge hatari ndani ya China likiwemo Genge la Red Blood.

Hivyo mali nyingi sana na maisha ya watu viliteketezwa inakadiriwa kuwa takribani watu laki tatu walipoteza maisha huku watu laki saba wakijeruhiwa vibaya sana pia maelfu ya majengo na mali mbali mbali zikiharibiwa vibaya sana ikiwa ni pamoja na miundombinu. Mlipuko huu ilibainika hapo baadae kuwa ni bomu lenye uzito wa megaton moja ambalo liliweza kupigwa na kuleta madhara ndani ya kilomita za mraba miambili yaani nusu ya eneo lote la Baoshan lenye wakazi takribani milioni mbili na nusu lilipata madhara ya bomu hili.

Na huko Shaoshan katika mji wa Hunan yalipokuwa makao ya Bwana Huang Feng hali ilikuwa ni vivyo hivyo

Na kuyafanya mashambulizi hayo kuwa ya kihistoria huku wananchi wakiyahusisha mashambulizi hayo na kundi la ISIS, kutokana na kamera nyingi za barabarani kuwaonesha wahusika wakiwa wanne ndani ya mavazi aina ya kanzu huku kichwani wakiwa wamefunga vilemba.

Lakini pia katika barabara zote walizopita hawa watu kuna miili mingi sana ya maaskari ilikuwa imetapakaa hovyo kutokana na majaribio ya kutaka kuwatia nguvuni hao magaidi, juhudi ambazo ni wazi kwamba hazikuzaa matunda zaidi ya kuondoka na roho za watu.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa mapambano kati ya wanausalama na hao magaidi zinadai kuwa kulishuhudiwa uwezo wa juu sana wa kimapambano ambao hawadhani kama umewahi kuonekana popote pale ulimwenguni.

Taarifa ya kwamba hawa watu walikuwa ni kikundi cha magaidi kilipingwa vikali na wataalamu wa kazi wa MSS wakidai kuwa hao hawawezi kuwa magaidi bali huenda wakawa ni majasusi kutoka CIA walioamua kuvaa mwamvuli wa ISIS.

Hoja hii iliungwa mkono na baadhi ya wakuu wa idara za usalama wa China hasa pale ilipobainika kuwa watu hao rangi ya ngozi zao ni nyeusi, wakaona kuna uwezekano mkubwa sana watu hao kuwa watu wa Marekani maana ndio taifa lisilojali kuhusu suala la rangi hasa yanapokuja mambo yanayohusu Usalama wa Taifa.

Inaaminika kuwa taasisi ya CIA ndio taasisi yenye idadi kubwa sana ya watu jamii ya rangi nyeusi kuliko Taasisi zote za kiintelijensia za nchi nyingine yoyote ile inayopatikana katika ukanda wa America na Ulaya mpaka Asia.

Simu iliuma kutoka Haidian mpaka George Bush Centre,Virginia, Marekani. Kwa watemi wa Intelijensia ya kigeni,(Foreign Intelligence).

Lakini majibu waliyoyapata ni kwamba hata CIA wenyewe wameshitushwa na taarifa za mashambulizi hayo na mpaka hapo wanafuatilia kwa ukaribu kupitia Operation Departments zao zilizopo ukanda wa Pacific Mashariki.

Kutokana na majibu hayo wakuu ndani ya Idara za MSS walishindwa kuelewa ni kikundi kipi haswa kilichohusika na mashambulizi hayo huku asilimia kubwa shutuma zao wakiitupia Marekani kutokana na kwamba kwanza maeneo yaliyoshambuliwa ni maeneo ambayo ni makao ya watu ambao wale wazungu aina ya Cherokee walihitaji kuonana nao.

Lakini taarifa za kuaminika kutoka nchini ufilipino zilidai kuwa wale wazungu wao walitekwa kama sehemu tu ya mipango baada ya kuwa wameamriwa kufanya vile walivyofanya. Na hii ni kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanyika baada ya wale watu kuokolewa na kuripoti kwenye vyombo vya usalama siku iliyofuata.

Hivyo basi vyombo vya usalama ndani ya China vilizipokea taarifa hizo kishingo upande, lakini baadae kitendo cha kuonyeshwa picha kutoka kwenye satelite waliamini japo kwa asilimia ndogo sana.

Surveillance ya hili tukio iliendelea maana walikiona kile kitendo cha Rubani wa Lile chopa kujiachia kutoka kwenye lile chopa na kutua kwenye ile speed boat.

Hili tukio lilikuwa likifuatiliwa kwa ukaribu sana na taasisi zote za kijasusi na walikuwa wakishangaa ni kwa namna gani mtu yule anaweza kujitosa kutoka juu umbali mkubwa kiasi kile mpaka kwenye boti na ikawa kama coincidence na kasi ya ile boti.

Hapa taasisi nyingi za kijasusi ziliweza kubaini kuwa hawa watu sio wa kawaida kabisa, kulikuwa na mjadala mkubwa sana wengine wakidai inawezekana ni magaidi kweli ila waliopata mafunzo ndani ya marekani chini ya CIA wenyewe au Urusi chini ya SVR-RF.

Na hii yote ilitokana na aina ya mabomu yaliyotumika kulipua miji hiyo, uchunguzi uliweza kubaini kuwa ni bomu aina ya Tsar Bomba lenye uzito wa megaton moja.

Hivyo mpaka hapa Wakuu wa Idara wa MSS waliamini kabisa kuwa CIA wanahusika kwa asilimia sabini na asilimia thelasini ziliwaangukia SVR na GU wataalamu wa Urusi.

Maana Mabomu hayo yana historia mpakano na nchi hizo mbili tangu enzi za vita vya pili vya dunia mpaka vita baridi ambavyo vimedumu mpaka leo hii.

(Na hii ndio sababu inayopelekea mataifa haya kutokuwa tayari kuingia vitani yenyewe kwa yenyewe maana kila mmoja anajua kuwa mwenzake ana silaha nzito za maangamizi.

Yaani kwa mfano ikitumika upumbavu wa hali ya juu kwa Mamlaka za mataifa haya na hawa wawili wakajikuta wako vitani wenyewe kwa wenyewe kama njia pekee ya suluhu, basi matokeo ya Makombora yatakayopigwa ni wazi kuwa Dunia inaweza kuangamia na ardhi kutitia kabisa. Hii ni habari ya kweli kabisa nayokupa mpenzi msomaji.

Kwasababu Mataifa hayo yamewekeza nguvu nyingi sana kwenye Silaha za maangamizi na Ujasusi wa kiwango cha juu sana.)

Survaillance iliendelea baada ya mtu huyu kuingia kwenye boti ile, waliishudia ikienda moja kwa moja na kuingia ndani ya jahazi lile.

Jahazi hili baada ya kutafuta taarifa zake, walipata kuwa ni mali ya kampuni ya 8-Waters Fisheries, kampuni inayomilikiwa na wale Macherokee wa Marekani.

Na Jahazi hili lilinunuliwa nchini Marekani kwenye kampuni ya Moonrakers chini ya mmiliki Mzawa Bwana Ralph Winter kwa wakati huo.

Ni vipi marekani inaweza kuziepuka lawama kwa namna mambo yanavyoonekana?

Mkurugenzi wa CIA Bw. Mike Athur, alipokea simu kutoka ODNI (Office of Director of National Intelligence) akiombwa ripoti juu ya hilo tukio,ripoti ambayo anajua fika kuwa haiko kamili.

Kuingia kwenye kikao na jasusi mkuu pamoja na wakuu wa idara nyingine za kiusalama huku akiwa anajua wazi kuwa hana taarifa za kutosha ambazo atawasilisha mezani, kidogo ilimtatanisha.

Hivyo kutokana na nafasi yake aliomba muda ili akusanye ripoti kamili juu ya magaidi hao. Lakini alimtumia Director kile kipande cha video ikimuonesha rubani alivyoruka kutoka kwenye chopa na kutua kwenye boti huku akilitelekeza lile chopa lililozama baharini baada ya muda.

Director of National Intelligence Bw.Tom Cooper, baada ya kukitazama kile kipande cha video alimakinika na mavazi ya yule rubani maana ni yeye tu ndie hakuwa amevaa kanzu.

Mavazi aliyoyavaa ni gwanda nyeusi yenye material ya kipekee sana. Cooper aliyatazama haya mavazi kwa umakini mkubwa sana. Pia mgongoni mtu huyu alikuwa amevaa begi jeusi nalo ni la material yale yale.

Kichwani alikuwa na kofia muundo wa helmet nyembamba inayovutika lakini ilikuwa na tabaka kwa juu gumu na linaloteleza hivyo haliruhusu hata risasi kupenya.

Mavazi haya yalimkumbusha bwana Cooper kuhusu lile kosi la damu la Ancient Guards of the Nation. Akawa ni kama anawaona vile.

Alikuwepo nchini jotokali miaka ile akiwa kama mwanadiplomasia alieenda kwa malengo ya kuzipatanisha zile nchi mbili, lakini nyuma akiwa amebeba ajenda tofauti za wakubwa.

Kwani ilikuwaje mpaka akaenda nchini Jotokali?



Anakumbuka miaka kadhaa iliyopita akiwa na baadhi ya maafisa kutoka mashirika tofauti ya Kimkakati aliitwa Mjini Tel Aviv, Israel.

Kulikuwa na kikao baina ya Matajiri wa kiyahudi raia wa Marekani, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani Bw William Roberts na Mkurugenzi wa Mossad kwa wakati huo Bw Asher Voronin.

Cooper anakumbuka wakati yeye na wenzake wanaingia walikuta kikao kimeisha tofauti na muda walioambiwa kikao kingeanza, kikaanza masaa mawili kabla hivyo yeye na wenzake hawakuwa sehemu ya majadiliano ya ajenda ya kile kikao lakini kutokana na umuhimu wake, taarifa alizipata kutoka kwa Bw.Roberts.

Wakati huo cooper alikuwa chini ya Shirika la N S A (National Security Agency).

Mkakati ilikuwa ni kwamba Cooper na wenzake wanatakiwa kwenda nchini Jotokali kwaajili ya kukutana na Viongozi wa taifa hilo ili kuandaa mipango itakayozaa vita baina ya Jotokali na Songomo.

Ambapo mara baada ya vita hiyo kuanza Jotokali ingepata misaada ya chakula na silaha kutoka kwenye shirika moja lililopo marekani.

Misaada hii ingeisaidia Jotokali kuivamia na kuuangusha utawala wa serikali ya Songomo hivyo ushindi huu ungemaanisha kuwa Songomo sasa ni eneo la Jotokali kimkakati. Utawala wa Jotokali ungewapa upenyo matajiri wa Marekani hususani wale wa kiyahudi kuingia Songomo na kuvuna mali,lakini eneo lengwa kabisa likiwa ni Lobeng ambapo Marekani alidhamiria kujenga kituo chake cha opersheni kikubwa kabisa na kuwa kama makao makuu ya masuala yote ya kiusalama kwa Marekani katika bara la weusi.

Na baada ya vita Songomo ingebaki na light Internal Sovereignity bila external ambapo mamlaka makubwa ya ndani na ya nje yangetegemea Jotokali.

Kiufupi Songomo ingepoteza mamlaka kamili ya kutambulika kama taifa ambapo mamlaka zote za uongozi na usalama zingekuwa zikipangwa Nchini Jotokali tena kupitia mashinikizo ya mataifa ya Magharibi.

** *** *****

Cooper na wenzake walifika Nchini Jotokali mapema miaka miwili kabla ya vita kuanza wakakaa miezi sita kisha Cooper na wenzake waliingia nchini Songomo wakiwa kama wamiliki wa shirika la kimataifa la kuhudumia na kutoa misaada kwa shule mbali mbali na taasisi zilizojihusisha na walemavu na mayatima.

Kukaa kwake nchini Songomo kulimwezesha kuipata vyema jiografia ya taifa na kuweza kubaini maeneo ya kimkakati ya kijeshi kumbuka walichagua shule ili iwe rahisi kwao kutembelea sehemu nyingi kwa wakati mfupi ambapo kwa siku walikuwa wakitembelea mpaka vijiji thelasini.

Shirika hili lilifanya kazi nchini Songomo kwa muda wa mwaka na nusu na kusitisha mkataba mara tu baada ya vita kuanza kunukia.

Cooper akarudi marekani kusubiri vita ishike hatamu kisha baada ya vita kuanza, akarudi akiwa na sura ya mtu mwingine kabisa akiwa kama mwandishi wa habari wa kimataifa kutoka shirika moja la nchini Uingereza, shirika la BIN (British International News).

Vita ilipiganwa nje ya matarajio ya Waanzilishi yaani perpetrators.

Matarajio yao ilikuwa ni hivi, kutokana na wataalamu waliopelekwa Magharibi kwa ajili ya mafunzo mazito ya kijeshi juu ya vita ndani ya miaka miwili, pamoja na misaada ya silaha nzito, basi Songomo haingehimili vita ile japo kwa miezi mitatu. Ingekuwa ishaangushwa na kusalimu amri.

Lakini vita iliendelea kwa miezi tisa na sasa ilikuwa inaenda kuhitimisha mwaka jambo ambalo Wamarekani na baadhi ya washirika wake walidai linaenda nje ya makubaliano.

Washirika waliona wanapata hasara kubwa kadri muda unavyozidi kusonga na baadhi ya matajiri wakaanza kuondoa pesa zao ndani ya Federal Reserve.

Jambo hili lilipelekea utawala wa Raisi wa marekani kusakamwa wazi wazi na wananchi wake kuwa anatoa misaada kuchochea vita bara la weusi ilihali taifa la Marekani limekuwa likitoa misaada ya kulijenga bara hilo haoni kuwa ni unafiki mkubwa?

Wananchi walianza kupiga kelele kuwa Serikali ya Marekani inatakiwa kumpiga mchokozi ambae ni Jotokali kwa Bomu zito ili asitishe vita kama ilivyokuwa kwa Japan miaka ile.

Ama sivyo aitishe mazungumzo ya amani kwa pande zote mbili ili kunusuru roho za watu wasio na hatia.

