Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

UCHU
KASHESHE
XI
Nkubana aliamua kuwasiliana na Col.
Gatabazi kwa simu ya upepo. Alipompata
alikuwa tayari amewasili Goma na
walikuwa wameanza mkutano. Nkubana
alieleza kwa kirefu yote yaliyotokea na
kisha akashauri. "Huyu Willy Gamba hajui
nguvu zetu. Hivyo, ameamua kwenda
kujinyonga huko Kibumba, mimi naelekea
huko kwenda kuongeza nguvu na
kuwashitua makamanda wetu ili
tumkamate kabla hajaleta kasheshe
zake".
"Sawa, fanya hivyo, Jean anahitaji
kumuona akiwa hai", Col. Gatabazi
alikubaliana na Nkubana na kumweleza
shabaha ya bosi wao Jean.
"Vilevile nitazungumza na makamanda
hapa ili waniruhusu tupeleke jeshi
mpakani kumsaidia Luteni Nyamboma
kudhibiti mpaka wa Zaire, mpaka hapo
amri ya kuishambulia Rwanda
itakapotoka. Sisi tuko tayari, naamini
uamzi utatoka haraka ili kazi ianze alfajiri
ya leo. Hebu ngoja kidogo usizime radio
yako", Col. Gatabazi aliwaeleza wenzake
mambo yalivyokuwa Gisenyi na jinsi
ambavyo Nkubana alikuwa akihisi kuwa
Willy ameelekea Kibumba. Mara moja
Jean alisimama baada ya kusikia habari
hii ya Willy kuelekea Kibumba. Haraka
alichukua radio na kutoa maagizo kwa
Nkubana.
"Sikia, sisi tunakuja huko sasa hivi,
tutakuja kwa ndege yangu na mimi
nitaondoka. Sasa hivi bado tunawasiliana
na Kamanda Bazimaziki awahi uwanja wa
ndege. Waeleze wakiwakamata Willy na
Bibiane wasiwaue kwanza mpaka tufike,
hao ni halali yangu", Jean alitoa amri.
"Unafikiri ni busara sisi viongozi wa juu
kwenda huko?", Anatoile kabuga alihoji.
"Bila shaka, huko ndiko yaliko majeshi
yetu na ndiko tutakapotoa amri", Jean
alieleza msimamo wake.
"Mimi pia nafikiri tuwe pale wakati
wanajeshi wanaelezwa kukaa tayari kwa
ajili ya kuanza vita alfajiri, hii
itawaongezea mori", Jenerali Kasongo
alijibu.
"Na mimi nimefurahi sana kwa uamzi
huo, kuanzia sasa ofisi yetu kubwa ya
kuratibu shughuli za vita itakuwa
hukohuko Kibumba, maana ndiko kwenye
vifaa vyote, sioni sisi tutafanya nini hapa
wakati kila kitu chetu kiko kule", Col.
Gatabazi alieleza kwa sauti ya juu.
"Sawa, wengi wape", Kabuga alijibu.
Kisha wakawasiliana na Col. Marcel
Bizimaki, ambaye ni Kamanda wa jeshi la
Akazu wakitumia njia ya simu ya satellite,
wakamweleza kuwa wote walikuwa
wanarudi hapo tena, kwa ajili ya kutoa
mwongozo na ruksa ya kuanza
mapambano dhidi ya adui alfajiri ile.
Vilevile, alielezwa aweke vikosi vyake
vyote kwenye tahadhari ili waweze
kumsaka na kumkamata Willy Gamba
akiwa hai.
"Karibuni, nitawapokea na nitawaweka
kwenye nyumba ya mkufunzi wetu mkuu.
Kamanda Moris ambayo ina ulinzi mkali
pia inalindwa na mitambo ya kisasa ya
usalama. Na mtakapokuwa pale kwake
itakuwa rahisi kwenu kuona kwa macho
jinsi majeshi yetu yanavyosonga mbele
kupitia mitambo ya kisasa kabisa", Col.
Bizimaziki alitamba.
