Riwaya: UCHU

KASHESHE-VI

Ilikuwa saa nne na nusu usiku, wakati
Jean na kundi lake walipoondoka
Kibumba kuelekea Goma.
"Hakika nimeridhika na ari ya wanajeshi
wetu na uwezo mkubwa wa vikosi vyetu,
pia nimefurahishwa sana na aina ya
silaha tulizonazo, hii inaonyesha ni jinsi
gani tumedhamilia kufanya kweli", Jean
alisema kwa kujiamini.
"Nilikwambia toka mwanzo kuwa ukifika
na kuona lazima utaamua tuingie vitani,
kwani hakuna sababu wala haja ya
kusubiri, vita vianze moja kwa moja,
tuchukue madaraka", Col. Gatabazi
alitamba huku Jean akitingisha kichwa
kukubaliana nae.
"Twendeni Goma tukafanye maamuzi.
Sijui kwa upande wa wenzangu, lakini
mimi nafikiri tuanze mashambulizi alfajiri
na mapema ila kwanza tukamate vikosi
vya hapa Gisenyi kabla ya jua
kuchomoza, maana adui hajui nguvu zetu,
sisi nguvu yake tunaijua", Jean alishauri,
wote kwa pamoja wakakubaliana.
"Mimi niko tayari wakati wowote, hata
sasa vijana wangu wako tayari, uamuzi
wenu tu ndio unasubiliwa", Col. Gatabazi
alijibu.
"Haya twendeni Goma tukafanye uamuzi
mara moja", Jean alijibu wakaondoka
haraka kuelekea Goma.

ITAENDELEA
 
asante Willy Gamba 1, shukrani, itakuwa vizuri sana ukiongeza tena.
 

kumbe inawezekana kumalizia kabisa. sasa shida ni nini? tuwape mji ni nini? weken no za m pesa niwape mji
 
Wakuu huwa mna type au mnapaste?kama inawezekana wakuu tuwekeeni audio ili iishe mara moja!dah
 
UCHU
KASHESHE
VI
Ilikuwa saa nne na nusu usiku, wakati
Jean na kundi lake walipoondoka
Kibumba kuelekea Goma.
"Hakika nimeridhika na ari ya wanajeshi
wetu na uwezo mkubwa wa vikosi vyetu,
pia nimefurahishwa sana na aina ya
silaha tulizonazo, hii inaonyesha ni jinsi
gani tumedhamilia kufanya kweli", Jean
alisema kwa kujiamini.
"Nilikwambia toka mwanzo kuwa ukifika
na kuona lazima utaamua tuingie vitani,
kwani hakuna sababu wala haja ya
kusubiri, vita vianze moja kwa moja,
tuchukue madaraka", Col. Gatabazi
alitamba huku Jean akitingisha kichwa
kukubaliana nae.
"Twendeni Goma tukafanye maamuzi.
Sijui kwa upande wa wenzangu, lakini
mimi nafikiri tuanze mashambulizi alfajiri
na mapema ila kwanza tukamate vikosi
vya hapa Gisenyi kabla ya jua
kuchomoza, maana adui hajui nguvu zetu,
sisi nguvu yake tunaijua", Jean alishauri,
wote kwa pamoja wakakubaliana.
"Mimi niko tayari wakati wowote, hata
sasa vijana wangu wako tayari, uamuzi
wenu tu ndio unasubiliwa", Col. Gatabazi
alijibu.
"Haya twendeni Goma tukafanye uamuzi
mara moja", Jean alijibu wakaondoka
haraka kuelekea Goma.
 
Ngoja tuanze ku copy na ku paste episodes zilizotangulia sasa maana tushaanza kusahau kama kuna riwaya inaendelea jeiefu...
 