Na hapo ndipo Cooper aliitwa tena arudi Marekani na kuambiwa aipelekee silaha za maangamizi Serikali ya Jotokali na baadhi ya wataalamu na majasusi waimalize Songomo ndani ya wiki moja. Yaani Songomo sasa ilitakiwa kupigana moja kwa moja na maspecialists wa vita kutoka Marekani waliofanya plastic surgery ya ngozi zao na kuwa weusi.



Mabaduni wa Serikali, walikuwa wakiendelea na mambo yao mengine mpaka pale walipopata taarifa kutoka kwa wale majamaa wa Yasenevo Moscow. Juu ya mkakati wa NSA kutuma majasusi wake vitani.

Majamaa wa Yasenevo waliona hakuna umuhimu wa kuruhusu majasusi wa NSA kuingilia ile vita maana ushindi ungepatikana kiwepesi sana na NSA na washirika wake kama CIA wangejisifu sana baada ya ushindi huo kuja kwao ilihali wamepigana na wanajeshi wenye ujuzi wa kawaida .

Hivyo SVR hawakutaka Marekani ipate ushindi wa mezani waliamua kuifanya kazi yao iwe ngumu tena sana.

Miezi tisa baada ya vita kuwa imepamba moto hatimaye majeshi ya Jotokali yalifanikiwa kuingia na kuteka majimbo matano ya Songomo likiwemo Jiji la Homabay na Lobeng.

Mapigano yaliendelea lakini, ghafla Mkuu wa Majeshi wa Jotokali aliripotiwa kuchinjwa na kitu kilichoaminika kuwa ni waya mwembamba mithili ya uzi wa kushonea nguo.

Alikutwa akiwa ameegemea meza yake ofisini huku damu zikiwa zimetapakaa chini.

Hawakukaa sawa ndege iliyokuwa imebeba wataalamu wa kazi kutoka Marekani ikadunguliwa.

Meli ya kivita iliyokuwa imebeba msaada wa vyakula na mavazi kwa wahanga wa vita ikapigwa bomu zito na mlipuko wake uliathiri robo ya Jotokali maana ndio kwanza ilikuwa inatia nanga.

Ukweli ni kwamba hii ndio meli iliyokuwa imebeba silaha zote za maangamizi za kuipa ushindi Jotokali.

Hivyo kuteketezwa kwake kuliibua mgogoro mkubwa sana baina ya Marekani na washirika wake maana fedha zilizotumika kununua silaha hizo zilikuwa ni nyingi mno inakadiriwa kuwa ni Dola billioni mia moja.



Hivyo kulipuliwa kwa meli hii ikiwa kwenye bandari nchini Jotokali kulipelekea kusambaa kwa zile kemikali za sumu na kuua watu wengi mno mpaka viumbe vya baharini na kwenye maziwa kulingana na ile sumu ilivyoweza kufika kwa msambao wa hewa.

Pwani yote ya Jotokali na miji ya jirani ilitapakaa mizoga ya watu, ndege na wanyama, miili iliharibika na kutoa harufu kali.

Hakika yalikuwa ni mauaji ya kimbali tena makubwa mno takribani watu milioni moja na nusu walikufa kwa sumu hiyo.

Baada ya kitendo hicho Marekani kupitia wizara yake ya mambo ya nje iliishutumu vikali Serikali ya Songomo kuwa imetumia silaha za sumu kuua raia wa nchini Jotokali hivyo imekiuka sheria za kimataifa juu ya vita na kutangaza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kijeshi Songomo.

Propaganda chafu zilianza kuenezwa kuhusu utawala wa Songomo kupitia vyombo vya habari kama VOA(Voice of America) na BIN(British Iternational News).

* **** ******

Cooper yeye anakumbuka alikuwa ikulu. Akiwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Jotokali na waandamizi wa kiusalama wengine kutoka mataifa washirika wa Marekani ndipo alishuhudia mauaji ya ajabu yakitekelezwa na miamba saba tu.

Mauaji yaliyotekelezwa katika mji huu wa Bakoma ambao ndio makao makuu ya nchi ya Jotokali, hajawahi kuyashuhudia popote pale, watu walichinjwa bila kujali kama ni askari ama ni raia wa kawaida. Yaani ndani ya dakika moja mtu mmoja alikuwa anaangusha zaidi ya watu mia kwa kasi ya ajabu, anayakumbuka mavazi yao meusi ambayo hayapitishi risasi na kofia zao mfano wa helmet.

Aliiona nembo ya fuvu linalovuja damu ikiwa upande wa kushoto kwenye mkono chini kidogo kutoka begani.

Mavazi haya aliyaona vyema na hio nembo aliiona pia.

Malaika hawa saba wa shetani walimwaga damu katika miji yote mikubwa na Ile yenye wingi wa watu. Walipiga mabomu mazito kwenye shule na hospitali kubwa, ni mazito yaani kiasi kwamba roho za watoto zisingevumilia hata mvuke wa mabomu hayo.

Ilikuwa ni dalili ya wazi kuwa mashetani hawa wanataka kuifuta kabisa Jotokali ni shughuli ya siku nne tu lakini ungeweza kuamini kuwa ikifikia siku ya kumi kuna uwezekano wa kutomkuta hata mbu au kunguni nchini jotokali.

Unaambiwa kuwa mjini Bakoma damu mitaani zilikuwa zimefika usawa wa magoti na bado hawa mashetani hawakuwa wameridhika ni kama kulikuwa na roho ya kishetani nyuma yao inayodai kuwa bado damu haijatosha.

Cooper na wenzake walikuwa ndani ya sehemu salama kabisa ikulu wakiwa wamejifungia huku maeneo hayo yakiwa yanalindwa vikali na kila aina ya askari.

Lakini wakati alipoyashuhudia yale aliona wazi hakuwa sehemu salama ni kama alikuwa wazi tu maana mauaji yaliyokuwa yakitendeka kwa chini huku wao wakiwa kwenye floor ya juu ya jengo hili kubwa lenye floor kumi ndani ya ikulu hii, yalimtisha hasa pale ilpofikia kuwa watatu kati ya wale malaika wa shetani hawaoni tena kwenye upeo wa macho yake.

Awamu hii alikuwa na sura yake ya Cooper maana alikuwa amekuja na mwamvuli wa Mwanadiplomasia.

Miongoni mwa jopo lililotumwa na Umoja Wa Mataifa kwenda kumaliza ile vita kwa njia ya kidiplomasia.

Baada ya kuona ile hali alimshauri Raisi wa Jotokali Bw.Shente Serero kuwa waingie kwenye Helicopter iliyokuwa kwa juu Mahususi kwaajili kumtorosha raisi na maafisa baadhi inapotokea dharura kama hizo.

Wakatoka nje na kukimbilia floor ya juu kabisa ambapo wangepanda helikopta hiyo na kutoroka na kwenda uhamishoni na Cooper kurudi nchini Marekani.

Basi baada ya kufika juu wakiwa wanasindikizwa na baadhi ya wanausalama Cooper alishangaa kuwakuta malaika wa shetani wawili pale juu ambapo mashambulizi dhidi ya watu hao hayakufua dafu maana wanausalama na baadhi ya majasusi kutoka Marekani aliokuwa ameambatana nao Bw Cooper walifyekwa ndani ya sekunde kadhaa wakabaki Cooper na Raisi Bw.Shente Serero.

Raisi yeye aliuawa pale pale mbele ya macho ya Cooper kwa kuchanwa tumbo mara moja na matumbo yote na damu kumwagika chini.

Mmoja alivua kofia na kufanya sura yake kuonekana vyema wa pili nae akafanya hivyo walikuwa ni Jiga Kinamba na Malone.

Jiga kinamba aliuokota mwili wa Shente Serero na kumwambia Cooper kuwa yeye anatakiwa abaki kama mjumbe wa kuzirudisha hizi habari kwao Marekani kama ambavyo mwanzo alikuja akiwa kama mwandishi wa Habari.

Wakati anamwambia hivyo alikuwa ameushikilia mwili wa Shente akiwa anauzungusha utumbo shingoni kama vile mtu azungushavyo Kamba juu ya fimbo ili iwe rahisi kubebeka.

Cooper alikuwa akimuangalia Jiga Kinamba kwa mshangao juu ya kile anachokifanya, ghafla Cooper alipata wazo la kutoroka hapo juu na kutokomea. Ni jasusi mbobevu hivyo vifaa vyote hutembea navyo, hivyo alichomoa Kamba nyeusi na kuigotosha kwenye nondo moja pale juu kisha aliteleza nayo kikomando kushuka chini.

Akawa na Imani na matumaini ya kuwa kasalimika, sasa ile anatua chini alishangaa kuona kiumbe mwingine akitua pembeni yake umbali kama mita saba akamtazama vizuri akashangaa ni Jiga Kinamba akamuangalia mgongoni labda nae ana Kamba hakuiona, mikononi pia hakuiona.

Akajiuliza ina maana huyu mtu ameruka kutoka kule juu, floor ya kumi na moja mpaka chini? Akashangaa mno .

Jiga Kinamba alimwambia kuwa anakimbiaje wakati bado hajapewa ujumbe wa kupeleka nchini kwao?

Cooper aliuliza tu “Who are you? And what’s your business on this matter”

“We are, by the Nation, for the Nation and the Nation itself.”
Alijibu Jiga Kinamba. Jibu moja lenye maana ya moja kwa moja kwa jasusi yeyote yule.

Cooper anajiamini maana ni mtemi wa kijasusi, sio mnyonge kihivyo. Alitoa kichupa kama kile chenye dawa ya wagonjwa wa pumu ambacho hutumia kuvuta kwa mdomo (metered dose inhaler).

Lakini hiki cha cooper chenyewe kina antidote ndani yake hii ilimaanisha kuwa Cooper alihitaji kumshambulia Jiga Kinamba kwa kutumia sumu mbaya yenye kiwango kikubwa cha Hydrofluoric Acid.

Lakini Jiga Kinamba alitoa kichupa cha Quaternary ammonium, pamoja na Gel yenye madini ya Calcium akamrushia akimwambia ukitumia hivyo hapo itakufaa zaidi.

Jasusi cooper alishangaa sana namna akili ya huyu mtu inavyoweza kuitangulia akili yake.

Cooper akajaribu kutumia mapigano kama njia peke ya kujinasua kutoka kwenye mikono ya huyu kiumbe lakini ndio kwanza alikuwa anakosea zaidi.

Cooper aliruka pigo moja aina ya Deceiving flying kick makarateka huita side yoko ama yoko tobi geri, ambapo mpigaji hujiachia kwenda hewani kisha mguu wa kulia hunyooshwa ukiwa umelenga kukita sehemu za siri na mguu wa kushoto hukunjwa kidogo ukiwa umekusanya nguvu zote kisha hukita shingoni au katikati baina ya kifungo cha tatu kutoka juu kuanzia kile cha kwenye kola ya shati. Hili ni pigo la mauaji kabisa kama litatumiwa na mjuzi.

Wenye taasisi zenu za mapigano mtanisamehe kidogo kwa kuifungua hii code ya kifungo cha tatu.

Jiga Kinamba alisogea kidogo tu kwa wepesi wa hali ya juu akatumia teke aina ya mikazuki kumpiga Cooper shingoni ampapo alidondoka chini lakini akainuka haraka sana kumkabili Jiga Kinamba. Haya yalikuwa ni mapigano baina ya watu walio juu sana katika medani ya mapigano wakiwa wameiva haswa.

Cooper akajaribu kutumia joint kick ama kansetsu geri, hapa alilenga amvunje goti Jiga Kinamba, lakini matokeo yakaja tofauti maana Jiga Kinamba alijiachia kwenda hewani kwa haraka sana na kuachia pigo aina mikazuki lililotua vyema kwenye koromeo la Cooper akaenda chini huku akikohoa mfululizo.

Akiwa anahangaika kujinyanyua pale chini, aliwahiwa akapigwa konzi nzito na mbaya kwenye mlango wa pinna la sikio, sehemu ile ambayo mara nyingi huwa na kishimo kitoacho uchafu kwa baadhi ya watu.

Pigo hili liliuathiri mfumo mzima wa neva za Olfactory na kupelekea shida ya kutosikia vizuri kwa Cooper maisha yake yote. Hivyo sikio la upande wa kushoto la Cooper halipokei mawimbi ya sauti kabisa mpaka leo hii.

Kisha alimpiga Cooper, cutting Marilo moja ya nyuma ya shingo na kumpelekea kupoteza fahamu kabisa.

Cooper alizindukia kwenye chumba kimoja akiwa ameketishwa juu ya kiti kimoja kikubwa cha chuma kilichotengenezwa maalumu kwaajili ya mahojiano ya kijasusi. Utaratibu ni ule ule alikuwa amevuliwa nguo zote yaani alikuwa uchi wa mnyama hakujua mazingira haya yalikuwa ni wapi lakini mbele yake walikuwepo Jiga Kinambana, Malone na Golo Zumba ambae alikuwa ametegesha kamera na mitambo tayari kwa ajili ya mahojiano.

Mahojiano yalianza ambapo Bw.Cooper alitakiwa atoe maelezo yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho juu ya mipango mizito iliyotekelezwa kabla na baada ya vita kuanza na kutoa lengo hasa la wao kuanzisha vita ile.

Cooper alikaa kimya tu akiwa anawatazama, ni kawaida ya majasusi wengi hata alipokuwa akiulizwa maswali alikuwa akijibu kwa kukwepa na mara nyingi kila baada ya sentensi mbili angecheka au kuanzisha mazungumzo yenye dhima ya kuchekesha.

Hii kijasusi hutumika kumvuruga mtu apoteze umakini na lengo la maswali yake yaani humtoa kabisa kwenye msitari wa kung’amua kitu hata kama ilibaki kidogo aunganishe doti.

Pia ni mbinu ya kununua muda ikiwa una uhakika kuwa muda si mrefu wenzako watafika kwaajili ya kukukomboa basi utaanzisha porojo nyingi ili kuwavuruga maadui zako.

Jiga Kinamba anajua watu wa kiwango cha akina Cooper sio wa kuwapa nafasi kubwa sana maana hawa wanaweza kutumia hata kivuli tu kukuhadaa.