Kundi zima liliondoka kuelekea uwanja wa
ndege, likiwa tayari kuelekea Kibumba,
ambako kuna umbali usiozidi dakika kumi
kwa ndege, Jean alifikiria kuwa ni vizuri
kuwa na ndege yake karibu, ikiwa kwa
bahati mbaya kikatokea kitu na kutakiwa
kuondoka ghafla na kujisalimisha aweze
kufanya hivyo kwa ndege yake. Wakati
wanaelekea uwanja wa ndege. Co.
Gatabazi aliwasiliana tena na Nkubana.
"Uko wapi sasa?".
"Nimekwisha kuwasili Kibumba na sasa
naelekea kwenye lango kuu la kuingilia
ndani, nimewasiliana nao kwa radio
wananisubiri", Nkubana alimweleza Col
Gatabazi.
"Sawa, kazi yako kubwa ni kumkamata
huyo Willy na kikaragosi chake huyo
Bibiane na uwalete kule mlimani ilipo
nyumba ya Kamanda Moris, sisi tutakuwa
huku muda si mrefu", Col. Gatabazi
aliagiza.
"Nitafanya hivyo afande. Mara hii kaingia
mkenge yeye mwenyewe", Nkubana
alijibu.
"Lakini mtu huyu ni hatari sana, naomba
umwambie Kamanda Bizimaziki mchukue
tahadhari kubwa sana. Hata tulipofika
sitaki makosa yatokee", Col. Gatabazi
alisisitiza.
"Sawa afande, tutafanya hivyo, lakini mtu
mmoja na mwanamke mmoja wanaweza
kufanya nini mahali kwenye kambi kubwa
ya jeshi kama Kibumba?", Nkubana
alihoji.
"Wewe chukua hadhari ya hali ya juu huyu
mtu si wa kawaida", Col. Gatabazi
alisisitiza na kuzima radio.
Nkubana alifahamu kuwa viongozi wake
walikuwa na mashaka na Willy, lakini
Nkubana yeye hakuna na wasiwasi.
Aliamini kuwa huu ndio ulikuwa mwisho
wa Willy Gamba. Ulinzi na uwezo wa
kambi ya Kibumba ulikuwa mkali mno,
kiasi kwamba ilikuwa vigumu sana kwa
mtu mmoja kuingia na kutoka salama.
Gari lilisimama na kumwondoa Nkubana
katika mawazo yake. Walikuwa wamefika
kwenye lango kuu na kusimama kama
ilivyo sheria ya kusimama na kukaguliwa
kabla ya kuingia ndani ya ngome hii.
Nkubana alipoangalia saa yake ilikuwa
yapata saa sita na nusu usiku
 
dah hii riwaya itatumaliza. mareche maliza tuwaze mengine
 
UCHU
XII
"Saa ngapi sasa?" Bibiane alimwuliza
Willy Gamba.
"Imefika saa sita na nusu sasa", Willy
aliMjibu.
Walikuwa tayari wana saa moja ndani ya
kambi hii ya kijeshi na bado walikuwa
hawajapata tatizo lolote. Sasa ndio
walikuwa wanaanza kutega mabomu
kwenye bweni la mwisho ili baada ya
hapo kama itawezekana watafute namna
ya kutoka nje, kwani mabomu waliyokuwa
wameyatega na kuyaprogramu kwa saa
ya Willy ili kuyalipuwa lazima wawe
mbali, maana yalikuwa na uwezo wa
kuharibu kambi nzima na vitu vyote
vilivyomo kama yangefanya kazi kama
ilivyotarajiwa. Wakati wanafikiri hivi,
ghafla taa za kiwanja cha ndege
zikawashwa.
"Aha, kumbe ule ni uwanja wa ndege!"
Willy alinong'ona.
"Ndio, unafikiri zile ndege za kijeshi
zinaruka kutokea wapi!", Bibiane ambaye
naye hapo awali alikuwa hajui uwanja
ulikuwa wapi, alijibu.
"Kwanini wanawashwa taa wakati huu?",
Willy alijiuliza.
Wakiwa wameduwazwa na kitendo hiki na
wakiwa sasa wameondoka kwenye ukuta
wa bweni la mwisho na kujibanza kwenye
kivuli cha lori kubwa la jeshi lililokuwa
limeegeshwa pale, Bibiane alijibu.