KASHESHE-VII

Ilipofika saa tano kamili za usiku, Willy
Gamba na Bibiane walikuwa tayari
wamewasili Kibumba. Bibiane alizijua
vizuri njia za vichochoro za sehemu hii.
Hivyo, walifika bila tatizo lolote. Bibiane
alimuonyesha Willy sehemu yalipo
maghala makubwa ya silaha ambayo
baada ya Willy kuyaona, alitaka
waanzishe mapambano dhidi ya watu
wakiwa kwenye maghala hayo kwani
aliamini hapo ndipo nguvu kubwa ya
Akazu ilikuwa imewekwa.
"Sehemu hii inalindwa sana", Bibiane
alimwambia Willy baada ya kutoka
kwenye msitu na kuona kambi kubwa ya
kijeshi ambayo ilimshangaza hata Willy.
"Walijenga lini kambi kubwa ya jeshi
kama hii?", Willy aliuliza kwa mshangao.
"Hapa kulikuwa na kambi ya jeshi la
Zaire, na Akazu walipewa kambi hii baada
ya matukio makubwa ya Rwanda, na
mara moja wakaleta vifaa vyao vya kivita
na kuifanya kuwa kambi ya jeshi ya
kisasa kabisa. Ina kila kitu kama
unavyoona, taa, maji, mawasiliano, yaani
kuna kila kitu cha kisasa nakwambia.
Hata maafisa wa mashirika ya kimataifa
yanayoshughulikia wakimbizi
wanapotokea hapa kwa bahati mbaya
wanaamini ni kambi ya jeshi la Zaire,
maana kambi za wakimbizi ziko kilomita
moja tu kutoka hapa upande ule wa
kilima, hata wakiuliza basi huambiwa
kuwa hii ni kambi ya jeshi la Zaire, na raia
hawaruhusiwi kabisa kusogea karibu na
kambi hii", Bibiane alimwambia Willy,
ambaye wakati huo alikuwa ameshikwa
na mshangao.
"Maghala ya silaha ni yapi?", Willy alihoji
huku akichungulia kuangalia vizuri kambi
hii akitumia kiona mbali. Bibiane alitumia
nafasi hiyo kumwelekeza kila kitu. Kwa
vile kambi ilikuwa ikiwaka taa utafikiri
mchana waliweza kuona kila kitu vizuri
kabisa.
"Kambi hii yote imezungukwa na
seng'enge yenye umeme wenye nguvu
kubwa unaoweza kumuua hata tembo
haraka kama inzi, yaani ukigusa tu
unakaushwa kwa umeme kama nyama",
Bibiane alieleza.
Willy aliamua kwanza walifiche gari la
jeshi walilokuwa wakitumia kwenye msitu
ule, wakachukua mizigo yao ya kazi na
kasha wakatafuta njia ya siri kwa ajili ya
kuingia pale kambini.
"Hii kambi inaweza kuwa na askari kama
wangapi kwa kukisia kwako?", Willy
alimuuliza Bibiane.
"Eeeh… wanafika elfu tano na zaidi, wenye
mafunzo ya juu sana, wale askari wa
kikosi cha Rais wako hapa pia na askari
wenye ujuzi mkubwa. Kuna makomandoo
waliofuzu vizuri kama mia tano, halafu
kuna askari wa kawaida wenye mafunzo
mazuri vilevile zaidi ya elfu nne na mia
tano. Hivyo, kuna askari kama elfu kumi
hapa, na ndilo tegemeo kubwa la Akazu
kurudi madarakani. Lakini kusema kweli
wanaweza kushika tena madaraka,
ukichukulia ari, uwezo na vifaa vya kijeshi
walivyo navyo", Bibiane alimweleza Willy.
KKwa kweli kambi hii ilikuwa kubwa sana
kiasi cha kumtia hofu Willy Gamba, kwani
hakutegemea kabisa kukutana na kambi
kubwa ya adui yenye idadi kubwa ya
askari kama hii.
"Hebu nipe muda nifikiri kabla ya
kujitumbukia huko", Willy alimwambia
Bibiane.
"Hatuna muda Willy, hatuna muda kabisa
kabisa, lazima ufahamu kuwa tunatafutwa
na adui, na wakihisi tuko huku hakika
tumekwisha", Bibiane alilalamika wakati
Willy akimwangalia tu bila kusema kitu.
Baada ya Willy kutafakari kwa dakika
kadhaa alilazimika kumwambia Bibiane.
"Nikisema nahitaji muda wa kufikiri nina
maana dakika tano tu, lakini niwe peke
yangu, naamini sasa umenielewa?", Willy
alimwambia Bibiane huku akielekea
kwenye kichaka kilichokuwa hatua chache
kutoka walipokuwa wamesimama.