Jiga Kinamba aliweka Jiko la gesi chini ya kile kiti cha chuma alichokalia Cooper, kisha akawasha moto. Kiti kikawa kama sufuria huku Cooper akiwa ameketishwa uchi wa mnyama juu yake akiwa amefungwa vyema asiweze kunyanyuka.

Cooper kuona hivyo alihamaki akaingiwa na hofu na hapo kiti kilishaanza kusharabu joto kwa kasi, akawa anasikilizia joto linavyoongezeka akiwatazama hawa watu usoni hawana muda nae, ndio kwanza wanataka kuondoka chumbani humo.

Cooper hakutaka kubanikwa kama nyama, kwanza anajua kuwa sehemu zake za siri haziwezi kuhimili kukutana na joto la nyuzi nyingi hivyo maelezo yake ndio salama yake.

Alianza kuwaomba wazime moto ili atoe maelezo lakini wanaume walikataa na kudai uharaka wake wa kutoa maelezo ndio utakaomuokoa kutoka kwenye hicho kiti.

Cooper alikuwa akitetemeka mwili mzima kutokana na hofu na kutotulia kwenye kiti ambacho sasa kilishaanza kuwa cha moto kabisa ila bado hakijabadilika rangi.

Cooper baada ya kuona watu hao wamedhamiria kumfanya ndafu, hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuzimwaga hadharani hazina za mabeberu ili akoe hazina zake za mwili.

Alitoa maelezo mengi ya kweli kwa haraka sana na kila swali alilokuwa anaulizwa alilijibu kiufasaha bila kusita kutokana na maumivu ambayo alikuwa anayapitia pale kwenye kiti.

Mpaka ikafika kipindi akawa anaweka sura kama anaetamani aulizwe swali lingine kwa haraka ili alijibu.

Alipoona kasi ya hawa watu ya kumuuliza maswali haiendani na uhitaji wake wa haraka ya kutolewa pale kwenye kiti akawa anajiuliza swali mwenyewe kisha analitolea maelezo.

Kwa mfano wa hivi; “Unajua malengo ya vita hii ni nini?” Kisha anajibu mwenyewe “Ni kuuondoa utawala wa Songomo uliopo na kuishikilia Songomo kupitia mamlaka za Jotokali ili iwe rahisi kwetu kuchukua tunachokihitaji ndani ya Songomo.”

Baada ya kutoa maelezo ambayo waliridhika nayo waliliondoa lile jiko na kumfungua atoke kwenye kile kiti.

Cooper alijirusha chini kama gunia lakini ngozi na nyama kiasi za makalio na mgongo uliokuwa umeegemezwa kwenye hicho kiti zilibaki kwenye kiti maana tayari kilishaanza kubadilika rangi na kuwa chekundu.

Alilala pale chini kifudi fudi uchi akisikilizia maumivu yasiyo na mfano kutoka kwenye majeraha ya kuungua.

Baada ya dakika tano wanaume walimshika na kumkalisha tena juu ya kile kiti muda huu kiti kilikuwa kimepoa kidogo lakini bado joto lilikuwepo maana hakipoi haraka.

Kitendo cha kukalishwa tena juu ya kile kiti huku akiwa na yale majeraha alipiga ukelele wa yowe lakini hawa watu hawakumjali hata kidogo, walimkalisha vile vile na kumtanua miguu.

Dhakari ikawa inaonekana wazi wazi, kisha Golo Zumba alitoka nje na kuingia akiwa ameambatana na mwanamke mmoja wa haja akiwa na sanduku la chuma dogo lenye urefu wa futi tatu na upana wa nusu futi.

Kutokana na kiti kuwa kimeinuka juu kiasi, lile sanduku liliwekwa chini ya kile kiti na kufunguliwa ukatolewamo mdenge mwembamba sana mithili ya spoku ya baisikeli. Kisha ukavutwa mpira wa gesi na kuwashwa ukawa unachomwa ule mdenge kwa moto wa bluu wa gesi.

Kwa kuwa ilikuwa ni chini ya kiti na Cooper hakuwa akiona yanayoendelea chini ya kile kiti, baada ya hapo lilifuatia zoezi lililomuacha Cooper mdomo wazi.

Mwanamke yule mwenye umbo matata akiwa ndani ya sidiria nyembamba iliyoacha wazi sehemu kubwa ya matiti yake na bukta moja fupi nyepesi iliyoishia chini ya makalio tu alianza kuzichezea nyeti za Bw, Cooper aliuchezea uume wake kisha akaanza kuunyonya taratibu mpaka akahakikisha Cooper ameanza kupata joto na uume kusimama kabisa.

Baada ya uume kuwa umesimama ile kisawasawa alianza kuupiga piga juu ya kiganja chake kisha, ghafla kwa haraka sana aliuchukua ule mdenge uliokuwa umepata joto na kuwa mwekundu haraka sana aliuchomeka ule mdenge kwenye njia ya mkojo ya uume wa cooper.

Moshi mwingi sana ulitoka kutokana na ule ute uliokuwa umeanza kumtoka kwenye uume,Cooper alipiga kelele kwa sauti ya juu sana ikifuatiwa na machozi mengi sana kisha akazirai kwa mwili wake kushindwa kuhimili yale maumivu.

Alikuja kuzinduka baada ya siku saba na hii ni kutokana na kwamba alichomwa sindano ya usingizi kisha akasafirishwa kwa ndege kutoka songomo mpaka nchi moja inayopatikana kaskazini mwa Bara la weusi ambako kulikuwa na uhakika kuwa angepata msaada kutoka kwa maafisa wa usalama wa Marekani waliopo katika nchi hiyo. Maana Taifa hilo lilikuwa likitawaliwa na utawala uliosimikwa madarakani na Marekani.

Alipokelewa na kulazwa hospitali ya nchi hiyo kwa matibabu zaidi ambapo kutokana na majeraha aliyokutwa nayo pamoja na uume wake kuwa umevimba na kuvilia usaha, sindano za usingizi ziliendelea kudungwa kwenye mwili wake huku akilishwa chakula kwa mashine.

Baada ya matibabu ya awali ndani ya hospitali moja ya kijeshi nchini humo hatimae hali yake ilitia matumaini ambapo waliruhusu awe na ufahamu wake ili aweze kusafirishwa kwenda nchini Marekani kwa matibabu zaidi. Na hiyo ni baada ya siku saba kuwa zimepita.

Cooper anaukumbuka ule ushetani maisha yake yote na hali ile ilipelekea Cooper kuwachukia sana wanawake wenye maziwa na makalio makubwa maarufu kama Curvy women.

Anakumbuka pia matibabu yake yalivyogharimu pesa nyingi na utaalamu wa hali ya juu sana wa upasuaji, kuweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida japo sio kama hapo awali.

Dunia baada ya kuona yale mauaji ya nchini Jotokali nchi nyingi ziliitupia lawama Marekani na kuishutumu vikali juu ya kuhusika moja kwa moja na vita ile, ilyopelekea nafsi za watu wengi sana kuangamia.

Ikaundwa kauli ya kuyaweka yale mauaji kwenye kumbu kumbu daima. Kauli inayosema “Few people cried and few laughed but many were Silent.” Ikiakisi hali ilivyokuwa baada ya yale mauaji kwamba wale wachache waliolia ni wale walioomboleza misiba ya ndugu na wapendwa wao. Ila wapo pia waliocheka, hususani wale waliosuka mipango ya kuwaingiza hawa watu vitani kwa maslahi yao. Lakini wengi zaidi ndio walinyamaza hapa anawazungumzia wale marehemu waliolala chini bila uhai wanajeshi kwa raia na viongozi wa pande zote mbili ambao hawana maslahi na hiyo vita iliyopiganwa.

Baada ya vita vile kukoma na mambo kutulia Raisi wa Marekani pamoja na waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya nje walijiuzulu kwenye nafasi zao baada ya kelele ndani ya Marekani kuwa kubwa. Huku watu wengi wakiamini kuwa watu hawa wanapaswa kuchukuliwa hatua kali kwa Uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Lakini kujiuzulu kwa hawa watu kulichangiwa na tishio la Mabaduni wa Serikali kuchapisha na kuachia ushahidi kutoka kwa Cooper mwenyewe ukionesha kukiri kuhusika kwa viongozi hao katika njama zile.

****** ******** *******

Cooper hawezi kuyasahau yale mavazi kamwe, hivyo alimpigia simu Athur na kumwambia aache kulifuatilia hilo suala kisha akakata simu na alifanya hivyo kwa mashirika yote kumi na saba yaliyo ndani ya CI (Community of Intelligence) Marekani.

Arthur alishangaa kwa maamuzi haya ya ghafla kutoka kwa DNI Cooper.

Akawaza “Si ni yeye ndie kanipigia simu akiwa na mchecheto wa kupewa ripoti juu ya tukio hili?” akaona hapana, ngoja ampigie ajue Cooper kagundua nini juu ya tukio hilo au ni kweli serikali ya Marekani inajua ama kuhusika na tukio hilo halafu yeye anabaki kuwekwa gizani bila kufahamishwa lolote.

Maana kwa nafasi yake aliona sio sawa mipango ya aina hiyo itokee halafu asipewe hata muhtasari tu.

Alimpigia Cooper na kumuuliza kuwa yeye kama yeye amegundua nini kupitia kile kipande cha Video?

Cooper alimjibu kuwa amegundua yote kuhusiana na hilo tukio.

Arthur akamuuliza anamaanisha nini kusema amegundua yote? Cooper akamwambia hivi, “Ukiona nakwambia acha, ujue namaanisha kuwa uache. Maana nakutakia mema wewe na kizazi chako.Wale ni Ancient Guards of The Nation”.

Arthur alijikuta akitetemeka mwili mzima, akaingiwa na baridi ghafla, vinyweleo vikamsimama mwili mzima akaitua simu mezani bila kupenda.

Arthur aliinua simu akapiga kwenda Haidian, Beijing.

Akawaambia kuwa hiyo shughuli imefanywa na Kosi la Ancient Guards of the Nation maarufu kama The Seven Angels of Lucifer.

Hivyo wakiamua wapambane ila wajue kuwa hiyo ni on their own risk, maana kuna uwezekano wa East China Sea na South China Sea kugeuka na kuwa damu tupu ikiwa hao mashetani wataamua kufanya mauaji ndani ya China.

Kitendo cha Wakuu wa CIA kujiweka kando na suala hilo kilitosha kuonesha uzito na uhatari wa kosi hilo la Ancient Guards of the Nation kwa wakuu wa MSS china.

Maana ukizingatia bajeti tu ya shirika la CIA ni takribani dola billion kumi na tano kwa mwaka iweje wakae kando na suala hilo ina maana nyuma kuna kitu kikubwa kinachowafanya wakae kando.

Ndio maana ya ile kauli kwamba ukiwa unafuga simba, ikatokea siku umeenda nae kuwinda, mara ukamuona anakupita kwa kasi ya ajabu akirudi nyumbani, basi na wewe unatakiwa sio tu ukimbie, bali uhakikishe kuwa unakimbia hadi unampita yule simba.

Wakuu wa MSS waliwasiliana na viongozi wa CPC ili kujadiliana, pia suala hili lilihusisha masecretary wote wa High congress wa Shanghai na Beijing ambapo idadi yao ilikuwa mia moja na kumi.

Hawa ndio watu ambao walitakiwa kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike kwa wakati huo.

Wengi wa hawa viongozi wakiwemo masecretary walisema hilo halihitaji hata kupigiwa kura maana kila mtu avute picha aone Beijing itafananaje baada ya maeneo kama Temple of Heaven, Tiananmen, Forbiden city na summer place yatashambuliwa unadhani ni nini kitatokea? Na wale wa Shanghai watafurahia kuona Yu garden,The Bund, Shanghai tower na Eneo lote linaloizunguka Oriental Tv tower yakiangushwa kwa makombora mazito?

Je ni watu kiasi gani wataangamia na itatuchukua miaka mingapi kuijenga tena miji hii ya kihistoria? Ambayo imejengwa kwa takribani miaka elfu tatu kurudi nyuma?

Hapa hakuna majadiliano juu ya hilo maana tayari kuna wapuuzi wawili waliosababisha ndugu zetu kufanyiwa haya na wao tayari hawapo. Hivyo sidhani kama ni busara kujiingiza vitani na watu hao Vinginevyo ni pale tu ambapo tuko tayari kukabiliana na madhara yatakayoletwa na hatua hizo.

Mjadala ulifungwa hivyo na wakuu wote wa idara za kiusalama walitahadharishwa juu ya kuibua mgogoro na Kosi hilo maana ikitokea mtu akafanya uzembe kwa namna yoyote itakayosababisha taifa kushambuliwa basi mtu huyo bila kujali nafasi yake itakuwa ni halali kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa.

***** ******* ******* *******

Wanaume baada ya kufika kwenye ufukwe wa kile kisiwa hawakutaka kwenda moja kwa moja kwenye lile Jahazi.

Walianza kukisaili kile kisiwa kwanza maana kwa vyovyote walijua walishaonekana tangu wakiwa kwenye maji kutokana na ule mlipuko.

Walizama vichakani na kuanza kupekua hatimaye waliona njia inayoingia katika pango moja wakaifuata kwa tahadhari Upande huu wa kisiwa walioingilia haukuwa na makazi ya watu zaidi ulitawaliwa na Mapori mazito mazito pamoja na baadhi tu ya majumba ambayo yalitumika kama mastoo ya kuhifadhia vifaa vya wavuvi na baadhi ya mizigo ya wafanya biashara hivyo utulivu ulikuwa mkubwa.

Hii ilipelekea mzingira yake kuwa rafiki kwa adui kuweza kuweka makao kwa muda huku akiichunguza Songomo bila kushitukiwa.

Walipoingia kwenye pango hili walitembea na uchochoro huo mpaka walipokutana na sehemu kwa mbele kabisa ikiwa imeandaliwa kama makazi na hii ilikuwa ni umbali wa kama kilomita moja baada ya kuwa wameingia humo ndani kuta za huu uchochoro zilikuwa zimejaa mawe makubwa kwa madogo.