"Huenda ndege za kivita zinatolewa ili
zikashambulie mahali ama ndege ya Jean
inataka kutua".
"Nafikiri hilo la pili ni sawa. Hii itakuwa
raha sana mimi kukutana uso kwa uso na
huyu bwana yako", Willy alikejeli Bibiane
akafadhaika.
"Si bwana yangu tena, bwana yangu ni
wewe Willy, maana wewe ndiyo uko na
mimi sasa, sema, fanya kila unachotaka
nifanye", Bibiane alijibu kwa sauti ya
mahaba. Willy alimwangalia, kisha
akamshika na kumbusu.
Mara wakasikia king'ola na askari
wakatoka na kuanza kuelekea kwenye
kiwanja cha ndege.
"Hapa kuna hatari, nafikiri
wametushitukia", Willy alisema huku ile
kengere yake ya hadhari ikilia kichwani
mwake. Kisha akaendelea. "Kinachotokea
hapa ni sisi kutoka ndani ya kambi hii.
Wataanza kutusaka sasa hivi".
Mara tena wakasikia mwungurumo wa
ndege na magari sita aina ya Landrover
ya wazi yakiwa yamebeba askari
yakielekea karibu na uwanja, yalipokaribia
yakasimama. Kisha, yakafika magari
mengine mawili aina ya Landcruiser GX
nayo yakasimama pale vilevile kusubiri ile
ndege itue. Pale kwenye uwanja mkubwa,
vikosi vya askari vilizidi kujipanga kwa
ajili ya mapokezi.
Ile ndege ilipotua watu wanne walitoka
ndani ya Landcuiser zilizokuwa
zimesimama kando na kusogea karibu ili
kuilaki ile ndege. Wakiwa bado
wamefichwa na kivuli cha lile Lori
walitumia viona mbali vyao na
kuwaangalia kwa makini wale watu
waliotoka kwenye yale magari.
"Yule aliyetangulia ni Col. Marcel
Bazimaziki, huyu ndiye kamanda mkuu
wa majeshi yote ya Akazu. huyo wa
kushoto ni Kapten Nkubana aliyekutoroka
Kigali, ndiye aliyetumwa kuniua, kumbe
naye keshafika huku. Wa kulia ni
kamanda Morris huyu ni mkuu wa vikosi
vya kukodiwa ambavyo vinafundisha
majeshi ya Akazu. Huyu wa nyuma
simfahamu".
Ndege ilisimama na milango ikafunguliwa
na watu wakaanza kutoka. Jean ndiye
alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya
ndege hii.
"Aha huyu ndiye Jean nafikiri?", Willy
aliuliza.
"Bila shaka huyo ndiye Jean, ambaye
ndiye mzizi wa fitina katika Rwanda. na
yule anayemfuatia ni Anatoile Kabuga,
huyo ndiye kiongozi wa Akazu, anayefuata
ni Jenerali Kasongo, kamanda wa majeshi
ya Rais wa Zaire, rafiki mkubwa wa Jean,
anayetokea sasa pale mlangoni ni Col.
Gatabazi na huyo anayetokea mwisho
simfahamu, maana sijawahi kumuona",
Bibiane alieleza.
"Asante, sijui bila wewe ingekuwaje,
umefanya kazi yangu iwe rahisi kiasi
fulani".
"Ni kweli, lakini ungetumia njia nyingine,
wewe si wa kushindwa jambo".
Baada ya kutoka ndani ya ndege, kundi la
Jean liliingia ndani ya zile Landcruiser
wakaondoka huku wakisindikizwa askari
kwa ulinzi mkali.
"Unadhani watakuwa wanaelekea wapi
sasa?", Willy alimuuliza Bibiane.
"Sijui, nilitegemea huenda wanataka
kuzungumza na vikosi vilivyofanya
gwaride pale uwanjani, lakini
wameondoka moja kwa moja kuelekea
upande ambao ndiko kuna lango kuu.