"Kumbe unaamini uchawi, wewe
unakwenda kuloga, mimi nifanyeje
sasa?", Bibiane alimkebehi Willy.
"Jifanyie lolote kwa imani yako", Willy
alijibu huku akipotelea kwenye kichaka.
Inasemekana katika hali kama hii ya
hatari Willy husali sana akimuomba
Mungu. Baada ya dakika kadhaa Willy
alirudi alimkuta Bibiane akiwa amebeba
silaha za kiasi chake akiwa tayari kwa
kusonga mbele kwa ajili ya mapambano
dhidi ya jeshi la Akazu.
"Ehe, sema sasa tunasonga mbele ama
tunarudi nyuma kumsubiri Col.
Rwivanga?", Bibiane aliuliza.
"Tunaendelea", Willy alijibu kwa mkato
huku akitoa vifaa vyake vya kazi kwenye
mkoba wake.
Willy alibeba silaha na vifaa vilivyokuwa
vimebaki, na kwa hadhari kabisa
wakaanza kuelekea kwenye ile seng'enge
yenye umeme.
"Mara nyingi ulinzi si mkali sana upande
wa ua kwa kuwa wanaamini hakuna kitu
kinachoweza kuzipenya hizi seng'enge
bila kufa kwa umeme, maana kila siku
wanyama wanakutwa wamejikaanga
wenyewe. Vilevile, kitu chochote
kinachokaribia mita moja ishara
inaonekana kwenye chumba maalum
kinachodhibiti usalama wa kambi hii
kama kuna kitu kinasogelea seng'enge
mara moja hatua za haraka za usalama
wa kambi zinachukuliwa.
"Yote haya yamefanywa lini?", Willy
alitaka kujua.
"Sababu ya pesa Willy, pesa, askari wa
kukodishwa kutoka Afrika Kusini ndio
wameleta vifaa na teknolojia hii iliyopo
hapa kambini. Tukifanikiwa utajionea
mwenyewe", Bibiane alidokeza.
Walipokuwa mita kumi kutoka usawa wa
seng'enge walisimama na Willy alitoa
kifaa maalum kwenye mkoba wake.
"Tutapita chini ya seng'enge, baada ya
kuchimba handaki".
"Itatakiwa liwe mita mbili kwenda chini,
vinginevyo tutakaushwa kama mikaa",
Bibiane alisema huku akionyesha
wasiwasi.
"Hili bomu", Willy alisema akiwa
ameshika bomu dogo lenye ukubwa wa
yai la kuku. "Lina uwezo wa kuchimba
handaki la urefu wa mita kumi na upana
wa mita tatu, na kina cha mita tatu
unasemaje?".
"Sikupingi, kwa teknolojia ya sasa hata
mimi nimeona maajabu mengi katika
vifaa vya vita, teknolojia imeendelea
sana. Haya chimba tuone".
Willy alishika kisu na kuanza kuchimba
shimo la mita moja kwenda chini, kisha
akawasha lile bomu na kulitumbukiza
pale shimoni na kulifukia.
"Litalipuka baada ya nusu dakika turudi
nyuma haraka tulale chini".
"Halitasikika baada ya kulipuka?".
"Hapana, bomu hili limetengenezwa
mahususi kwa ajili ya matumizi kama
haya, ili kuziba mlio ndio sababu
tunalizika chini ya ardhi", Willy
alimwambia Bibiane na kumtoa hofu.
Baada ya nusu dakika bomu lile lililipuka
na kutoma sauti kidogo, hii yote ilitokana
na kazi ya Willy na kukatokea handaki
zuri kwa ajili ya wao kupita bila kikwazo.
"Bwana, hakika kazi yako nimeipenda,
sasa tuingie ndani tukafanye kazi
iliyotuleta, kikwazo hiki ndicho kilikuwa
kinanipa wasiwasi mkubwa", Bibiane
alisema wakati wakiingia ndani ya
handaki ili wapite kwa ajili ya kuwakabiri
wanajeshi zaidi ya elfu kumi ndani ya
kambi yao.


ITAENDELEA
 
Asante sana mkuu kid kud. Hadi kamalaria kangu kanaanza kupungua kwa faraja ya riwaya hii
 
Ngoja niingie mzigoni nivitafute hivi vitabu nitawajulisha wadau.nimetafuta vitu mara nyingi ti na kuvipata vingine vilikuwa vina fichwa katikati ya mapaja na nimefanikiwa kuvipata ndio iwe hv vitabu,subirini

Mkuu umefikia wapi issue ya vitabu?
 
Mh!! nifanyeje sasa inabidi kuwa mpole
 
duh mtatuua nyie vijana mnaoonekana kufahamiana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…