Upande wa kulia waliona uchochoro mwingine kama huu waliokuja nao, mara wakasikia hatua za watu wakija huku wakizungumza lugha ambayo bila shaka ilikuwa ni Kimandarin kutokana na lafudhi yao.

Wakajibanza kisha kuwapisha watu hao waliwaona wakiwa wanne wakiwa wamebeba maboksi ya chuma. Kwa muonekano ni kwamba maboksi hayo yalikuwa mazito sana kutokana na namna walivyokuwa wameyabeba. Hao watu walikwenda moja kwa moja mpaka lile eneo kisha walikata kona kwenda kulia wakawa wametoweka kwenye upeo wa macho yao.

Malone alifuata kule walikoelekea watu hawa na Jiga Kinamba alifuata uelekeo wa kule walikotokea hawa watu.

Jiga Kinamba alitembea taratibu akiifuata njia inavyokwenda ambapo kwa mbele kidogo aliweza kutoka nje kabisa ya hayo mapango akakutana na Gari ikiwa imepaki aina ya Toyota Hilux milango miwili.

Pembeni mwa ilipopaki hii gari kulikuwa na Godauni ambalo lilikuwa na walinzi watatu wenye bunduki aina ya SMG. Hawa ni raia wa Songomo bila shaka.

Jiga Kinamba alitoa kifaa mfano wa simu ndogo ya button akabofya kitufe kikachomoka kisindano kidogo na chembamba sana mithili ya unyoya wa mbwa.

Kile kisindano kilikwenda moja kwa moja kama vile risasi kikazama kwenye shingo ya mmoja wa wale walinzi. Zoezi hili lilifanyika kwa wote watatu, mara muda huo wote miili yao iliishiwa nguvu na kuanguka chini huku wakirusha rusha miguu mithili ya mtu mwenye dege dege.Baada ya takribani sekunde thelasini wakatulia wakiwa hawajitambui kabisa.

Jiga Kinamba aliusogelea mlango huu akajaribu kama anausukuma kidogo ulikuwa umefungwa. Huu ni mlango wa grill mzito na ulikuwa unatumia Digital security system, Zile ambazo ni more advanced zaidi.

Yaani mlango huu bila kudukua mfumo wake ni ngumu sana kuufungua. Huu haukuwa muda wa kuanza kucheza na huu mlango maana kazi ilihitaji isonge kwa wepesi wa hali ya juu sana.

Mwanaume alipachika bomu kwenye huu mlango, kitu kikajipa na kuacha uwazi mkubwa pamoja na vumbi lililokuwa likitimka. Kupitia lile vumbi kwa nukta kadhaa mwanaume alishazama ndani na kuchukua nafasi yake yaani kitendo cha yeye kuchumpa ndani kilitangulia kama sekunde mbili tu kisha risasi nyingi sana zilimiminwa uelekeo wa mlangoni.

Jiga Kinamba aliweza kuyaona vizuri mazingira ya mle ndani kwenye godauni. Kulikuwa na Watu vipande haswa, yaani wameiva ile mbaya ukiwaona ni lazima mwili ukusisimke.

Inaonekana walikuwa zao busy kuunganisha mitambo maana vitu vilivyokuwa mezani vilikuwa vinajieleza masanduku mbali mbali yakiwa wazi na baadhi ya nyaya na rimoti nyingi na mabomu ya aina mbali mbali.

Jiga Kinamba alivua begi lake na kuliweka chini maana kwa namna alivyowaona hawa watu alitambua kwamba sio tu kundi la Red Black bali humu aliwatambua watu wawili kutoka kwenye himaya ya tano ya kuzimu.

Aliwatambua maana hawa walikuwa ni tofauti sana na Red blood hivyo hawa watu walidhamiria kweli kuipindua Songomo na kuwaweka watu wanaowataka, pia alisikitika sana hasa akifikiria kuwa ndani ya Songomo kuna watu wanashirikiana na watu hawa ambao hawana hata chembe ya utu.Alijua kuwa baadhi ya hawa viongozi wanatetea ugali wao bila kujua kuwa mifumo ya hawa watu itaathiri mpaka maslahi yao hapo baadae maana wote watakuwa watumwa chini ya hawa wazungu. Ndio maana wanatumia kila aina ya nguvu kuweza kusimika tawala zao.

Aliwaza pia kuhusu mikataba ambayo China imekuwa ikiingia na Bara zima la Weusi kwa ahadi ya kuleta maendeleo ndani ya Mataifa hayo akasikitika sana lakini pia inachekesha sana maana mikataba hii haina tija zaidi nikwamba kila mmoja anajaribu kutumia njia yake kuingia kuchota na kuwaacha Wazawa wakibaki masikini sana juu ya ardhi yao inayotajirisha wengine.

Hakuna Taifa linaweza kuliletea taifa jingine maendeleo.

Jiga Kinamba aliihisi nguvu kubwa sana ya kishetani kwa wale watu wawili pia aliweza kuiona mishipa iliyosimama shingoni ikiwa imejaa weusi sana ndani yake na ndio maana akawatambua watu hao haraka sana.

Hawa watu wawili ni elite Assassins. Kuwakabili inahitaji sala. Maana wana nguvu nyingi sana za kishetani ndani yao pia Wameimudu mbinu ya kuvuna sumu kutoka kwa wanyama na wadudu wenye sumu kali ukiwatazama meno yao ni meusi kabisa na wakikung’ata lazima upooze mwili mzima.

Jiga Kinamba baada ya kuona hivyo aliingia katika mode ya kishetani moja kwa moja bila kujali kama anaokabiliana nao wana nguvu za kishetani kubwa kiasi gani.

Pale pale aliwasogelea wale watu kwa kasi ya ajabu huku ujio wake ukiwa kama wa maruwe ruwe kwenye macho ya wale watu.

Wale wawili walijua level ya huyu kiumbe sio ya hapa duniani hivyo na wao walihama na kuchukua nafasi zao tayari kwa vita na huyu mtu.

Jiga Kinamba alimfikia yule mmoja wa Red blood ambae hakuwa amehama bado alimpuliza sikioni na ngumi moja nzito yenye ujazo, hakumpata kabisa lakini ni upepo tu ndio ulimpuliza jamaa alipepesuka na kwenda pembeni akistaajabu ni nguvu ya aina gani hii iliyomo ndani ya huyu mtu, asielewe kamwe.

Wale wawili kuona hivyo walitema mapigo ya ajabu kumwelekea Jiga Kinamba la kwanza lilitua kifuani na la pili lilitua kichwani mwanaume alidondoka chini kwenye sakafu.

Hajawahi kudondoshwa kamwe tangu akiwa na miaka kumi na saba mpaka leo hii akiwa na miaka thelasini na mitano.

Yeye mwenyewe alishangaa lakini haikuwa kwa uzito huo maana waliomdondosha ni watu kutoka kwenye himaya ya kishetani pia, alichunga tu wasishinde maana wakishinda watalitia doa kosi hili ambalo heshima yake imetawala dunia kwa karne nyingi. Pia atakuwa amewatia aibu waliotangulia kuliongoza hilo kosi ambao wengi walikwisha tangulia mbele za haki.

Aliikumbuka ile beji ya dhahabu yenye muhuri wa moto, Sio kila mtu anaweza kuishika ile beji hivyo yeye kuwa nayo ilimaanisha kuwa kuna matumaini ya mamilioni ya watu ameyabeba anakumbuka kiapo chake kabla hujakabidhiwa beji hiyo, anayakumbuka pia maumivu ya kutiwa muhuri wa moto kwa kisu cha kishetani huku yakiwa yanashabihiana na yale ya kwenye beji ila tofauti tu ni kwamba ya begani yameandikwa kwa muundo wa duara.

Mwanaume alisimama macho yakabadilika rangi na kuwa meusi kisha kichwani kukaanza kufuka moshi mzito kama vile kichwa kinataka kuwaka moto.

Wale jamaa watatu kuona hivyo wakahamaki na kuingiwa na hofu maana hawa wawili wanaijua hii ishara kule kuzimu haina wema ndani yake hata kidogo.

Mle ndani kuliingia giza zito ghafla japo ilikuwa ni mchana na nuru ilikuwa ni ya kutosha kabisa, Baridi pia iliongezeka ikawa kali sana.

Giza na baridi vilidumu kwa dakika mbili tu kisha Giza likahamia nje ndani kukirejewa na mwanga. Giza hili lilitembea mithili ya kivuli cha mbuyu mkubwa kabisa nyakati wa jua kali la utosi. Lilikuwa ni giza zito lililojitenga na kuwa kama chaka jeusi kubwa. Lilitembea kuufuata ule uchochoro unaoingia mapangoni na katikati ya hili giza ndimo alikuwemo Jiga Kinamba.

Huku ndani iliachwa miili ya watu watatu ikiwa matumbo na kifua wazi kumaanisha kuwa viungo vya ndani vyote havikuwemo.

Giza lile kadri lilivyozidi kusonga kuingia mapangoni ndivyo lilikuwa likipungua na hatimaye alibaki Jiga Kinamba akionekana mzima mzima bila shida.

Hapo ndipo kalamu yangu inashuhudia kuwa midomo ya huyu mtu ilikuwa imejaa damu hivyo kujenga hisia kwamba huenda vile viungo alivitafuna huyu mtu. Mmh!! Ogopa sana.

Baada ya kama dakika kumi kupita ulisikika mlipuko mkubwa katika lile godauni maana yake ile miili mitatu pamoja na wale maaskari waliokuwa wamelala pale chini kwa sindano za usingizi wa pono iliteketea kabisa, huruma ni kwa wale maaskari waliolala na kupitilizia huko huko.

Maana kama isingekuwa lile bomu kwa lengo la kuyaharibu yale makombora wangeamka baada ya masaa ishirini na nne.

Lakini ndio hivyo roho zao ziliangamia maana pesa iliwafanya wakae kwenye msitari wa uovu hivyo maangamizi ya ule uovu yalipita nao bila kuwachambua kusudi lao ndani ya malango ya uovu.

Jiga Kinamba alipofika pale walipoachania na Malone alimuona akija huku macho yakiwa meusi na kichwa kikifuka moshi Mkononi alikuwa na tarakishi mpakato nne kampuni ya fujitsu, Baada ya kukutana Malone alimchukua Jiga Kinamba na kumpeleka kule alikotoka yeye ambapo waliikuta miili kumi na mbili ikiwemo miili ya watu wa Red Blood lakini wengine wakiwa ni raia wa Songomo wabobevu wa mawasiliano na mitambo mbali mbali.

Huko walikuta mitambo ya kisasa ikiwa imeunganishwa, na eneo hilo lilikuwa limejengwa kwa vifaa maalumu na kuwa kama chumba cha maabara ya kisasa zaidi Waliunganisha zile laptop na kuanza kukagua taarifa zote na mifumo yote hatimaye walitambua malengo ya watu wakubwa waliowapa kazi hawa watu.

Baada ya kujiridhisha na yale waliyoyaona eneo hilo, Malone aliagiza chopa mbili ambazo zilifika na kutua kwa juu karibu na lango la kichochoro mojawapo cha kuingilia humo pangoni kisha vijana walianza kusomba vile vitu.

Baada ya hapo Malone na Jiga Kinamba waliliendea lile jahazi na kulikagua kwa umakini mkubwa sana.

Ndani kulikuwa na mtambo mmoja wa kisasa ambao hawakuelewa kazi yake ni nini lakini baada ya kutafuta taarifa zake waligundua ulikuwa ni mtambo maalum kwaajili ya kuzalisha virusi Fulani ambao wangekuja kutumika kama silaha ya kibaiolojia hapo baadae.

Na hii ilikuwa ni kazi ya Marehemu Huang Feng. Hili jahazi nalo ilibidi waende nalo, ambapo vijana wa JISA walilipeleka hadi karibu na maji ya kimataifa eneo ilipo arsenal ya hili kosi. Maana huu mtambo utaweza kulifaa hili kosi la Mabaduni hapo baadae, kwaajili ya kuzalisha silaha zitakazowawezesha kuwakabili maadui hapo baadae.

Safari ilianza ya kuondoka hapo kisiwani, ambapo ilibidi wapande chopa, maana hawakuwa na usafiri mwingine wa kuwatoa hapo kisiwani, baada ya ile boti ya kukodi kurudi punde tu ilipowafikisha ufukweni mwa hiki kisiwa.

Baada ya kuondoka eneo hilo, chopa lililowabeba akina Malone lilisogea eneo moja ambalo lilikuwa si mbali sana na ilipo bandari. Ambapo walishushwa hapo na kuanza safari ya kwenda bandarini kulikagua eneo lote kwa ufanisi tena.

Waliridhika baada ya kuyakuta mazingira yakiwa kama awali ambapo waliamua kuondoka, njiani wakipishana na magari matatu ya watu wa kitengo cha kupambana na uingizwaji Silaha haramu nchini Songomo.

Hawa ni watu wa serikali chini ya wizara ya ulinzi hivyo silaha na mitambo ile iliyomo kwenye godown ingeweza kutumika huko jeshini na kwenye idara baadhi za kipolisi nchini Songomo.

Wanaume waliufunga ukurasa wao wa kwanza kihivyo na sasa ilikuwa ni kufungua ukurasa wa pili kutibua mipango na safu za watu wa mashariki Mwa Songomo, ingawa ni wabishi na hawakati tamaa kirahisi.

***** ******** ****** ******** ***

Ndani ya Ofisi moja kubwa sana yenye kiyoyozi cha gharama, kiyoyozi kilichohakikisha waliomo ndani ya ofisi hii wanabaki kulisikia joto kama hadithi tu. Huku nyimbo mbali mbali za kuusifu na kuunadi uzalendo zikisikika taratibu kabisa.

Mezani kulitawala vinywaji vya gharama na korosho safi zile toleo la kwanza kabisa. Unapoingia mlangoni upande wa kushoto kuna meza na kiti kikubwa kabisa cha kisasa. Ambacho hakichoki kuubembeleza mgongo wa mkaaji maana kinanyumbulika atakavyo mkaaji, kimenakshiwa kwa madini maalumu ya gharama.