Huenda wanakwenda kupumzika kwa
kamanda Morris, nyumba na ofisi ya
kamanda Morris iko juu ya hicho kilima,
huwezi kuona ukiwa hapa kwa vile
kumefichika kwa miti", Bibiane alieleza.
Kati ya magari yaliyobeba askari moja
halikuendelea na msafara isipokuwa
lilielekea kwenye gwaride. Gari hilo
lilipofika hapo lilisimama na watu
waliotoka ndani walikuwa Nkubana na
askari wengine watano. Kisha Nkubana
akaanza kuhutubia hilo gwarinde na
kikosi kimoja wapo kikapiga hatua moja
mbele na vingine vikatawanyika. Willy na
Bibiane hawakuelewa nini kilikuwa
kinaendelea.
"Lililopo ni sisi kuondoka hapa kambini
haraka iwezekanavyo. Vinginevyo
tutakamatwa hata kabla hatujamaliza kazi
iliyotuleta", Willy alieleza.
"Mimi bila kummaliza huyu Jean siendi
kokote ng'o", Bibiane alijibu kwa hasira.
"Lazima ufahamu kuwa hatuwezi
kukabiliana na watu wote hawa, lazima
kutumia akili ya ziada, wewe unajua
katika kazi yetu hii swala ni kuendelea
kuishi; lazima uhakikishe unajilinda ili
ubaki salama. Hapa tukitaka kuanza
mapambano ni sawa na kujinyonga sisi
wenyewe. Pili ili tuweze kulipua mabomu
tuliyotega ni lazima tutoke nje kabisa ya
eneo hili, la sivyo sisi pia tutakuwa
tumejiteketeza pamoja na adui", Willy
alimuasa Bibiane kisha wakaona wale
askari wa kikosi wanakabidhiwa silaha na
kuelekea kwenye seng'enge ya ua wa
kambi.
"Ehe, umeona kazi hiyo, hawa jamaa
wanategemea tutakuja hapa, lakini
hawajui kama tumeingia ndani na kazi
imefanyika", Willy alieleza.
"Lakini wakifika pale tulipoingilia lazima
watajuwa tuko ndani", Bibiane alijibu.
"Ndio sababu nikasema tutafute njia
tutoke humu ndani", Willy alisisitiza.
Wakati wote Willy alikuwa akipanga mbinu
za kuweza kutoka ndani ya kambi hii
wakiwa salama.
"Hebu nifuate tuangalie hali ikoje upande
wa lango kuu", Willy alimwambia Bibiane.
"Kule hatuwezi kupita, afadhari tuwahi
palepale mahali tulipotumia mwanzo",
Bibiane alisema na Willy akamuunga
mkono na kuona alikuwa na mawazo
sahihi hivyo, haraka haraka wakaelekea
sehemu waliyokuwa wameingilia, huku
askari wa doria wakizidi kujipanga na
kupewa silaha ili kuzidi kujipanga kando
ya ua huu wa seng'enge wakiwa tayari
kulinda kambi yao. Ile tembetembea ya
hawa askari kiasi fulani iliwasaidia sana
akina Willy na Bibiane kutobainika
mapema kwani walikuwa wamevaa
mavazi ya kijeshi kama wale askari.
Nkubana na watu wake waliweka ulinzi
mkali upande la lango kuu wakiamini
kuwa Willy angeweza kujaribu kuingia
pale kambini kwa kutumia lango kuu.
Hakuna askari wala kiongozi katka kikosi
chicho aliyefikiri kuwa adui wangeweza
kupitia sehemu nyingine yoyote kwani
waliamini kwamba hakuna kitu ambacho
kingeweza kupita ua ulioizunguka kambi
hii. Hivyo, hata hawakuweka askari
kuzunguka ua ilikuwa ni kwa hadhari tu.
Kumbe kitu ambacho hawakujua ni
kwamba teknolojia yotote inaweza
kushindwa na teknolojia nyingine yenye
maarifa ya juu zaidi. Willy alikuwa ndani
na tayari alikuwa ametega mabomu kila
upande.
 
Mareche pokea pongezi zangu umesema utamu ndo unakuja ombi langu kila upatapo wasaa tupia walaji tupo.
 
Back
Top Bottom