Meza ni ya kioo kitupu kubwa nzito yenye screen kubwa kiasi hapo hapo kwa juu kiasi cha mtu kuwa anapangusa huku ikiwa imeunganishwa katika mfumo mmoja na ofisi karibia zote za kiserikali.

Kwenye pembe moja ya meza hii kuna kioo cha digital kinachowaka kikionyesha bendera ya chama cha Revolutional Movement. Yaani bendera hii imo ndani ya kioo hicho hivyo huwezi kuigusa na muda wote kioo hicho kinawaka kuyafanya mazingira ya meza hiyo kuvutia sana.

Meza hii ni ya kidijitali inatumia umeme hata makabati yake yanatumia mfumo wa kidijitali kufunguliwa.

Ndio iliyobeba mfumo wa muziki unaosikika hapo ndani.

Nyuma ya hii meza kwenye kiti, kaketi mtu mmoja mwenye kipara amevaa suti ya rangi ya kahawia, imemkaa vyema.

Juu ya meza hii pia kuna sehemu kwaajili ya kuweka tarakishi na juu yake ipo tarakishi ya kampuni ya Apple.Tarakishi hii ni muundo wa all in one.

Pembezoni mwa hii meza kushoto na kulia kuna viti viwili vya wageni. Kifupi ofisi hii ina hadhi kubwa sana na ni ndoto ya wasomi wengi kuamkia kwenye ofisi za sampuli hii. Hasa pale wanapokuwa wamehitimu masomo yao, lakini kwa walio wengi ofisi za namna hii hubakia kuwa ndoto tu katika maisha yao. Maana hizi ni ofisi ambazo hukaa watu wenye elimu kubwa hususani shahada ya uzamivu maana hawa ndio hufanikiwa kuingia kwenye vitengo nyeti vya mashirika makubwa na vitengo nyeti Serikalini.

Ndio ukweli wenyewe unakuta asilimia kubwa ya watu wanaota kuwa na maisha ya watu wenye elimu za juu sana ilihali wao wana elimu za kawaida kama shahada ya kwanza na hawataki kujiendeleza hadi shahada ya Uzamivu. Unakuta mtu ana shahada ya kwanza halafu ameridhika na anatamba kuwa yeye ni msomi hivyo anataka na mifumo ya ajira imtambue hivyo.

Sio rahisi sana katika dunia hii inayobadilika kwa kasi sana kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya mashine. Ukweli ni kwamba mashine hizi zinachukua nafasi za ajira za wale watu wenye elimu ndogo na kati .

Na wadau wa masuala ya kazi na ajira wapo tu wanatoa macho huku wimbi la watu wasiokuwa na ajira likiongezeka maradufu lakini pia gharama za maisha zinapanda bila zuio. Tuachane na hilo turudi mchezoni.

Ilikuwa ni nyakati za mchana muda wa kupata chakula cha mchana ambapo kupitia mlango mkubwa wa kioo aliingia mtu wa chakula akiwa anasukuma kitroy chenye bufee kwa juu. Alianzia kwenye meza kubwa ambapo alishusha makabrasha kadhaa ya chakula na kwenda kwenye meza nyingine ndogo nzuri lakini sio kama ile kubwa, napo aliweka vifurushi na kisha alirudi na kuvuta kiti kwenye meza kubwa kisha akaketi.

Kitendo hiki ndicho kilimfanya yule aliyepo nyuma ya meza kuacha shughuli aliyokuwa akiifanya kwenye tarakishi na kumpa umakini mtu huyu aliyeketi. Maana hata aliposalimiwa aliitikia kwa mazoea tu huku macho akiwa kayagandisha kwenye kioo cha tarakishi.

Baada ya kumtazama vyema mtu wa chakula ndipo aligundua sio yule anaewahudumia siku zote. Akataka kubonyeza vitufe kadhaa pale juu ya meza lakini mtu huyu akamzuia akimwambia asijaribu kufanya chochote, atulie tu wafanye mazungumzo ya amani kisha yeye ataondoka bila kufanya chochote ofisini humo.

Hii ni ofisi ya m wenyekiti wa chama cha Revolutional Movement na huyu ndie Mwenyekiti wa chama hiki.

Mwenyekiti aliuliza swali moja tu, “Wewe ni nani na unataka nini kutoka kwangu?”

“Nahitaji taarifa kamili kutoka kwako juu ya mtu mmoj tu, Suzana Muguki”
Alijibu Mtu huyu.

Mwenyekiti alimwambia mtu huyu kuwa aondoke upesi sana ndani ya hii ofisi vinginevyo ataita askari waje kumshughulikia.

Mtu huyu alimuuliza kuwa maaskari hao watapitia wapi kuingia ndani humo?

Swali hili lilimfanya Mwenyekiti atazame mlangoni ambapo kupitia kioo cha mlangoni alimuona mtu mmoja akiwa kawapa mgongo amesimama wima hana habari.

Hapo ndipo mwenyekiti akajua kuwa kumbe ujio huu umekokotolewa vya kutosha na watu wako kazini hawatanii.

Kwenye meza ya pembeni alikuwepo mwanamke mmoja mrembo sana kaketi akiwa na macho ya duara makubwa na uso Fulani uliobeba upole juu yake akiwa amevalia vazi ambalo liliacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.

Huyu alikuwa ni kama zawadi kwa mwenyekiti kama kiburudisho tu, maana muda mwingi alikuwa ametulia akila chakula chake kwa mikogo huku mkono wa kushoto akichezea simu yake kubwa na haya mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ni wazi kuwa hakuwa akisikia chochote wala hakuonekana kuwajali wawili hao.

Mwenyekiti mara alipaza sauti na kumtaka mtu huyu kuondoka ofisini hapo akidai hana taarifa zozote za kumpa mtu huyu.

Sauti ya Mwenyekiti ndiyo ilimzindua mwanamke yule ambaye haraka alinyanyua simu yake aliyokuwa kailaza mezani muda wote huo.

Kitendo cha kuonekana ananyanyua simu, ilisikika mlio wa mpasuko wa ile simu huku ikisambaa sakafuni vipande vipande ni risasi moja iliyoachiwa kutoka kwenye bastola ya mtu huyu. Risasi hii iliondoka na ile simu pamoja na vidole viwili vya yule mwanamke akabaki akilia kwa maumivu makali, akivitazama vidole vyake pale chini akiwa amebakiwa na vibutu viwili mkono wa kushoto.

Mwenyekiti baada ya kuona hivyo aliamua kunyoosha maelezo pindi alipobaini kuwa anatazamana na mdomo wa bastola hapa na hapa.

Akasema yeye aliletewa jina la Suzana Muguki mezani kwake na kupewa maelezo kuwa jina hilo ndio linatakiwa kupita na si vinginevyo.

“Je umewahi kumfahamu hapo kabla?” Aliuliza mtu huyu ambae sura yake ilikuwa ni ngeni.

“Hapana sijawahi kumfahamu kabisa tofauti na ile siku niliyoletewa jina lake.” Alijibu Mwenyekiti.

“Je kabla ya kupokea maelekezo hayo ninyi kama chama mliazimia kulipitisha jina lipi?” Aliuliza mtu huyu tena.

“Jina ambalo wanachama wengi walitaka lipitishwe ni la Joseph Daro.” Alijibu mwenyekiti huku akiwa anavuja jasho kwa wingi licha ya kiyoyozi kuwepo.

“Basi mwambieni Daro ajiandae kwaajili ya kuwania kiti cha Uraisi maana muda wa nuru umewadia hivyo giza halina nafasi tena katika taifa hili na kama na wewe ni sehemu ya hilo giza utaisahau ofisi hii na mema yote uliyojiwekea kupitia giza hilo.” Alisema mtu huyu bila kueleweka mara moja anachomaanisha.

Kisha walionekana kuteta kwa sauti ndogo sana, inaonekana mwenyekiti alikuwa akimpa mtu huyu orodha ya watu waliomshinikiza kufanya vile.

Maana aliinamia Baobonye kisha alichapa barua moja na kuichapisha kisha alimkabidhi mtu huyu.

Kisha mtu huyu alinyanyuka na kumuaga kwa kumpa mkono huku akimtazama machoni akimtakia kazi njema iliyojaa weledi ndani yake.

Mwenyekiti aliupokea mkono ule huku uso wake ukiwa umejawa na mashaka sana hakuwa anaamini kama huyu mtu anaweza kumuacha akiwa hai.

Lakini tofauti na matarajio yake, mtu huyu aliondoka na kuvuta mlango wa kioo akatoka nje kabisa ya hii ofisi ambapo aliungana na yule aliyekuwa pale nje, wakaondoka na kuingia kwenye lifti iliyowapeleka floor ya chini kabisa, kutoka hii floor ya saba juu. Katika jengo hili ambalo lilikuwa kati kati ya jiji.

Ambapo Chama hiki kilikuwa kimenunua floor hii kutoka kwa kampuni ya MOSEINS GROUP, ambao ndio wamiliki wa majengo matatu yaliyopo kati kati ya jiji hili ikiwa ni eneo moja zuri sana la kibiashara.

Baada ya kufika chini waliingia kwenye gari lao la kifahari na kutokomea zao. Sio wengine bali ni Jiga Kinamba na Malone. Na aliyeingia kwa mwenyekiti alikuwa ni Malone huku Jiga Kinamba akibaki nje ya ile ofisi.

** ****** ****** *******

Saa tatu za usiku ilimkuta Jiga Kinamba akiwa busy kwenye tarakishi yake mpakato aina ya Macbook, kuna taarifa alikuwa akizifanyia kazi muda huu akiwa kwenye sura ya Seif kule kule mtaa wa Napa street.

Lakini leo Mwana hakuwepo mazingira haya, ni baada ya kuwa amepata kile roho yake ilikuwa inahitaji sasa angerudi kufanya nini hapo? Na zaidi ni kwamba tayari kurunzi ya manyamela ilikwisha kumumulika. Hivyo kuendelea kukaa kihasara hasara ingemletea mushkeli maana, (wabaya….. watu).

Taarifa zote kumuhusu Suzana Muguki zilikuwa hitaji maalumu kwa sasa. Jiga Kinamba alichimbua Historia ya Mwanamama huyu mwenye umri wa miaka 43, hatimaye aliweza kumjua huyu mwanamke ni nani.

Suzana Muguki alizaliwa miaka 43 ililyopita kwenye familia moja ya kitajiri kiasi, maana wazazi wake wote walikuwa watumishi wa Serikali. Mama akihudumu katika uwanja wa sheria baba yeye alikuwa kwenye Wizara ya Nishati na Madini.

Mh. Muguki Wanjele alipata nafasi ya kuhudumu kama Waziri pia katika wizara hii na ni katika uongozi wake ambapo ilidaiwa wachimbaji wadogo hasa wa ndani kunyang’anywa na kufutiwa leseni mara kwa mara pale waliposhindwa kupeleka commission kwenye mamlaka ya wizara hii.

Huu wote ulikuwa ni mkakati wa kuchuma mali nyingi, maana hata wawekezaji hawakupewa nafasi ya kupumua. Kuanzia wale wamiliki wa migodi mpaka wale Masonara wakubwa, wote waliwekewa mifumo ya kugawa asilimia za mapato kwa huyu Waziri. Ulipopinga ulikutana na kikwazo kwenye sahihi yake.

Hivyo hata watoto wake wengi aliowapata kwa wanawake tofauti tofauti wengi aliwapeleka huko Magharibi kwaajili ya kusoma.

Lakini baadae alipata tuhuma nzito zilizopelekea yeye kutimuliwa huku akifilisiwa na kufutiwa usajili wa kuajiriwa nchini Songomo kisha alifungwa miaka mitano jela na kutozwa faini kubwa.

Hata baada ya kutoka gerezani Bw. Muguki hakuwa mnyonge sana kiuchumi maana alibakiwa na kiasi kikubwa tu cha fedha alichokuwa amekificha kwenye masanduku ya chuma sehemu ambayo aliijua yeye peke yake. Hivyo baada ya kumaliza kifungo chake na kuwa huru aliamua kufanya biashara akibebwa vyema na connections nyingi na wakubwa.

Hii ilimfanya kupanda haraka sana kiuchumi ukizingatia Mzee Muguki ni ile aina ya watu wenye roho ngumu sana ya kujitoa pale anapotaka mambo ya pesa yaende upande wake.

Watu ambao hawaoni hatari kucheza michezo ya hatari ilimradi waingize pesa. Alianza na biashara ya ununuzi na uuzaji wa mawe ya dhahabu ambapo hakudumu sana humo baada ya kuona kasi yake haiendani na malengo yake.

Akahamia kwenye mambo ya ufugaji, hapa baada ya kukaa mwaka mzima akiseti mambo yake aliona panamfaa sana ambapo alianza ufugaji wa ng’ombe wa maziwa mwanzo alianza na pori la heka sabini akianza na ng’ombe kumi na tano. Baada ya miaka sita alipanua wigo kwa kununua eneo la heka elfu kumi akaongeza na idadi ya ngombe na akaingiza na mbuzi wa maziwa kwenye hilo eneo lake.

Kisha alinunua nyumba mjini Homabay na kuigeuza kama kituo cha kuuzia maziwa fresh na ya unga.

Huko shambani kwake alisimika kabisa mtando wa kusindika maziwa yaani sasa Mzee Muguki alikuwa na mradi uliokamilika wa Maziwa akizalisha na kusindika na kuuza mwenyewe sokoni huku akiwasambazia wateja wengine wa jumla kona mbali mbali za nchi.

Mradi huu ulimwinua sana mpaka akajuta kuchelewa kuwekezamo. Kutokana na connection yake na watu wakubwa aliweza kuteka na kulimiliki soko nchi nzima kwa ukiritimba mwingi pia, maana jasiri haachi asili yake.

Hivyo Suzana Muguki yeye alizaliwa kwa mama mmoja ambaye walikutana na mzee Muguki mara moja, wakati huo Mzee Mguki alikuwa kwenye ziara tu ndipo akapatikana huyu Suzana na wala watu wengi hawakuwa wakijua kama huyu ni binti wa yule aliyekuwa Waziri hapo zamani. Maana hawakuwa na ukaribu hata ukiangalia umbali wa makazi waliyoishi familia ya Suzana na kule alikoishi mzee Muguki na mke wake.

Baada ya Suzana kumaliza elimu yake ya msingi ndipo alipelekwa kwa baba yake kutambulishwa ambapo mzee yeye hakuwa na makuu. Alimpokea na baada ya vipimo vya vinasaba kuonyesha kuwa yeye ndiye baba mzazi aliamua kumpeleka masomoni nchini Marekani.

Suzana amesomea na kuishi huko huko Marekani ambapo alikuwa anafanya kazi katika shirika moja la habari la huko Marekani. Lakini kuna taarifa ambazo haziwekwi wazi kuwa huyu mwanamama alipitia mafunzo ya kijeshi akiwa nchini marekani. Pia inaaminika kuwa hata baada ya kuingia katika lile shirika bado alikuwa ni jasusi mzuri na mvujishaji wa taarifa fiche. Kifupi ana ujuzi mkubwa sana wa udukuzi wa tovuti za mashirika ili kunasa taarifa fiche.

Kuletwa kwa mwanamama huyu, ilikuwa ni maagizo ya Magharibi juu ya kuendeleza mipango yao ya kujaribu kuitawala Songomo kupitia mapandikizi serikalini.

Baada ya kujiridhisha juu ya taarifa za huyu Mwanamama, Jiga Kinamba alifunga ukurasa wake wa upelelezi juu ya Suzana Muguki. Baada ya lisaa hivi alipokea simu kutoka kwa Fanton Mahal mwenyewe. Hii ikiwa ni siku kumi tangu walipoachana pale kwenye arsenal yao.

Hii ilimaanisha kuwa na wao walisharudi kutoka huko mashariki ya kati.

Jiga Kinamba aliandaa ripoti kamili kuhusu mwenendo mzima wa kazi na matukio na hatua zinazofuata. Kisha mida ya saa saba alipanda kitandani kuuchapa usingizi mpaka mida ya rakaa ya kwanza alfajiri walipokutana kwenye msikiti wa Diyarbakir.

***** ****** *****

Ndani ya Grand palace, ndipo yalikuwa makazi ya Suzana Muguki, jumba moja la kifahari lililopo kushoto kabisa ukiwa unaingia geti kuu. Kulia unayaacha majumba kadhaa ya kifahari yanayolifanya eneo hili kuwa kijiji cha kipekee ambacho kinapatikana kusini mwa jiji la Homabay.

Zikiwa zimesalia siku kadhaa tu uchaguzi mkuu kufanyika, ambapo ni zoezi la kupiga kura kwa wananchi wote. Mida ya saa tatu kamili usiku walinzi wa eneo hili walikuwa wapo makini lindoni wakiwa na silaha zao. lakini ulinzi ukiwa umeimarishwa zaidi tangu Bi Suzana Muguki alipotangazwa kuwa mgombea rasmi kupitia chama cha Revolutional Movement.

Mara ilifika gari nyeusi aina ya Range Rover Vera na kuingia moja kwa moja mpaka ndani ya geti na kupaki mbele ya jumba lile alilokuwa anaishi Bi Suzana Muguki.

Gari iliyoakisi ukwasi wa waliomo, kwanza iliingia kwa mwendo wa taratibu sana. Kutokana na giza basi taa zake ziliwaka katika mtindo wa upekee uliovutia na kumfanya mtu wa hali ya chini kufanya dua ili Mola wake amjaalie afikie kiwango cha maisha hayo.

Kutoka kwenye gari hii waliteremka watu wanne, wawili wakiwa ni wazungu na wawili ni waafrika, waliweza kuonekana kupitia nuru safi iliyotoka kwenye mataa makubwa yaliyotoa mwanga wa wastani usiokera kwa anaetazama kupitia mwanga huo. Lakini pia ukiendana na mazingira yale.

Watu hawa waliingia ndani wakikaribishwa na mwenyeji wao Bi. Suzana Muguki kisha mlango kujifunga.

Walikaa takribani masaa mawili mle ndani kisha wote kwa pamoja walitoka wakimuacha Bi Suzana Muguki na kuingia kwenye gari ile ambapo Dereva alikuwa akiwasubiri.

Baada ya kuingia kwenye gari dereva aliondoka hapo kwa mwendo wa kawaida.

Wakiwa njiani zikiwa zimepita takribani dakika kumi, ndipo waligundua kuwa kuna gari nyingine nyeusi kama ya kwao inawafuatilia.

Mmoja kati ya hawa watu akasema “Hivi James ataacha lini utoto?, yaani hata ukimwambia tunahitaji kuwa peke yetu bila ulinzi lazima atajipenyeza na kukaa sehemu ilimradi tu jicho lake haliondoki kwetu.”

“Lakini si ndio jukumu lake tulilompa?” Alidakia yule mwingine huku wazungu hawa wawili wakiwa kimya.

Safari iliendelea lakini hawa watu waligundua kuwa mwenendo waa dereva anaewafuata kwa nyuma ni ni tofauti na ule wa James. Maana huyu yeye alikuwa ni kama anawanyatia kuliko kuwawekea ulinzi.

Wakajikuta wanaingiwa na taharuki, kisha wakamwambia dereva aongeze kasi ya mwendo, dereva wao alifanya hivyo mpaka walipofika njia panda bado ile gari ilikuwa inawafuata.

Baada ya kufika njia panda, dereva alifanya kuiacha barabara ya kushoto na kunyooka moja kwa moja kwa kuuzunguka nusu mzunguko round-about.

Ile ya nyuma nayo baada ya kufika hapo sekunde kadhaa tu, mara ilitokea gari nyingine kwenye ile barabara ya kushoto aina ya Ford yenye ngao ya chuma kwa mbele, ikaigonga hii gari ya nyuma iliyokuwa inawafuatilia wale watu.

Iliigonga ubavu wa kushoto kwa nguvu sana na kupelekea ile Range kubingirika mara kadhaa ambapo ilivuka ile sahani ya round-about na kwenda upande wa pili ambapo iliingia mtaroni.

Ajali hii ilikuwa mbaya mno, baada ya wale waliokuwemo kwenye ile gari ya kwanza kuona tukio hilo, ilibidi wasimame na kushuka ili kushuhudia ni jambo gani linaloendelea. Maana walidhani kuwa wanafuatiliwa halafu ghafla inatokea gari nyingine na kuigonga ile waliyodhani ilikuwa ina hatari kwao.

Yule mtu wa kwanza akasema “Isijekuwa James kasababishiwa ajali, hii itakuwa hatari zaidi kwetu,” Huku wakiwa wanazipiga hatua hafifu kulisogelea lile gari lililopata ajali.

Lakini walipotazama kule kwenye ile ford, walimuona James akiwa anashuka kwa kujiamini kutoka kwenye gari.

Wakamfuata haraka kutaka kujua kulikoni. Ndipo akawaeleza kuwa muda wote yeye alikuwa akiwafuata kwaajili ya kuwawekea ulinzi, mpaka alipobaini kuwa wako kwenye hatari kutokana na kufuatiliwa kwa muda mrefu na gari ile.

Kisha wote wakaungana na kwenda kuangalia ni nani huyo ambaye hajipendi kiasi cha kuyaingiza maisha yake hatarini kwa kuwafuatilia watu hao.

Baada ya kuifikia ile gari waliichunguza huku wakijaribu kuipekua kwa umakini kubaini ni nani alikuwemo, walipigwa na butwaa baada ya kuona gari iko peke yake bila mtu ndani yake.

Damu zikawasisimka zaidi, maana inawezekana vipi gari ile ikose mtu hata kama amedondoka kwanini asionekane wala alama za damu basi.

Taharuki na hofu vikawa juu yao lakini ghafla wakamuona mwenzao akiwa kama anaekabwa hivi. Maana alikuwa akitapatapa kwa kurusha miguu wakawasha tochi za simu zao wakamuona akikatwa koromeo lake kwa vidole.

Wakachomoa bastola zao na kuanza kufyatua risasi hovyo kumwelekea yule mtu. Juhudi ambazo hazikuzaa matunda zaidi ya kumdidimizia risasi mwenzao, maana walimuona akienda chini peke yake wakashindwa kuelewa ni nani aliyekuwa anamuua mwenzao.

Wakapatwa na wenge mara mzungu mmoja naye akadakwa na kuvunjwa shingo pale pale akiachwa ulimi nje huku kivuli kikihama kutoka kwenye mwili ule kwa kasi ya ajabu na kuhamia kwa James.

Ni kelele tu ndio zilisikika huku mwili wa James ukienda chini, matumbo yakimwagika nje bila mpangilio.

Waliobaki ilibidi kukimbilia ile gari ya kwanza kama njia pekee ya kusalimisha maisha yao. Lakini hatma ilihakikisha hawafiki mbali. Wote walianguka mavumbini na kuusahau ukwasi na mipango mikubwa waliyokuwa nayo. (Kazi ya Macka Shinea).

Zilisalia siku nne kampeni zifungwe ili kuwapa wananchi nafasi ya kuyatafakari yale ambayo walikuwa wameyasikia kutoka kwa wagombea wao na kufanya maamuzi sahihi. Maamuzi ambayo ni wazi ilikuwa ni unafiki tu maana tayari watu wakubwa walikwisha kupanga safu yao ya uongozi, kisha wananchi kuletewa majina ili wachague katika hayo maana hata kama kura zao zingeenda kwa yule wananchi wanaemtaka basi asingepita ikiwa si chaguo la wakubwa fulani. Hivyo hii ilitosha kuziita chaguzi nyingi ndani ya ulimwengu huu batili.

Kutokana na kuonekana kama vile wananchi hushirikishwa moja kwa moja kufanya maamuzi juu ya uongozi, ilihali ni tofauti na vile watu wengi huaminishwa.

Mjini Cadmon, eneo la Dingo Area. Eneo kubwa la wazi mahususi kwaajili ya mikutano mikubwa. Bi. Suzana Muguki alikuwa kwenye jukwaa akinadi sera zake kama ifuatavyo,

“Ni furaha kwangu leo kuwa mbele yenu wananchi wa Songomo wakazi wa Cadmon, shukrani nyingi na za dhati kabisa tunatakiwa kuzielekeza kwa Mungu wetu kutufikisha siku hii ya leo tukiwa wazima.

Nami nichukue fursa hii kuwaomba wananchi wenzangu, msikubali kudanganywa na mtu yeyote yule mwenye nia ya kuwahadaa kuwa mumchague kwa kigezo eti ataleta maendeleo katika taifa letu hili na Cadmon kwa ujumla.

Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu unaotokana na chama kilichokwisha kuimarika ambacho hakitetereki katika kutoa maamuzi yenye tija kwa taifa.

Hivyo ni tumaini langu kwenu kuwa mtanichagua mimi pamoja na chama changu hasa ukilinganisha uzoefu tulionao kwenye kuongoza taifa tangu hapo awali.” Aliweka kituo, kisha akaendelea.

“Nitahakikisha namuinua mwananchi mmoja mmoja kwa nafasi yake kupitia mikopo ya bila riba.

Akina mama nitahakikisha nafasi yetu inatambulika kitaifa na kuwa juu pengine kuwazidi wababa, ambao wametupiga bao katika Nyanja nyingi.

Maana ukiangalia kuanzia bungeni wanawake ni wachache sana, pia viongozi wa dini wamekuwepo wakike lakini kwa uchache sana. Na nitahakikisha mwanamke anapata haki sawa na mwanaume yaani nitaisimamia ile kampeni ya 50/50 kikamilifu.”

Kauli hii iliibua vigelegele kwa wanawake wengi, wakashangilia kama vile ni wakristo wamemuona Masihi.

Baada ya kumaliza kauli hii, ghafla alipanda mtu mmoja jukwaani akiwa kavaa kanzu nyeupe na kichwani kafunga kilemba. Akamchoma kisu tumboni mara nne Bi Suzana Muguki.

Mwanamama huyu alianguka chini huku walinzi wakihangaika kumdhibiti muuaji huku watu wengine wenye hasira kali wakitafuta nafasi ya kumkaribia ili wamtoe roho na yeye.

Bi. Suzana Muguki alichukuliwa haraka sana na kuwahishwa hospitali, huku ndani ya gari la wagonjwa madaktari walikuwa wakipambana kuokoa maisha ya huyu Mwanamama kwa kadri ya uwezo wao.

Lakini juhudi zao hazikuweza kumpoka Malaika wa mauti roho ya Suzana Muguki. Walisalimu amri na kumuacha Suzana apumzike kwa amani huko aendako.

Vilio vya kumlilia mwanamke huyu aliyeonekana kama mkombozi wa wanamama vilikuwa kote nchini. Vyombo vya habari vilipiga propaganda za kutosha na kulaani mauaji yale kutokana na posho nzito walizopewa ili kukilaani kile kitendo.

Watu wenye mipango yao walijua fika kuwa lile lilikuwa ni pigo takatifu juu yao na mipango yao.

Mashirika ya kutetea haki za wanawake na watoto yalicharuka vibaya sana na kulaani tukio lile, ilifika kipindi taarifa na propaganda zile zikawa ni kero maana hawakutaka kunyamaza kamwe.

Marekani na baadhi ya Mataifa ya Ulaya walilaani sana kitendo kile na kuushutumu vikali Uislamu kutokana na muhusika wa mauaji yale kuonekana akiwa na vazi la kanzu.

Kitendo ambacho kilipelekea Masheikh na Maimamu wachumia tumbo na wavizia pesa za mabeberu nyuma ya pazia, kuwaza itakuwaje mara baada ya uhusiano baina yao kuingia doa? wakiona kuwa huenda wakakalia kuti kavu.

Propaganda zile ziliibua chuki na utengano baina ya watu wa madhehebu ya Kiislamu na Kikristo kiasi wakawa hawajali tena kama wote ni weusi.

Bwana Abdul bin Asa’ad aliwekwa chumba maalumu na kufanyiwa mahojiano, watu wakitaka kujua ni nini hasa kilipelekea yeye kufanya mauaji yale kwa Bi Suzana Muguki.

Abdul alisema kuwa, kwanza anaomba kile kitendo kisihusishwe na dini yake kwa namna moja ama nyingine japo ni kweli yeye ni Muislamu. Yeye amefanya yale aliyoyafanya kutokana na msukumo wake binafsi wa ndani na wala si juu ya dini maana hata mtu wa dini tofauti angefanya vile.

Akasema kuwa amefanya vile kwasababu anapenda kuliona taifa la Songomo likiwa ni taifa huru, na watu wake wakiwa na furaha kuliko kuongozwa na mtu ambae kwanza misimamo yake inaonyesha udhaifu wa wazi hata kwenye kampeni zake.

Hivyo atapenda watu wote ndani ya Songomo wamtambue na kumkumbuka kama nembo ya uhuru wao bila kujali itikadi, dini ama kabila. Na anawapenda sana na kuwatakia yaliyo mema.

Aliulizwa je hakuiona hatari ambayo ingemkabili mara baada ya tukio hilo?

Akasema kuwa linapokuja suala la utaifa, kila mwananchi anatakiwa kuwajibika bila kujali kama anaukanyaga msitari wa kifo na huo ndio uzalendo kamili si vinginevyo.

Abdul alikuwa amevimba kutokana na kipigo alichokutana nacho kutoka kwa maaskari polisi waliopewa maelekezo maalumu ya kuhakikisha kuwa mtu huyo anapatiwa mateso makali ili ajutie kile alichokifanya na kuwa kama mfano kwa wale wanaojaribu kufanya vitendo kama hivyo.

Baada ya mahojiano hayo Abdul alitakiwa kuhifadhiwa sehemu maalumu ambayo ilikuwa ya siri, ateswe hadi aseme nani walimtuma na wana mipango gani.

Basi aliondokewa kituo kikuu cha polisi Cadmon na kuingizwa kwenye gari tayari kupelekwa kusikojulikana.

Abdul baadae alipotea katika mazingira ya utata na kutoonekana kabisa licha ya jitihada mbali mbali za vyombo vya ulinzi zilizofanyika kumtia nguvuni, huwezi amini mtu huyu alikuwa ameyeyuka na kubaki kuwa hadithi katika midomo ya watu.

Serikali ilitangaza donge nono kwa mtu ambaye angefanikiwa kutoa taarifa za uhakika kumuhusu Bwana Abdul bin Asa’ad, lakini hayo yote ilikuwa ni bahati nasibu, maana Abdul alitoweka katika macho ya watu. Wapo baadhi waliodai serikali ilifanya siri sana na kumuua Abdul kwa sindano ya sumu kuepuka migogoro na uislamu baada ya tukio hilo kuchukua taswira ya udini.

Lakini ukweli ni kwamba Abdul Bin Asa’ad alichukuliwa na Mabaduni wa serikali na hii ni baada ya kuonekana ni mtu mwenye uzalendo wa kweli na taifa lake.

Watu wa sampuli hii ndio hutakiwa na Fanton Mahal siku zote. Abdul alipelekwa moja kwa moja kwenye kikosi cha JISA kwa aajili ya kutumikia hapo baadae itakapotokea Baduni yeyote ameaga dunia.

Huku duniani aliwekewa most wanted ya maisha, huko underworld mwanaume alikuwa akiandaliwa kuja kuwa nyamela la kwenda hasa ukilinganisha uwezo wa akili yake wa kudadavua mambo na kuweza kubaini ajenda zilizojificha ndani ya kauli ya mtu.

Mwenyekiti wa Baraza la seneti alikuwa anarejea nyumbani kwake mida ya saa mbili usiku, siku hii alikuwa amechelewa kurudi kulingana na ubize uliomshika kutokana na kusogezwa mbele tarehe ya uchaguzi baada ya mgombea mmoja kuuawa. Hivyo kura za seneti zilitakiwa kupigwa upya, ambapo vyama visingewasilisha upya majina ya wawakilishi wao isipokuwa kwa chama cha Revolutional Movement pia chama cha Liberation Front kisingeshiriki kutokana na kwamba kura hizi za mara ya pili zililenga kumpata mtu mmoja ambae angeziba ile nafasi iliyoachwa wazi na Suzana Muguki.

Akiwa ndio amefungua mlango, ile anaingia sebuleni alikutana na familia yake ikiwa yote imekaa sebuleni inaangalia tamthiliya kwenye runinga, lakini kuna mtu mmoja wa ziada alikuwepo hapo mezani na pengine huyu ndiye aliyepelekea harufu ya marashi ambayo ilikuwa ngeni kwenye pua zake.

Maana harufu za perfume za familia zetu huwa tunazifahamu hivyo ikitokea ukahisi harufu ya tofauti lazima utamakinika tu kutaka kujua imetokea wapi? Ni kawaida.

Mgeni huyu alikuwa amekaa akiwa anapata kinywaji, alichohudumiwa na binti mkubwa wa huyu Mwenyekiti.

Mwenyekiti alipiga hatua huku macho yake yakiwa hayabanduki kwa huyu mgeni ambae hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote ule. Familia hii ilikuwa ya mke mmoja na watoto watano, watatu wakiwa wa kike na wawili wakiwa wa kiume. Lakini huyu akiwa ni mke mdogo maana hata kiumri muonekano wake ulionyesha ni mdogo kwa huyu mwenyekiti.

Baada ya mke kumpokea begi mwenyekiti huku akimnong’oneza sikioni kuwa “Mgeni wako huyo” na kupandisha ngazi kuelekea floor ya juu ambako ndiko kilipo chumba chao,mwenyekiti alimpa ishara mgeni wake kuwa waende eneo la mazungumzo nje kwenye balcony ya juu ambapo hapo wangekuwa peke yao.

Mgeni huyu akiwa amevalia suti moja matata alinyanyuka toka pale kwenye kiti na kumfuata mwenyeji wake ambapo walianza kupandisha ngazi kuelekea juu.

Baada ya kufika juu waliketi kwenye viti vizuri vilivyokuwa hapo, huku mfanyakazi wa hapo nyumbani akileta chakula na vinywaji wakaanza kunywa taratibu huku mazungumzo yakiendelea.

Mwenyekiti, Bwa.Hunga Kayoko alianzisha mazungumzo kama ifuatavyo, “Ndugu yangu karibu sana, pia wakati tunapata kinywaji si vibaya kama nikikufahamu japo wewe unaonekana kunifahamu.”

“Huu sio muda wa kutambuana bwana Hunga, sikiliza nina maagizo machache kwako. Tunatambua kuwa kwa nafasi yako, wewe ndio kitovu hasa kinachotazamwa na macho ya wengi wakiwemo wale wenye njama ovu dhidi ya taifa hili. Hivyo kwa namna moja ama nyingine unaweza kuwekewa shinikizo na hao watu ili kupindisha mambo yakae upande wao.

Sasa maagizo mapya juu yako ni kwamba haitakiwi kumpitisha mtu yeyote yule kwenye nafasi ya kugombea Uraisi mwenye mafungamano na magenge ya wizi na rushwa katika nchi hii. Pili haitakiwi kumpitisha mtu yeyote yule, ikiwa mtu huyo ameshawahi kulitumikia jeshi au taasisi yoyote ile ya usalama na ulinzi hata kama mtu huyo anayo taaluma ya uongozi na utawala.

Hivyo ni vyema katika majina yote yaliyopo mezani kwako ukafuatilia wasifu wa watu hao. Ili usije kufanya kosa tena kama ilivyokuwa hapo awali, maana kosa lako la kwanza limesahihishwa, natumaini umenielewa.”

Mwenyekiti alimtazama huyu mtu na kucheka kidogo,kisha akamuuliza, “Ndio maana mlimuua Suzana Muguki? Sikiliza wewe kijana, watu wakubwa wanapofanya mikakati yao ni vyema mkakaa kimya au mkasema kama ni pesa mnahitaji ili mkatibu njaa zenu. Na nani kakuruhusu kuingia kwenye himaya yangu kuja kuniambia huu upuuzi?

Bila sisi matajiri kupambana, ninyi masikini mnaweza kufanya nini? Hebu tazama makampuni yetu yanavyolipa kodi kubwa Serikalini na pesa hizo ndizo huja kuwalipa mishahara ninyi masikini na watoto wenu kupata walau senti ya kidonge.

leo unazungumza kuhusu kupanga safu ya uongozi wa nchi hii?

Sikiliza wewe kibaka, nenda kawaambie na hao wenzako. Najua mnataka tu mpewe pesa, kawaambie kuwa mlifanya makossa makubwa sana kumuua Suzana Muguki na hili haliwezi kupita hivi hivi, kwanza nawaoneeni huruma. Japo sijui ni kitu gani kinawasukuma kuingilia mambo ya watu”

Kipindi chote Mh Hunga anamwaga ngonjera zake, mgeni wake alikuwa bize na chakula na vinywaji, ilikuwa ni kama hamsikilizi Bw.Hunga.

Lakini baada ya kujifuta mdomo kwa tissue nyeupe, alimtazama Bw.Hunga na kumuuliza “Je ni kwaajili ya hizo takrima kiduchu na maisha bora unayohakikishiwa ndio vinakufanya usione tabu na shida ambazo wananchi wengi wanapitia? Hivi mmelewa sana haya madaraka kiasi cha kuhisi kuwa nchi hii ni ya kwenu peke yenu?”

Bw. Hunga alijikoholesha kidogo kuliweka koromeo lake tayari kwa kutema sumu, “Kijana nadhani historia ya hii nchi unaifahamu vyema. Hebu niambie ni lini masikini amewahi kusafiri kwenda nje ya nchi kutafuta namna ya kuliinua hili taifa kiuchumi, achana na hilo, niambie ikiwa itatokea njaa, je nani kati ya masikini au tajiri atakaechangia pesa na chakula kulinusuru taifa? Ukipata majibu ya hayo maswali utatambua kuwa taifa hili linawahitaji matajiri walisaidie na wakati masikini wanalihitaji taifa liwasaidie.”

Kwa mtu mjinga ni rahisi kuamini kauli za mwenyekiti Bw.Hunga.

“Bw.Hunga naona unajiegemeza kwenye hoja dhaifu, zilizojijenga kutokana na mifumo mliyoizalisha wenyewe.

Sasa chagua moja ufanye vile nilivyokuambia na baada ya uchaguzi uendelee na majukumu mengine ukiwa unafurahia matunda ya kazi zako na familia zako mbili ama uende tofauti na ukose vyote vitatu yaani maisha yako, familia yako na nafasi yako.” Alitema cheche mgeni.

Bw.Hunga aliwahi kuwa askari wa jeshi la nchi kabla ya kuachana na kazi ya jeshi na kujiunga kwenye siasa na biashara.

Jeshini kwenyewe inasemekana alifukuzwa baada ya yeye na wenzake kutafuna pesa za ujenzi wa nyumba ama kota za maaskari wakiwa kwenye kamati ya ujenzi.

Kwakuwa ripoti hizi hazikufika kwa raia wengi basi ilibaki kuaminika kuwa aliamua kuachana na jeshi ili afanye shughuli za kisiasa na biashara.

Hivyo kurubembe huyu anajiamini sana hasa ukiangalia ana mafungamano na wakubwa jeshini na ukizingatia historia yake amehudumu nyadhifa kubwa sana nchini kwa muda mrefu. Kifupi miaka yake sabini na tatu inadhihirisha kuwa ni mkongwe wa siku nyingi sana.

Mpaka kufikia kupewa uenyekiti wa baraza hili, haikuwa jambo dogo kabisa. Kuna kitu waliona ndani yake, unaambiwa kuwa kigezo cha kwanza ambacho magenge ya wezi wa mali za umma huangalia ni roho ngumu ya kujitoa mhanga. Sasa ni kwa namna gani wangemuacha mtu kama Hunga, mwenye tamaa na uchu wa mali uliopitiliza.

“Kijana niwasihi tu wewe na wenzako msihangaike na jambo hili maana hii nchi hamjaikopesha kiasi chochote kile. Nikuombe tu mjikite kwenye mambo yatakayowasaidia ninyi na familia zenu, kuliko kuhangaika na mambo ambayo yako nje ya uwezo wenu mtaangamia ninyi nawaambia.

Wewe hapo, unalingana na kijana wangu wa pili, ndio maana natumia hekima kuongea na wewe maana nakuona wewe bado ni kijana mdogo mwenye safari ndefu mbele yako.

Nisingependa kuyaona maisha yako yakiishia gizani kama baadhi ya wapumbavu waliokwishakutangulia mbele za haki, wakiziacha familia zao katika umasikini wa kunuka.

Ni vyema ukajikita kwenye masuala ambayo yatabadilisha hatma ya kizazi chako na watu wako wa karibu, kuliko hiki mnachopambania.

Unavyoniona hapa sio kwamba siipendi haki hapana, bali ni kwamba wakati wewe unaimba kuhusu haki, ukigeuka nyuma unakuta wenzako wanavuna mali na kupeleka kwao. Yaani ukizubaa utashangaa hata mtu wa cheo kidogo kabisa katika kitengo chako amekupita kimaendeleo na wewe ni bosi wake.

Kijana wangu kuishinda tamaa ya mlungura ni vigumu sana, sawa unaweza kuniona nakosea wakati huu lakini ikiwa ni wewe kwenye nafasi hii naamini hata wewe utafanya hivi pengine zaidi ya mimi navyofanya.

Na unafikiri ni rahisi kumshawishi masikini alietoka kwenye umasikini kupitia njia ya usomi, arudi tena kuishi katika umasikini? Wewe mwenyewe unaziona shuruba za kuwa masikini, hata hao wanaharakati wanaokesha wakipiga kelele kuhusu wizi wa fedha za hazina, unadhani wakiipata nafasi ya kuiba wataziacha hizo fedha? Sio rahisi.” Alihitimisha Mh Hunga ndani ya kauli zake akijaribu kujenga hoja za kuunga mkono yale wanayoyafanya yaonekane ni halali kwao kufanya hivyo.

“Fikra zako Bw.Hunga zimejijenga hivyo kutokana na kwamba ni mifumo ambayo mmefanikiwa kuiunda na mmeonja asali ya mifumo yenu. Hivyo hampo tayari kuachana nayo hata kwa makali ya kisu shingoni, lakini ni muda sasa wa kulitenganisha giza na nuru.” Alisema mgeni huyu.

“Kijana wangu kwa ushahidi wa kumbukumbu zako ni wangapi waliojaribu kuleta mabadiliko mnayoyaota na wakayeyuka bila kujua misimamo yao na itikadi zao za uanaharakati zilipoishia?

Najua wengi waliongozwa na njaa kama ilivyo leo hii kwenu, ila ukiona unakula halafu mbwa pembeni yako anakubwekea basi we mrushie mfupa tu, au mpe pande la mnofu uone kama ataendelea kukubwekea. Kumuua Bi Suzana Muguki hakumaanishi kuwa mmeweza. Nguvu iliyopo nyuma ya hii mifumo ni kubwa sana na sidhani kama mtaweza kupambana nayo maana wengi walishindwa.” Aliongezea Mwenyekiti Bw.Hunga.

“Walishindwa kwa sababu tulikuwa upande wenu na hatukuzijua ajenda na malengo yenu kisiasa ilikuwa ni kulileta taifa katika mifumo ya ukabaila na ukiritimba wa namna hii.” Alizungumza mgeni kwa msisitizo huku macho yake yakitoa nuru iliyotahadharisha.

“ Kijana kwani ninyi ni akina nani na kwanini mnaamini kuwa mnaweza kuzuia mipango iliyokwishakupitishwa?

Sikiliza, nguvu iliyoko nyuma ya mifumo hii sio ya hapa nchini tu, bali pia inatokana na Mamlaka ya huko Magharibi. Hivyo hata mkifanya nini bado watamuweka mtu wanaemtaka na hakuna wa kupinga hilo kutimia” Alisema Bw.Hunga.

“Na unaamini vipi kuwa ndani ya brigedi zote saba za Ikulu tunaweza kukosa mtu wetu? Vipi kwa wale wa bustanini? Ushajiuliza ni kwanini katibu wako amebadilishwa? Vipi kwa wasaidizi wenu majumbani kuanzia walinzi mpaka kwa madereva wenu? Je ni wewe ndie unaeamua ni nani awe dereva wako au mlinzi wako pale getini? Kama sio wewe basi tambua kuwa tunaweza kufuta mipango yenu yote.

Na unauliza kuhusu sisi ni nani? Sisi ndio msingi wa hili taifa, sio ninyi wanasiasa wala rushwa, msiojali kuhusu taifa zadi ya matumbo yenu” Alimalizia mgeni huku akiwa ameuinamisha uso wake karibu na uso wa Bw.Hunga.

“Nimekuonya kwa muda mrefu lakini unaonekana ni mgumu kuelewa.” Bw.Hunga alitamka maneno haya huku mkono wake ukiichomoa bastola yake haraka sana kutoka kiunoni.

Kumbuka huyu ni mwanajeshi, lakini ile anafyatua alijikuta yuko peke yake mezani, mbele yake mtu haonekani kaelekea wapi.

Ile kutazama nyuma alipigwa konzi nzito ya utosi. Kutokana na umri wake kuwa umeenda, alianguka kutoka kwenye kiti kwenda chini huku akijigonga kwenye kingo za meza. Bastola yake ikaambaa kwenda pembeni.

Akabaki kuhangaika anyanyuke kutoka pale chini. Ukizingatia na mwili mkubwa aliokuwa nao, mwili uliotokana na maisha mazuri yaliyojitenga na dhiki akiwa na kilo za kutosha.

Mara akasiginiwa sakafuni kwa mguu juu ya paja la kulia. Akagugumia kwa maumivu makali sana. Kisha mgeni wake alimchuchumalia pale chini na kutoa beji ya dhahabu ya Ancient Guards of the Nation na kuiweka mbele ya macho yake.

Akimwambia, “Unadhani tuliamka tu na kujikuta kwenye nafasi tulizopo? Kuna watu walitoa kafara damu zao ili sisi tufike hapa kwa ahadi kuwa tutaviangazia nuru vizazi vyao.

Ninyi mnakula tu raha na kufurahia maisha huku mkitukejeli, mnajua ni mangapi tunayafanya kulilinda taifa hili wakati huo ninyi mmelala na familia zenu? Yaani sisi tunapambana na adui huku ninyi mnashirikiana nae,mnategemea tuwaache si ndio?”

Bw. Hunga alitetemeka kama vile ameona kitanzi cha kunyongea mbele yake. Habari za hawa mashetani anazo maana ni mkongwe wa siku nyingi.

Alijikuta haja ndogo ikimtoka pale chini hakuwa tayari kufa na kuyaacha maisha haya matamu, akivuta picha ya sehemu za starehe anazotembelea na aina ya wanawake ambao huburudika nao, daaah!!

Hapana.!! Hakuwa tayari kufa, bado mema ya nchi aliyahitaji tena sana. Ingewezekana vipi afe kirahisi hivi ayaache maua yanayokomaa kwa wingi kila uchwao tena yakivutia zaidi kila iitwapo leo?

Yeye kufa haraka namna hii aliona ni uzembe mkubwa wa yeye kushindwa kufanya uchaguzi sahihi na hilo halikutakiwa kabisa. Hivyo alinyoosha mikono yake hewani akiwa ni kama anamuomba mungu wake. “Ndugu yangu nakuomba sana, yasalimishe maisha yangu na nitafanya vile mnavyotaka nakuomba sana kwa jina la ardhi na siku ile niliyozaliwa, sitaki kufa mimi. Wewe unajua fika kuwa sio maamuzi yangu ni kwamba tunatishiwa na kulazimishwa kufanya haya tunayoyafanya sio kwa mapenzi yetu.” Maneno haya alikuwa akiyatamka huku akiwa amefumba macho yake tena kwa sauti kubwa.

Lakini alizinduliwa na sauti ya mke wake aliekimbilia juu baada ya kumsikia mumewe akiwa ni kama vile ananena kwa lugha. Ambapo alimkuta akiwa anapiga makelele yale huku macho yake kayafumba, ndio kumshitua.

Bw. Hunga alishituka na kushangaa, ndipo akakukumbuka kujiweka sawa huku akijitahidi kumficha mkewe asijue kiwewe alichokuwa nacho muda huo.

“Mume wangu mbona unapiga kelele na kutubu juu ni lini umeanza kufanya maombi kwa hisia namna hii? Na vipi kuhusu mgeni ameondoka saa ngapi bila hata kuja kutuaga? Na kapitia wapi wakati anaondoka hata tusimuone?” Aliuliza Bi Suta mke wa Bw.Hunga.

“Ameondoka sasa hivi tu kwani hamjapishana hapo kwenye ngazi?” Alidanganya Bw. Hunga

“Na mbona silaha iko chini? Ni ya nani? Kuna usalama kweli hapa?” Aliuliza mfululizo Bi Suta, maswali ambayo ni wazi hayakumpendeza Bw.Hunga.

“Hebu niache kwanza, nahitaji kuwa peke yangu maana unaniuliza maswali mfululizo juu ya mambo ambayo hayakuhusu” Aliongea Bw. Hunga kwa ukali maana hakuonekana kupendezwa na maswali yale.

Bi suta alishuka zake ngazi taratibu kuepusha shari na mwanaume huyu. “Kazi yangu ni ipi kwani si ni kula na kumtunza huyu mwanaume mengine hayo ni juu yake” Alijisemea Bi Suta.

Mgeni yeye alikwishakutokomea zake na kumuacha Bw. Hunga achague nini afanye. (Kazi ya Team Leader )

* ** ** ***

Mwenyekiti wa chama cha Revolutional Movement aliwasilisha jina la Mgombea wake, ambae hakuwa mwingine zaidi ya Joseph Daro. Kura zilipigwa upya na baraza la seneti na idadi kubwa ya kura hizo alipewa Joseph daro kuwania kiti cha uraisi ambapo angechuwana vikali na Bw. Fredinand wa chama cha Liberationa front.

Joseph Daro akiwa bado kijana, umri wa miaka arubaini na tano, mtu mwenye fikra za kimapinduzi na mikakati yenye matumaini ya kuleta mageuzi nchini Songomo.

Akiwa amezaliwa na kukulia nchini Songomo ambapo elimu yake ya msingi na Sekondari aliipatia nchini Songomo na chuo kikuu akisomea Tasmania University huko Australia.

Ni huko mashuleni alipoonyesha misimamo yake iliyokinzana na mwenedo wa viongozi wengi kiasi cha kufahamika kama mwanamageuzi na tegemeo kwa taifa hapo baadae.

Mtu wa nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe. Mtu ambaye watu waliamini kuwa anahitaji tu apewe nafasi na ulinzi na watu wenye uwezo kama ule unaosemwa, wa kosi la Damu au The Seven Angels of Lucifer na hapo mageuzi yangeweza kutokea bila shida.

Leo hii ile ndoto ya walio wengi inakwenda kutimia tena wao hawajui sasa kuwa anawekewa ulinzi na wale mashetani saba wa kutisha. What a coincidence?

Uchaguzi ulifanyika japo kulikuwa na mikiki mikiki ya hapa na pale, lakini kosi la Mabaduni wa Serikali lilikuwepo kuhakikisha hakuna jambo linaharibika. Waliamini huu ndio muda wa kuwatendea wema na kuwatumikia wananchi wa taifa la Songomo ipasavyo.

Hatimaye Joseph Daro aliibuka mshindi wa kura za wananchi na kufanikiwa kuwa Raisi wa Songomo.

Akiwa ni Raisi kijana pia kama ilivyokuwa kwa Hayati Mwibale Moha, maana nae aliingia madarakani akiwa bado kijana wa umri huu huu wa Joseph Daro.

Baada ya kushika dola Mh Raisi akiwa na kamati kabambe ya ulinzi iliyosheheni watu kutoka karibu kila idara walienda Lobeng na kufanikiwa kupata kiasi kikubwa sana cha fedha ambazo zilikuwa zimefichwa na magenge yale.

Kilikuwa ni kiasi kikubwa sana ambacho kingesaidia kuanzisha mageuzi. Pesa hizi zilipatikana kwa msaada wa taarifa kutoka kwa hayati Mwibale Moha siku zile za karibu na umauti wake, alipomuita Golo Zumba kule gerezani.

Haikuwa pesa tu, mpaka matofali ya dhahabu ya mabilioni ya Dolari na vipande vikubwa vya almasi vilikuwemo.

Mali hizi zingesaidia pakubwa kutibu donda la uchumi lililokuwepo nchini Songomo.

Mwanaume alianza kwa kunyoosha vilivyopinda, na kama ujuavyo uozo na uovu kwenye serikali nyingi za ulimwengu huu na watu hawa huwa hawapendi kabisa kuguswa, na wana umoja haswa.

Yaani Magenge haya yameungana Dunia nzima japo ni vigumu kwa mtu wa kawaida kung’amua hili, lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Mabaduni wa Serikali waliamua kufanya tafrija chini ya Mkula mwenyewe, Fanton Mahal. Ambapo pia ingefanyika harusi ya Jiga Kinamba ambaye anatambulika kama Seif Hussein na Mwana. Hotel mojawapo ndani ya SHATOTO COMPLEX ndimo shughuli hii ilitakiwa kufanyika.

Huku wageni waalikwa wakiwa wengi kutoka sehemu mbali mbali ndani ya Bara la Weusi kutokana na umaarufu wa Mfanyabiashara nguli huyu, Fanton Mahal.

Ukumbi ulikuwa unanukia kipesa pesa tu, huku mgeni rasmi akiwa ni Raisi wa Jamhuri ya watu wa Songomo, Mh. Joseph Daro.

Watu walikuwa wakiingia taratibu huku wakionekana kukunwa vilivyo na kibao cha muziki kilichokuwa kinasikika vyema ndani ya ukumbi. Kazi safi ya Mwanamuziki Patrick Balisidya kutoka huko Afrika Mashariki, kibao kinaitwa Kuoana ni jambo la sifa. Vijana wa Golo Zumba walikuwa kazini kuhakikisha picha na video zinapatikana katika ubora wa hali ya juu sana. Hakika siku hii ilikuwa imefana sana.

Ulinzi ulikuwa umeimarishwa vya kutosha, yaani ukisikia watu wa JISA unatakiwa kuelewa kuwa ni ulinzi wa kiwango kingine huku wadunguaji wakiwa wamemwagwa kila sehemu mpaka umbali wa mita miatano kutoka kwenye hoteli hii.

Huku vyumba vya ulinzi wakiwa ni watu wa JISA wakirudufu taarifa picha kutoka kwenye Satelaiti. Ogopa sana. Hii yote ni kuhakikisha kuwa Raisi mpya hauawi. lakini pia kuhakikisha kuwa tukio hili la kihistoria kwa Jiga Kinamba linakamilika bila rabsha ya aina yoyote ile.



Mabaduni wa serikali walitokea wapi haswa?

Historia yao inarudi nyuma karne moja enzi za utawala wa Raisi wa awamu ya tatu wa Songomo Bw.Mungi Kakeli.

Tutawaelewa vizuri katika kitabu kingine kinachoitwa, ( SIRI YA MEZA ) panapo majaaliwa huko tutawachimbua historia yao kwa undani zaidi. Eee Mungu tujaalie uzima na afya tele sisi waja wako tuendelee kuwa pamoja.

******* ****** ****** ***** ****** ****** ******* ********



.Na Sonko Bibo. +255,653-532222. ( jina, Tiko Stana).

Kwa wale wenye moyo safi, Tunaomba mchango wa kiasi chochote kile utakachohiyari kutuchangia kama njia ya kutushika mkono kupitia namba hiyo ya Tigo hapo juu. Tutashukuru sana kwa hilo. Kumbuka kuwa mchango wako ni wa muhimu sana kwetu ili tuweze kupiga hatua katika haya tunayoyafanya, ahsanteni.

.Mwisho .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom